Friday, April 26, 2019

MZIKI WA KUOLEWA UNAHITAJI TABIA NA SI VINGINEVYO



Wanaume wanavyotafuta mke wa kuoa kiu yao sio kupata mwanamke maarufu, mwenye jina kubwa, mwenye shule kubwa, mwenye kuongea sana, anayetaka kujulikana kila akiwa kwenye jumuiko la watu, la hasha. Wao wanaangalia vijitabia vilivyofichika, wanachunguza vile unavyodhani sio muhimu kwao, wanaangalia utayari wako kuwepo kwa ajili ya mume na watoto, utayari na ujuzi wako kwenye kuandaa mlo, usafi wako na mazingira yako sio masaa 24 ukobize kulinda kucha zisichafuke. Kutwa umeshika simu unakenua meno tu kufurahia ubuyu wa kwenye mitandao. Usiringie uzuri wa sura na wa umbo, wenzako hawaangalii hilo sana, kaulize wanawake wenzako walio navyo hivyo vyote lakini wanazeekea kwa wazazi wao au kuishia kuwa mahawara tu. Unazani ni kwamba hawataki kuolewa? Nooo!! Nikwamba bidhaa hainunuliki. Kwani wangapi wamekuahidi kukuoa wakaishia kuoa wengine na tena wakaoa ambao wewe umewazidi uzuri?? Change your priorities my dear, lasivyo UTASUBIRI SANA Tu huku ukishona sare za harusi za wenzako tu. Huu mziki unataka tabia sio vingine. Jifunze kutofautisha daftari na jalada la daftari .

from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2Pzlm6C

No comments:

Post a Comment