Saturday, April 27, 2019

KUJICHUA HUZAA TABIA HIZI ZAAJABU





Huu ndiyo ukweli, tena ukweli unaouma! Kujichua kuna madhara makubwa hata kama unaona kunakupa raha. Kujichua kunaweza kukufanya ukawa mtumwa wa tendo hili na ukifikia hatua hii basi ni dhahiri kuwa kumeshaathiri afya yako ya akili kwa kiasi kikubwa.
Kila kitu utaanza kukitafsiri kinyume, hautaona kama unapata ladha yoyote ya tendo la ndoa na mwenzi wako. Lakini sio kweli kama ladha ya mwenzi wako imebadilika au kupotea, la hasha, ila kujichua kumeshabadili akili yako na mbaya zaidi umeshakuwa mtumwa wa kitendo hiki kutokana na kukifanya mara kwa mara.
Kwa kuwa akili yako imeshaelemewa na kujichua, itakuwia vigumu kwako kuacha na ukweli ni kwamba ukishafikia hatua hii, huwezi kufanikiwa kuacha kwa jitihada zako mwenyewe. Jitahidi kutafuta msaada wa kitabibu, kisaikolojia na kidini. Hapa namaanisha madaktari, wanasaikolojia na watumishi wa dini kwa pamoja ndio watakaofanikisha kukusaidia kuacha kujichua.
Na hizi ndizo faida utakazozipata ukiacha kujichua. Kujichua kutaimarisha afya ya mfumo wa akili yako na kukukinga dhidi ya hatari ya kupata magonjwa ya akili kama vile sonona. Jaribu kufikiria, upo ndani umejifungia, taratibu unaanza kujitengenezea mazingira ya kukaribisha hisia za kufanya tendo la ndoa, unaanza kuvikumbuka vitu vinavyoamsha hisia zako, (wengi wameniambia huwa wanaangalia video za ngono) na hatimaye unaanza kujichua.
Lakini ukweli ni kwamba baada ya kujichua ni dhahiri kinachofuata pale ni kujilaumu, na unatumia muda mwingi kujilaumu kwa kitendo ulichokifanya kwa raha za dakika chache tu. Taratibu unaanza kujikuta unaugua sonona bila kujijua kutokana na mawazo na kujilaumu kila unapomaliza kujichua. Hatimaye unajikuta unaanza kuwachukia watu wa jinsia ya tofauti na wewe unapoteza hisia kwa vile vitu muhimu ambavyo awali vilikuwa vinakupa furaha. Hii ni dhahiri kuwa unaugua sonona na kujichua kumekusababishia hali hii. Acha kujichua sasa.
Kuacha kujichua kutakusaidia kurudisha nguvu zako za kijinsia na kuwathamini watu wa jinsia tofauti na wewe. Ukweli ni kwamba kujichua kunamfanya mtu asione thamani ya mtu wa jinsia tofauti na yeye. Kwa sababu tayari akili yake umeshaathirika kisaikolojia anajiona kuwa haja yake ya kimapenzi anaweza akaitimiza yeye mwenyewe pasipo ushirikiano na mtu mwingine.
Kwa mwanamke aliyekuwa mtumwa wa kujichua, ni vigumu sana kuiona thamani ya mwanaume kwake kwa kuwa anajiona anaweza akajikidhi yeye mwenyewe; na hali kadhalika kwa wanaume pia. Hii ni mbaya sana. Lakini pia, kujichua kunachangia kupoteza uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.
Kwa mwanaume kunaweza kumsababishia uume kulegea au kuwahi kufika kileleni, na kwa mwanamke kujichua kunampotezea ile hali ya kuhimili tendo la ndoa (sexual drive).
Kuacha kujichua kutasaidia kuyakabili matatizo haya na hatimaye mtu atajikuta taratibu anaanza kuthamini uwepo wa mtu wa jinsia nyingine, kurudisha nguvu za jinsia na kumfanya afurahie tendo la ndoa na mwenzi wake kama inavyotakiwa.

from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2vm3dAb

No comments:

Post a Comment