Ilipoishia, Sehemu ya nne, Alipomaliza kula akaanza safari ya kurejea nyumbani kwake.Mlango wa chumba cha mage ulikuwa wazi lakini hakuwa na hamu hata ya kutaka kuchungulia ndani .Moja kwa moja akaenda chumbani kwake na kuufunga mlango akapanda kitandani kulala kwani tayari siku yake ilikwsha haribika endelea………………
Dakika kama kumi hivi toka isack arejee chumbani kwake ukaingia ujumbe mfupi katika simu yake. Akaichukua na kuutazama ujumbe ule ulitoka wapi. Ulitoka kwa mage. Ujumbe ulisomeka hivi ” isack mbona hujanijibu? bado nakusubiri ili tule chakula.Nimepika chakula cha watu wawili.Naomba unijibu tafadhali” isack akatafakari na kuamua kumjibu mage
” Mimi nimetoka kula mgahawani. Nilitaka tule wote lakini niliogopa baada ya kumkuta mumeo mpya. Sikutaka kukuletea matatizo. Nashukuru mage naomba uendelee kula mimi sintakuja”
akausoma tena ujumbe ule akaridhika kisha akautuma Baada ya dakika moja ukaingia tena ujumbe toka kwa mage
” isack uliogopa bure ,yule si bwana wangu. Yule ni kaka yangu wa kuzaliwa tumbo moja na alikuja kunitazama baada ya kumtaarifu kwamba nimeachana na yule bwana wangu.Kaka yangu yule anafanya kazi mamlaka ya mapato na alikuja kuniona kama nina tatizo lolote anisaidie kwa sababu katika famila yetu tuko watoto wawili tu.” Isack akatabasamu baada ya kuusoma ujumbe ule mfupi kisha naye akaandika ujumbe wa kumjibu mage
” Samahani sikujua kama yule ni kaka yako. Nilifikiri labda ni mume mpya. Nisamehe kwa kukufikiria vibaya mage” akautuma ujumbe ule na baada ya muda ujumbe ukaingia tena toka kwa mage
” isack mimi ni mwanamke ninayejiheshimu sana tofauti na unavyonifikiria. Nashukuru hata hivyo kwa kuniona ni mtu mwenye tabia za kubadilisha wanaume. Sikutegemea kama ungeweza kunifikiria hivyo”
Isack akajilaumu sana kwa kumuwaza mage kwa ubaya namna ile.Alitambua kwamba mage alikwisha chukia kwa hiyo akaanza juhudi za kumpooza. Akaamua kumpigia simu ambayo ikaita bila kupokelewa. akapiga tena lakini simu ikaita na haikupokelewa. isack akainuka na kukaa kitandani
” Nimeshharibu kila kitu. mage amechukia na hataki hata kuipokea simu yangu.Kwa nini lakini niliamua kumweleza vile? Sikupaswa kumwambia vile.Wivu wangu wa kijinga sasa umeniharibia kila kitu.Sijui nitamwambiaje ili aweze kunielewa na kupunguza hasira zake.Akawaza sana na kisha akaamua kuandika ujumbe mfupi wa maandishi.
“Naomi nafahamu umechukia sana kwa maneno niliyokuambia.Nakuomba usikasirike tafadhali. Nisamehe kama nilikuudhi halikuwa lengo langu kufanya hivyo. Nilipomuona yule kaka yako ni kweli nilifikri labda ni mtu wako na nikajisikia vibaya kwa sababu baada ya kuachana na yule bwana wako nilitegemea kwamba ungekaa mwenyewe na kujijenga kwanza.Nakujali na sipendi mwanaume yeyote akulaghai kama yule uliyeacha naye.Nadhani umenielewa.Ulale salama” akausoma ujumbe ule na kuhakikisha kwamba uko safi kisha akautuma halafu akajifunika shuka na kutafuta usingizi.
Mage alipoupata ujumbe ule wa isack alitabasamu.
” Sasa nimeamini kwamba isack ananijali na kuna kila dalili kwamba ananipenda kwa sababu kama asingekuwa na hisia za kimapenzi juu yangu asingekuwa na wivu kwa kaka yangu.”
” Hizi ni dalili njema sana kwangu.Ninampenda isack na sasa nimeamini hata yeye ananipenda. Kitakachofuata sasa ni kuanza kumfahamu kiundani. Nataka kuzifahamu tabia zake zote za ndani na nje.Nitaweza kuzifahamu tabia zake iwapo nitakuwa na mazoea naye ya karibu.” akawaza mage huku akitabasamu na kuufunga mlango wake akapanda kitandani kulala.
**************************************************
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2DEPnNn
No comments:
Post a Comment