ILIPOISHIA Sikutaka kabisa kuendelea kuwepo maeneo yale ya sebuleni kwani huenda hali ya hewa ingechafuka na kuzuka balaa kubwa. “Namshukuru Mungu kama naye ni mzima wa afya”. Ilinikuta nikiwa mlangoni kuingia chumbani kwetu. SASA ENDELEA Nikiwa chumbani nilibadilisha nguo haraka haraka na kwenda kujimwagia maji ili kuondoa uchovu pamoja na mawenge niliyokuwa nayo. Nilibadili nguo safi na zile chafu nikaziweka katika kapu la nguo chafu. Kisha nikaelekea sebuleni ambako alikuwako mke wangu. Pale nilimkuta mke wangu amekwishaandaa staftahi tayari na alikuwa akinisubiri mimi tu ili tuweze kujumuika pamoja. “Chai hii tamu sana mke wangu hakika wewe ni fundi wa mapishi”. Nilijibaraguza pale kumsifia mke wangu kwa lengo la kuficha madhambi yangu niliyoyatenda usiku uliopita. “Ahsante sana mume wangu. Pia kuna jambo moja ambalo nataka kukushirikisha mume wangu”. Aliongea mke wangu huku akinitazama machoni. Moyo wangu ulinipasuka paa! Nilihisi mambo huenda yalikuwa yameharibika. Nilidhani kwamba mke wangu alikuwa tayari kashagundua usaliti ambao nilikuwa nimemfanyia. Nilitamani ardhi ipasuke nami nitumbukie na kujificha humo. “Jana nilikwenda hospitali kupima baada ya kujiona kwamba afya yangu ni tofauti. Majibu yameonesha kwamba nina ujauzito wa miezi miwili”. Sikuyaamini macho yangu na masikio yangu kwa kile ambacho nilikuwa nikikisikia. Ni jambo ambalo nilikuwa nikiliomba kwa muda mrefu sasa kwa mwenyezi Mungu ya kwamba atujaalie kupata mtoto. “Waaaaaaoooow! Wasema kweli mke wangu? Dah! Yaani siyaamini masikio yangu. Ahsante sana mke wangu kwa kunipa zawadi hii adhimu. Nakupenda sana mke wangu na nitazidi kukupenda milele”. Niliongea kwa furaha kubwa sana maneno ambayo sidhani kama yalikuwa na ukweli ndani yake kwa sababu kama ningekuwa nampenda mke wangu nisingethubutu kumsaliti hata siku moja. Nilisimama kutoka pale nilipokuwa na kumfuata mke wangu. Nilimkumbatia na kumpa mabusu mengi na motomoto ambayo yalimpa wehu mke wangu na niliihisi furaha yake ambayo aliikosa kwa muda mrefu kutoka kwa mume wake. Mke wangu Rose alijisikia furaha kubwa sana kwa mapenzi ya dhati kabisa ambayo nilimwonyesha bila kutarajia siku ile kwani ni kwa kipindi kirefu sana sijawahi kumwonesha kwamba namjali. “Sasa itabidi nianze kuhudhuria kliniki mume wangu na tunapaswa kuhudhuria pamoja kwa ajili ya maelekezo ya afya ya mama na mtoto na familia kwa ujumla”. Mke wangu aliniambia kwa msisitizo. “Wala usijali mke wangu yaani hata kama hiyo kliniki iko ulaya mi nitakupeleka tu. Nakupenda sana mke wangu”. Nilimwambia Rose mke wangu maneno ambayo yalimfurahisha na kuuona uso wake umechanua kwa furaha kubwa sana. Tuliendelea kupata kifungua kinywa pamoja pale mezani huku tukibadilishana mawazo kwa vicheko vilivyoambatana na furaha kubwa sana. Baada ya kumaliza kupata chai mimi nilimuaga mke wangu kwamba nakwenda katika majukumu yangu ya kila siku huku nikimwahidi kwamba nitawahi kurejea baadaye. Mke wangu alinitakia kila la kheri katika mizunguko yangu. Siku ile mchana wote niliupitisha kwa Maggie huku tukipeana mahaba tele. Siku hiyo nilimpa penzi moto sana zaidi ya lile ambalo nilimpa usiku wa jana yake. Maggie alizidi kuchanganyikiwa nami na kuahidi kwamba hatakuwa radhi kunipoteza kutoka katika mikono yake kwa hali yoyote ile. Alasiri ya siku ile nilimuaga Maggie kwamba nilikuwa naenda kunyosha nyosha miguu kwa marafiki zangu hivyo tutakutana kesho. “Kwa nini usirudi kuja kula chakula cha usiku honey mbona mimi nitakuwa mpweke mpenzi”. Aliniambia Maggie kwa sauti ya kubembeleza sana iliyokuwa ikitokea puani. “Nitakuja kesho mpenzi wangu wala usijali. Nakupenda sana darling”. Nilimwambia maneno hayo huku nikimuaga kwa kumpa busu zito sana ambalo lilimchanganya sana. Maggie ilibidi akubaliane na mimi ingawa alikuwa hajaridhika kutoka moyoni kwa mimi kukataa kurudi usiku ule kula chakula pamoja naye. Baada ya kutoka kwa Maggie moja kwa moja nilinyoosha kwenda nyumbani. Nilikuwa nina imani kwamba siku ile mke wangu angefurahi sana kwani hakuna siku ambayo nimewahi kurudi nyumbani mapema kama siku ile tena huku nikiwa safi kabisa. Pia siku ile nilikuwa sijapata pombe hata kidogo hali ambayo ilikuwa haijawahi kutokea kabisa hata siku moja katika maisha yetu kwani kila siku nilikuwa nikirejea nyumbani nikiwa chapachapa kwa kilevi. Kwa kifupi mke wangu alikuwa si mlevi na alikuwa ni mtu ambaye alikuwa akimcha Mungu sana. Yaani nilikuwa na bahati kubwa sana kuwa na mke mwema na bora kama huyu ingawa mimi mwenyewe nilikuwa sijitambui. Nilipofika nyumbani nilishangaa sana kwa hali niliyoikuta pale. Mke wangu alikuwa amenuna kweli. Nilimsalimia lakini alinijibu kwa unyonge sana kama mtu ambaye alikuwa ni mgonjwa vile. Niliogopa kwa kweli. Nilijua hapa tayari mambo yalikuwa yameharibika. Tumbo lilianza kuniunguruma. Nilijipa moyo kwamba litakalokuwa na liwe. Lakini moyoni nilikuwa na hofu sana kwani mwili wangu ulikuwa umejaa sana madhambi ya uzinzi na ulevi kuanzia unyayoni mpaka utosini. Niliendelea kujibaraguza pale sebuleni kwa kumwongelesha mke wangu lakini hola. Nilishangaa sana. Mbona mke wangu asubuhi nilimwacha katika hali ya furaha kabisa na tukaagana kwa chereko, nderemo na vifijo sasa saa hizi imekuwaje tena. Ama kweli Stanley mimi nilikuwa na mtihani mkubwa sana leo hii. Lakini mambo haya nilikuwa najitakia mwenyewe hivyo hata sikuilaumu nafsi yangu. Ulikuwa ni ulimbukeni na tamaa zangu za ngono ndizo ambazo zilikuwa zikiipiga dafrao ndoa yangu Hali ilizidi kuwa tete pale sebuleni. Mke wangu alikuwa amenuna hasa. Mimi nilikuwa nikishika na kuacha kila kifaa ambacho nilikuwa nikikiona mbele yangu. Mara nishike rimoti, mara nijifanye kusoma magazeti, mara nitandike vizuri vitambaa, mara nipige mluzi, mara niimbe yaani ilimradi kujibaraguza tu. Mke wangu alikuja pale sebuleni na kuketi katika sofa lililokuwa mkabala na lile ambalo nilikuwa nimekaa mimi. Alinitazama kwa muda wa kama dakika mbili usoni bila ya kuzungumza chochote. Hatimaye niliyashuhudia machozi yakimtoka mke mke wangu kutoka katika mboni za macho yake na kuporomoka kupitia katika mashavu yake laini kuelekea kidevuni na kuanguka kifuani mwake. Dah! Hali ile ilinihuzunisha kwa kweli na kuipatia nafsi yangu unyonge wenye mashiko. Nilimwonea huruma mke wangu kuwa katika hali ile ya simanzi ambayo alikuwa nayo kwa muda ule. Nilitamani nisimame nimfuate na kumkumbatia ili kumfariji lakini nilikuwa na hofu kwamba chanzo cha machozi yake ilikuwa ni mimi kumsaliti. Nilinywea kimya kama kondoo anayesubiri kuchinjwa huku macho yangu yakiona aibu kumtazama mke wangu kipenzi. “Stanley mume wangu, hivi unafahamu ya kwamba mimi ninakupenda sana kuliko wanaume wote hapa duniani?”. Mke wangu aliniuliza swali ambalo lilinishtua kidogo. Kwa mwanaume wa kawaida swali hili lilikuwa ni swali la kawaida sana lakini kwangu mimi ambaye nimezoea uzinzi na kutoka nje ya ndoa yangu lilikuwa ni swali lenye maana kubwa sana. “Ndiyo nafahamu mke wangu kwani hilo liko wazi kabisa”. Nilijikakamua kujibu kwa upole huku nikiwa nimenywea kwani nilikuwa ninafahamu kuwa mambo yalikuwa yamekwisha haribika. “Sasa naomba unieleze kwa dhati toka moyoni mwako jana ulilala wapi?” Mke wangu Rose aliongea huku akiwa amenikazia macho. Mungu wangu! Mambo yalikuwa yamekwishaharibika. Tumbo langu lilianza kuunguruma tena sasa sifahamu lilikuwa ni tumbo la uharo au ilikuwa ni hofu. Halafu kwa mbali nilianza kuhisi kama kizunguzungu hivi. Pia nilianza kuihisi baridi wakati kulikuwa na joto kali sana la kutumia feni kabisa. Hakika nilikuwa katika kimuhemuhe. “Si nilikwambia kwamba ninalala kwa rafiki yangu Morris kwa sababu ya kuzuiwa na ile mvua kubwa ya jana usiku!” Nilijaribu kumjibu mke wangu huku sauti yangu ikiwa na uoga ndani yake. Unajua unapokuwa umekosa, ni lazima mtu unakosa ujasiri kabisa. Hata kama ni mwanaume wa shoka ni lazima utanywea tu ila utajitutumua tu lakini mh! “Sasa mbona nguo zako zina harufu ya manukato ya kike?” Mke wangu alinitandika swali ambalo lilinipa kiwewe kidogo na kunifanya nikose jibu kwa muda kidogo. “Unajua…. Unajua……. Unajua asubuhi nilipanda daladala …… ah! Hapana nilimpa lifti mwanamke ambaye alikuwa amejipulizia manukato hayo”. Mh! nilijigonga kwa kweli kwani mimi huwa sipandi daladala nina usafiri wangu binafsi na ndio gari niliyokuja nayo asubuhi. “Sawasawa mume wangu nakubaliana kabisa na wewe. Sasa je, na ile nguo ya ndani ya kike uliyokuwa umeivaa imetoka wapi?”. Mke wangu alinipachika swali jingine la moto. Duh! lilikuwa ni swali lililonipandisha presha yangu. Kizunguzungu kilizidi na sikuelewa nitajibu vipi ili nieleweke. ***************** Kuwa sambamba nami katika sehemu ya 04
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/39lQmAL
No comments:
Post a Comment