CHAGUO LA MOYO WANGU
SEHEMU YA 7
kingine,mzee samwel baada ya kuona machela inatoka katika chumba cha michael alitimua mbio kuifuata ile machela na kuwauliza madaktari nini kimetokea maana haelewi elewi, madaktari walimueleza kwa kifupi kilicho tokea,baada ya kupata taarifa ile mzee samwel alipata mshtuko wa ghafla na taratibu nguvu zilimuishia na kujikuta akikaa chini kutokana na miguu kushindwa kustahimili uzito wa kiwiliwili chake,hakika alichanganyikiwa,alitamani arudishe masaa nyuma ile arekebishe yaliyotokea lakini hilo nalo kamwe halikuwezeana,alijua nini maana ya mshtuko,alijua madaktari wasipo fanya jitahada basi atampoteza mwanae,alilia kwa uchungu sana na kujikuta akijutia maamuzi ambayo aliyachukua,alizidi kulia kwa uchungu na kumuomba mungu apiganie maisha ya mwanae pamoja na michael waweze kupona,na aliapa endapo watapona basi kitakacho fuata ni mipango ya harusi na atamuozesha michael binti yake,hakuna kingine alichowaza zaidi ya hicho endapo michael na judith watapona,alisha
kubaliana na kila hali na alipanga endapo mwanae na michael watafunga ndoa atawakabidhi miradi yake karibu yote na yeye atabakia na miradi michache ambayo aliona itamsogeza mbele kwani aliamini kabisa kwa maovu aliyoyafanya siku zake za kuishi duniani zilikua zimekaribia na alikua akimuomba mungu amsamehe kwa makosa ambayo aliyafanya toka alipozaliwa mpaka hapo alipo,alionesha wazi kweli alikua akijutia makosa aliyoyafanya kipindi chote cha maisha yake,alikua akilia kama mtoto mdogo,ungeweza kumtazama siku hiyo hakika ungemuonea huruma…..
Mzee samwel alikaa muda mrefu sana pale hospitali huku machozi yakimtiririka katika mashavu yake,alijutia sana maana maamuzi aliyoyachukua ambayo yamesababisha mapaka mwanae kipenzi judith kupata mshtuko,baada ya kukaa kwa muda mrefu huku akilia,ghafla aliacha kulia na kusimama kisha alitoa kitambaa katika moja ya mfuko uliyopo katika koti alilokua amevaa,alijifuta machozi na kisha kuwaza,mimi ni mwanaume yanipasa kusimama imara na kupigania uhai wa michael na mwanangu judith,kukaa kwangu hapa na kulia hakusaidii chochote japo kwa kiasi fulani kumenipunguzia maumvu ndani ya moyo wangu yanipasa kusimama kama mwanaume na kuhakikisha michael pamoja na judith wanapona mapema na haraka iwezekanavyo ili waweze kufunga ndoa yao ambapo na amini wataishi kwa furaha na amani, baada ya kuwaza hayo taratibu alinyanyuka sehemu ambayo alikua amekaa na kuelekea katika chumba cha daktari,alipofika aliamua kugonga mlango ambapo daktari alimruhusu aingia nae bila kupoteza mda aliingia,baada ya kuingia alirudishia mlango na kukarishwa na daktari aketi katika moja ya viti vilivyopo katika chumba kile na baada ya salamu daktari yule alimuomba mzee samwel aeleze shida yake ili kama kutakua na uwezekanao wa kumsaidia atamsaidia na kama hamna uwezekano basi watajua namna ya kufanya, baada ya daktari yule kumaliza alimtazama mzee kwa macho yalioshiria kua alikua anataka kujua shida yake na bila kupoteza muda mzee samwel alianza kujieleza na kujitambulisha kua yeye ni mzazi wa michael pamoja na judith na yupo hapo ili kutaka kujua wanae hao wawili wanaendeleaje,
daktari yule alikohoa kidogo kisha kumuangalia mzee samwel kwa umakini mkubwa na baada hapo alianza kwa kumpa pole kwa matatizo yaliyomkuta kwani matatizo ni moja ya changamoto tunazokumbana nazo katika maisha ya kila siku,baada ya maelezo hayo aliweka kituo na kisha kuendelea,mzee wanao wanaendelea vizuri hasa yule mwanao wa kike ambae nafikiri atakua judith,yeye ameshapata fahamu na inawezekana wakamruhusu mda wa jioni, kwa upande wa michael nae hali ni nzuri japo sio sana na hii ni kutokana na kupoteza damu nyingi hasa kutokana na majeraha aliyokua nayo na nafikiri baada ya wiki moja hali yake itakua sawa,.
ITAENDELEA…………………………….
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/35dlijo
No comments:
Post a Comment