Friday, December 27, 2019

SIMULIZI YA KWELI:NIPENDE TENA 01




SIMULIZI YA KWELI:NIPENDE TENA

SEHEMU YA 1.
Barabara ya 11, Tanga.
Hadrath alikuwa barabarani kwa mwendo wake wa madaha, huku sura na umbo lake akiwa amejisitiri kwa baibui na ushungi.Alitembea polepole kama kinyonga, “kwinyoo kwinyoo” nyonga alizinyonga na kufanya wapita njia, wenda kwa miguu na wendao kwa vyombo vya moto kumtumbulia macho. Haikuhitajika sura yake kuonekana kuthibitisha kuwa ni mrembo umbo tu lilisadifu uzuri ambao alikuwa nao. Mikono yake ambayo ilikuwa imechorwa kwa hina na urembo wa asili ilionekana na kuzidi kufanya watu kumshangaa. Wasio na imani au wenye imani haba walidiriki kusema labda huenda ni jini ambalo lilikuwa lipo mawindoni ili liweze kuwalaghai watu hasa wanaume wenye tamaa. Milindimo ya makalio yake yalitosha kabisa kuwachanganya watu. Ni kama vile mwanamke huyo alikuwa akifanya makusudi lakini la hasha ukweli ni kwamba alijaliwa umbo jembamba kwa juu lakini makalio na nyonga kubwa.Unaweza kusema alikuwa na umbo namba nane au nyigu mwenye kijungu mchongoko.
“Pipipiiiii” ilikuwa ni honi ya gari aina ya Nissani Morano ambalo ilisimama hatua chache mbele yake. Kioo cha gari hilo jeusi kilishushwa na sura ya mwanaume ambaye alikuwa ni mwarabu ilionekana.
“Samahani dada unaelekea wapi” lilikuwa swali la Mwarabu huyo ambaye aliongea Kiswahili vizuri.
“Mtaa wa pili”  Hadrath alijibu kwa madaha yake aliyojaliwa. Kope  na nyuzi zilizokuwa zimewekwa vikorombezo vya urembo alizichezeshachezesha na kumchanganya kabisa mwanaume huyo.
“Ok, naweza kukusindikiza?”
“Hapana, nimeshafika asante. Hadrath alijibu na kuanza kupiga hatua na kuondoka.
“Samahanai kama nimekukera lakini nilikuwa na ombi moja tu kutoka kwako.”*****ITAENDELEA***


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2F1rqjU

No comments:

Post a Comment