Sunday, December 29, 2019

Simulizi: SONONEKO (04)




ILIPOISHIA “Sawa sawa mume wangu nakubaliana kabisa na wewe. Sasa je, na ile nguo ya ndani ya kike uliyokuwa umeivaa imetoka wapi?”. Nke wangu alinipachika swali jingine la moto. Duh! lilikuwa ni swali lililonipandisha presha yangu. Kizunguzungu kilizidi na sikuelewa nitajibu vipi ili nieleweke. SASA ENDELEA Yaani penzi la Maggie jana lilinipagawisha hata asubuhi nilipokuwa nikivaa nguo kumbe badala ya kuvaa chupi yangu niikuparamia “mkwego” wa Maggie bila kutambua na kuutundika mwilini mwangu. Hata asubuhi kwa sababu ya kihoro nilichokuwa nacho sikuwa makini kujikagua mavazi yangu. Dah! Bonge la faulo. “Unajua mke wangu …….. unaju…… unajuua…..yah!.... you know ….. unajua nilikuwa nataka nikufanyie surprise. Niliinunua ile nguo ili nije nikukabidhi kwa mtindo wa pekee nikiwa nimeivaa. Ni surprise tu mke wangu”. Nilijigongagonga pale huku nikitoa maelezo ambayo yalikuwa hayaeleweki kabisa. “Ok, nimekuelewa mume wangu mpenzi, sasa mbona chupi yenyewe ilikuwa imetumika kabisa. Je, hapo utaniambia nini?”. Rose mke wangu aliniuliza kwa sauti yake ileile yenye upole uliotukuka. “Nili…. Nili….. nilitaka …….. nilikuwa…….!” Midomo yangu iligoma kabisa kupatana na kuunda uongo ambao ningeweza angalau kumfanya mke wangu aweze kuniamini hata kidogo tu. “Pole mume wangu najua unapata shida sana namna ya kunijibu swali hili lakini mimi ni mtu mzima naelewa kila kitu. Wewe ndio baba wa nyumba mimi sina lolote la kusema mume wangu”. Mke wangu aliongea maneno ambayo yalinichoma moyo na kunifanya mtu mzima niporomokwe na machozi. Baada ya maneno hayo mke wangu alisimama huku akilia kwa uchungu na kuelekea chumbani kwake. Alijitupa juu ya kitanda huku akilia sana. Nilimfahamu vyema Rose mke wangu. Anapokuwa katika hali ile haikupaswa kumsemesha chochote. Alitakiwa aachwe hivyohivyo alie weeeee! Ndipo hasira zake hupungua na huamua kusamehe yote. Lakini la safari hii lilikuwa kubwa sana la kurudi na “mkwego” wa kike nyumbani dah! Stanley mimi nilikuwa hatari sana. Nilisimama kutoka pale sofani na kutoka nje. Nililifuata gari langu la kifahari aina ya “Toyota surf” na kuliwasha. Kwa mwendo wa kasi nilipotea kutoka maeneo yale ya nyumbani kwangu. Kwa upande wa wakati ilikuwa ni majira ya saa moja na dakika kumi na mbili jioni. Niliikamata barabara kuu ya Tunguhza ambayo ilinichukua mpaka katika mtaa wa Mateku. Katika mtaa huu palikuwa na baa moja maarufu sana ambayo mimi huipenda sana. Baa hii ilikuwa ikiitwa “Highway Bar”. “Mariam mambo vipi?” Hebu nipatie “Le grande Cologne” tano hapo mezani fasta fasta”. Nilimwambia muhudumu yule wa baa ile ambaye nilikuwa nimezoeana naye kwani hapo awali nilikwishafanya naye ngono mara kadhaa na hata ninapokuwa na hamu ya mwanamke mara nyingi huwa nazini na huyu dada mrembo wa hapa baa. “He! Bosi Stanley kulikoni tena mbona hivi. Hujanywa siku saba nini?” Aliuliza Mariam kwa mshangao na kwa utani kwani “Le grande Cologne” ni pombe ya kifaransa ambayo ilikuwa ni kali sana na yenye kilevi asilimia tisa. “Acha longolongo zako wewe, lete pombe hapa au wataka nikupe mambo nini?” Nami nilimchombeza kwa maneno ya bashasha kwani Mariam alikuwa ni mtani wangu. “He he he he he! Unalo babuuuuuu! Hapa leo hupati kitu”. Aliongea Mariam kwa mbwembwe huku akiniletea vinywaji nilivyoviagiza katika ile meza niliyomwelekeza. “Haya kaa hapo mwanamke kula pombe toka kwa mpenzi wako wa nguvu Stanley”. Nilimwambia Mariam ambaye alikuwa tayari amekaa hata kabla ya kukaribishwa kwani alikuwa akiufahamu utaratibu mzima. “Eenh! Nipe maneno darling, mbona leo uko tofauti kabisa kulikoni”. Alihoji Mariam baada ya kunigundua kwamba siku ile nilikuwa tofauti kabisa toka muda ule nilipokuwa nimeingia pale baa. “Dah! Eeh bwana mwenzio leo nimelikoroga kweli na natamani hata dunia ipasuke na mimi nijitumbukize ndani yake ili nijifiche”. Nilianza kumweleza Mariam ambaye licha ya kuwa ni mpenzi wangu lakini pia alikuwa ni rafiki yangu mkubwa sana. “Imekuwaje tena? Mbona wanitisha mwana wa mwenzio?” Alihoji Mariam huku akiionesha dhahiri hofu ambayo alikuwa nayo. “Tulia mwanamke nikupe mkanda mzima. Basi si nilipata mwanamke mmoja kwa ajili ya kupooza hamu……” Mara Mariam alinikatisha. “Hebu ishia hapo hapo, wewe si nilikwishakukataza habari za kuzoazoa wanawake. Hivi unafikiri kwamba mimi siumii kwa matendo yako hayo ya kuchukua wanawake hovyo. Mi nakupenda sana na nahitaji uwe na mimi pekee. Naumia unapotoka na wanawake wengine”. Aliongea Mariam akioonesha dhahiri alimaanisha kile alichokioongea. “Sawa lakini mimi si nilikwishakwambia toka awali kwamba siku nikiwa na hamu ya haya mambo na wewe ukiwa mbali ni lazima nitachukua mwanamke mwingine. Halafu pia wewe si unafahamu ya kwamba mimi nimeoa. Sasa je, kwani mke wangu naye haumii mimi ninapotoka na wewe?”. Niliongea maneno ambayo yalimchoma sana Mariam. “Haya bwana we endelea tu kuniumiza. Hivyo si ndivyo ambavyo unapenda. Haya hebu endelea kunisimulia huo upuuzi wako”. Mariam aliongea hukua akionesha wazi alikuwa amekereka kwa mimi kutembea na mwanamke mwingine zaidi ya mke wangu. “Ndiyo hivyo bwana. Baada ya mambo yetu haya si nikarudi asubuhi nyumbani. Sikujikagua kumbe nilikuwa nimevaa nguo ya ndani ya yule binti niliyekuwa naye. Moto uliowaka huko nyumbani nashindwa hata namna ya kuuzima”. Nilimwambia Mariam huku nikiwa naendelea kuzibugia zile pombe mithili ya buge. “Pole bwana lakini mambo haya unajitakia mwenyewe. Mtindo wako wa kuzoazoa wanawake ndio ambao unakusababishia matatizo hayo”. Mariam aliongea maneno ambayo yalikuwa na mantiki ndani yake lakini alisahau kuwa hata yeye pia alikuwa ni miongoni mwa hao wanawake ambao nilikuwa nikiwazoazoa. Tuliendelea kula pombe mpaka zikatufahamu kuwa sisi ni akina nani. Mariam naye katika kubugia pombe alikuwa ni mtaalamu sana. Na hilo ndilo ambalo nilimpendea kwani mara nyingi alikuwa akinipa kampani ya kutosha si unajua utamu wa pombe ni sharti muwe wengi. Kuna kipindi fulani Mariam alilazimika kusimama na kuniacha pale mezani peke yangu kwani alikwenda kuhudumia wateja wengine. Alipowahudumia alirudi na kuendelea kujumuika nami katika kuzitandika pombe. Siku ile nilizinywa pombe kupita kiasi. Utashi na akili zangu vilihama kabisa na nikawa sijitambui. Mariam kidogo ndo alikuwa msaada kwani yeye hakulewa sana kama mimi kwa sababu yeye alikuwa ni muhudumu na alitakiwa aendelee kuwa na ufahamu kwa lengo la kuifanya kazi yake vyema bila ya dosari. ******************* Yalikuwa ni majira ya asubuhi ya saa nne ndipo ambapo nilizinduka kutoka katika usingizi mzito sana. Kichwa kilikuwa kikinigonga sana kutoka na pombe ambazo nilikuwa nimezipiga usiku wa kuamkia leo. Mwanga mkali wa jua ulikuwa ukiingia kupitia madirisha makubwa ya chumba cha kulala ambacho kwa wakati ule kilikuwa kimefunguliwa mapazia na kuingiza hewa safi pamoja na nuru ya kutosha sana ambayo ilileta burudani safi. Mke wangu alikuwa anapenda kuyatunza mazingira ya nyumba yetu kikiwemo chumba chetu cha kulala katika hali ya usafi na unadhifu mkubwa sana. Nyumba yetu muda wote ilikuwa inapendeza na kuvutia sana. Sikuelewa nilifikaje mle chumbani kwani kumbukumbu zangu zilinikumbusha kwamba kwa kudra za mwenyezi Mungu nilifanikiwa kuliendesha gari kutoka baa na kufika salama nyumbani ingawa humo njiani nilinusurika kuwagonga watu wasio na idadi. Pia nilikwishanusurika kama mara tano kugongana na magari mengine na pia niliponea chupuchupu kuzivaa nguzo za taa za barabarani. Nilipofika katika geti la kuingilia nyumbani kwangu nikaona nisiwasumbue waliokuwa wamelala ndani kwa kupiga honi bali nishuke na kulifungua mimi mwenyewe kwani funguo za geti hata mimi nilikuwa nazo. Niliposhuka chini kutoka garini, nilikula mweleka mmoja matata ulionifanya nidondoke chini na kutapika kiasi fulani cha pombe ambayo nilikuwa nimeibugia. Baada ya hapo nilipoteza fahamu. Nilijitazama mwilini. Nilishangaa baada ya kujikuta nipo katika mavazi ya kulalia huku mwili wangu ukionekana nadhifu ikimaanisha nilikuwa nimeoga. Mh! Haya yalikuwa makubwa tena. Niligeuza kichwa changu na kutazama upande wa pili wa chumba ambapo nilimwona mke wangu akiwa amejikunyata huku akiwa ameukumbatia mdoli mmoja mkubwa ambao nilimnunulia zamani sana kama zawadi katika kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Machozi yalikuwa yakimporomoka huku akilia taratibu kwa kwikwi ndogondogo. “Pole sana mume wangu, wajisikiaje sasa?”. Mke wangu aliniuliza swali ambalo lilitia aibu na kunifanya nimshangae sana mwanamke huyu. Hivi alikuwa ni mwanamke wa namna gani huyu?. Licha ya madhambi, mateso na kila aina ya ubaya niliomfanyia lakini bado alikuwa na huruma nami Stanley mwanaume mwenye roho mbaya iumizayo wanawake. Kwa kweli niliumia sana moyoni kwa mapenzi ya dhati ambayo mke wangu alikuwa nayo juu yangu lakini mimi nikiwa na akili zangu timamu kabisa nilikuwa nikijitahidi kuyabomoa. Kweli wanawake wameumbwa tofauti kabisa na ni watu wavumilivu sana na wenye mapendo ya dhati kwa wenza wao. Niliona hata aibu kumjibu mke wangu maana nafsi yangu ilikuwa ikinisuta ndani yangu. Ni kweli nafsi ilinisuta hasa. Bila kutarajia nilijiona nikiporomokwa na machozi ya uchungu kutoka moyoni mwangu. Nilijilaani kwa nini nilikuwa nikimwumiza mwanamke huyu wa pekee ambaye alikuwa na mapenzi ya dhati juu yangu. Je, hivi yeye aliumbwa kuipata tabu hii ambayo alikuwa akiipata. Hivi hakustahili kuipata furaha katika maisha yake. Je, ni nani wa kuisababisha furaha katika maisha yake? Hakika nilikuwa ni mimi. Mwanaume ambaye nilikuwa sijui kupenda ninapopendwa wala kumjali mtu anayenipenda na kunijali. *************** Kutana nami katika sehemu ya 05 ya simulizi hii.

  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2ZwUmcY

No comments:

Post a Comment