Tuesday, December 3, 2019

Sehemu Ya Tano 5B






Ni siku ya Jumanne asubuhi na mapema isack alikwisha amka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda kazini.Kichwa chake kilikuwa na mawazo mengi sana kutokana na mage kukasirika jana yake wakati wakijibizana kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi.Kichwa kilimuuma sana ni namna gani anageweza kumpooza mage ambaye hakutaka hata kupokea simu yake.Alifikiria jinsi ya kuendelea kuudumisha urafiki wao ulioanza kukua kwa kasi.Wakati akiwaza huku akijiandaa kwenda kazini mara mlango wake ukagongwa.Ilikuwa ni asubuhi sana na hakujua ni nani ambaye alikuwa akimgongea mlango.Akaufungua mlango na kukutana na sura yenye tabasamu ya mage.isack akajikuta akitabasamu 

” Ouh mage….habari yako” akasema isack 

” Umeamkaje isack” akasema mage ambaye mkononi alikuwa ameshika mfuko 

” Nimeamka salama” akasema isack huku akitabasamu 

” isack huu mzigo wako.Ni shea yako niliyokuwa nimekuandalia jana.Kula kabla hujakwenda kazini” akasema mage huku akitabasamu na kumfanya isack acheke kidogo huku akiupokea mfuko ule halafu mage akaondoka zake.Ndani ya mfuko ule kulikuwa na chakula kilichopikwa usiku na isack akagoma kwenda kula.isack akatabasamu na kukiweka chakula kile jikoni. 

kisha akaondoka na kuwahi kazini kwake. 

Siku hii alishinda mwenye furaha kuzidi siku iliyotangulia.Kitendo cha mage kumletea chakula asubuhi kilimdhihirishia kwamba hakuwa amekasirika tena.Wakati wa mapumziko ya mchana isack akamuandikia mage ujumbe mfupi 

wa maandishi 

” mage nashukuru kwa chakula ambacho kimenipa nguvu na sihitaji kula tena mchana.Samahani kwa kutokuja kula jana ila naomba uniruhusu niilipe siku ya jana kwa kukualika kwa chakula cha usiku siku ya jumammosi kama utakuwa na nafasi” isack akautuma ujumbe ule na baada ya muda mfupi ujumbe toka kwa mage ukarejea. 

” Nashukuru isack lakini sintakuwepo kwa siku kadhaa.Nimepata safari ya kikazi nitarudi jumamosi.Kama hutajali naomba tufanye jumapili” 

Isack akatabasamu halafu akaandika ujumbe wa majibu 

” Nashukuru kwa kukubali mwaliko wangu.hakuna shaka tutapata chakula cha usiku siku hiyo ya jumapili.Safari njema ” akautuma ujumbe ule na baada ya dakika moja ukarejea ujumbe toka kwa mage ukisomeka 

” Ahsante” 

Isack akatabasamu na kujawa na furaha kubwa moyoni. 

************************************************** 


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2qguF3n

No comments:

Post a Comment