Tuesday, December 3, 2019

Safari Ya Mapenzi - YA 03



Safari yangu ya mapezi, Ilipoishia sehemu iliopita. “Kijana nini kimetokea? Mbona mwenzio amekuja ameniletea malalamiko kwamba umekuwa ukimpiga? Balozi mzee mwapa akamuuliza mumewe mage ambaye akamtazama na kisha kwa dharau akauliza, “wewe unaongea kama nani? Mambo yangu mimi na mke wangu yanakuhusu nini? 

SONGA NAYO SASA….. 
Mzee Mwapa akaangaliana na wale wazee wenzake kisha akamgeukia na kusema “Sikiliza kijana. Mimi ni balozi wa mtaa huu, Ninamfahamu mage toka alipohamia hapa mtaani. Ni mwanamke anayejiheshimu sana na sikutegema kama siku moja ungeweza kumfanyia kitendo kama hiki cha kumpiga. Nimekuja hapa kusikiliza sababu iliyopelekea wewe kumpiga mkeo na kumuumiza mkono namna hii kabla sijamruhusu aende mbele zaidi kwa hatua stahiki dhidi yako.” 

“Balozi mimi nakushangaa sana mtu mzima kama wewe kuanza kuingilia ugomvi wa vijana. Naomba jamani muondoke humu ndani na mniache mimi na mke wangu tuyamalize mambo yetu sisi wenyewe. Naomba mkaendelee na kazi zenu” Akasema mume wa mage 

“Kijana naomba uwe na adabu kwa wazee wako, Usiongee kama vile unaongea na wahuni wenzako huko mitaani. Nina uwezo wa kukuchukulia hatua sasa hivi” akafoka mzee Mwapa 

“Unichukulie hatua kwa kosa lipi wewe mzee? Ugomvi haukuhusu wewe unaingilia Mimi nimekwaruzana na mke wangu wewe yanakuhusu nini?…” Akasema kwa ukali . 

“Kijana nakuomba uwe na adabu tafadhali. Msikilize balozi wako anataka kusema nini” akasema mzee mmoja kati ya wale wawili waliokuwa wameongozana na balozi Mwapa 

“Balozi mimi sitaki malumbano zaidi na huyu mtu, Ninachokisema ni kwamba nimechoka naye na simuhitaji tena hapa kwangu. Ninachotaka yeye achukue begi lake na aondoke zake sitaki tena kumuona hapa ndani kwangu.” Mage akasema kwa ukali akiwa amesimama nyuma ya balozi. 

” Kijana umesikia mwenzako anavyosema ? Amekuchoka na hataki tena kukuona ndani kwake.” Akasema balozi Mwapa. “Hapa si kwake, Hapa ni kwangu mimi na hana nguvu yoyote ya kunitoa humu. Kama ni kuondoka aondoke yeye” akasema mumewe. 

Mzee mwapa akamwangalia kwa makini na kusema “Kwanza mimi sikufahamu kabisa katika orodha ya watu wangu wa mtaa huu. Ninayemfahamu ni mage pekee, Wewe si mtu wa mtaa huu. Nakuomba kijana usiendelee kufanya fujo hapa, Nitaita askari sasa hivi waje wakuchukue na kukuweka ndani.” akasema balozi Msuya. 

‘Niwekwe ndani kwa kosa lipi? Kugombana na mke wangu nikawekwe ndani? akauliza kwa ukali 
“Huyu kijana anaonekana hanifahamu vizuri” Mzee Mwapa akasema na kuchukua simu yake akazitafuta namba fulani na kupiga. 

“Halo Afande Sadiki, Habari yako ndugu yangu” akasema mzee Mwapa  “Afande ninaomba msaada wako wa haraka. Kuna kijana mmoja amevamia chumba cha msichana mmoja hapa mtaani kwangu na analeta fujo, amempiga na hataki kutoka .Naomba unitumie vijana wawili ili waweze kutusaidia kumtoa kijana huyu” akasema mzee Mwapa akatulia kusikiliza upande wa pili wa simu na kisha akasema 

“Nashukuru sana afande, Waelekeze wafike pale nyumbani kwangu ” akamaliza kuongea na simu na kuikata kisha akamgeukia mume wa mage 
” Nilikuwa naongea na mkuu wa kituo, Anawatuma askari wawili sasa hivi ili wakuchukue wakakuweke ndani ” akasema mzee mwapa 

“Lakini huu ni uonevu jamani, Kwa nini lakini mnafanya namna hii? Kwa nini mnavunja ndoa yangu? akalalamika mume wa mage. mage alionyesha kukerwa na kauli ile ya mumewe 

“Ndoa ! Umemuoa nani hapa? Nimesema chukua begi lako na uondoke sitaki kukuona tena ndani kwangu.” Akasema mage huku akilichukua begi dogo la kijani na kuanza kupakia nguo za mumewe ambaye alikuwa amekaa kitandani akiwa amevaa nguo ya ndani pekee akainuka na kuvaa suruali yake na shati halafu akavaa viatu vyake vya kuchomeka. 

“Begi lako hili hapa, Naomba uondoke na sitaki tena kukuona hapa kwangu” mage akasema akiliweka begi mezani 

“Kweli mage unadiriki kunifukuza? akamuuliza mage huku akimuangalia kwa jicho kali. “Jaribu kuwa mwelewa, Mwenzako amekwisha kuambia kwamba ondoka nyumbani kwake na ndiyo sababu ya kuita uongozi wa mtaa kama mashahidi.

Unapoendela kumghasi ghasi kwa maswali unafikiri atabadili mawazo yake? Chukua mizgo yako na uondoke. 

Je James atakubali kuondoka na kwanini anaweka  ngumu kuondoka ?



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/33DuNHO

No comments:

Post a Comment