Tuesday, December 3, 2019

Safari Ya Mapenzi - Ya 02 ILIPOISHIA. “





Isack nisaidie ananiumizaa!!!!!  mage akalia huku akijitahidi kujitoa katika mikono ya mumewe 


SONGA NAYO SASA 

Nikamuonea huruma mage alivyokuwa akilia nikashikwa na hasira “nakuomba tafadhali usiendelee kumpiga mkeo. Nakuomba ndugu yangu niko chini ya miguu yako muache mkeo. Unamuumiza ” nikasema taratibu ukunikimusii amuachie mkewe. “Isack naona hujanifahamu vizuri mimi ni nani. Nimekwambia ugomvi wangu mimi na mke wangu unakuhusu kitu gani? Tafadhali ondoka humu ndani mwangu haraka.” akafoka. “Mshenzi wewe humu ni kwako? Una kitu chochote unachoweza kusema ni chako humu ? ” mage akamwambia mumewe kwa ukali. Kwa hasira akamnasa kibao kizito. 

“Malaya mkubwa wewe nimekwisha kuonya siku nyingi juu ya matusi yako unayonitukana. Umepata kiburi baada ya mwanaume wako kuja kukusaidia? Ngoja sasa niwaonyeshe adabu wewe na malaya mwenzako” mume wa mage akasema kwa ukali. Kauli ile na kitendo cha kumnasa mage kibao kilinikasirisha sana Kwa nguvu nikamvaa mume wa mage na kumsukuma akaangukia kitandani mage akaitumia nafasi hiyo kuchukua kitenge na kujifunga kisha akatoka nje huku akilia. 

“Inuka sasa upigane na mimi wewe si kidume? Nakwambia inuka upigane na mwanaume mwenzako”nikssema kwa hasira uku nikiwa nimefula kwa hasira. “Isack nimekwambia toka ndani mwangu haraka sana. Nitakuitia mwizi sasa hivi!!! akasema mume wa mage kwa ukali akiwa amekaa kitandani “Nimekwambia inuka unipige mimi badala ya mkeo….”nikasema kwa kujiamini  “Isack nimekwambia toka ndani mwangu. Unaingilia mambo yasiyokuhusu kwa nini? Ugomvi kati yangu mimi na mke wangu unakuhusu nini? Halafu huna hata adabu unaingia ndani mwangu bila hodi na kutukuta tukiwa watupu” akafoka mume wa mage “Hata kama ni mkeo,hupaswi kumpiga kama mnyama. 

Nimekufahamu muda mrefu sana lakini sikutegemea kama unaweza ukafanya kitendo cha aibu kama hiki cha kumpiga mkeo bila huruma. Umenishangaza sana, Kwa taarifa yako ni kwamba siku hizi wanawake hawapigwi kama unavyofanya. Wanawake wameamka na wanadai haki zao. Akikupeleka katika vyombo vinavyohusika na haki za wanawake unaweza ukachukuliwa hatua kali sana.” Nikasema na kuanza kuipunguza jazba niliyo kuwa nayo. 

“Isack wewe huna mke na huelewi matatizo tunayokumbana nayo sisi watu tunaoishi na wanawake ndani. Siku ukioa ndiyo utafahamu haya ninayokwambia. Huyu mage unayemtetea amebadilika sana siku hizi. Amekuwa na kiburi cha ajabu, Sijui ni kwa nini amebadlika namna hii. Ninahisi kuna mwanume amempata ambaye anampa kiburi mage hakuwa hivi, mage hakuwa mtu anayesimama na kujibizana na mimi” 

“hata kama amekukosea hukupaswa kumpiga, kama mwanaume ulitakiwa uwe na busara ukae chini na mkeo na muongee kama mke na mume na kisha muyamalize matatizo yenu na maisha yaendelee. Ninamfahamu mage vizuri na sidhani kama ana tabia kama hizo unazohisi anazo. Mbona mkeo ni mtu anayejiheshimu sana tofauti na wanawake wengine hapa mtaani. Jaribu kukaa na mkeo muongee na muyarekebishe yale yote yaliyotokea. Mnapopigana mnajiabisha ninyi wenyewe, Mnawafaidisha majirani ambao wanabaki wanawacheka kila mpitapo. Tafadhali ndugu yangu nakuomba kama mwanaume mwenzangu kaa na mkeo na mjaribu kutafuta suluhu ya matatizo yenu.”nikasema na mara mlango ukafunguliwa mage akaingia akiwa ameongozana na balozi wa mtaa mzee Mwapa pamoja na wazee wengine wawili. 

“Kijana nini kimetokea? Mbona mwenzio amekuja ameniletea malalamiko kwamba umekuwa ukimpiga ? Balozi mzee mwapa akamuuliza mumewe mage ambaye akamtazama na kisha kwa dharau akauliza

“wewe unaongea kama nani? Mambo yangu mimi na mke wangu yanakuhusu nini? Mzee Mwapa akaangaliana na wale wazee wenzake kisha akamgeukia na kusema “Sikiliza kijana, Mimi ni balozi wa mtaa huu, Ninamfahamu mage toka alipohamia hapa mtaani. Ni mwanamke anayejiheshimu sana na sikutegema kama siku moja ungeweza kumfanyia kitendo kama hiki cha kumpiga. Nimekuja hapa kusikiliza sababu iliyopelekea wewe kumpiga mkeo na kumuumiza mkono namna hii kabla sijamruhusu aende mbele zaidi kwa hatua stahiki dhidi yako.” 

“Balozi mimi nakushangaa sana mtu mzima kama wewe kuanza kuingilia ugomvi wa mke na mume…….. 

Je Mwapa atafanya nini? Tukutane KATIKA mwendelezo


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2P6o0RO

No comments:

Post a Comment