Sunday, February 2, 2020
PETE YA KIKE Sehemu Ya 22
"ati nini"
"mdogo wako.. Tunamuona hapa"
"wapi"
"hapa Tanga Bites"
Lakini wakati huo huo wakiongea, muna Aliweza kusikia kila neno kwani yeye anatumia hisia za asili ya pili ambayo ni jini,....
"ok nisubiri hapo hapo nakuja"
"chukua toyo jamani asha"
Wakati huo asha anatamani amtafute mama yake hapo kazini ili ampe habari hizi, lakini mbaya zaidi hajui mama anafanyia kazi upande gani hapo ndani,... Hivyo asha aliamua kuondoka lakini kazini keshasajiliwa tayari,...
Punde sii punde TANGA SPECIAL BITES asha anafika, kwa haraka haraka akawaona rafiki zake ambao ni fatuma, na amina...
"we Fatuma, haya yuko wapi surian mdogo wangu"
Aliongea asha huku akiwa na shauku ya kumuona ndugu yake, ingawaje mwanzoni alikuwa akimchukia kwakua kapendelewa elimu.. Wakati huo surian na mke wake wanakula vyuku kwa kwenda mbele na ila surian hajui kama kaonwa na rafiki zake asha...
"mdogo wako yule pale"
ENDELEA..........
Asha anatamani sana amuone mdogo wake ambaye anashutumiwa kumuua kisa ni pesa,... Sasa ili jambo hilo liwe safi katika maisha yake ni lazima surian aonekane,... Amina na Fatuma ni marafiki wa asha ambao walikuwa karibu naye toka kufungua kwa saluni yake,... Lakini walikuja kumwonea wivu baada ya asha kuanza kukusanya pesa nyingi, lakini wakati akikusanya pesa nyingi kutokana na wateja,... Mdogo wake alipotea katika mazingira ya kutatanisha,.. Hii leo rafiki zake wanamwita asha aje kumwona mdogo wake....
"mdogo wako yule pale"
Aliongea fatuma huku akinyoosha kidole, lakini ghafla hawakuwa wakiona mtu, hata wao wenyewe walijikuta hawaoni mtu,...
"yuko wapi"
Aliuliza asha huku akiangaza macho katika eneo husika
"walikuwa pale na mwanamke mmoja mzuri sana"
"sasa wako wapi"
"walikua pale karibu na meza ile pale"
Asha aliona rafiki hao walikuwa wakimzingua na kuendelea kumtania au kumchokoza kutokana na kashfa alio nayo,...
Lakini surian na maimuna, walikuwa pale pale wakiendelea kula kuku maeneo hayo, ila maimuna kamshika surian sikio na ndio sababu hawaonekani, na surian anajua kashikwa kikawaida tu kumbe hapo alipo haonekani,.... Asha aliondoka zake kwa hasira, mana rafiki zake ndio wenye kumchezea akili,... Hata akina Fatuma na Amina waliona ni kama maajabu, kwani sekunde chache waliwaona pale, sasa iweje wasiwaone kwa mara nyingine,... Waliona kweli surian kauwawa kwani ni lazima ule utakuwa ni mzimu wake
"amina, hii sio bure... Kweli surian sio binadamu"
Aliongea fatuma huku wakiwa wanarudi majumbani mwao,
"ni kweli, mana dakika ile ile walikwenda wapi"
"na kwanini alivyokuja asha tu,.. Wakatoweka, ni kweli asha kamuua ndugu yake"
Walizidi kuongea mengi sana, lakini hawajui lolote
Baada ya wiki kadhaa kupita, siku zilizidi kwenda na kiwanda kilizidi kuzalisha bidhaa na kuzisambaza mikoani, na ubora wa bidhaa hizo kutoka MICCO, ilifanya hata wafanyabiashara wa nguo aina hizo wasiagize kutoka dubai au maskati, ama oman,.. Hivyo wamiliki wa maduka ya nguo za Kiislamu walihamia katika kiwanda cha nyumbani,... Kiwanda kulipwa kipaumbele kwani kiliajiri Watanzania 500 na wote wanalipwa kwa mishahara mikubwa kutokana na viwango vya elimu zao,....
Asha akiwa ndani ya kiwanda na ni wiki kadhaa zimepita toka kuanza kazi hivyo sio mgeni tena katika kiwanda hicho,... Mpaka sasa ni miezi miwili toka Kuanzishwa kwa kiwanda hicho lakini boss mkuu hajulikani sura wala sauti, kwani alipewa masharti ya kuto onekana na wafanyakazi, lakini licha ya siku hizo kuisha surian kawa mzoefu wa kuto onekana na wafanyakazi, na hata hakumbuki umuhimu wa kwenda kuiona familia yake,....
Wakiwa ndani ya idara yake na rafiki zake ambao aliwakuta kabla yake,...
"nyie fanyeni kazi boss huyo"
Aliongea asha huku wakiwa wameshika vitambaa wakiwa tayari kwa kuviweka mapambo kwa niaba ya kutengeneza kanzu,...
"nani boss?"
Aliuliza rafiki yake mmoja huku asha akijibu
"si huyo hapo anakuja"
"heeeeee nani kakwambia huyo ni boss?.. Huyo ni Meneja anaitwa sadiki"
Siku zote za asha alizokaa hapo alijua sadiki ndio mkurugenzi mkuu wa kampuni hio, kumbe huyo ni Meneja,....
"sasa boss wa hii kampuni, ni nani"
Aliuliza asha huku akitamani sana kumjua boss, mana anakumbuka mama yake alisema boss wao ni mdogo mdogo, sasa asha akadhani labda ni sadiki, kumbe boss ni mtu wa familia yao lakini hawajui na hata boss hajui kama familia yake ipo humu,
"mmmhhh mwenzetu, hata sisi hatumjui, ni mwezi wa pili huu tunalipwa lakini boss hatumjui"
Sasa sadiki alifika katika eneo husika ambalo asha yupo,...
"asha?, nakuhitaji ofisini mara moja"
Aliongea sadiki huku akiendelea kuzungukia baadhi ya idara kama zinazalisha vyema, au wanapiga stori tu....
"afu mbona meneja anapenda sana kumuita asha, au ndio wameanza nini mahusiano"
Aliongea msichana mmoja baada ya kumwona asha anaitwa itwa kila siku na Meneja
"kwani hukumbuki ndio aliokuja kumfundisha mwenyewe"
"mmmhhh, haya watu na bahati zao"
Aliongea dada mmoja, na wakati huo asha anaelekea ofisini,... Kaitwa na Meneja,... Mama akiwa anafanya usafi alimwona mtoto wake akielekea ofisini,.. Mama huyo haruhusiwi kujionyesha kwani kawekwa kwa kificho, ili apate riziki
"asha,.. Mbona upo kimya toka juzi Nasubiri meseji yako... Nimekununulia simu ili tuwasiliane"
Aliongea sadiki huku asha akijing'ata vidole, kana kwamba watu hawa wana mpango wa kuwa na mahusiano...
"lakini boss, mimi nitakujibu... Alafu sasa boss akijua una mahusiano na mfanyakazi, itakuwaje"
"boss nani tena... Mimi ndio mwenye kauli ya juu, na sitaki kujulikana mimi ndio boss mkuu kwasababu watu sio wazuri hapa mkoani tanga... Najiita meneja ili nionekane wa kawaida tu"
Aliongea sadiki kama vile kujipa nafasi ya uboss mana anampenda sana asha, lakini sasa asha yeye anatamani uzuri wake autumie kwa boss mkuu, hio ndio nia yake, mana maisha yalisha watupa mkono, na kama tunavyomjua asha mwanzoni alikuwa ni msichana wa kudanga danga sana hivyo hata kuja hapa kwenye hii kampuni shida yake apate mwanaume wa kumchuna,.... Sasa aliposikia kuwa boss wa kampuni hii ni kijana mdogo akajua uzuri alio nao ataweza kumteka awe naye ili maisha yaendelee,.. Sasa alipokutana na sadiki akajua huyo ndio boss mwenyewe, kumbe sadiki ni Meneja na boss ni kaka yake kabisa baba mmoja mama mmoja, ila hajui kama kaka yake ndio mmiliki wa hapa...
"mbona nilisikia kuna boss mwingine"
"ndio, ni ili mimi nisijulikane"
"ok, lakini daki.. Mi naomba vuta subra kidogo nitakujibu tu"
"asha, mtoto mzuri kama wewe, yanini nikukose... Nataka mke, ona nina maisha mazuri lakini sina mke"
"ni sawa diki, lakini nipe nafasi ya kufikiri, tatizo ninyi wanaume hamuaminiki"
"sio wote asha,... Please naomba kesho unipe furaha ya moyo wangu, kama ni mshahara mimi nitaupandisha mara dufu"
Aliongea sadiki na kujigamba sana kuhusu nafasi yake....
"kweli diki"
"ndio, kwani we watakaje... Sema lolote nifanye"
"usijali, ila kikubwa nataka mama yangu ahamishwe kitengo kutoka kusafisha vyoo kuja kiwandani au hata awe mpishi sio mbaya"
Aliongea asha akiwa na nia ya kumsaidia mama yake asiende na kazi ya usafi wa vyoo kwa haipendi
"kumbe yule ni mama yako"
"ndio"
"ok ni hilo tu?... Au una Lingine"
"ni hilo tu, na mshahara wangu sio mbaya kama utapanda kidogo"
"usijali"
"mimi shida yangu ni kukumiliki wewe na uwe mke wangu, wala sitaki kukuchezea asha"
Asha ni msichana mzuri sana sema aliutumia uzuri wake vibaya, na mpaka sasa bado ni kisu, na ndio maana meneja kanasa mwenyewe
Wakati huo huo suria akiwa ofisini kwake, oda zilikuwa zikiingia nyingi kwa njia ya simu ya secretary, kisha secretary anamtumia boss wake kule ndani na boss anamtumia meneja masoko ili afanye kazi na watu hao, asha anatoka ofisini kwa sadiki, akiwa haamini kama anapendwa na boss, na hapo anapopita ndipo mlango wa boss mkuu ulipo, na ni ndugu yake kabisaaaa, ila hajui
Ilipofika jioni mida ya saa 12 na nusu, suria akiwa ndio wa mwisho kabisa kutoka,... Na ni ili asionekane na watu, sasa haijulikani ni kwanini mana siku za masharti ya jini maimuna zilisha isha, lakini suria bado haihitaji kuonwa na watu kana kwamba kesha zoea kujificha ficha...
Sasa huku nyumbani kwa akina asha, akiwa na mama yake jikoni wanapika, kwa sasa maisha yao sio mabaya mana mama keshapokea mshahara wake wa kwanza wa laki nne, sasa hawana ziki za hapa na pale... Wakati huo baba yao akiwa msikitini wao wapo jikoni wanaongea, kama unavyojua mama na mtoto wa kike walivyo...
"wewe asha,.. Mchana ule niliogopa kukuona na Meneja unakwenda ofisini, nikajua unafukuzwa kazi"
Aliongea mama yake asha huku asha akitabasamu tu,...
"mama, ina maana kila nikienda ofisini nakwenda kufukuzwa"
"ndio, mana juzi tu kuna wasichana wawili walifukuzwa kwa kuvaa nguo fupi, nikajua na wewe pia"
"hapana mama... Afu mama yule sio meneja ni boss mwenyewe"
"weeeeeeeeee, usikute kakupenda ndio mana kakudanganya... Yule ni meneja pwiiiii, hata siku nakwenda kuomba kazi, nilimuona kwenye foleni na vyeti vyake"
"haaaaaaaaa mama unasema kweli"
"ndio, yule ni Meneja.... Kwani kuna nini"
"basi mi nikajua ni boss"
"we asha, hebu niambie ukweli mwanangu, nini kinaendelea wewe na Meneja sadiki"
"mmmhhh mama bwana tuyaache hayo"
"najuaaaa,... Najua keshakupenda yule"
"ni kweli mama, ila mi namtaka boss mwenyewe..."
"asha mwanangu, umefuta kazi fanya kazi.... Ina mana unataka kurudia ujinga wako wa zamani"
"mama... Ina maana mimi nikiwa na mahusiano na boss mkuu ni vibaya"
Aliongea asha huku mama akiangalia chini kama anawaza na kumjibu kuwa
"sio vibaya mwanangu, lakini kumpata boss mkuu sio mchezo mchezo, ni sawa na kwenda kumuona raisi uso kwa uso"
"sasa nifanyeje mama.... Ina mana uzuri wangu ipotee bure tuuu"
"asha... Kama sadiki ana nia nzuri, mlete atujue wazazi wako... Achana na huyo boss mkubwa mwanangu, na pia boss mkubwa naskia ana mke"
"mke?? We ai umesema ni mdogo"
"ndio, ila ana mke"
"ila mama kwani si muislamu, nitakubali niwe hata mke wa pili... Nataka tukiwa kwenye mahusiano, atujengee nyumba"
Aliongea asha bila kujua boss huyo huyo ni mdogo wake kabisa tumbo moja, lakini kwakua hajawahi kumuona, sio rahisi kujua....
"ni kweli, lakini hata sadiki anaweza"
"sitaki bwana..."
"tatizo lako mwanangu unapenda pesa za haraka jamani... Hebu ngoja nitajaribu kupeleleza ili hata nipate namba ya huyo boss mkubwa"
Aliongea mama huyo bila kujua boss huyo ni mtoto wake, yaani anataka kumpigania mtoto wake wa kike aolewe na boss ambaye ni mtoto wake wa kiume, ila hawajui wote na hata surian hajui kama familia yake ipo hapo ndani...
Tukija huku kwa akina surian na mke wake, wakiwa jikoni wote wanapika..
"mke wangu, nataka nikuletee mfanyakazi wa ndani"
Aliongea surian huku mke akianza kununa, mana naye ana wivu
"kwa kazi gani sasa ulete mfanyakazi, kwani ni lini ukakuta nadeki humu ndani... Mana nyumba inajideki wenyewe kila siku... Inajifuta vumbi yenyewe, nguo zinajifua zenyewe, sasa mfanyakazi wa nini"
Aliongea mke huyo mana ikumbukwe maimuna ni jini, ila ni jini mwenye asili mbili,
"mimi sipendi uwe unatumia nguvu zako za kijini kufanya usafi, na hii asili siitaki, nataka uwe wa kawaida tu"
"ni sawa mume wangu, ila mimi ni jini na nitabaki kuwa hivyo.... Kwanza mtoto wako ananipiga mateke"
Aliongea maimati kana kwamba mtoto alioko tumboni
"mmmhjh wa juzi tu"
"hapana... Kwenye asili yetu ya majini hua hatukai miezi tisa kama binadamu wa kawaida... Tunakaa miezi minne na nusu... Na shetani anakaa miezi miwili na nusu"
"heeeeee... Kwahio keshokutwa tu nina mtoto"
"sanaaaaa"
"waooooooo.... Nakupenda jamani mke wangu"
"nakupenda pia baba watoto wangu"
Suria alinogewa na penzi la jini huyo na kufumbwa macho asione popote
Kesho yake ikiwa ni siku nyingine tena, asha akiwa ndani ya kiwanda lakini alionekana kukasirika sana kwasababu mwanaume aliojipendekeza sio yule aliomtaka yeye,... Asha Alishika simu yake ambayo kanunuliwa na sadiki, kwani asha hakuwa na simu baada ya kuiuza,...
"hallo diki mambo"
"poa mzima asha jamani"
"mzima... Nipo kiwandani, nataka tutoke kidogo nikakujibu ombi lako"
"sawa mama... Toka nikukute nje ya geti hapo kuna hoteli moja nzuri sana nakuja"
"ok sawa, uwahi mana nataka nirudi kazini"
"usijali asha wangu"
Sadiki aliongea hayo kana kwamba kweli kampenda sana asha, lakini asha alikuwa hamtaki sadiki kwani hakuwa boss alio mkusudia,... Asha alitoa laini zake kwenye simu ili akampe simu yake huko nje...
Huku ofisini sadiki anafurahi kwani anajua anakwenda kupewa utamu wa mwili, ikiwa ni mpenzi mpya kwake, kumbe anakwenda kupewa simu yake.... Sadiki alitoka nje ya kampuni akiwa kama meneja, hivyo hakukua na wa kumuuliza, asha alisha toka nje ya geti kwa kisingizio cha kwenda kununua dawa kwani hajiskii vizuri kiafya.... Walikutana nje kisha sadiki akachukua taxi, kwani angelitoka na gari yake labda angeulizwa anakwenda wapi kwani ilikuwa ni majira ya saa tisa alasiri,
Sasa huku kwa surian kashika simu yake ya mezani na kumpigia shadya au Cecilia aliopo mapokezi....
"hallo boss"
"shadya"
"abee boss"
"mwambie sadiki akakague products kabla muda wa kazi haujaisha"
"aaahh sorry boss, sadiki katoka kidogo nadhani kafuatilia oda"
"ok basi, nitakwenda mwenyewe"
Aliongea surian kisha akakata simu,.. Sasa shadya kaka akijiuliza anakwenda mwenyewe yeye au nani, mana toka kampuni kuanza surian hajawahi kwenda kukagua kiwanda wala kuangalia wafanyakazi wake,... Sasa kwa mara ya kwanza surian anatoka kwenye upande wa kiwanda ambako kuna wafanyakazi takribani 500, na wote hao hawamjui boss....
Shadya alishangaa kweli boss anatoka kwenda kiwandani,... Shadya haamini macho yake, yaani ni kama ndoto, afu mbaya zaidi ile ile idara ambayo asha alikuwepo ndio surian anaingia kuanza ukaguzi wake, kana kwamba kama asha angelikuwepo, basi angemuona ndugu yake, lakini hakuwepo... Wasimamizi walikuwa kipaumbele kumwelekeza boss, kwani shadya alitangulia kuja kutoa taarifa kuwa boss anafika hivi punde,.. Sasa wafanyakazi kila mmoja anasema yakwake...
"kumbe ni katoto tu... Mi nikajua kuubwa"
Mmoja kati ya wasichana aliongea hivyo...
"ila ni hensam jamani,.. Hivi ana mke kweli"
"heeee mwenzangu mi najuaje kama ana mke au hana"
"waaoooo kazuri kweli.... Asha yuko wapi si alikuwa anataka kumjua boss mwenyewe"
"asha atakuwa kaenda uwani"
Wafanyakazi wa kike walikuwa wakimuwazia sana boss surian... Sasa katika pitapita yake kwenye ukaguzi, akakuta sehemu moja ni chafu...
"hapa vipi hapa... Mbona idara hii sio safi"
Aliongea hivyo huku wafanyakazi na wasimamizi wakitetemeka mno
"hapa palimwagika maji boss"
"nani kaingia na maji... Na toka wakati wote kwanini msipakaushe"
"samahani boss..... Nyie, hebu chukueni dekio kausheni hapo"
huyo ni msimamizi mwenye kutoa sauti hio..
"sjapenda kabisa... Mabwana usafi wakija hapa ni tatizo kubwa sana... Hivi kama kiwandani ni hivi, je huko chooni kutakuaje..."
"hapana boss, chooni ni kusafi kila wakati boss"
"hapana.... Lazima nikakague usafi wa vyoo, mana mtafanya kampuni ipigwe faini au kufungiwa kwasababu ya uchafu"
Aliongea surian huku akielekea chooni, na vyoo hivyo vinafanyiwa usafi na mama yake mzazi, na hajui kuwa mama yake naye anafanya kazi kwenye kampuni yake, na hata mama naye hajui kama mwanaye ndio mmiliki wa kampuni hio,...
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2vAB4bN
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment