Sunday, February 2, 2020
PETE YA KIKE Sehemu Ya 23
"asha atakuwa kaenda uwani"
Wafanyakazi wa kike walikuwa wakimuwazia sana boss surian... Sasa katika pitapita yake kwenye ukaguzi, akakuta sehemu moja ni chafu...
"hapa vipi hapa... Mbona idara hii sio safi"
Aliongea hivyo huku wafanyakazi na wasimamizi wakitetemeka mno
"hapa palimwagika maji boss"
"nani kaingia na maji... Na toka wakati wote kwanini msipakaushe"
"samahani boss..... Nyie, hebu chukueni dekio kausheni hapo"
huyo ni msimamizi mwenye kutoa sauti hio..
"sjapenda kabisa... Mabwana usafi wakija hapa ni tatizo kubwa sana... Hivi kama kiwandani ni hivi, je huko chooni kutakuaje..."
"hapana boss, chooni ni kusafi kila wakati boss"
"hapana.... Lazima nikakague usafi wa vyoo, mana mtafanya kampuni ipigwe faini au kufungiwa kwasababu ya uchafu"
Aliongea surian huku akielekea chooni, na vyoo hivyo vinafanyiwa usafi na mama yake mzazi, na hajui kuwa mama yake naye anafanya kazi kwenye kampuni yake, na hata mama naye hajui kama mwanaye ndio mmiliki wa kampuni hio,...
ENDELEA........
Hakuna kitu kinauma kama kumkuta mama yako anafanya kazi za ajabu ingali una uwezo wa kuwapumzisha nyumbani, yaani wawe wanakula matunda yako tu,... Lakini kwa upande wa surian alitamani sana kuwasaidia wazazi wake lakini kutokana na masharti ya jini maimuna, anatakiwa awasaidie kwa njia ya ajira, yaani awaajiri, kitu ambacho surian alikataa kabisa, hawezi kuwatumikisha wazazi wake kisa pesa,... Lakini bila kujua hali za wazazi wake, zilikua mbaya na waliona matangazo na kuja kuomba kazi,... Lakini surian hajui kama mzazi wake mmoja yupo hapa kazini pamoja na dada yake... Na mbaya zaidi mzazi kapangiwa sekta moja mbaya sana, yaani mama wa tajiri akafanye kazi chooni??? Haiwezekani
Wasimamizi mbalimbali na viongozi wakiwa wanamuongoza kwenda katika vyoo hivyo ili kuhakikisha usafi unakuwa mzuri,.. Sasa shadya alishangaa kumuona boss anaelekea kule chooni,... Na mfanya usafi wa kule chooni amewekwa kwa siri kwasababu umri wake hauruhusu kufanyakazi kwenye kampuni hiyo,. Shadya haraka haraka alimpigia mama yake surian simu....
"samahani, namba ya mteja unayempigia haipatikani, tafadhali jaribu tena baadaye"
Ilikuwa ni sauti ya vodacom ikimjulisha shadya kuwa namba ya mteja haipatikani,.. Sasa shadya kichwa kinapata moto kwani yeye ndie alie fanya ujanja mpaka mama huyo akapata kazi, na umri wa mama huyo hauruhusu kabisa.... Shadya alijaribu na kujaribu, lakini wapi simu haipatikani,.... Surian anafika katika eneo la vyoo, wapambe wakaanza kuongea...
"boss?? Angalia vyoo ni visafi kila wakati"
Aliongea kiongozi mmoja ambaye ni kama mpambe tu... Na kweli palikuwa pasafi kabisa,... Sasa mama huyo alikuwa anafanya usafi ndani ya choo, hivyo hana taarifa kuwa boss mkuu yupo nje ya vyoo bavyo anavifanyia usafi kila wakati,.. Sasa boss karidhika kuona usafi ambao unafanyika hapo chooni,. Na karidhika nao kwa asilimia zote,... Bila kujua anaye fanya usafi ni mama yake mzazi,.. Aiseee surian anageuka na kuondoka, na mama naye anatoka chooni baada ya kumaliza kufanya usafi,... Mama alishangaa tu kuona kundi la watu wakimalizikia kuondoka, lakini hakujua kama boss wake alikuwepo hapo,... Yaani ilikuwa kiduchu tu aonwe na boss.... Sasa surian hakuwa na haja tena ya kutembelea idarani, alirudi zake ofisini,... Wakati huo shadya anatetemeka kwani anajua tayari kimebumburuka huko chooni,... Alishangaa boss kaingia ofisini kwake bila tabu na mtu.... Shadya alihema kwa nguvu kuashiria labda hakuna kitu,... Lakini hakuamini alitoka kwenda mpaka chooni kuhakikisha...
"Shikamoo mama"
"marahaba mwanangu hujambo"
"sijambo... Vipi, simu yako iko wapi"
"nimeiweka chaji kule dukani"
Aliongea mama huyo huku shadya akiwa haamini kama hajaonwa
"vipi, boss hajakuona"
Aliuliza shadya huku mama akishangaa
"boss? Kwani kaja huku"
"eeeh mungu wangu, Afadhali hata hajakuona"
"kwani kaja"
"ndioooo... Kafika mpaka hapa"
"weeeeeeee shadya muongo"
"ndio, yaani nilikuwa nishaanza kukusanya vitu vyangu mana nilijua kazi sina tena"
"eeehh mungu wangu weeeee, Afadhali hajaniona jamani"
Aliongea mama huyo, maskini ya Mungu bila kujua kumbe boss ni mtoto wake wa kumzaaa, yaani ilikua ni bahati juu ya bahati.... Basi ikawa ndio hivyo na hali ikaishia hivyo,... Mara ghafla simu ya shadya ikaita
"yes boss"
"uko wapi napiga simu ya mezani hupokei"
"nakuja boss, Samahani"
Shadya alikimbia kwenda ofisini, huku mama akiwa haamini kama boss kaja na hajamuona....
Sasa huku kwenye ki restaurant Kimoja hivi, asha anamtolea nje sadiki
"samahani sana kaka, nakueshim sana... Kiukweli Sitaweza kuwa nawe"
Aliongea asha huku akimpa simu yake na uzuri hajawahi kumchuna...
"asha, kwanini lakini,... Unautumiaje uzuri wako kunikosesha raha ya maisha namna hii"
"Kiukweli siwezi, Utanisamehe.... Niache kwanza nina maumivu ya mapenzi hivyo sihitaji kuumia tena kwa sasa"
"lakini asha, nimesha kwambia wanaume tupo tofauti asha... Nitakupenda mama"
"hapana,... Niache niende kazini"
Asha aliondoka huku sadiki akiumia roho,... Asha anataka kujipendekeza kwa boss mkuu japo hajui hata jina la boss huyo na hata sura hajawahi kumuona...
Asha anafika ndani ya kiwanda anasikia kuwa boss mkuu alitembelea muda sio mrefu...
"weeeee hadija... Unasema kweli"
"weeee, afu ni kitoto kabisa kizuriiiiii"
Asha roho ilimuuma mana ndio mwanaume ambaye anatamani kuwa nae hivyo moja kwa moja tunajua asha kaja kujipatia bwana ili amchune vizuri, lakini sasa anga anazo lenga ni mbaya sana... Hajui anampenda ndugu yake kabisa wa kuzaliwa naye..
"nakwambia shosti asha umekosa uhondo,... Afu alipotoka hapa akaenda chooni kule kuangalia usafi wa vyoo"
"mungu wangu jamani..."
Asha kwa hasira alitoka kwenda mpaka chooni kwa mama yake...
"mama, eti naskia boss katoka nje"
Aliuliza asha huku mama nae akampa moto mwanae
"ndio, kaja hapa na kundi la watu... Jamani kijana ni mzuri huyo"
Mama nae anazidi kumuumiza mtoto wake ingali hata yeye mama hajamuona mtoto huyo, na ni mtoto wake...
"mamaaaa... Namba zake hujapata"
"mbona una haraka we mshenzi kweli, na ulikuwa wapi hujamuona"
"nilitoka na Meneja kwenda kumpa simu yake"
"kwahio humtaki meneja tena"
"silitaki bwana... Nataka huyo saizi yangu, mi naona meneja mkuubwa"
"ehehehehehehe, we mtoto acha kuchagua wanaume mwanangu"
"booooo..... Mi naenda ndani,.. Ila fanya mpango wa namba mama"
"hebu nenda tusije kuonekana tuna njama fulani"
Mama alimfukuza mtoto wake ili wasije kuonwa kama kuna njama wanapanga hapo chooni....
Ilipofika saa kumi na moja za jioni ikiwa ndio saa za kutoka kazini na kiwanda kufungwa, mabasi yalikuwa yakibeba wafanyakazi ili kuwapeleka,... Wafanyakazi ni wengi kana kwamba lazima mabasi yarudie wafanyakazi, ila wale wenye nauli au kwao ni karibu, hawana budi kuwahi..
Mama surian akiwa ndani ya basi na mtoto wake, alishangaa na shadya nae huyo kwenye siti ile ile nae leo kaja kupanda gari ya wafanyakazi wa kawaida...
"heeeeeee mwanangu, nyie si mna magari yenu nyie"
Mama alimuongelesha shadya kuwa wao wana mabasi yao maalum
"ndio, ila limejaa, sasa mpaka waturudie ni saa ngapi.. Bora nipande hili hili tu"
Aliongea shadya huku wakibanana kwenye siti ya watu wawili akifosi wakae wawili ili awahi....
"Uuuuuuuuuwiiiiiiii jamani nimesahau chaja yangu jamani"
Aliongea shadya na kuacha mkoba kisha akashuka ili aende ofisini kuchukua chaja yake,... Sasa mkoba kawaachia mama surian na asha... Saa ngapi mama hajaingiza mkono kwenye mkoba wa shadya na kutoa simu kubwa ambayo ndio anayo itumia shadya....
"we, hii ndio simu alipigiwa na boss, sasa tutapataje namba zake humu"
Aliongea mama huyo huku basi likiwa sailensa kitaka kuondoka lakini kwakua mmoja kashuka hivyo limesimama kwa muda...
"sasa kama ina loku itakuwaje mama"
"hebu jaribu, wewe si unazijua kuzitumia hizi simu... Mana mimi sijui hata nagusa wapi hapa"
Aliongea mama huyo huku asha akiichukua ile simu,.. Wakati huo wafanyakazi kila mmoja bize na simu yake mana huko kiwandani hawaruhusiwi kuingia na simu, sasa wakiwa kwenye basi, kila mtu bize na simu yake mana mchana kutwa hako nayo...
"heeeee mama haina loku"
"sasa mimi najua jamani... Angalia wewe si unazijua hizi simu"
"ndio... Sasa nafanyaje hapa"
"alipigiwa muda ule"
Aliongea mama suria kisha asha akabonyeza sehemu ya namba zilizopigwa au kupiga...
"sasa itakuwa ni ipi hapa mama, mana kapigiwa na watu wengi"
Aliongea asha huku wakiangalia namba zilizopigwa muda sio mrefu
"enheeee, kuna hii imeandikwa BOSS SURE"
asha aliona namba ilioseviwa kwa jina la boss sure akiwa na maana boss suria, sema kaliandika kama kwa Kingereza fulani hivi kama swaga,...
"itakuwa ndio hio... We ichukue sasa"
Aliongea mama huyo kisha asha akasema
"naichukua na nini sasa na sina simu"
Aliongea asha huku mama akiwa haamini kuwa wanaikosa hio namba mana asha karudisha simu ya watu alio nunuliwa, na mama nae simu yake ipo chaji huko dukani kwa jirani yao... Afu mbaya zaidi shadya anakuja, na namba bado hawajachukua...
"mama mi naona tuikariri tu"
"hebu tujaribu, 0714419487... Mimi nitashikilia hio 071441....na wewe shikilia hio 9487"
"sawa... Rudisha sasa huyo anapanda gari"
Wakarudisha ile simu kisha wakafunga mkoba wake,.. Wakatulia kimya..
Kiukweli familia ya surian imekumbwa na maisha magumu kana kwamba mpaka mama anakubali mtoto ajipendekeze kwa boss, tena mbaya zaidi mama ndio anampa msaada mtoto wake ili afanikiwe na maisha yao yaendelee kuwa mazuri zaidi, mana hapo mama kibarua chake kipo hatiani muda wowote anaweza kufukuzwa pale atakapo gundulika kuwa ni mzee asiotakiwa kufanya kazi kwenye kampuni hiyo... Hivyo anamtafutia mwanaye chansi kama Ataweza kumpa iwe rahisi katika maisha yao... Familia iliojaa dini lakini kutokana na maisha hawana budi kuwa watu wa aina hio,
Huku ofisini baada ya wafanyakazi kuisha wote, surian ndio anatoka na kufunga milango ya ofisini, kwani yeye hutoka wa mwisho kabisa kama alivyo zowea kutoka kila siku,.. Aliwasha gari yake ya maana ambayo ndio wanaitumia yeye na mke wake,...
Tukija huki kwa akina faima akiwa na tariki,... Mpaka leo tariki bado hajalubaliwa kwani faima alikumbushwa na shaimati kuwa surian yupo na yupo kwenye kiwanda cha nguo za Kiislamu,...
"afu tariki mbona nimekuona umeshushwa na gari la STAFF BUS la Kampuni ya MICCO"
Aliongea faima huku tariki akiwa haamini kama kaonwa, mana anajitapaga kuwa ana pesa chafu sasa leo kashushwa na gari la staff bus
"ndio, kwani sijakwambia kuwa mimi ndio meneja wa ile kampuni"
Aliongea tariki huku faima akijibu
"aka, hata nikuulize ili iweje"
"ok sasa lile jibu langu vipi, mana umebadilika ghafla"
"naweza kukubalia, lakini nikupe mtihani mmoja,.. Nitafutie picha ya mmiliki wa kampuni hio yakwenu"
Aliongea faima ili ajue kama kweli surian ndio mmiliki au vipi
"mmiliki si unamaanisha boss wetu au"
"ndio"
"sasa fey jamani... Majibu yangu na huyo boss wapi na wapi jamani fey"
"kwanza anaitwa nani"
"aaahhh anaitwa sadiki"
"sadiki??... Ni rangi gani"
"mweusi hivi, mnene... Lakini fey, kwani ana nini"
"nataka uniletee picha hapa"
"haaaaaaa.. Feiiiiiiiiiiiii, sio kwa mtihani huu lakini"
"kama unanipenda, utaweza, lakini kama hunipendi hutoweza"
Aliongea faima kisha akamuacha tariki hapo hapo barabarani kisha yeye akapanda Bajaji kwenda zake nyumbani kwani giza lilikuwa likilindima kwa wakati huo.... Tariki kapewa mtihani mkubwa sana ambao hajui aanzie wapi na aishie wapi mana kweli anajua boss wa kampuni ile sio sadiki,.. Na kama sio sadiki je ni nani,.. Mana tariki hajawahi kumuona boss kwasababu mchana alipotembelea kiwandani, hakumaliza kiwanda chote, aliishia katikati na kwenda kukagua usafi wa vyoo... Hivyo hajafika kwenye idara ambazo tariki yupo... Hivyo hata tariki haijui sura ya boss....
Sasa tukija huku kwa mama surian na mwanae asha...
"wewe asha, tujaribu ile namba kabla baba yako hajarudi msikitini"
Aliongea mama huyo huku wakiwa na shauku ya kupiga namba hio, na na waliishika nusu nusu....
"sasa mama, tunapiga kwenye simu yako, kwani ina salio"
Aliongea asha huku akiangalia salio kwenye simu ya mama yake...
"weeeeeee tumia laini yako,.. Mana ukitumia yangu afu akapiga kwangu nitamjibu nini mimi"
"sawa basi ngoja tutoe laini yako niweke yangu,... Ila yangu haina vocha ni sms tu"
"nitakupa miatano ukanunue"
Basi asha alimuachia mama yake aweke laini kisha akaenda kununua vocha, ili ampigie na usiku huo huo.. Ikiwa ni saa mbili kasoro, baba kaenda msikitini kuswali swala ya Ishah
"hii hapa.. Lete niiweke"
Aliongea asha huku mama akimpa mwanae simu ili aweke vocha ajiunge kisha ampigie....
Wakati huo huku kwa suria katulia ndani anaangalia TV, na mkewe akiwa jikoni anapika, alikuwa akiangalia kipindi kimoja cha maigizo kinachoitwa MIZENGWE hivyo alikuwa akicheka sana, kana kwamba furaha kwake ilitawala sana
Sasa huku kwa mama na mtoto,... Kumbe namba wamesahau, sasa wakawa wanabuni buni...
"kwanini wewe ulishikaje jamani mama"
"tatizo mimi nilishika namba nyingi ndio mana nimesahau mwanangu"
Aliongea mama huku asha akiwa kashikilia namba zile za mwisho ambazo ni 9487, na mama kashika namba za mwanzo, afu kasahau...
"jamani mama,... Bahati imepotea hivi hivi na mtu mwenyewe yule hatupandi nae gari mara kwa mara, leo ilikuwa kama bahati tu jamani mama"
asha alilalamika sana kwa kitendo cha mama yake kusahau namba za mwanaume anayetamani kuwa naye kimapenzi ambaye ni boss wake, lakini bila kujua ni ndugu yake...
"lakini kama vile kulikuwa na nne nne nyingiii"
"aaahh bwana mama... Naenda zangu kulala..."
"sasa njoo jamani"
"sasa mama wewe unasema nne nne nyingi, ni namba gani inaanza na nane"
Aliongea asha huku akitamani kulia, mana ndio basi....
"heeeeeee uyoooooo njooo uko, nazikumbuka"
Aliongea mama huyo huku akitabasamu kwani alimdanganya mtoto wake kuwa kazisahau,...
"haya taja sasa jamani kabla hajalala... Mana ni tajiri yule analalaga mapema mno"
Aliongea asha huku mama akicheka
"mmmhhh jamani kupenda tabu,.. Heeee tu unalo mwanangu... Haya andika ni 071441 hizo ndio nimeshika mimi"
Alipomaliza kutaja mama yake, kisha asha akamalizia kuzijazia zile alizokariri yeye,... Kisha akamuuliza mama yake kuwa...
"sasa nimsevu nani"
"we msevu vile vile boss sure"
Asha alifanya kama alivyosema mama yake kisha akabonyeza kitufe cha kupigia
"kohoa kidogo... Afu punguza uzito wa sauti yako... Bana sauti hata imtoe pangoni"
Aliongea mama huyo kama kumfundisha mtoto wake jinsi ya kumteka mwanaume kwa sauti... Kweli asha kakohoa na kuseti sauti yake,... Mara simu inaita.... Na ni kweli ilikuwa ni namba ya surian, suria alikuwa bize na mchezo wa TV, lakini aliona bora apokee simu hio..
Sasa alivyo pokea tu kabla hajasema hallo,.. Asha keshasema
"Hellow, Samahani, naongea na boss sure"
Aliongea asha kwa sauti ya kuvutia zaidi,..
"samahani utakuwa umekosea namba... Mimi sio boss sure"
Sasa huku kwa asha, ghafla alikata simu na kushtuka...
"kasemaje? Ndio yeye au"
Mama alimuuliza mtoto wake baada ya kukata simu
"mama... Mbona ni sauti ya kaka surian"
Aliongea asha kana kwamba kaijua sauti ya kaka yake,...
"we mshenzi wewe, usinikumbushe machungu ya mtoto wangu, we niambie kakwambiaje"
Mara simu ikaita tena,....
"haya huyo kapiga yeye, pokea umsikie mwanao"
Aliongea asha huku akimpa mama yake simu
"asha mwanangu, mpokelee mwenzio bwana acha utani"
"hapana mama... Ni sauti ya kaka surian"
Aliongea asha huku mama akaichukua ile simu na kuipokea kisha akaiweka sikioni....
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2UdwMBA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment