Friday, February 28, 2020

Tatizo la Mwanamke Kukosa Hamu ya Tendo la Ndoa, Sababu na Suluhisho Lake.







Tatizo la kukosa hamu ya kufanya mapenzi huwatokea zaidi wanawake kuliko wanaume lakini ni wanaume wanaokerwa zaidi na tatizo hili kulio wanawake. Wakati ambapo ni asilimia 15 hadi 16 ya wanaume wenye tatizo hili, idadi ya wanawake ni mara mbili ya hii ya wanaume. Lakini wakati ni asilimia 23 ya wanaume wanaonyesha kuridhika kuishi na tatizo hili, asilimia 46 ya wanawake wapo radhi kabisa kuendelea kuishi na tatizo hili.

Si lazima kuendelea kuishi na tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa sababu kuna mambo mengi unayoweza kuyafanya ili kuondokana na hili tatizo.

Hali ya kupenda kufanya mapenzi au tendo la ndoa kwa mwanamke inabadilikabadilika sana ikipanda na kushuka kulingana na matukio mbalibali yanayomtokea katika maisha yake. Baadhi ya matukio yanayoathiri hamu ya mwanamke kufanya mapenzi ni pamoja na kuanza na kwisha kwa mahusiano ya kimapenzi na mwanamme, kupata ujauzito, na magonjwa. Kama wewe mwanamke umepatwa na ha hii unaweza kukabiliana nayo kwa kubalisha jinsi unavyoishi, kufanya mambo kadhaa yatakayo badilisha hali hii au kutumia baadhi ya dawa zinazosaidia kuondoa tatizo hili.

Jee, Utajuaje kama Una Tatizo?

Kuna vitu vingi ukiviona vinakutokea, ujue una tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya mapenzi.Tulivijadili viashiria hivi kwa kina tulipozungumzia tatizo hili la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa wanaume. Unaweza kusoma tulivyojadili kwa kusoma ukurasa huu “Mwanamme Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa

Sababu Za Kukosa Hamu Ya Kufanya Tendo La Ndoa

Sababu zinazoweza kupelekea mwanamke kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa ni nyingi lakini kwa ujumla karibu zote tunaweza kuzigawanya katika makundi manne:

1. Mahusiano Baina Ya Mwanamke Na Mwanamme Kwa wanawake walio wengi ukaribu wa kihisia ndicho kitu cha kwanza katika kujenga mapenzi kati yake na mwanamme. Hivyo, mahusiano mabovu yaweza kuwa ndicho chanzo cha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa kwa mwanamke. Mwanamke atakosa hamu ya kufanya mapenzi endapo hakutokuwa na mawasiliano baina yake na mumewe, kutakuwa na migogoro kati yake na mumewe isiyokwisha, kutakuwa na ukosefu wa mawasiliano kuhusu mahitaji yake ya kufanya mapenzi na jinsi ambavyo yeye angependa kufanyiwa kimapenzi na kama atahisi kuna ukosefu wa uaminifu katika ndoa au mahusiano yao.

2. Matatizo Katika Maisha Yako Matatizo mbalimbali katika maisha ya mwanamke humsababishia kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Baadhi ya matatizo ambayo huweza kusababisha mwanamke kukosa hamu ya kufanya mapenzi ni pamoja na magonjwa, mabadiliko katika mwili wake na hata matumizi ya baadhi ya madawa:

Matatizo Katika Kufanya Tendo La ndoa. Kama mwanamke anapata maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa au kama mwanamke anakosa kufika kileleni, hali hii inaweza kusababisha akakosa kabisa hamu ya kufanya mapenzi.

Matatizo ya afya. Magonjwa mengi husababisha mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya magonjwa ni maumivu ya viungo vya mifupa (arthritis), kansa, ugonjwa wa kisukari, high blood pressure, matatizo katika mishipa ya damu ya arteri na matatizo ya akili.

Matumizi ya madawa. Baadhi ya madawa yakitumiwa, huondoa kabisa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Mfano wa dawa hizo ni madawa ya kukabiliana na msongo wa mawazo.

Mtindo wa maisha. Matumizi ya pombe kuzidi kiwango, uvutaji wa sigara na madawa ya kulenvya huathiri hamu ya kufanya mapenzi.

Upasuaji. Upasuaji uliofanyika katika maeneo ya maziwa au katika maeneno ya viungo vya uzazi humbadilishia mwanamke mwonekano wake, huathiri ufanyaji kazi wa viungo hivyo na mwisho kuathiri hamu yake ya kufanya mapenzi.

Uchovu. Uchovu unaotokana na kulea watoto wadogo au vikongwe kuweza kuathri hamu ya mwanamke ya kufanya mapenzi.

3. Mabadiliko Katika Mfumo Wa Homoni. Kukoma Hedhi.Mabadilko ya viwango vya homoni katika mwili wa mwanamke yanaweza kusababisha kukosa hamu ya kufanya mapenzi kwa mwanamke. Kupungua kwa Estrogen katika mwili wa mwanamke katika kipindi cha kuelekea kukoma hedhi kunaweza kusababisha ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi. Upungufu wa homoni hiyo husababisha uyabisi wa wa viungo vya sehemu nyeti na kusababisha maumivu wakati wa kufanya tendo la ndoa.

Mwanamke pia huweza kuwa na upungufu wa homoni ya testosterone, homoni ambayo husaidia kuongeza hamu ya kufanya mapenzi kwa wanaume na wanawake, hivyo mwanamke huyo akapungukiwa na hamu ya kufanya mapenzi.

Pamoja na kuwa wanawake wengi huendelea kupata hamu ya kufanya mapenzi baada ya kukoma hedhi, baadhi kupungukiwa na hamu hiyo baada ya mabadiliko haya ya viwango vya homoni katika miili yao.

Ujauzito na kunyonyesha. Mabadiliko katika mfumo wa homoni wakati wa ujauzito, baada ya kujifungua na wakati wa kunyonyesha huweza kusababisha mwanamke kukos hamu ya kufanya tendo la ndoa.

4. Matatizo Ya Kisaikolojia 
Matatizo ya kisaikolojia yana mchango katika kumfanya mwanamke akose hamu ya kufanya tendo la ndoa. Baadhi ya mtatatizo hayo ni:

Waswasi na kuwa na msongo wa mawazo
Kuwa na mawazo mengi kuhusu matatizo ya kifedha au kikazi
Kuhisi kutothaminiwa katika jamii
Kuwa na historia ya kunyanyaswa kimwili au kijinsia kama kupigwa au kubakwa
Kuwa na historia mbaya ya kimapenzi

Njia Za Kuondoa Tatizo La Kukosa Hamu Ya kufanya Tendo La Ndoa

Hakuna dawa ya moja kwa moja toka hospitalini kwa sasa hivi kwa ajili ya kuondoa tatizo hili, hata hivyo wanawake wengi wanaweza kurudi kwenye hali zao za kawaida kwa kushirikiana na waume zao waelewa. Jaribu kufanya mambo tuliyoyadokeza katika mada yetu ya “Mwanamme Kukosa hamu Ya Kufanya tendoLa Ndoa” ukisaidiana na mumeo. Unahitaji kuchunguza taratibu na kwa kina chanzo cha tatizo lako, na taratibu lifanyie kazi kwa msaada wa mume wak






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2w8WWvf

No comments:

Post a Comment