Friday, February 28, 2020
NAMNA YA KUJITUNZA WAKATI WA DAMU YA MWEZI(PERIODS)
Damu ya mwezi si ugonjwa wala haifai kuwa sababu ya wanandoa kutengana ila ni muhimu ukajua namna ya kujitunza ili usimghasi mume katika kipindi hiki.
_
Kimila ni aibu kwa mumeo kuona damu yako- ila kwa dharura- kwa hivyo jaribu kuwa muangalifu unapokaa, unapolala na unapotumia choo kisafishe ili mume asikumbane na mapande ya damu. Vilevile hakikisha unaifunga pad yako kwa karatasi(isiyoonyesha ndani) kabla hujaitia kwenye pipa la taka. Kuna watu huwa na tabia ya kutupa pad iliyotumika ikiwa wazi Haipendezi.
_
Ni aibu kwa mwanamke aliyeolewa kurundika chupi chafu. Fua chupi pindi tu inapochafuka kwa damu. Kwenye upande wa kitanda unaolala, tandika leso/khanga nzito chini ya shuka ili damu ikichuruzika isipite kwenye mattress. Vilevile, weka akiba ya upande wa leso/khanga kitandani ili unapochafua shuka kwa bahati mbaya uweze kuifinika bila kulazimika kumuamsha mume kwa ajili ya kutoa shuka.
_
Usiache kuoga na mumeo kwa sababu upo mwezini. Tangulia chooni ujisafi sehemu ya siri na kutupa pad kabla mume hajaingia bafu kisha muoge kama kawaida. Hakikisha unajikamua kidogo ili damu isibaki tupuni na kuchuruzika wakati mnaoga. Harufu mbaya ni sababu nyengine inayotenganisha wanandoa wakati wa damu ya mwezi. Hakikisha unaoga angalau mara 2 kwa siku na unabadilisha pad kulingana na wingi wa damu yako. Usishinde na pad moja siku nzima utanuka vumba.
_
Unapostanji chukua muda wako kutia kidole kwenye sehemu yako ya siri ili kutoa uchafu na ujikaushe vizuri kabla hujavaa pad kwani majimaji husababisha harufu mbaya Mavuzi huleta ugumu katika usafi wa sehemu ya siri. Jinyoe siku kadhaa kabla hujaanza period ili iwe rahisi kujisafi.
_
Wakati wa damu ya mwezi ndio unapofaa kunukia vizuri zaidi kuliko nyakati zengine. Tumia manukato. Fukiza chumba, nguo, nywele na sehemu yako ya siri. Vaa kikuba. Tandaza vilua na asumini kitandani. Usiache kujiremba na kuvaa viguo vya kumtega mume. Damu ya mwezi isiwe sababu ya wewe kutopendeza.
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/388NbKM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment