Sunday, February 2, 2020

PETE YA KIKE Sehemu Ya 21




"nipo... Mbona kama ulikuwa unalia"
"we acha tu dada shuu,... Ni mwezi wa tatu kama sio wa nne, surian wangu sijamuona, naumia sana..."
Aliongea faima huku akilia na kumuegemea shamimu....
"mbona surian yupo na hata jana nilimuona"
Shamimu katumbua jipu lililoiva....
"unasemaje dada shuu"
"surian wako jana nilimuona... Na jinsi ya kumpata ni rahisi sana... Ila unatakiwa kuwa mpole, mvumilivu, mnyenyekevu, na mwenye utulivu..."
"sawa dada shuu... Nipo tayari kutii vigezo vyote,.. Hebu niambie... Nampataje na yupo wapi kwasasa"
Faima aliuliza kwa umakini huku akiwa katoa macho
"unaijua kampuni mpya inayotengeneza nguo za dini hapa mkoani Tanga"
"ndio.... Si hii inayo itwa MICCO"
"yeeees.... Mmiliki wa kampuni hio ni surian na mke wake"
Faima kashtuka kwa kusikia neno SURIAN NA MKE WAKE
"hivi umesema surian peke yake au surian na mke wake"

ENDELEA.......

Katika maisha haya hakuna kitu kinauma kama kusikia ya kwamba mtu umpendae ameoa au kaolewa, inauma sana,....

Faima alipatwa na mshangao wa hali ya juu baada ya shaimati kumpa ukweli wa mambo,.. Faima ametokea kumpenda surian toka moyoni mwake, na kajitunza mpaka kesho kwa ajili ya suria, siku zote husikia kuwa suria kafariki dunia tena kwa kuuwawa na dada yake,.. Leo anasikia kuwa suria ndio mmiliki wa kampuni mpya iliofunguliwa hivi karibuni, shaimati pia hakutaka kumficha kuwa suria keshaoa japo kaoa mwanamke ambaye sio asili yake,...

"hivi umesema surian peke yake au umesema surian na mke wake"
Faima aliuliza kwa mshangao wa hali ya juu,
"faima, surian bado ni wako tu.. Ni kweli surian kaoa, lakini bado ni haki yako kwasababu haki za kibinadamu zikiingilia kati, nina uhakika aliokuwa naye atachukuliwa hatua za kisheria, japo hawato muweza"
Aliongea shaimati na yote hio ni kwasababu ya wivu wa mapenzi, hivyo kaona kuliko maimuna afaidi mwenyewe, bora tunda hilo lirudi kwa aliekua nalo awali,...
"una maana gani dada shuu, ina maana nu kweli surian kaoa"
Aliendelea kulia msichana faima huku shaimati akijihisi kua na raha sana kwani tayari keshalitumbua jipu
"ndio, ila kuoa kwake sio tatizo, mana anamilikiwa na kiumbe kama mimi"
Faima alishtuka sana kusikia kua suria anamilikiwa na kiumbe kama huyu, kana kwamba rafiki yake huyo sio binadamu bali ni kiumbe,...
"una maana gani? Ina maana wewe sio binadamu"
Aliongea faima lakini shuu ama shamimu alimjibu
"mimi ni nusu ya binadamu, ila ni mapema mno kunifahamu"
Shuu alijibu kisha akaondoka zake kwa hatua za kawaida tu, wakati huo faima anamwangalia tu mpaka akapotelea uchochoroni,...

"mbona sielewi, au naota mie?"
Fey alijiuliza mara kadhaa kua huenda ni ndoto labda ndio imemjia mchana huo... Lakini aliamini haikuwa ndoto bali ni ukweli mtupu

Huku nyumbani kwa mzee Rashidi akiwa na mtoto wake asha, mana mama kaenda kazini, sasa baba ana wasiwasi na mke wake kwasababu kitengo alicho kipata hakiendani na mshahara ambao analipwa mkewe
"mwanangu asha, hebu fanya hima ukaombe kazi pale... Mimi nina wasiwasi na mama yako... Ina mana hata wewe inakuingia akilini hio.. Mfagia vyoo alipwe laki nne,.. Hapana.. Hebu kaombe kazi mama"
"baba, mi najua mama hana lolote ni wasiwasi wako tu baba... Mimi nataka nikaombe wiki ijayo"
"aahhhh sawa mimi sina wasiwasi sana, ila inawezekanaje Mfagia vyoo alipwe laki nne"
"huezi jua baba.. Ni bahati ya mtu tu"
Wakati huo asha akipika chakula cha mchana,.... Ghafla mlango unagongwa, asha akaacha safuria ichemke, akaenda kufungua mlango..
Hakuamini kumuona shamimu
"haaaaaaa jani shuu, mambo"
"poa, mbona umebadilika hivyo, ulikuwa unavaa vizuri, unajisitili sasa mbona umebadilika"
Aliongea shamimu mana alimuacha akiwa anapiga hela na anajua kwanini alikuwa akipiga pesa....
"we acha tu shuu, yaani ulipo niacha biashara yangu ilikuwa nzuri, lakini pia ilikuja kuwa mbaya baada ya kusikia kuwa mimi nimemuua mdogo wangu, Kiukweli sikua na raha kabisa"
"wewe umemuua mdogo wako? Kwani una ndugu wangapi"
"mmoja tu"
"sasa umemuua yupi tena"
"aahh bwana tuyaache hayo... Mambo mengine vipi"
"safi tu... Vp surian yupo"
Shamimu aliuliza makusudi japo yeye ndio anajua surian alipo
"aahh sasa shuu, si ndio nimekwambia hapa surian hayupo, yapata miezi minne sasa na ndio mana nimeambiwa nimemuua ili nipate pesa"
Aliongea asha huku akitaka hata kulia,
"sikiliza asha.... Ile pete, ndio ilikuwa sababu ya biashara yako kuwa nzuri, na kama ni surian mbona yupo... Na hata jana nikua naye usiku"
Aliongea shaimati lakini asha kwa hasira na ghazabu za kujua kua shamimu anaongea uongo, kwani surian hawezi kuwepo mjini bila kuja nyumbani kwao, tena kwa jinsi surian anavyo mpenda mama yake, hawezi kaa hata siku moja bila kuja,..sasa leo anasikia ya kua surian yupo tena hata jana alikuwa naye....
"asha.... Asha... Njoo basi rafiki"
Shamimu aliita lakini asha hakutaka kusikia kwani alichokisema shuu ni uongo mtupu, na hatamani kuusikiliza tena,... Basi shaimati aliondoka zake baada ya kujua kuwa asha kagoma kuongea naye... Nia ya shamimu ni kutangaza uwepo wa surian, ili amkomeshe jini mwenzie ambaye anapata raha kupitia mtu huyo,

Ilipofika mida ya jioni mama asha akiwa nyumbani baada ya kurudi kazini, na kila akirudi kiuno humuuma kwa vile anavyo inama kila wakati kwa kusafisha vyoo, mana vyoo hivyo huchafuka kila wakati,.... Mama asha akiwa nyumbani akifanya maandalizi ya kupika chakula cha mchana, na hapo alikuwa akimpa stori mtoto wake asha
"wewe ungekuja kuomba kazi mwanangu,... Wasichana wenzio wapo wamejaa tele, yaani wamama hakuna kabisa"
Aliongea mama huyo huku asha akiwa na msimamo wake kuwa atakwenda lakini ni wiki ijayo
"nitaenda mama"
"tena naskia skia huyo boss ni mtotoooo"
"heeeeee mama,.. Kumbe ndio mana baba ana wasiwasi, haya hivyo umevijuaje"
"si wafanyakazi walio muona wanasema"
Mara fsima kaingia huku akiwa na furaha kwa kitendo cha kusikia kuwa surian ndio mmiliki wa kile kiwanda cha nguo za Kiislamu...
"heeee mwali wangu huyooo karibu mama"
"ahsante mama, shkamoo"
"marahaba mwali hujambo"
"sijambo, shkamo wifi asha"
"marahaba mambo fey"
"poa...."
Lakini kabla faima hajaanza kusema, ghafla mama asha kaanza kusema kuwa
"hivi faima mwanangu... Mbona hujaenda kuomba kazi kwenye kile kiwanda kipya... Yaani wasichana weeengi wapo humo"
Aliongea mama huyo huku faima akiuliza
"kwani wewe umepata kazi"
"ndio"
"boss wa kampuni hio unamjua"
Faima aliuliza makusudi tu mana kaambiwa kuwa boss wa kampuni hio ni surian
"ndio tena ni kijana mdogo tu"
"aahhh nitakwenda kuomba tu"
Sasa faima kajiuliza sasa kama mama mtu anafanya kazi huko na kamjua boss, ina maana shamimu kamdanganya kuwa surian ndio mmiliki wa kiwanda hicho,....
"nendeni, hata sasa hivi nilikuwa namwambia wifi yako hapa... Aende ili tupate pesa nzuri"
"sawa mama nitakwenda"
Faima alianza kupata huzuni tena mana kaja kutoa taarifa kuwa surian yupo pale, sasa anakuja kujua kumbe mama mtu anafanya kazi hapo, sasa kama ni kumuona si angemuona kabla,... Faima akatulia tu wala hakuongelea swala la surian tena mana ataanza kuliza watu,... Ila katika moyo wake alimlaumu sana shamimu kwani kamdanganya vikubwa sana kuhusiana na mchumba wake,....

Sasa tukija huku nyumbani kwa akina surian akiwa jirani na mkewe wakiwa wamebanana kwenye sofa moja,.. Surian kasahau kama anatakiwa kwenda kuiona familia yake, kasahau kila kitu,...
"mme wangu,... Nina jambo nahitaji nikwambie"
Aliongea maimuna huku surian akiwa makini
"niambie"
"nina mimba"
"aaaaaacha utani muna"
"kweli vile"
"umepima saa ngapi na wote tulikuwa kazini leo"
"mimi sina cha kupima... Ina maana umenisahau"
"aaahh hapana sijakusahau mke wangu, ila sikufahamu kwamba hata mimba mnaweza kuzifahamu bila kupima"
"uwezo tulio nao ni mkubwa sana,.. Na hata hapa baada ya miezi miwili tuna uwezo wa kujua hata jinsia ya mtoto wetu"
"ole wako awe wakike, atakuwa sio wangu huyo"
Aliongea surian huku wakifurahia swala hilo, mana ni muda mchache tu hata mwezi hakuna toka kufunga kwao ndoa, lakini muna anadai kuwa na mimba...

BAADA YA WIKI MBILI KUPITA

Ni siku nyingine tena, na ni mwezi toka kampuni ya MICCO kufunguliwa, hivyo wafanyakazi wameshakula mishahara ya kwanza kwanza,... Siku hio mke na mume wakiwa kazini,... Mje alitamani kutoka na mume wake wakatembee mjini, kwa sasa masharti yameisha kwani tayari ule wakati umekwisha,...
"we nenda tu"
Aliongea surian kana kwamba hataki kutoka hata nje yaani mazoea ya masharti yamekuwa kweli,
"jamani baba Rashidi, twende tukale hata chipsi jamani, kila siku uletewe humu, noo bwana twendeee"
"mama chidi, naomba uende wewe tu"
"hapana,..."
"lakini nipo bize, ona oda zinavyo miminika, naondokaje sasa"
"ok... Shadya?, Shadya"
"abee boss"
Aliitwa sekretari Shadya kupewa ile laptop ya boss...
"fuatilia hizo oda zote hakikisha zinatoka, sawa"
"sawa boss, nitaifanya kazi hii"
"haya sasa upo bize tena"
"lakini mke wangu,... Ile kazi yapaswa nifanye mimi"
"hapana, wewe ni boss now, unahitaji kutuma tu, hebu twende bwana ukanitembeze kwenye mji wenu"
Aliongea mwanamke huyo huku surian akikubali kishingo upande,... Gari yao hua wanaipaki pembeni kidogo ya ofisi yao hivyo hata wakitoka hakuna mfanyakazi ambaye atawaona,.. Basi surian aliingia na kupandisha kioo cha gari, kwani tayari tabia ya kuto onekana na watu imeanza kumzoea, yaani hataki kuonwa na watu kabisa... Kasahau kuwa kuna familia yake,...

MLINZI WA GETI alifanya kazi yake kisha mke na mume wakatoka, lakini ile wanatoka tu na asha nae ndio anaingia, yaani kiduchu kiduchu waonane, na asha hana tetesi zozote kuhusu mdogo wake ndani ya kampuni hio,... Asha akiwa kashikilia vyeti vyake kaja kuomba kazi kama alivyokuwa akilazimishwa na wazazi wake,... Asha anafika ofisini boss hayupo,
"yaani boss katoka sasa hivi tu"
Aliongea shadya huku akiwa bize na kazi ambayo kapewa
"kwahio unanisaidieja dada angu"
"mmhhhh, hebu ngoja nijaribu kumpigia simu"
Shadya alichukua simu ya mezani kisha akampigia simu boss wake...

"umeona sasa, nimetoka sasa hivi tu, na simu napigiwa, ndio mana staki kukaa mbali na ofisini"
Aliongea surian baada ya kuona simu ya shadya
"Enhee sema kuna nini tena"
"aahhh boss... Kuna msichana kaja kuomba kazi"
"documents zake zimekamilika"
"mmmhh ndio, ziko sawa"
"ok mwambie sadiki amsajili na aanze kazi kesho... Afu pia akampange mahali penye upungufu wa wafanyakazi"
"ok sawa boss ahsante"
"ok"
Shadya alikata simu kisha akampeleka asha kwa sadiki,... Sadiki ndio meneja mwajiri wa kampuni hio, hivyo yeye ndio anajua kila kitu kuhusu wafanyakazi, na ni kijana mdogo lika na surian,...
"boss,... Kuna mgeni hapa"
"ni nani na katoka wapi"
"samahani boss,.. Kaleta barua ya maombi ya kazi"
"aaaoo ok mwambie aingie"

Huku mjini surian akiwa na mke wake walipaki gari mahali fulani, kisha wakaingia sehemu moja iliokwenda kwa jina la TANGA SPECIAL BITES, waliingia hapo lakini surian alitaka kukaa ndani, japo kwa nje kuna nafasi, yaani surian kwa sasa keshakua mtu wa kujificha ficha kwani keshazoea yale masharti na kayatamani yaendelee vile vile...
"ndani kuna joto mume wangu, tukae hapa nje"
Aliongea maimuna huku baadhi ya wanaume wakitoa macho kwani muna ni mwanamke mrembo sana, wakijua ni mwanamke wa kawaida tu
Surian alikubali kukaa pale nje lakini hajapenda kabisa kukaa hapo nje, kakaa kwa niaba ya mke wake tu,... Basi waliagiza vyuku vipsi na vitu vingi hususan vinywaji safi,... Midomo yao ilianza kuchangamka, lakini ghafla ilisikika sauti ikisema
"jamani, ona ule sio mzimu wa surian ule?"
Aliongea dada mmoja ambaye ni mpita njia eneo hilo,.. Lakini muna aliisikia hio sauti peke yake....
"heeeeee afu mbona ni surian kweli"
"wewe, sio surian, ule ni mzimu wa surian"
Walikuwa ni rafiki zake na asha, kama unawakumbuka hawa ndio wale kimbelembele waliomtangazia kuwa kamuua mdogo wake,.... Mara moja walipiga simu kwa asha...
Wakati huo asha ndio anatoka kiwandani baada ya kuonyeshwa kitengo ambacho kesho atakuja kufundishwa,...
"heeeeee we mnafiki mzanditi, leo unanipigia simu ya nini"
Aliongea asha akiwa hata getini hajatoka,
"asha Punguza jazba.... Wahi hapa Tanga Special Bites ujioneee"
"nijionee nini, mlivyo nitangazia mimi nimemuua mdogo wangu, mji mzima natengwa kwa ajili yenu..."
"sasa sikia, surian mdogo wako tunamuona hapa anakula kuku kwa mrija,... Yaani ni tajiri, sasa sijui ni mzimu"
"ati nini"
"mdogo wako.. Tunamuona hapa"
"wapi"
"hapa Tanga Bites"
Lakini wakati huo huo wakiongea, muna Aliweza kusikia kila neno kwani yeye anatumia hisia za asili ya pili ambayo ni jini,....
"ok nisubiri hapo hapo nakuja"
"chukua toyo jamani asha"
Wakati huo asha anatamani amtafute mama yake hapo kazini ili ampe habari hizi, lakini mbaya zaidi hajui mama anafanyia kazi upande gani hapo ndani,... Hivyo asha aliamua kuondoka lakini kazini keshasajiliwa tayari,...

Punde sii punde TANGA SPECIAL BITES asha anafika, kwa haraka haraka akawaona rafiki zake ambao ni fatuma, na amina...
"we Fatuma, haya yuko wapi surian mdogo wangu"
Aliongea asha huku akiwa na shauku ya kumuona ndugu yake, ingawaje mwanzoni alikuwa akimchukia kwakua kapendelewa elimu.. Wakati huo surian na mke wake wanakula vyuku kwa kwenda mbele na ila surian hajui kama kaonwa na rafiki zake asha...
"mdogo wako yule pale"








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2RNJwx2

No comments:

Post a Comment