Tuesday, December 3, 2019

WAUME SOMENI HAPA






`Sasa wewe mwanamume una mke mzuri wa sura na tabia na anaifuata dini yake vizuri anakutekelezea haki zako , michepuko au mpango wa kando ni wa nini? 

Ndani unakuwa kama shetani unacheka asubuhi mchana ushanuna, salaam kwa mkeo ya nadra unatoka kazini ukifika nyumbani huna tabasamu, huna salaam ya bashasha kwa mpenzi mkeo. 

kama mmepata watoto ndio linageuka jina lake mama khadija, au mama Ali hee huoni haya ulipokuwa unamfukuzia mwanzo wa ndoa ulikuwa unamwita nani? ile sweetie, my love. honey baby imeishia wapi? 

Kama hamna mtoto ndio unamkata jina hata mbele za watu wee Saida, Salima, Maimuna n.k kama mtoto mdogo heshima na thamani yake iko wapi ukimwita mke wangu utapungukiwa nini? 

Humtimizii mkeo mahitaji, humrembi ukafurahia urembo wake huna habari na bajeti ya vipodozi ni bora ukahonge mchepuko/mpango wa kando elfu mbili akasuke wakati mkeo hata mia moja ya kusukia inakushinda kumpa. 

Mchepuko/mpango wa kando unampeleka out kwenye hotel nzuri mnamaliza elfu kadhaa mkeo nyumbani dagaa na mchicha havina mwanzo wala mwisho wa mwezi, na hizo hotel hujawahi mpeleka tangu umemuoa. 

Kurudi kwako usiku wa manane kila siku trafic jam nzima zinakukuta wewe tuu, siku akikuona mapema ujue huna hela. 

Hata siku ya weekend ambapo ni muda mzuri wa kukaa na mkeo naye akadeka kidogo kwa mumewe ndio kwanza utapanga safari zisizo kuwa na msingi akikuuliza unamwambia wacha ukatafute hela atakula nini. heee alifuata kula kwako?

Na siku utakayojaaliwa kuwa nyumbani ni mazogo yasio na sababu ili mradi karaha mtindo mmoja mpaka mkeo anaomba Mungu upigiwe simu uondoke looh. 

Siku utakayoamua kumpa mapenzi ndio kabisaaa maana huna raha unamkamata mwanamke kama unagombana nae kumtomasa kama unakanda ngano akitoka hapo hoi hana kiungo kisicho maumivu. 

Ulimuolea nini? Ukahangaika kwenda kumposa, ukachukua namba za simu ukapanga mipango ikapangika ulimaliza soli za viatu ukampa ahadi zingine hazitekelezeki, mpaka ukamtoa kwao kwa vigele gele hiyo michepuko yako ilikuwa wapi? 

Kila siku kumtoa hila mkeo kama wewe umekamilika vile kosa dogo kwako kubwa siku hiyo utasema usiku kucha mkeo halali masikini anaishia kulia tuu kaomba msamaha huelewi ndio kwanza kakutia funguo ya kashfa, matusi ya reja reja. 

Ukweli wanawake wengi sana wanaishi kwenye ndoa si kwa mapenzi bali labda kwa ajili ya watoto, mali wamechuma wote sasa anaona akiondoka ataenda kuanzaje maisha, wengine mashinikizo ya wazazi, wengine wanaionea aibu jamii kuwa wataonekana wameshindwa ndoa zao 

Badilika ndoa yataka malezi 



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2Rhp2Nj

No comments:

Post a Comment