Sunday, December 22, 2019

SMULIZI MPYA: HOUSEGIRL WA KITANGA 02





SMULIZI MPYA: HOUSEGIRL WA KITANGA
MTUNZI : KIZARO MWAKOBA

SEHEMU YA 2

ILIPOISHIA
Tulipofika nje ya geti la Ubungo tuliingia kwenye Pajero moja kali sana ya rangi nyekundu ambayo ndiyo alikuwa amekuja nayo mama yule. Niliingia kwenye gari ile huku nikishangaa shangaa. “Ama kweli mjini raha” Nikajiambia ndani ya moyo wangu baada ya kuona msururu mrefu wa magari yaliyokuwa kwenye foleni pale kwenye mataa ya Ubungo. Majumba marefu na wingi wa watu vilinifanya nigundue utofauti uliokuwepo kati ya kijijini kwetu Tanganyika na pale jijini Dar es salaam.
 Mama yule aliendesha gari lake kwa kunyata na kulibembeleza. Jamani nyie mjini kutamu, kijijini kwetu havikuwepo vitu kama vile. Kama nisingekwenda mjini mambo yale ningeyaonea wapi? Unadhani ningepanda lini gari kama lile la Bi.Fatma? Siwaongopei jamani mjini kuzuri, sio kama kwetu kijijini ambako nilikuwa nimezoea kuona ngedere na ndege. Mjini ni magari, mataa ya barabarani, na majumba marefu marefu hadi mbinguni. “Ooh Mama Kibo ubarikiwe sana, bila ya wewe nisingefika huku Ulaya” nilizungumza mwenyewe kimoyomoyo huku nikizunguusha macho kutazama majumba marefu.
****
ENDELEA…..
Bi.Fatma alikuwa ni mwanamke wa makamo aliyekuwa ameolewa na mfanya biashara mmoja maarufu pale jijini Dar es salaam aliyekuwa akifahamika kwa jina la Sekiza. Mwanaume huyo alikuwa anamiliki maduka makubwa ya nguo na viatu yaliyokuwa mjini kariakoo na mengine Mwenge. Yeye Bi.Fatma alikuwa akiuza moja ya maduka hayo ambalo lilikuwepo Kariakoo.
Bi.Fatma na mume wake walibahatika kupata watoto wawili wa kiume amabao walikuwa ni Imran na Fadhili. Imran ambaye alikuwa ni wa kwanza kuzaliwa alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni moja iliyokuwa ikijishughulisha na kudizaini matangazo na nembo za mashirika mbalimbali iliyokuwa ikifahamika kwa jina la KMC. Kampuni hiyo ilikuwa ikipatikana maeneo ya Posta mpya.
Fadhili ambaye alikuwa ni mdogo kwa Imran yeye alikuwa akiuza kwenye duka la viatu la baba yake lililokuwa maeneo ya Mwenge. Kijana huyu alipomaliza elimu yake ya chuo kikuu baba yake Mzee Sekiza akamkabidhi duka lile la viatu kusimamia. Kwa maana hiyo hakuwa na shida ya kuajiriwa mahali kokote kwasababu baba yake alikuwa akimlipa vizuri kuliko sehemu ambayo angekwenda kuajiriwa na watu ama mashirika mengine.
Familia hiyo ya Bi.Fatma na Sekiza ilikuwa ikiishi maeneo ya Mabibo karibu kabisa na sehemu ilipo hosteli ya Mabibo ambako wanaishi wanafunzi wanaosoma chuo kikuu cha Dar es salaam na DUCE. Pembeni ya nyumba yao walikuwa na fremu ambayo walimpangisha mwanamke mmoja wa kinyakyusa ambaye alifungua biashara ya kuuza chakula kwa wanafunzi waliokuwa wakiishikwenye hosteli hizo za Mabibo.
****
Utofauti uliokuwepo kati ya maisha ya kijijini na maisha ya mjini haukunisumbua sana awali kwasababu wakati wote nilikuwa ni mtu wa ndani ya geti. Sikuwa nimepata mwanya wa kutoka mbali na nyumbani. Mara nyingi nilipokuwa nikimaliza kufanya kazi zangu za mchana nilikaa sebleni kutazama runinga na nilipojihisi kuchoka niliingia chumbani kulala hadi jioni ambako niliamka na kuanza kufanya shughuli za jioni kama vile kuandaa chakula cha usiku.
Mara nyingi Fadhili yule aliyekuwa anauza duka la baba yake alikuwa akirejea nyumbani kula chakula cha mchana kisha anarejea tena dukani. Kwa kiasi fula nilijikuta nikifarijika na kuzoeana na kijana yule kuliko mtu mwingine yeyote pale ndani. 
Umbo la Fadhiri lilikuwa ni dogodogo lililomfanya kuonekana kuwa na umri ambao ulikuwa unakaribiana kabisa na umri wakwangu mimi. Lakini hali halisi alikuwa amenizidi kama miaka mitano hivi. 
Nilikuwa nikimpenda sana Fadhili kwasababu alikuwa ni kijana mstaarabu, mcheshi na mwenye heshima kwa kila mtu utafikiri alikuwa amekulia kijijini. Zaidi ya hivyo Fadhili alikuwa ni kijana mwenye muonekano mzuri ambaye alikuwa anapendeza sana akivaa nguo zake. Nisiongee sana jamani kusema kweli Fadhili alikuwa ameukosha mtima wangu. Najua utanishangaa ndugu msomaji kwasababu ilikuwa ni mapema mno, lakini sikuwa na kosa lolote kwani hata mimi ni binadamu na nina moyopia.
“Tumuuu!” Ilikuwa sauti ya Fadhili ikiniita nilipokuwa nimejipumzisha chumbani kwangu. Nilihisi moyo wangu ukipiga paaa! kutokana na hisia nilizokuwa nazo juu ya kijana yule ambaye sidhani kama alikuwa anafahamu lolote juu ya mawazo yangu.
“Abee” nikaitika kwa sauti ya kutoka usingizini huku nikijiinua kutoka pale kitandani. Nilichukua khanga na kujifunga kiunoni na nyingine nikajitanda kichwani kama ambavyo nilikuwa nimezoea kuvaa kule kijijini kwetu Tanga. Nguo zangu nyingi zilikuwa ni magauni marefu na khanga. Hivyo ndivyo nilivyokuwa nimefunzwa kuvaa kule Tanganyika kwetu.
Nilipotoka nikamkuta Fadhili amekaa kwenye kochi huku macho yake yakitazama kwenye mlango wa chumba nilichokuwa nimelala. Niliinamisha shingo chini kukwepa kukutanisha macho yangu na yake.
“Vipi dada ulikuwa umelala nini?” alihoji Fadhili
“Hapana kaka Fadhili sikuwa nimelala usingizi”
“Vipi umenisubiri sana enh?”
“Nimekusubiri hadi nikajiwa na usingizi”
“Dukani leo kulikuwa na wateja wengi sana, ndomaana nimechelewa” Fadhili alizungumza huku akiinuka kutoka kwenye kochi na kuelekea kulipokuwa na meza ya chakula. 
“Sawa hamna shida” nilimjibu
“Vipi wewe umeshakula”
“Bado” nilijibu huku nikichezea vidole vya mikono yangu.
“Kwanini sasa ukae hadi saa hizi bila kula?” Fadhili alihoji huku nakinitazama na mkono wake wa kulia ukiwa umeshikilia kiti cha mezani pasipo kukivuta wala kukisukuma.
“Jamani kaka Fadhili mwenzio sijazoea kula pekeyangu” nilimjibu huku nikitoa tabasamu lililofanya ule mwanya wangu mdogo kuonekana.
“Haya njoo tule huko na mwanya wako” alinambia huku akivuta kiti. 
Maneno yake yale yalinifanya kutoa kicheko kidogo ambacho kilimfanya naye kucheka pasipo na sababu ya msingi. Nilivuta kiti kilichokuwa mbele yake tukawa tumegeukiana yaani nikiinua macho namuona usoni. Alipakuwa chakula kwenye sahani yake kisha akanipa na mimi kijiko.
 “Haya tuendelee” alinambia huku akifunua hotipoti iliyokuwa na mboga.
Nilichukua kile kijiko cha chakula na kujipimia kiasi ambacho kilikuwa kinanitosha. Fadhili akanisogezea hotipoti iliyokuwa na mboga. Nikasogea na kupakua mboga kwenye sahani yangu ya chakula.
 “Haya Bismillah” Fadhili alisema na kuanza kula msosi ule niliokuwa nimeupika mimi.
 “Mnh!” nikamsikia akiguna alipokuwa anameza chakula.
 “Vipi kaka Fadhili?” nikahoji kwa wasiwasi nikiamini chakula hakikuwa kizuri.
 “Mambo ya kitanga haya” alisema huku akitafuna chakula.
 “Yepi tena kaka fadhili?”
 “Madikodiko” alisema huku akimeza chakula alichokuwa anatafuna.
 “Jamani kaka Fadhili wewe, mbona cha kawaida tu” nilizungumza huku nikinyonganyonga shingo yangu huku nikigonganisha gonganisha mapaja yangu pamoja. Midomo yangu niliing’ata na yale macho yangu malegevu nikayarembua.
 “Vipi mbona hauli sasa?”
 “Nala” nilijibu kwa lafudhi yangu ya kitanga.
 “Wala enh?” Fadhili akanitania kwa ile lafudhi yangu.
 “Halafu we Kaka Fadhili wanchokoza hivyo” nilizungumza huku nikitazama chini kwa aibu. 
 “Wala sikuchokozi mwaya enh! wenyewe twajilia madikodiko ya kitanga” Fadhili alizidi kuleta masihara huku nayeye akiwa ameinamisha shingo yake upande kama nilivyokuwa nikifanya mimi. Nikaangua kicheko ambacho kilikuwa kimejawa na aibu lukuki. Fadhili naye akacheka kwa kujilazimisha.
 “Kula bwana mdogo wangu mi nakutania” Fadhili alizungumza huku akisogeza karibu sahani yake ya msosi na kukupiga vijiko viwili vya haraka. 
Sikuwa nimefurahishwa na kauli yake ile ya kuniita mdogo wake. Nilihisi kama vile kulikuwa na kitu alichokuwa anataka kuninyima. Nilipenda sana aniite kwa jina langu.
Nikawa nimeinamia kwenye sahani yangu ya chakula huku nikimtupia jicho moja moja la wizi. kumbe na yeye alikuwa akifanya vile vile. Mara kadhaa tulikutanisha macho yetu na kutabasamu.
****
Kitendo cha kushinda nyumbani pekeyangu hakikuwa kinamfurahisha mama. Yaani Bi.Fatma. Asubuhi moja alipokuwa anataka kutoka kuelekea kazini aliniita.
 “Hivi Tumu huwa unajisikiaje unaposhinda peke yako hapa nyumbani?” alihoji mama yule kwa sauti ya upendo.
 “Kawaida tu mama huwa nikimaliza kazi nalala” 
 “He! kwahiyo unachokifahamu wewe ni kazi na kulala tu?”
 ‘Ndio mama mbona nimekwisha zoea” nilizungumza kwa kujiamini.
 “Hapana usifanye hivyo. Kama ukiwa umemaliza kazi zako zote, unaweza kwenda hapo mgahawani kwa mama Bupe kujichangamsha, sio unajifungia ndani tu kama utumbo” alisema mama kwa msisitizo.
 “Lakini mama mie nimekwisha zoea” nilijaribu kumueleza mama kwasababu huko alikokuwa ananiambia kwenda kukaa na kuzungumza nilikuwa sikuzoeana na mtu hata mmoja. Halafu ningezungumza nao kitu gani? wao ni watu wa mjini na mimi nilikuwa mtu wa kijijini. Hizo stori zingekwenda vipi. Kwa kigezo hicho sikuona sababu ya kwenda huko mgahawani kukaa na kupiga soga.
 “Sasa mwanangu utakaeje ndani tu kama utumbo? toka nje angalau uoshe macho” mama alizungumza kwa upole. 
Kwa kiasi fulani niliuona umuhimu wa maneno ya mama lakini kikwazo changu kikabakia pale pale. Nitakwenda kuanza vipi kuzungumza na hao wauza mgahawa waliopangisha flemu pale nyumbani. Hata hivyo nikaona hakukuwa na sababu ya kumbishia mama ingawa sikuwa nategemea kufanya vile alivyokuwa amenishauri.
 “Sawa mama nimekuelewa” nilisema kwa upole.
 “Haya mie natoka ila leo nitakuja na mgeni, usichelewe kuandaa chakula cha jioni” alizungumza Bi.Fatma kwa msisitizo.
 “Sawa mama” nilijibu na kwenda kufungua geti.
Mama aliingia kwenye gari yake na kuiwasha, Alitoka kinyumenyume hadi nje ambako aligeuza na kuiweka barabarani tayari kwa kuondoka.
 “Haya Mwanangu” mama aliniaga
 “Sawa mama kazi njema” nilimjibu na kuanza kusukuma geti kulifunga huku mama naye akiondoa gari kutoweka katika mazingira ya nyumbani. Nilipomaliza kufunga geti niligeuka nyuma ili kuelekea ndani kuendelea na kazi. Nilimkuta kaka Imran amesimama hatua chache kutokea pale nilipokuwa nimesimama mimi. Kusema ukweli kaka Imran sikuwa nimemzoea kama ambavyo nilikuwa nimemzoea Fadhili. Nilikuwa nahofia hata kukutana naye kama tulivyokuwa tumekutana siku hiyo.
 “Hee kumbe nawewe unatoka?” nilihoji haraka haraka ilimradi nimpite.
 “Bado kidogo, nilikuwa nakutafuta wewe”
 “Mimi?” nilihoji kwa wasiwasi.
 “Ndio wewe”
 “Sawa” nilijibu huku nikimsikiliza kwa makini nikiwa na hamu kubwa ya kutaka kufahamu kile alichokuwa ameniitia.
 “Njoo ndani” kaka Imran aalizungumza na kugeuka kuingia ndani, nami nikamfuata nyuma huku nikiwa na wasiwasi tele ndani ya moyo wangu. Aliingia chumbani kwake na kuniambia nimsubiri sebleni. Baada ya dakika kadhaa alitoka akiwa ameshikilia mfuko wa Rambo mkononi.
 “Chukua hii ni zawadi yako” alisema kaka Imran huku akinikabidhi kale kamfuko ka rambo.
 “Yakwangu mimi?” nilihoji kwa kuhamaki.
 “Ndiyo mdogo wangu nimekuletea wewe”
“Ahsante sana kaka Imrani” nilipokea mfuko ule huku nikihisi furaha ndani ya moyo wangu ingawa nilikuwa bado sikufahamu kilichokuwemo ndani yake. 
“Usijali mdogo wangu” alisema kaka Imran na kutoka nje akiwa ameningi’niza funguo ya gari mkononi. Aliingia kwenye gari yake na kuiwasha kisha akapiga honi. Nilitoka na kwenda kumfungulia geti. Alitoa gari polepole na alipofika katikati ya geti akasimama na kuninyooshea mkono kuniaga. Huku nikiwa nimejawa na furaha kutokana na zawadi niliyokuwa nimeletewa namimi nilimnyooshea mkono kumuaga.
Nilifunga geti na kwenda ndani mbio. Nilichukua kale kamfuko nilikokuwa nimepewa na kuingia nako chumbani kwangu. Harakaharaka nilikafungua kwa hamasa kubwa. Nikakutana na nguo zimekunjwa pamoja. Furaha niliyokuwa nayo iliongezeka zaidi na kuanza kukunjua mojamoja ili kuzithaminisha. Kwanza kabisa mikono yangu ilikunjua nguo za ndani ambazo zilikuwa mbili. Nilifurahi sana nilipoziona nguo zile na sikuwa na hata chembe ya wasiwasi juu ya kitendo kama kile. Niliona ni jambo la kawaida sana na kuhisi kaka Imran alikuwa ameninunulia nguo za aina ile kama mdogo wake tu na si vinginevyo. Nilipofungua nyingine ndipo nikajikuta nikichoka mwenyewe. Nilikunjua kisketi kimoja kilichokuwa kifupi kuliko maelezo sijui ndio kinaitwa kimini? Ah sikuwa na uhakikika lakini kilikuwa ni kifupi mno.
 “Mnh!”  nikaguna mwenyewe huku nikikigeuza geuza mbele na nyuma.
“Sasa kaka Imran anionaje! mie ni wa kutembea uchi kweli?” nilijiuliza mwenyewe pasipo kujipatia majibu. Nikaiweka kiunoni sketi ile ili kuipima. Nilipobaini ilikuwa inaishia kwenye magoti nikasonya na kuitupa kitandani kisha kwa haraka nikakunjua ile ya mwisho iliyokuwa imebakia.
“Eboo!” nikashangaa kwa lafudhi ya kitanga baada ya kuikunjua na kuiona nguo yenyewe. Nguo ile ilikuwa ni blauzi ambayo ilikuwa na mikanda iliyopita kwenye mabega na kwa huku nyuma kulikuwa na uwazi wa kuonesha mgongo. Furaha yote ya kuletewa zawadi ikatumbukia nyongo. Nilihisi kama vile kaka Imran alikuwa amenidhalilisha kwa kuninunulia vinguo vya ajabu ajabu. Ile blauzi nayo nikaitupa kitandani kisha nikazisogelea zile nguo mbili za ndani na kuzishika tena. Niliachia tabasamu la matumaini kwasababu nguo nilizoziona zinaweza kunifaa ni zile tu. Lakini zile nyingine sikuzifagilia hata chembe.
 “Hapa amepatia’ nilisema huku nikiikunjua nguo moja ya ndani kwa vidole vya mikono yangu kuithaminisha. Kwa mbele kulikuwa na viua vitatu vyekundu vilivyoendana sawia kabisa na ile rangi ya pinki ya nguo yenyewe.
 “Hodiii” nilisikia sauti ya mtu kutokea nje ikibisha hodi.
 “Karibuu” niliitika na kutoka nje haraka.
Nilifungua geti dogo na kumkuta BUPE yule mama wa kinyakyusa aliyekuwa akifanya biashara ya mgahawa kwenye fremu ya pale nyumbani.
 “Karibu” nilimkaribisha mara tu nilipofungua geti.
 “Aksante, hujambo wewe?”
 “Sijambo shikamoo”
 “Naomba uniazime chaja ya nokia” alisema mama yule.
Sikutegemea kama shida yake ingekuwa ni kuazima chaja ya simu. Nilitulia kidogo kama vile nikitafakari jibu la kumpa.
 “Usiwe na wasiwasi binti, huwa ninaazima” alijieleza mama yule. Nilimtazama kwa sekunde kadhaa huku nikitafakari nitoe ama nisitoe. Sikuwa nimepewa ruhusa ya kuazimisha vitu vya mule ndani. hata hivyo nikakumbuka mama alipoondoka alinitaka niende kukaa kwa mama yule, hivyo nikaona isingekuwa vibaya kumpatia.
 “Ngoja niangalie kama ipo” nilisema huku nikiingia ndani.
 “Ipo bwana, kila siku nakuja kuazima” alisema Bupe kwa kujiamini.
Kwa bahati nzuri nilifanikiwa kuiona chaja ile pale sebleni. Niliichomoa na kuja kumkabidhi.
 “Ahsante binti”
 “Haina shida” 
 “Kumbe unaitwa nani vile?” alihoji mama yule huku akinichekea chekea
 “Mwantumu au Tumu” nilijibu.
 “Unatokea wapi?”
 “Tanganyika” nilijibu kwa kifupi.
Jibu langu lilionekana kumchanganya mama Yule. Akatulia kwa sekunde kadhaa huku machp yake akiwa ameyakazia aldhini. Alipoinuka akahoji tena.
 “Tanganyika ndio wapi?”
 “Kijiji chetu kinaitwa Tanganyika”
 “Ni mkoa gani?” Mama Yule wa kinyakyusa alizidi kuhoji maswali ambayo nikahisi yakianza kunikera.
 “Tanga” Nikajibu kwa ufupi.
 “Mnh! kwahiyo wewe ni binti wa kitanga?” alihoji mama yule huku akitabasamu. 
Sikumjibu kitu zaidi ya kucheka tu huku nikiwa nimeinamia chini kwa aibu.
 “Watokea Tanga mapenzi yaliko zaliwa, inabidi uje unipe somo na mimi niwe fundi” Bupe alizungumza na kuondoka huku akicheka cheka kama mwehu. Wala hakuwa amenifurahisha na vile vineno vyake vya ajabu ajabu. Heti natokea Tanga mapenzi yaliko zaliwa. Mara Ooh nije namimi unipe somo niwe fundi, Kwani mimi ndio somo wa mapenzi? Mtu mzima Hovyoo!” Nilizungumza pekeyangu huku nikifunga geti.
ITAENDELEA


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2QistS2

No comments:

Post a Comment