Saturday, February 1, 2020
LUGHA IPI YA MAPENZI INAYOKUFAA? NA MWENZA WAKO JE?
Utajuaje Lugha ya mapenzi inayomfaa mwenza wako? Kila mtu hupendelea kitu tofauti.
Moja ya furaha ambayo nilikuwa nikiitafuta maishani, ni kwamba mimi sio kama watu wote wanavyofikiri. Nilikuwa nikijua kuwa mimi ni zaidi ya watu wengine, na ni chini ya wengine kuliko ninavyofikiri.
Nilikuwa napigania kutoka mahali fulani ili nifike ninakotamani kufika. Nikatambua kuwa wapo watu wengi wanafikiri kama mimi. Wanahangaika kuliko mimi. lakini sikujua jinsi gani kila mtu anajitafuta mwenyewe.
Kwa upande mwingine . ni rahisi kufikiri kuwa watu wako kama mimi lakini sio, mpaka hapo nilipoelewa.
Aina Tano Za Lugha za Mapenzi.
Watu huonyesha mapenzi kwa njia mbalimbali, kila mtu na njia yake, na watu hujisikia kupenda na kupendwa kwa njia tofauti tofauti. Mtu yeyote anaweza kujisikia kupendwa pale tu mtu anapoonyesha lugha yake ya mapenzi. kama mapenzi yanaelezea lugha tofauti, Kwa hio Upendo wa kweli haujawahi
Lugha hizi ni …
Ukiri wa Maneno
Thamani Ya Muda na Nafasi
Kupokea Zawadi
Mguso wa mwili.
Kama mmoja anapenda na kujisikia kuhudumiwa vizuri na mwingine anapenda kupewa Muda tu , basi kutakuwa na shida mahali.
Ni vizuri kufahamu mwenza wako anapenda lugha ipi ya mapenzi, vinginevyo hata kama ukaonyesha kiwango kikubwa cha upendo kama hujagusa anachohitaji ni kazi bure, hawezi kujisikia kupendwa.
Unawezaje kujua lugha ya mpenzi wako? Jiulize swali Kitu gani mwenza wako huwa analalamikia? Anathamini nini? hamtumii muda kwa pamoja , hamtembei pamoja. kama mwenza anapenda zawadi kubwa halafu wewe kila siku unapeleka pipi, hamtaelewana.
Jiulize utawezaje kuonyesha upendo wako? lakini pia ni kitu gani kinampa mwenza wangu furaha? lazima ukielezee unachokipenda ili mwenzako akijue.
Mwingine anaweza kusema kwake yeye lugha ya mapenzi huja yenyewe, sihitaji mguso wala kutumia pesa ili kupata zawadi, kwa jinsi hio lugha yako haitaeleweka.
Jaribu aina zote tano ili ujitambue uko kwenye ipi.
Kutafuta maarifa ni kutafuta Furaha. na ninafikiri njia hii itasaidia mahusiano kupona kwa haraka. Kila mtu ajifahamu mwenyewe vizuri, na mwenza wake, na hata nje ya mapenzi.
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2Uib5Ai
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment