Tuesday, February 4, 2020

KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA NNE (4)







Maisha ya Magosho na mdogo wake yalizidi kuwa magumu kila kulipo kucha. Wote wawili walikuwa wakiishi kwenye chumba kimoja kwasababu nyumba yao walikuwa wameiuza ili wapate pesa za kumtibia mama yao. Pesa zote za mradi wa vitumbua na mihogo nazo walizitumia kule kwa mganga Kutuzo kumuagua mama yao jini maiti.
Mtu aliyekuwa akitegemewa na familia ile ya watu wawili alikuwa ni Magosho. Ilimbidi kufanya juu chini kuhakikisha mdogo wake anakula, anavaa, na kulala. Hakuwa tayari kumuona dada yake huyo mpendwa akilala na njaa kitu ambacho pengine kingesababisha kumkumbuka mama yao mara kwa mara.
ENDELEA….4
Magosho alifanikiwa kupata pesa na kumpa mdogo wake kufungua mtaji mdogo wa kukaanga mihogo. Na yeye mwenyewe aliweza kupata mtaji wa kuuza maji ya pakti. Maji ambayo alikuwa akiyachota mtoni na kuyafunga kwenye vikaratasi vya nailoni baada ya kuyachemsha. Alipeleka kwenye jokofu la mtu ambalo alikuwa analipia kiasi fulani cha pesa. Kwa kiasi waliweza kuendesha maisha yao wenyewe.
Mungu hamtupi mja wake, Magosho alipata kibarua cha kufanya kazi za ndani maeneo ya Kariakoo nyumbani kwa mhindi mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jila na NAKESHIWAR. Kitendo kile Magosho na mdogo wake walikiona kama vile ilikuwa ni bahati kubwa sana kwao. Hivyo Magosho akawa anatokatoka nyumbani asubuhi na kurejea jioni.
Maisha ya Magosho yalikuwa ni tofauti kabisa na yale ya awali alipofariki mama yao. Kutokana na mshahara ambao alikuwa akilipwa ingawa haukuwa mkubwa lakini aliweza kupanga chumba kingine karibu na nyumbani kwao ambacho aliishi mdogo wake. Pia aliweza kufufua mtaji wa kuchoma vitumbua na kukaanga mihogo ambao alikuwa akijishughulisha mama yao enzi za uhai wake.
* * *
Nakeshiwar alikuwa ni baba wa watoto wawili yaani RACHNA  na VASHAL. Rachna alikuwa ni binti wa kwanza wa mzee Nakeshwar ambaye kwa wakati ule yeye alikuwa nchini India kimasomo. Kwahiyo nyumbani pale walikuwepo Nakeshiwar mkewake Bi.Fahreen, pamoja na kijana wao mdogo wa kiume ambaye ni Vashal.
Shughuli za Nakeshiwar zilikuwa ni za kusafiri mara kwa mara kibiashara. Hivyo mara nyingi nyumbani pale alikuwa akisalia Magosho na bosi wake wa kike Bi.Fahreen, na Vashal akitoka shule wanakuwa watatu.Wafanya kazi wengine walikuwa wakijishughulisha na kazi za nje zaidi, hivyo walihesabika kama vile hawakuwepo.
Siku moja jioni baada ya kumaliza kazi Magosho alikuwa akijiandaa kuondoka kurudi nyumbani. Ghafla akasikia sauti ya Bi. Fahreen ikimuita hatua chache kutokea pale alipokuwa.
“Gosoo” aliita Bi Fahree kwa lafudhi yake ya kihindi.
“Naam mama” Magosho aliitikia kwa heshima.
“Sasa veve nenda rudi, nenda rudi kila siku, hapana choka?”
“Nimesha zoea mama”
“Mimi taka veve kae hapa hapa, harafu ongezea sahara. Au nanaje veve?” alihoji bi Fahreen huku akiwa ameshika kiuno akimtazama Magosho.
Neno kuongezewa mshahara ndilo alilolisikia zaidi Magosho. Akavuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu. Alikuwa akitamani sana bahati kama ile, na hatimaye aliiona ikimjia yenyewe. Akawaza kama yeye angeongezewa mshahara basi mdogo wake angeishi Maisha mazuri kidogo. Lakini kikwazo ni kwamba angewezaje kumuacha mdogowake na kuishi mbali naye?
“Sawa mama lakini nipe muda nifikirie” Magosho akajifanya kuomba muda.
“Hapana fikiria Goso, mimi ongeza mara mbili tena na tena” alisema Bi.Fahreen akizidi kuongeza dau kumshawishi Magosho kukubaliana na lile alilokuwa akilitaka yeye.
Magosho alikuwa tayari kufanya kama vile alivyokuwa anataka yule bosi wake mwanamke, tatizo ni kwamba hakuwa tayari kuishi mbali na mdogo wake kipenzi Ashura. Hata hivyo Magosho alipanga kwenda kuzungumza na dada yake kwanza, kama asingekubali basi asingemkubalia Bi.Fahreen.
* * *
Ilikuwa ni furaha kubwa kwa Ashura kusikia kuwa kaka yake alikuwa anatakiwa kuongezewa mshahara. Hakuwa na kipingamizi chochote juu ya uamuzi wa tajiri wa ndugu yake huyo wa kuhamia nyumbani kwa Nakeshiwar. Ashura alipiga magoti na kumshukuru muumba.
Magosho akahamia nyumbani kwa Muhindi huyo na kumuacha dada yake pale nyumbani pekeyake. Kwa kiasi fulani aliumia sana kuwa mbali na ndugu yake lakini hali ya maisha ilimsukuma kufanya vile.
Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwa Bi.Fahreen kwa kitendo cha Magosho kukubali kuhamia nyumban pale. Alimhakikishia kumuongezea mshahara mara tatu ya ule aliokuwa akimpatia awali kama ambavyo alimuahidi.
Waswahili wanasema usilo lijua ni sawa na usiku wa giza. Uamuzi aliouchukua Bi.Fahreen ulikuwa na madhumuni yake ambayo aliyafahamu pekeyake.
Ilikuwa ni mchana wa majira ya saa saba. Baada ya kuandaa chakula Magosho alijiandaa tayari kwa kumfuata mtoto Shuleni. Ilikuwa ni kawaida yake kwenda shuleni kwa Vashal kumchukua kila ilipotimia mida ya kumaliza masomo. Kwakuwa Magosho hakuwa anajua kuendesha gari, dereva wa nyumbani pale alimsindikiza.
“Mama mimi namfuata Vashal” alisema Magosho.
“Ngoja tuongozane” alisema Bi.Fahreen huku akiingia chumbani kwake.
Baada ya dakika kadhaa mama wa kihindi alitoka akiwa amependeza. Kama kawaida yake alikuwa amejipulizia manukato ya mazuri nay a gharama kubwa. Kwakweli mama yule alikuwa amependeza sana, sijui enzi za usichana wake alikuwaje kwasababu hapo alipo alikuwa anavutia utadhania ni binti wa miaka ishirini na mbili hivi.
“Haya tende zetu Goso” alisema Bi.Fahreen na kutangulia mbele.
Magosho alimfuata nyuma mwanamke yule pasipo kuzungumza kitu. Walipofika nje walimkuta dereva amesimama pembeni ya gari akimsubiri Magosho wamfuate mtoto Vashal. Bi.Fahreen alinyoosha mkono wake kuchukua funguo za gari kutoka kwa dereva yule pasipo kuzungumza neon lolote. Dereva naye hakuwa mbishi kwa bosi wake akamkabidhi funguo za gari.
Mama aliingia na kugeuza mwenyewe gari. Alisimamisha karibu na miguu ya Magosho akimpa ishara ya kuingia. Magosho alitaka kuingia mlango wa nyuma lakini mama yule akamwambia akae mbele. Pasipo kipingamizi chochote Magosho akaingia kwenye gari lile na safari ya kuelekea shuleni ikaanza.
Kitu ambacho kilimshangaza Magosho ni pale mama yule alipoacha njia ya shuleni na kupita barabara iliyokuwa ikielekea sehemu nyingine tofauti. Alitamani kuhoji lakini akawaza pengine mke wa bosi wake alikuwa anapitia sehemu fulani. Safari ilikomea kwenye barabara ya vumbi mbali kabisa na makazi ya watu. Mama alisimamisha gari na kumgeukia Magosho.
“Vipi toto zuri, iko sikiaje kuwa na mimi hapa leo?” alizungumza mwanamke yule wa kihindi.
“Kawaida tu mama. Lakini tunatakiwa kumuwahi Vashal, si unajua mida hii ndio anatoka shuleni?” alisema Magosho kwa upole.
“Mimi iko tambua hiyo. Kwani Veve taki jua endesa gari?” alihoji Bi.Fahreen huku mkono wake mmoja ameupitisha kwenye mabega ya Magosho ambaye alikuwa ameketi kwa wasiwasi. Si unajua tena ukiwa na bosi wako lazima heshima zote zionekane hata kama ni za kinafki.
“Napenda sana mama” Magosho alijibu kwa furaha.
“Sasa mimi fundisa veve leo. Iko furahi?” alihoji Bi.Fahreen huku akimpapasa Magosho kwenye mabega yake.
“Nashukuru sana mama” alijibu Magosho kwa furaha na hamasa kubwa.
Ndugu msomaji unaweza ukafikiri ni zali lilikuwa limemdondokea Magosho lakini ni mipango tu ya Mungu.
“Haya kuje kae huku” alisema Bi.Fahreen akimtaka Magosho akae pale alipokuwa amekaa yeye. Magosho alitaka kuteremka ili kuzunguuka lakini mama yule akamzuia na kumwambia wapishane mle mle ndani ya gari.
Kwakuwa Magosho hakuwa na chochote alicho kifahamu alikubali kupishana na mke wa bosi wake mle mle ndani ya gari.
Bi. Fahreen akasogea kwa Magosho huku akiwa amekaa na kuegemea kiti cha gari na kumwambia apite juu yake. Magosho akasimama huku ameinama kidogo kujizuia kugonga juu ya gari na kutaka kumvuka mke wa bosi wake. Alipofika kati kati yaani akiwa amempa mgongo Bi. Fahreen akajikuta akivutwa chini. Akawa ameketi juu ya mapaja ya mama yule wa kihindi. Magosho alishituka sana na kuhisi amefanya kosa kubwa sana, hivyo alitaka kuinuka kwa haraka kabla mama yule hajakasirika.
“Oh! Pole sana Goso” alizungumza mama yule wa kihindi.
“Samahani mama” alisema Magosho huku akijiinua kwa tahadhari.
“Hapana jali. Ila ngoja sije umiza mimi” alisema Bi.Fahreen akimzuia Magosho kuinuka kutoka kwenye mapaja yake akidai kuwa angeweza kumuumiza.
Mwanamke yule wa kihindi alipeleka mikono yake kwenye miguu ya kijana yule na kuanza kumpapasa taratiibu. Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakimuenda mbio kiasi ambacho Magosho aliweza kuyasikia kupitia mgongo wake ambao ulikuwa umelala kifuani kwa mama yule. Chuchu zake ambazo zilikuwa zimetuna zilisababisha msisimko kwenye mishipa yake ya damu na kusafiri hadi ubongoni.
“Tar…Tara…Taratibu Goso sije umiza mimi bhanaa” Bi.Fahreen alizungumza kwa taabu na sauti akiwa ameibadilisha kwa kuitolea puani.
Magosho akazidi kuogopa na kuhisi alikuwa anamuumiza mke wa bosi wake. Yeye alihisi Sauti ile ya mama ilitokana na maumivu ya kukaliwa. Magosho akajitahidi hadi kujinasua kutoka kwenye mapaja ya Bi.Fahreen.
Mama yule alibaki amelegea kwenye kiti huku akihema juu juu kama vile alikuwa ametoka kukimbia mbio za olimpiki mita mia tano. Magosho akamtazama na kumuonea huruma mke wa bosi wake. Akaamini kwa asilimia miamoja kuwa kibarua chake kilikuwa njiani kuota nyasi.
“Samahani sana mama” Magosho alizungumza kwa unyenyekevu huku akiwa ameketi kwenye kiti cha jirani na kile alichokuwa amekikalia Bi. Fahreen.
Mama yule wa kihindi aligeuza shingo na kumtazama Magosho kwa jicho lililokuwa limelegea utafikiri alikuwa anataka kukata roho jambo ambalo lilizidi kumtisha Kijana wa watu. Kusema ukweli kilichomfanya kuwa na hali mbaya sio kwasababu heti alikuwa ameumizwa na Magosho, bali ni hisia zake za kimwili dhidi ya mtoto wa watu ndizo zilizokuwa zikimchanganya.
“Vipi mama mbona hivyo?” Magosho alihoji huku akisogelea kiti cha Bi.Fahreen. Pumzi yake ikamfikia mama yule wa kihindi na kuifanya hali ya mwanamke wawatu kuzidi kuwa mbaya.
ITAENDELEA





from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/3974KMg

No comments:

Post a Comment