Tuesday, February 4, 2020

KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA 12





ILIPOISHIA
Mansoor alijikuta akipandwa na hasira dhidi ya viumbe wale wawili waliokuwa wakifanya usafi kule kwenye maua. Alikuwa akihisi kama vile mke wake ndiye aliyekuwa fanya utumbo ule. Akasimama kwa hasira huku akitoa simu yake mfukoni na kuvuta namba za Mr. Nakeshwar.
“Kama noma na iwe noma ngoja leo tukomeshe uchafu huu” alizungumza Mansoor huku akibonyeza namba za Mr. Nakeshwar.

ENDELE…
Sijui tuseme ilikuwa ni bahati mbaya au ni bahati nzuri maana Mansoor alipiga simu ya Nakeshwar lakini haikupatikana.
“Vipi hapatikani?” alihoji mlinzi wa getini kwa hamasa kubwa.
Mansoor hakuta jibu lolote zaidi ya kusonya na kupiga kwa mara nyingine. Hata hivyo majiu yalikuwa ni yaleyale simu ya Mr. Nakeshwar haikuwa inapatikana.
“Shida ya huyu bwana ndiyo hii ya kupenda kuzima simu” alizungumza Mansor huku akionekana kukasirika zaidi.
“Kwahiyo utafanya nini sasa?” mzee yule mlinzi alihoji.
“Ngoja nikawashikishe adabu mimi mwenyewe” Alizungumza Mansoor kwa hasira huku akivuta hatua kuelekea kule bustanini kulipokuwa na purukushani za Magosho na Bi. Fahreen. Hata hivyo yule mlinzi alimuwahi na kumdaka mkono kumuomba amsikilize.
“Sikiliza baba nikwambie kitu” alizungumza mzee yule kwa sauti ya chini.
“Mzee mimi nakwenda kuwaua wale kunguni” Mansoor alizungumza kwa hasira huku akitetemeka utafikiri Bi. Fahreen alikuwa ni mke wake.
“Sikiliza baba, haya mambo hayataki haraka mwanangu” alisema mlinzi.
“Mzee huyu mama anatutia aibu, ni nani asiyefahamu ukaribu wangu na Mr. Nakeshwar?” alizungumza Mansoor.
“Ni kweli baba, lakini tafadhali usipende kufanya maamuzi wakati una hasira”
“Nisifanye maamuzi wakati bosi wangu anaibiwa huku nikishuhudia?”
“Ni kweli baba, hata mimi sipendezwi na tabia ya mwanamke huyu, lakini…”
“Lakini nini, au na wewe unashirikiana na yule kijana?” alihoji kwa jazba Mansoor.
“Aaaah huko sasa siko kijana wangu” mzee yule akazungumza kwa kuhamaki baada ya kusikia kauli ile kutoka kwa Mansoor.
“Kama kweli haushirikiani nao, niachie nikaliwashe” alizungumza Mansoor huku akijaribu kuvuta mkono wake uliokuwa umekamatwa vyema na mzee yule.
“Tafadhali sikiliza Busara zangu zitakusaidia kufanya maamuzi yenye hekima” mzee yule mlinzi alizungumza kwa kusihi.
Maneno yale ya babu mlinzi yaliyokuwa na kauli za hekima na busara ndani yake zilimfanya Mansoor kutuli kidogo na kujaribu kumsikiliza.
“Mr. Nakeshwar anampenda sana mke wake” alizungumza babu mlinzi.
“Kwahiyo kama anapendwa ndio afanye ufuska?”
“Sina maana hiyo kijana wangu”
“Kumbe unamaanisha nini?”
“Unaweza kufanya jambo kesho na keshokutwa ukaonekana wewe ndio mbaya halafu wenyewe wakaendelea na mapenzi yao” mzee yule akazungumza kwa umakini.
Maneno yale yalionekana kumuingia Mansoor na kuzidi kushusha hasira zake. Nafikiri kama kweli angekwenda kule bustanini ni lazima mtu angetolewa roho kutokana na hasira alizokuwa nazo. Akavuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu kisha akarejesha simu yake kwenye mfuko wa suti na kuondoka kwa mwendo kwa spidi pasipo kuzungumza neno lolote lile la ziada.
Babu mlinzi alimtazama mwanaume yule alivyokuwa akitembea kwa kushindilia hatua chini kutokana na hasira alizokuwa nazo. Baada ya kumshuhudia Mansoor akiingia kwenye gari yake na kuondoka, babu mlinzi kageuza macho yake na kuyatupia kule kulikokuwa na bustani ya maua kisha akatikisa kichwa chake kwa masikitiko huku akiachia tabasamu la huzuni.
*****
Kule nyumbani kwa Zawadi, Ashura aliipokea glasi ya wiski na kuitazama kwa makini,
"Nini hii? Pombe?"
"Wacha maswali bwana kunywa" Zawadi alizungumza huku akisukuma birauli yake mdomoni na kupiga funda moja dogo huku akionekana kuisikilizia ilivyokuwa ikikatiza kwenye koo lake.
“Duh inaonekana si mchezo!” Ashura alizungumza huku akimkodolea macho rafiki yake yule.
“We onja ujionee mwenyewe maswali ya nini” alisema Zawadi huku akipeleka kiganja cha mkono wake wa kushoto na kufuta midomo yake.
"Sawa nitakunywa. Turudi kwenye habari za hicho kitumbua cha kihindi ambacho kimekufanya mwenzangu uwe na maisha mazuri kiasi hiki" Alizungumza Ashura huku akiiweka ile birauli juu ya meza.
"Shost nawe uking'ang'ania kitu, Mie mwenzio nafanya biashara ya kuuza vitumbua kama ya kwako" alizungumza Zawadi kwa kujiamini.
"Wacha masihara Zawadi bwana, mwenzio mie nina hamu"
"He! yamekuwa hayo tena! Haya niambie una hamu ya nini mwenzangu?"
"Nina hamu ya kujua"
"Ujue nini tena wakati tayari nimekwambia ninafanya biashara ya kuuza vitumbua" alisema Zawadi kwa msisitizo.
"Mie hata sikuelewi" Ashura alisema na kuipeleka glasi ya wisk mdomoni.
Naam Ashura alikunja uso wakati anameza kinyaji kile utafikiri alikuwa akimeza vipande vya chupa. Alifumba jicho moja na jicho lililobaki likawa likikitazama kwa makini kile kinywaji kilichokuwemo kwenye birauli. Alikohoa mara mbili mfurulizo kisha akavuta pumzi ndefu na kuziachia taratiibu.
Zawadi alipomuona shoga yake akitapatapa baada ya kuonja kinywaji kile, aliangua kicheko kilichomfanya apaliwe na mate na kujikuta na yeye akikohoa mfurulizo.
"Nyoo! Unacheka nini sasa?" Ashura alihoji huku na yeye akijichekesha.
"Aka! wacha nicheke mwenzangu, we unameza wisk utafikiri unameza furushi la miba" alizungumza Zawadi huku akiendelea kucheka.
"Kinywaji gani hiki kinakata utafikiri viwembe. Mie ndio kimesha nishinda hivyo" Alisema Ashura huku akisogeza pembeni birauli ile huku Zawadi akIendelea kukaukia kucheka.
"Bwana zawadi wacha kucheka unipe habari za kitumbua cha kihindi mwenzio" Alisema ashura.
Zawadi alijiinua kutoka pale huku akiendelea kucheka ingawa alipunguza kidogo.
"Nifuate" alisema Zawadi huku akiuendea mlango.
Ashura aliinuka pasipo kuzungumza kitu chochote na kumfuata. Walitoka chumbani na kwenda moja kwa moja hadi jikoni. Zawadi alifingua kabati lililokuwepo ukutani na kutoa chuma cha kukaangia vitumbua na kumuonesha Ashura.
"Hii ndiyo siri ya mafanikio yangu"
"Hicho si chuma cha vitumbua?" Ashura alihoji kwa mshangao
"Kwani mimi nimekwambia nafanya biashara ya nini?"
"Lakini Zawadi una masihara wewe! Hivyo vitumbua ni vya aina gani?" Ashura alizidi kupatwa na mshangao juu ya habari za rafiki yake. Zawadi akaangua kicheko kilichodumu kwa muda wa sekunde kadhaa.
"Sasa unacheka nini?"
"Ok. Ngoja nikujibu" Zawadi alizungumza huku akiwa anajizuia kuendelea kucheka. Alipeleka mkono wake usoni na kujifuta machozi ambayo yalisababishwa ba kile kicheko chake.
"Mimi nafanya biashara ya kitumbua cha kihindi"
"Sasa hapo ndipo unapo nichanganya shoga yangu"
"Nakuchanganya kivipi?"
"We umeng'ang'ania kitumbua cha kihindi...kitumbua cha kihindi, sasa mie nitaelewaje?" Ashura alizungumza kwa kunung'unika.
Zawadi akamtazama rafiki yake usoni na kujikuta akipatwa na huruma dhidi ya Ashura. Alivuta hatua na kusogea hadi pale alipokuwa amesimama Ashura kisha akaweka mikono yake kwenye mabega ya Ashura.
"Sikiliza Shoga yangu, mimi ni mfanya biashara. Lakini biashara zangu ninashirikiana na mhindi mmoja ambaye yeye ndiye aliyenipa mtaji na kunifanya niondokane na umasikini" Zawadi alizungumza kwa upole.
"Ni biashara gani ambayo unafanya wewe na huyo muhindi?"
"Kama nilivyo kwambia mwanzo, ni biashara ya vitumbua" alizungumza Zawadi na kutoa tabasamu kwasababu alifahamu jibu lile Ashura alikuwa amelichoka na hakupenda kulisikia tena.
*****
Shughuli aliyokuwa akishughulika Magosho kwa Bi. Fahreen ilipelekea mwanamke yule wa kihindi kuwa kama chizi wa mapenzi. Kwakuwa alitamani kuwa karibu zaidi na Magosho muda wote ilimbidi kumbadilishia kazi kijana yule kutoka House boy na kuwa dereva wake. Ndiyo iliwezekana, kama udereva alimfundisha mwenyewe atashindwaje kuwa dereva wake.
Kitendo kile cha kupandishwa cheo kilimfurahisha sana Magosho na kumfanya kuwa mbunifu zaidi katika kuhakikisha mama wa kihindi anaridhika kwa kila ambacho alikuwa anakihitaji kutoka kwake.
Magosho alikubali kufanya yote hayo kwaajili ya kuhakikisha mdogo wake Ashura anaishi katika maisha ya furaha na amani. Alitamani sana siku moja nay eye awe miongoni mwa watu mbele ya watu.
Bi. Fahreen alifanikiwa kumuweka karibu zaidi Magosho baada ya kumpatia kazi ya udereva. Muda wote, wakati wote na mahali popote Bi. Fahreen na Magosho walikuwa pamoja. Wakatumia mwanya huo kuponda raha na kujirusha kwa uhuru zaidi pasipokuwa na wasiwasi wowote ule.
Pamoja na kwamba Bi. Fahreen alikuwa akihisi anafanya matendo yake kwa siri, lakini kuna baadhi ya watu walikuwa wameshawashitukia na kufahamu kila kitu. Miongoni mwa watu waliokuwa wakifahamu uchafu ule waliokuwa wakiufanya wawili wale alikuwa ni pamoja na Mansoor. Ni yule yule Mansoor aliyewahi kushuhudia gemu kwa macho yake mawili kule kwenye bustani ya maua. Ni Mansoor yule yule aliyekuwa amepiga simu kumuita Mr. Nakeshwar kushuhudia uchafu wa mke wake, ni Mansoor huyo huyo aliyekuwa amepandisha hasira na kutaka kuingilia kati mchezo wa kabumbu kule kwenye bustani ya maua.
Kichwa cha Mansoor hakikukaa sawa tangu aliposhuhudia uchafu uliokuwa ukifanywa na mke wa bosi wake. Hata shughuli zake pia hakuwa akizifanya kwa ufasaha, alijilaumu sana kwa kukubali ushauri wa yule babu mlinzi wa geti la Mr. Nakeshwar.
“Yule mzee naye ni mshenzi sana, angeniacha nikawafunza adabu kunguni wale” alizungumza Mansoor huku akipeleka mikono yake kichwana na kuikutanisha kwenye kisogo.
“Pumbavu! Siwezi kuvumilia upuuzi huu. Lazima nifanye kitu” alizungumza Mansoor huku akipiga ngumi mezani kwa hasira.
Mansoor akijisogeza kwa kujivuta na kiti chake cha matairi hadi kwenye simu ya mezani ofisini pale na kuinua mkono wa simu, akabonyeza namba za simu za Mr. Nakeshwar kisha akaiweka sikioni.
Mungu hamtupi mjawake, ile simu iliita na punde simu ile ikapokelewa upande wa pili.
“Halloo” sauti ya Mr. Nakeshwar ilisikika kwenye simu.
“Yes Mr.Nakesh, Mansoor hapa naongea” Mansoor alijitambulisha.
“Oh Mansoor, habari bhana kubha?”
“Niko sawa Bosi”
“Iko problem veve, sauti iko sikika mbaya sana” Nakeshwar aliposikia tu sauti ya Mansoor alihisi kijana yule alikuwa na tatizo.
“Mimi mzima mkuu ila nina jambo nataka kuzungumza na wewe” alisema Mansoor.
“Iko mutu chezea veve?” alihoji kwa umakini.
“Ah…ah..ni kwamba…Aah..” Mansoor alijikuta akipata kigugumizi kuzungumza kile alichokuwa anakikusudia.
“Kama iko mutu chezea veve sema bhana kubha, mimi kuje toa roho yake mara moya” alizungumza Mr. Nakeshwar kwa kujiamini na majigambo ya hali ya juu.
ITAENDELEa





from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2RWyo11

No comments:

Post a Comment