Tuesday, February 4, 2020
KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA 11
ILIPOISHIA
Ashura aliingia chumbani mle na kujikuta katika hali ya mshangao zaidi baada ya kuona mazingira ya chumbani mle jinsi yalivyokuwa yamejitosheleza. Ilimjaa zaidi hamu ya kutaka kufahamu jinsi ambavyo rafiki yake yule alivyoyapatia maisha yale.
"Shoga hebu nipe siri ya mafanikio yako" Ashura alihoji mara tu baada ya kuketi kitandani.
"Sio siri, ni KITUMBUA” Zawadi alizungumza huku akimimina wiski kwenye birauli.
"Kitumbua?" Ashura akahoji kwa mshangao.
"Ndio kitumbua, tena kitumbua cha kihindi"
"Unamaanisha nini?"
"Una maswali mingi kwani we ni polisi? hebu karibu kinywaji" Zawadi alizungumza huku akimkabidhi Ashura birauli ile iliyokuwa imejaa wisk.
ENDELEA...
Waswahili wanasema mramba asali harambi mara moja. Kauli hii imethibitka hasa baada ya Magosho kukutana kimwili na mke wa bosi wake ndani ya gari. Bi.Fahreen alikuwa amechanganyikiwa na kudata kabisa na penzi la mfanya kazi wao wa ndani.
Magosho alikuwa ameshikilia mpira wa maji akimwagilia maua yaliypokuwa yameoteshwa nje ya nyumba ile kwa ustadi mkubwa. Kijana yule alikuwa akiipenda sana kazi yake hasa ukizingatia ndiyo iliyokuwa ikitegemewa zaidi na familia yake, yaani yeye na mdogo wake Ashura.
Bi Fahareen alitembea kwa kunyata kuelekea pale alipokuwa amesimama Magosho akiendelea na shughuli yake. Mwanamke yule alifika na kumziba macho Magosho kwa nyuma.
Magosho aliipapasa mikono ile ya mwanamke wa kihindi na kuhisi kumfahamu vizuri sana.
“Mama…” Magosho aliita baada ya kupata harufu ya pafume aliyokuwa akiitumia Bi. Fahree.
“Nani iko mama yako?” alizungumza Bi. Fhreen huku akiwa bado ameziba macho ya mwanamke yule.
“Jamani niachie basi” Yasini alizungumza kwa sauti ya kudeka kidogo baada ya kumfahamu mtu aliyekuwa amemziba macho.
“Hapana achia veve, sema mimi iko nani?” Bi. Fahreen alizungumza huku akiwa bado amemkamata kisawasawa kijana yule.
“Darling..”
“Nop…”
“Sweetie”
“Nop..”
“Yahabibi”
“Nop..”
“Baby”
“Good! Kumbe mimi iko toto?” Bi. Fahreen alizungumza huku akimuachia Yasini.
“Mbona nilikufahamu mapema sana” Magosho akazungumza kwa kujitutumua mbele ya mwanamke yule.
“Veve iko jua mimi kuliko hata Mr. Nakeshwar!” Alizungumza mwanamke yule huku akiwa ameweka mikono yake kwenye mabega ya Magosho.
“Hapana bwana mama, Bosi Nakeshwar ndio anakufahamu zaidi kuliko mimi” Alizungumza Magosho huku akiendelea na shughuli yake na mwaname yule akiwa bado amemshika mabegani.
“Sikia Goso yangu ambie veve kitu makini” alizungumza mwanamke yule kwa umakini.
Magosho aliwacha kufanya kile alichokuwa anaendelea nacho na kumgeukia Bi. Fahreen kuweza kusikia kile alichokuwa anataka kukizungumza.
“Ile dozi veve iko patia mimi kila siku, hapana siku moya Nakeshwar iko onesa mimi” mwanamke yule alizungumza kwa sauti ya kulalamika huku akipeleka mkono wake wa kuume kwenye kidali cha Magosho kilichokuwa kimevimba kutokana na mazoezi ya viungo.
“Lakini mama…”
“Nooo! Nani iko mama yako?” Bi. Fahreen akazungumza kwa ukali kidogo baada ya Magosho kumuita mama.
“Basi baby…” Magosho akazungumza kwa sauti ya upole huku akiachia tabasamu la huba mbele ya mwanamke yule wa kihindi.
“Veve Goso kila siku iko kosea mimi bhanaa”
“Basi nisamehe mpenzi wangu” Magosho alizungumza huku akimshika Bi. Fahreen kwenye mashavu.
“Kama iko taka samehe veve tibia mimi”Bi. Fhreen alizungumza kwa sauti ya kudeka huku akizunguusha macho utafikiri roho ilikuwa inataka kuacha mwili.
“Naam..” Yasini alishituka kidogo baada ya kusikia kauli ile kutoka kwa Bi. Fahreen.
“Tibie mimi bhanaa iko gonjwa” alizungumza Bi. Fahreen kwa msisitizo.
“Mng! Acha masihara basi”
“Hapana leta sihara mimi, iko gonjwa sana”
“Hivi mume wako akirudi ghafla kutatokea nini?”
“Hapana sida yoyote, mimi ambia yeye, veve iko dokta yangu” mwanamke yule alizungumza huku akimtomasa tomasa kijana wawatu kwenye mabegani.
“Wewe mwanamke wewe usitake kuniletea balaa. Mimi huo udaktari nimeusomea wapi?” Magosho alizungumza kwa mkazo kidogo uliochanganyikana na chembechembe za mahaba.
“Kama veve iko tibia mimi, basi veve iko daktari ya mimi” mwanamke yule aliendelea kuzungumza kwa msisitizo.
“Bwana ngoja mimi nimalizie kumwagilia maua” Magoshoalizungumza huku akibana mpira wa maji na kuyarusha kwenye maua ya mbele kidogo.
“Leo mimi iko taka onja ile tamu yako hapahapa” Jamani nyie sijui watu wengine wana mapepo! Mana hata mimi mwandishi naandika lakini mwanamke huyu naona simuelewi. Amesahau kabisa kama Magosho ni kijana wa mwanamke mwenzie haipaswi kumbemenda Eboo!
“Subiri basi tukitoka Out, leo nakuahidi kukupa dozi nzito zaidi hadi ukahadithie kwenu Bombey” Magosho alizungumza kwa kujidai huku akimkata jicho la wizi Bi. Fahreen na midomo yake akiichezesha chezesha kimahaba na macho ameyalegeza kigogo mtoto wa kiume.
“Au unataka nikumwagilie na wewe” Alizungumza Magosho huku akiendelea kumwagilia yale maua yaliyokuwa yakishangilia penzi lile mtoto wa kibantu na mama wa kihindi.
“Woow! Iko taka magilia mimi?” Bi. Fahreen alionekana kufurahishwa sana na ile kauli ya kumwagiliwa aliyokuwa ameitoa Magosho.
“Kwani wewe unafikiria ni kumwagiliwa nini?” magoshoalizungumza huku akiachia kicheko kidogo ambacho kilizidi kumchanganya mwanamke mtu mzima.
“Veve iko sema taka magilia mimi. Sasa mineno mingi toka wapi?” alisema Bi Fahreen huku macho yake yakionekana wazi kulikuwa na kitu anakitafuta kutoka kwa Magosho.
Magosho alianza kuhisi hisia zake zikijitahidi kuuchota ubongo wake na kuupeleka kule alipokuwa anakutaka Bi. Fahreen.
“We mwanamke una lako jambo unalolitafuta na utalipata muda sio mrefu” alizungumza Magosho kwa sauti kavu kisha akakohoa mara mbili na kujikohoza kukuna koo lake mara tatu mfurulizo.
“Mimi taka veve tibia mimi, Veve taka magilia mimi. Mambo mukidee” Bi. Fahreen alizungumza huku akipeleka mikono yake kushika kiuno cha Magosho.
“Ngoja nikuoneshe nilichokuwa nakimaanisha” Magosho alizungumza na kugeuka na ule mpira wa maji kuanza kummwagialia mwilini mama wawatu wa Kihindi.
Bi Fahreen alishituka sana baada ya kufanyiwa kitendo kile na Magosho. Hakuwa na namna zaidi ya kutimua mbio kuyakimbia maji yale. Magosho naye alimuunganishia mama wawatu na kumkimbiza kwa nyuma huku amekamatia vyema mpira wa maji, alikuwa amedhamiria kumlowanisha mama yule.
Ndugu msomaji kama ungepata bahati ya kuwaona wawili wale nafikiri ungehisi walikuwa ni watoto wa chekechea wanacheza kidali poo. Kila mmoja alikuwa akikimbia huku akicheka kwa furaha na Amani ndani ya moyo. Magosho aliweza kusahau kabisa ile hali ya umasikini kule uswahilini kwao.
Ghafla Bi.Fahareen alijidondosha chini na Magosho kwasababu hakuwa ametegemea kitendo kile alijikuta akimvamia na kumdondokea mama yule wa kihindi. Kwakuwa walikuwa wameshazoea kupeana ushirikiano wakati wowote na mahali popote, kitendo kile kilikuwa ni sababu tosha ya kuelekea kwenye mashambulizi ya makombora ya kivita. Wale waliopata nafasi ya kusikia mkasa wa vita vya pili vya dunia wanaelewa ninachokimaanisha hapa.
Kukuru kakara kukuru kakara kwenye maua mke wa mtu na mtoto wa mtu. Yani ukiangalia kwa mbali hivi unaweza kusema pale katikati kulikuwa na mpambano mkali kati ya simba na punda milia.
Ndugu msomaji huwezi kuamini hiki ninachokwnda kukuambia sasa hivi. Kumbe muda wote ule wawili wale walipokuwa wakichokozana na kuanza kucheza kuchikuchi kwenye bustani ya watu ya Mr. Nakeshwar, kulikuwa na mtu ametulia tu pembeni akiusoma mchezo na mchezo ukasomeka vyema na kueleweka vizuri.
MANSOOR alikuwa ni mfanyabiashara aliyekuwa akishirikiana na muhindi Nakeshwar. Kwa namna Mansoor alivyokuwa akiishi na Mr. Nakeshwar ungeweza kusema walikuwa ni ndugu wa baba na mama mmoja kasoro rangi za ngozi zao tu ndizo zilizokuwa zikiwatofautisha.
Mansoor pamoja na mlinzi wa getini ndio waliokuwa pembeni wametulia wakishirikiana kuusoma mchezo ule. Hata hivyo jambo lile halikuwa geni sana machoni mwao kwasababu penzi la Bi. Fahreen na Magosho halikuwa la kuficha. Watu wengi sana walikuwa wanafahamu kilichokuwa kinaendelea.
Ilikuwa ni rahisi watu kufahamu kwasababu wawili wale hawakuwa wakifanya starehe zao kwa kujificha. Walikuwa wakifanya yote hayo kwasababu Mr. Nakeshwar alitumia muda mwingi kusafiri kibiashara. Ni mara chache sana Mr. Nakeshwar kuwa nchini Tanzania na familia yake. Pengine ndiyomaana Bi.Fahreen aliamua kutafuta kibenteni wake. Sina uhakika sana kwa hilo mana hata mimi ni mgeni.
Mansoor alijikuta akipandwa na hasira dhidi ya viumbe wale wawili waliokuwa wakifanya usafi kule kwenye maua. Alikuwa akihisi kama vile mke wake ndiye aliyekuwa fanya utumbo ule. Akasimama kwa hasira huku akitoa simu yake mfukoni na kuvuta namba za Mr. Nakeshwar.
“Kama noma na iwe noma ngoja leo tukomeshe uchafu huu” alizungumza Mansoor huku akibonyeza namba za Mr. Nakeshwar.
ITAENDELEA
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2ScsRlG
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment