Wednesday, December 25, 2019

SMULIZI: HOUSEGIRL WA KITANGA 14





SMULIZI: HOUSEGIRL WA KITANGA
MTUNZI : KIZARO MWAKOBA

SEHEMU 14

ILIPOISHIA
Jamani nyie mambo yalikuwa ni magumu mno, omba kwa mungu yasikukute na uishie kusoma hivihivi kwenye chombezo. Nakwambia pale nilipokuwa nimesimama nilihisi kijasho chembaamba kikinitiririka mapajani. Nilitamani nimbebe mmoja wapo na kwenda kumtupa nje ili msala ule usiendelee. Kiranga chote kilikuwa kimeniishia nakwambia nikabaki kutetemeka tu utafikiri mgonjwa wadengue.
“Bro unajua tunadhalilishana, angalia tusije tukavunjiana heshima” alizungumza Fadhili kwa hasira.
“Fadili unasemaje? Wewe ni mtoto mdogo mno! Wala usijidanganye hata siku moja nitakuharibu!” Jamani nyie kaka Imran alizidi kupandwa na hasira huku nikimuona wazi alikuwa anatafuta chanzo tu cha kuanzisha mapambano ya masumbwi.
ENDELEA….
“Okay sawa nimekuelewa, basi na yaishe Bro” Fadhili alizungumza kwa kutaka kumaliza msala ule.
Umeona sasa ndugu msomaji? Nakwambia Fadhili ndio mwanaume wa ukweli, yani aliniburudisha kinoma kwa kile kitendo chake cha kujishusha baada ya kuona moto ulikuwa umewaka balaa. Najua hakuwa anamuogopa kaka Imran bali aliamua tu kujishusha ili kulinda amani ya ndani mle.
“Alaaa!” alitamka kaka Imran huku akijaribu kuteremsha hasira.
“Basi mkubwa na yaishe” Fadhili aliendelea kujishusha kabisa.
“Sasa sikiliza we binti, ole wako nimkute tena Fadhili chumbani mwako” kaka Imran alizungumza kwa jazba huku akininyoioshea kidole cha onyo.
Niliitika kwa kichwa kukubaliana na lile agizo lililokuwa limetoilewa na kaka Imran. Alimtazama Fadhili kwa chuki kisha akageuka na kuondoka. Fadhili alitoa msonyo kwa sauti ya chini ambayo kaka yake hakuisikia. Nafikiri kama angesikia sijui moto ambao ungewaka tena nani angeuzima.
“Unaona sasa” nilizungumza kwa kumtupia lawama Fadhili juu ya kile kilichokuwa kimetokea. Ndio! Kama angenisikiliza na kuondoka mapema chumbani kwangu yote yale yasingetokea. Hata hivyo Fadhili naye hakukubali kulaumiwa na mimi.
“Toka zako na wewe, kama mnabiashara zenu hukoo!” Fadhili akazungumza kwa hasira huku akielekea chumbani kwake. Mtoto wa kike nikabaki shushu limenishuka nakwambia. Nikahisi kukosa bara na pwani.
****
Kitendo cha kuwafarakanisha Fadhiri na kaka yake Imrani kilinifedhehesha sana. Nikajiona kama vile shetani niliyekuwa nimetumwa kuisambaratisha familia ile ambayo ilikuwa ikiishi kwa upendo na amani kabla ya kufika kwangu.
Nilijikuta nikikubalina na wale wanaosema maisha ni shule, Nikweli kabisa maisha ni shule tena ni chuo kikuu. Kwa muda mfupi tu tangu nilipofika pale jijini niliweza kujifunza mambo mengi sana, na moja ya mambo niliyokuwa nimejifunza ni pamoja na kuwa na nidhamu hasa katika masuala ya mahusiano.
Ndio niliamua kuwa na nidhamu kwasababu nilijiona nilikokuwa naelekea kulikuwa siko na matokeo yake ni kuwa mtumwa wa mapenzi. Kwakuwa namimi ni binadamu niliyekuwa nimekamilika ikabidi nichague mwanaume mmoja tu ambaye pekee ndiye ningemkabidhi moyo wangu.
Najua hata kama ningekupa nafasi ya kunichagulia ungenichagulia Fadhili, kama kuna mwengine ambaye unaona angenifaa basi hilo ni chaguo lako wewe, mimi mwenyewe nilikuwa nimemchagua Fadhili kwasababu ndiye niliyekuwa nikimpenda tangu siku ya kwanza naingia pale jijini Dar.
Sasa changamoni ni kwamba, mtu ambaye nilikuwa nimemchagua kumpa mamlaka ya kumiliki penzi langu alitokea kunichukia kupita maelezo. Huwezi amini lakini ule ugomvi kati ya Fadhili na kaka Imran ndio uliopelekea mabadiliko kwa mpenzi wangu Fadhili.
Nikiwa nimeketi sittingroom nikimsubiri kwa hamu Fadhili arudi ili tuweze kupata chakula cha mchana kama ilivyokuwa kawaida yetu. Akili yangu ilikuwa ikiwaza kuolewa tu na mwanaume huyo na kumzalia watoto.
“Fadhili mpenzi wangu ukinioa nitakuzalia watoto hao…wanne” nilizungumza pekeyangu huku nimeketi kwenye kochi na kukumbatia mto mdogo wa kochi kifuani kwangu.
“Mtoto wangu wa kwanza atakuwa wa kiume na atafanana sana na wewe, nitampa jina zuuri la baba yako mzee Sekiza” niliendelea kuzungumza huku nikitabasamu kwa matumaini.
“Nitakuwa namuita, we Sekiza hebu niletee rimoti hiyo niongeze sauti kwenye TV, au nitamuita we Sekizaaa njoo haraka nikutume dukani ukamuite baba aje ale chakula tayari” masikini ya mungu binti wawatu niliendelea kuyajenga maisha yangu ya baadae nitakapokuwa nimeolewa na Fadhili.
Nilikurupuka haraka kutoka kwenye lindi la mawazo baada ya kusikia geti likigongwa. Niliamini kwa asilimia zote kuwa mtu aliyekuwa akigonga geti alikuwa ni Fadhili, baba watoto wangu mtarajiwa, baba yake Sekiza. Nikatoka haraka sana kwenda kufungua geti.
“Ooh kumbe ni wewe!” nilizungumza huku nguvu zikiwa zimeniishia baada ya kufungua geti na kumkuta dada Bupe amesimama nje.
“Vipi shost ulikuwa umelala nini?” alihoji dada Bupe mara tu aliponiona huku akijichekesha chekesha.
“Hapana!” nilijibu kwa mkato.
“Vipi una mishe gani huko ndani?”
“Hamna, nipo tu”
“Twende basi mgahawani jamaa anakuita” alizungumza dada Bupe kwa sauti ya chini.
“Jamaa gani?” nikahoji kwa sauti ya ukauzu huku nikijifanya sielewi chochote kumbe tayari nilikuwa nafahamu alichokuwa anakizungumzia dada Bupe.
“Acha basi Tumu, si jamaa yako” dada Bupe alizungumza huku akiendelea kujichekesha chekesha.
“Jamaa! Mimi nina jamaa gani?” nilizungumza huku sura yangu ikionekana kukosa masihara.
“Unajua usinizingue Tumu, unafikiri mimi namuongelea nanai kama sio Endru?”
“Endru ndio nani? Simjui mtu huyo!” nilizungumza na kutaka kufunga geti lakini dada Bupe aliudaka mlango na kuuzuia.
“Mmnh ngoja kwanza Tumu!” dada Bupe akazungumza kwa mshangao huku akizuia mlango usifungwe.
“Unasemaje?” nikahoji kwa ule uso wangu wa kauzu.
“Kwani mtoto wa watu amekukosea nini jamani Tumu?” dada Bupe alihoji kwa sauti ya kubembeleza lakini iliyokuwa imejaa mshangao. Mwantumu aliyezoea kumuona siku zote hakuwa Mwantu yule aliyekutana naye siku hiyo.
Nilimtazama mwanamke yule mtu mzima kwa macho makali yaliyokuwa yamejaa chuki na hasira. Kwakweli sikuweza kumuelewa lengo lake juu yangu. Nikajaribu kujifikiria alikuwa amenionaje hadi kufikia hatua ya kunitafutia wanaume mtoto wa mwanamke mwenzie. Ukisikia mtu mzima hovyo basi ndio yule. Niliinua macho yangu na kumtazama usoni kwa makini.
“Unajua dada Bupe, mimi sihitaji mwanaume yoyote yule kwa sasa” nikazungumza kwa sauti ya upole lakini iliyokuwa imejaa msisitizo wa hali ya juu.
“Eh! Mara hii umeshamtema kijana wawatu?” dada Bupe alizungumza kwa mshangao.
“Kijana gani? Mbona mimi sina uhusiano wowote na huyo mtu!” nikajaribu kueleza kwa sauti ya msisitizo.
“Eh! Ndio mapenzi ya kitanga hayo?” dada Bupe aliendelea kuhoji kwa kebehi.
“Naomba unielewe dada Bupe, nimekuja hapa kufanya kazi na sikuja hapa kutafuta wanaume” nikatoa maelezo mafupi lakini yaliyokuwa yamejaa uzito.
“Mnh! Ndio kusema Imran amekwisha chukua goma nini, au ndio mapenzi motomoto na Fadhili yamenoga?” Dada Bupe akahoji kishambenga.
“Ni wewe wasema”
“Sasa nikamwambiaje?”
“Nani?”
“Si baby wako Endru”
“Kwaheri dada Bupe, naona kama vile haunielewi” nilizungumza na kuanza kufunga geti dogo ambalo mara nyingi hutumiwa na watu kuingilia.
“Kwahiyo nikamwambiaje?” alihoji dada Bupe nilipokuwa nafunga geti.
“Kamwambie simtaki, tena akome kunifuatilia!” nikazungumza kwa jazba huku nikiwa nimekwisafunga geti na kurejea ndani.
***
Maneno yangu yalimfedehesha sana dada Bupe. Hakuweza kuamini kama kauli zile kali zilikuwa zikitoka kwenye kinywa cha binti wa kitanga ambaye alifikiria ni msichana mrahisi rahisi na wa kuchezea hovyo hovyo. Nakwambia mtu mzima sura ilimshuka na kumporomoka utafikiri ftari ya magimbi. Akarudi mgahawani kwake huku amechoka hoi utafikiri ametoka kufanya kazi ya kuchanganya zege.
“Vipi sister, mrembo wangu yuko wapi?” Ilikuwa ni sauti ya Endru ambaye wakati wote alikuwa ameketi mgahawani akinisubiri kwa hamu kubwa.
“Mrembo gani?” dada Bupe alihoji kwa mkato huku akivuta kiti na kuketi.
“Kwani tumekubaliana ukamuite nani? Si mtoto wa kitanga”
“Hakuna cha mtoto wakitanga wala mtoto wa kisumbawanga” Dada Bube akazungumza kwa sauti ya kukata tamaa.
“Kwani kumetokea nini sister, mbona umepoa ghafla?”
“Mimi nilikwambia kuwa kale katoto kana mashetani ukanibishia, sasa utaamini” dada Bupe akazungumza kwa msisitizo.
“Kwani kamekuwaje?”
“Yani nakwambia kamenishushua utafikiri mtoto mwenzake” alizungumza dada Bupe kwa jazba.
“Ah we ungemwambia mimi ndio namuita”
“Haaa! Yani wewe ndio hakutambui kabisaa, utadhani hakuwahi kukuona tangu azaliwe.” Dada Bupe alieleza kwa msisitizo.
“Wewe dada Bupe bwana umeharibu, ingekuwa mimi wala asingezingua, mtoto tayari nimekwisha mseti”
“Sasa si uende mwenyewe kwani unashindwa nini?”
“Umenipeperushia ndege wangu bwana”
“We chizi nini!” dada Bupe alizungumza kwa hasira na kuamka kutoka kwenye kile kiti na kuelekea jikoni.
“Unakwenda wapi sasa?”
“Achana na mimi wewe” alizunguma dada Bupe huku akichukua ndoo na kuiweka bombani kwaajili ya kukinga maji.
Itaendelea


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2Zu7NKP

No comments:

Post a Comment