Wednesday, December 25, 2019

SIMULIZI: HOUSE GIRL WA KITANGA 22



SIMULIZI: HOUSE GIRL WA KITANGA  
MTUNZI : KIZARO MWAKOBA  
  
SEHEMU 22

ILIPOISHIA
Kitu kibaya zaidi mimi na baba tulikuwa tunakimbizana kutokea chumbani mwake na ukiunganisha na yale mavazi niliyokuwa nimeyavaa ndio usiseme. Mama hakuwa anapenda kuniona nimevaa nguo za aina ile, pamoja na kwamba watu wengine walikuwa wakinitetea na kunishawishi nivae mavazi yale.
Baba alipobaini mama alikuwa anatuangalia tukifanya vituko vile, alianza kuhisi tumbo la kuhara likimchomachoma. Alitamani ile siku ambayo Yesu aliahidi kurudi iwe imefika ili asipate nafasi ya kuhojiwa na mke wake ambaye kwa siku za nyuma alikuwa ameshaanza kuhisi penzi lake lilikuwa na dalili ya kudokolewa na house girl.
ENDELEA….

Sio baba tu ambaye alikuwa amechanganyikiwa kutokana na tukio lile bali hata mimi nilihisi miguu ikigongana kadri nilivyokuwa nikikimbia. 
 Kwa akili ya kuzaliwa ambayo baba alikuwa amejaaliwa ilifanya kazi kwa haraka na kukimbia hadi alipokuwa amesimama mke wake na kumshika kwa nyuma kama vile alikuwa akiomba msaada.
 Na mimi ikabidi nijiongeze na kuendelea kumkimbiza baba, tena ikabidi nianze na kupiga kelele zisizo eleweka. Nilielekea moja kwa moja hadi alipokuwa amesimama mama na kuvuta mwiko uliokuwepo mkononi na kutaka kumtandika  mama kichwani. 
 Kama vile picha la kichina mama alifanikiwa kukwepa mwiko ule na kusogea nyuma kidogo kuusoma mchezo ambao hakuwa anauelewa. Niliendelea kupiga kelele huku nikirusha mwiko hovyo hovyo nikijifanya nataka kuwatandika wote wawili.
 “Ni kitu gani kinaendelea jamani?” mama alihoji huku na yeye akitimua mbio kunikimbia.
 “Kimbia mke wangu atakuua huyo mtoto!” baba alizungumza huku akimshika makono mama na kutimua nae mbio kuelekea sebleni.
 Nakwambi mtoto wa kike kama vile nilikuwa nimechochewa, baada ya kubaini tulikuwa tumefanikiwa kumchanganya mama. Niliwaunganisha wote wawili na kuwatimua utafikiri nimechanganyikiwa.
 Nikaingia jikoni ambako nilichukua ndoo ya maji na kujimwagia mwilini huku nikijifanya nilikuwa nimepandwa na mapepo. Nilipiga kelele na kujitupa chini huku nikigalagala. Wote wawili baba na mama walikuwa wamejawa na woga na wasiwasi. Hata baba mwenyewe hakuelewa kama ile ilikuwa ni kweli ama picha la kihindi.
 “Amepatwa na nini mtoto wa watu Mungu wangu” mama alihoji huku akihofia kunikaribia.
 “Hata sielewi, nimeshangaa tu anapiga kelele na kunifuata chumbani huku ameshika mwiko na kuanza kunitandika nao” alizungumza baba huku akishikilia pua yake.
 “Mungu wangu, ndio amekuumiza hivyo?” alihoji mama kwa wasiwasi baada ya kuona pua la mume wake limevimba kama andazi.
 “Au malaria yamepanda kichwani?” baba akahoji.
 “Nenda sasa kamsaidie” mama alisema.
 “Nenda wewe!” baba alizungumza huku akionekana kuogopa kunisogelea.
 “Mwanaume mzima unaogopa! Nenda kamsaidie mtoto bwana” mama alizungumza huku akisogea nyuma.
 “Niende ili anipige tena! Nenda wewe si mwanamke mwenzio?” baba alijitetea.
Nikiwa pale chini nimelowana na maji nakwambia mtoto wa kike nikazidi kujigalagaza huku nikiwasikiliza walivyokuwa wakibishana kunisogelea.
 “Au amepandwa na mashetani?” mama alihoji.
 “Kwani ana mashetani?” baba akahoji.
 “Sasa mimi nitajuaje”
 “Kwani wewe si ndio umemleta humu ndani!” baba alizungumza na kujifanya kulaumu mimi kuletwa ndani mle.
 Nilipoona mambo yamekuwa sawa nikatulia taratibu huku nikiwa nimelala chali, mguu mmoja mashariki na mwingine mgagharibi, moko wa kushoto huku na wa kulia kule.
 “Ametulia sasa, haya nenda ukamsaidie” mama alizungumza.
Kwa tahadhari kubwa baba alinyata na kunisogelea pale nilipokuwa nimelala. Masikini ya mungu kumbe kile kitendo cha kujimwagia maji na lile pozi langu nililokuwa nimelala nilikuwa namuweka baba katika wakati mgumu. 
Mwili wangu ulikuwa ukionekana waziwazi kutokana na kulowana na maji. Madafu yangu ya kifuani yaliyokuwa yametuna kisawaawa na ncha kali kwa mbele yaliweza kuonekana waziwazi kutokana na ile blauzi laini niliyokuwa nimevaa kulowana kwa maji.
Kale kasketi kafupi nako kalizidi kuniwacha wazi kutokana na kuchoshwa na maji niliyokuwa nimejimwagia mwilini kwa makusudi ya kuua soo.
 Baba aliinama huku akijifanya kuogopa lakini macho yake akiwa ameyakodoa kifuani kwangu. Akapeleka mkono wake kwenye mashavu yangu na kujaribu kunitikisa huku akiniita.
 “Mwantumu mama” baba aliita huku akihamishia mkono wake wa kushoto na kuuweka kiunoni kwangu. Nafikiri lengo lake lilikuwa ni kunisaidi ingawa sina uhakika sana.
 Mama naye akasogea na kuchutama pembeni ya mume wake huku akinitazama kwa macho yaliyokuwa yamejaa hofu na mashaka. 
 “Vipi mume wangu, tumpeleke hospitali” alizungumza mama alipokuwa akichutama.
 “Hebu ngoja kwanza” baba alizungumza huku akijaribu kunitikisa kwa mikono yake ambayo mmoja ulikuwa kwenye shavu langu na mwingine kwenye kiuno changu kilichokuwa kimechongoka na kuugawanyisha mwili wangu kwa mpangilio mzuri.
 Niliposikia masuala ya kupelekana hospitali ikabidi nijikohoze na kujigeuza kulala kwa upande wa kulia.
 “We Mwantumu” mama aliita.
Nilitoa sauti ya kuitika kama vile nilikuwa kwenye usingizi mzito sana kisha nikajikohoza.
 “Asante Mungu!” alizungumza mama.
 “Hebu lete nguo tumfunike” baba alizungumza huku akijishaua heti hakuwa anapenda kuniona nikiwa nimelala kihasara hasara kiasi kile.
 Maneno ya baba yalizidi kuongeza Imani kwa mume wake juu yangu, hivyo alielekea chumbani kwaajili ya kuchukua nguo ya kunifunika.
 “We mama wa mwiko hebu amka” baba alizungumza kwa sauti ya chini huku akinipapasa mama alipoondoka. Nikafumbua macho na kumtazama baba kwa hasira.
 “Ahaa bado unanishika eeh? Au nikachukue mwiko wangu” nikazungumza kwa msisitizo baada ya kumuona akinipapasa kwenye mapaja yangu pamoja na kifuani.
 “Pumbavu, hebu lala huko!” baba aliniamuru baada ya kuniona naendelea na misimamo yangu ileile.
 “Ukinipapasa tena nalianzisha upyaaa” nikazungumza kwa msisitizo huku nikiendelea kufumba macho.
Mama alirudi mbio huku ameshikilia upande wa kitenge kwenye mikono yake. Alipokaribia tu nikafumbua macho kama vili nilikuwa nimeamka kutoka usingizini.
 “Vipi anaendeleaje?” mama alihoji masikini ya mungu.
 “Ndio amefumbua macho” baba akajibu huku akipokea lile tenge na kunifunika kuanzia kifuani hadi kwenye miguu.
 “Vipi Mwantumu unaendeleaje mama” Bi Fatma alihoji kwa sauti ya upendo.
 “Sijambo” nikajibu kwa sauti ndogo utafikiri nilikuwa mogwa mahututi.
 “Haya inuka twende hospitali” mama alizungumza.
 “Ngoja kwanza mke wangu, mbona hata sio mgonjwa wa hivyo huyu” alizungumza baba kwasababu alikuwa akifahamu kilichokuwa kinaendelea.
 “Unasema sio mgonjwa huyu wakati amekuhondomola pua lako hilo” mama alizungumza kwa msisitizo.
 “Hapana mama mimi nipo sawa” nikazungumza baada ya kuona mama alikokuwa anaelekea kulikuwa siko.
 “Si nimekwambia mimi” baba akaniunga mkono.
 “Umeniambia nini! Mtoto wawatu akitufia hapa utasemaje?” mama alizungumza kwa msosotizo kidogo baada ya kubaini baba hakuwa analiunga mkoso suala la mimi kupelekwa hospitali.
 “Hapana mama siumwi, hali hii iliwahi kunitokea nikiwa kijijini” nikazungumza ilikupinga suala la kupelekwa hospitali wakati sikuwa naumwa kitu chochote.
 “Imewahi kukutokea?” mama akahoji kwa mshangao baada ya kusikie maneno yangu yale.
 “Ndio lakini ni zamani sana” nikaongopa.
 “Sababu ni nini?”
 “Walinambia sijui mashetani” nikaendelea kudanganya nakwambia wakati tangu nimezaliwa sikuwahi kupandwa na huyo shetani sijui pepo sijui ibilisi.
 “Eeh haya tena makubwa!” mama alizungumza kwa kuhamaki.
 “Usijali, hebu amka ukapumzike ndani” baba alizungumza huku akitaka kuniinua kutoka pale chini.
 Mtoto wa kike nikajiinua na kusimama huku nikijifanya kuyumbayumba na kupepesuka.
 “Hebu mshike, mpeleke chumbani kwake” baba alizungumza baa nay a kuniona nikikosa nguvu za kutembea mwenyewe.
 Mama alinikamata vyema na kunikokota kuelekea chumbani kwangu huku nikijifanya sikuwa na nguvu za kutosha.
 Tulipofika chumbani mama aliniweka kitandanikisha akasimama pembeni na kunitazama kwa umakini.
 “Mwantumu” mama aliita.
 “Abee mama”
 “Vipi unaendeleaje?”
 “Kwa sasa sijambo”
 “Au nikurudishe kijijini?” mama akahoji kwa umakini.
 “Hapana mama, naomba usinirudishe kijijini” nikazungumza kwa kuhamaki baada ya kusikia wazo la kurudishwa kijijini. Heti ndugu msomaji, raha zote hizi ninazozipata huku mjini halafu mtu anakwambia akurejeshe kijijini kweli inahusu? Kwakweli kijijini harudi mtu labda wanibebe nikiwa nimelala.
 “Hakikisha unabadilisha nguo, ndipo upumzike” alizungumza mama alipokuwa anaondoka, nani nilijiinua nipokuwa nimlala na kuketi kitako. Ndani ya kichwa changu nikavuta taswira ya matukio yote yaliyotokea tangu baba aliporejea kutoka kazini hadi wakati ule. Nikaachia tabasamu la ushindi na kujitupa tena kitandani.
 Nikiwa pale kitandani mawazo juu ya kipenzi changu yakaanza kunijia. Sikuona sababu ya kuyakatisha bali niliyapa nafasi yautawale ubongo na muda wangu. Ndio, nilijikuta nikimpenda sana mpenzi wangu Endrus nafikiri ni kwasababu ya vituko nilivyokuwa nikiletewa na wanaume wa mle ndani.
 Nilikumbuka yale maneno ya Fadhili ya kunikataza kwenda kule mgahawani kwa dada Bupe. Sikuweza kufahamu ni kwa namna gani ningeweza kukutana na mpenzi wangu Endrus pasipo kufika mgahawani kwa dada Bupe.
 Vilevile maneono ya kaka Imran kuniruhusu niwehuru kwenda kwa dada Bupe yalinipa matumaini ya kuweza kuonana na kipenzi cha roho yangu. Nilitamani nitoke na kwnda kwa dada Bupe hata wakati ule lakini vigezo havikukidhi. Nikakumbatia mikono yangu kifuani huku nikivuta taswira ya kukumbatiwa na mpenzi wangu Endrus.
*****

Baada ya siku chache kupita maisha ya kufungiwa kwenye geti kubwa yalielekea kunishinda. Jambo kubwa ambalo lilikuwa ni kama mzigo mzito kwanu ni kushindwa kuonana na mpenzi wangu Endrus. Nilitamani sana japo kuonana na dada Bupe ili anipe habari za kijana yule aliyekuwa amenichanganya akili yangu. Lakini niliheshimu sana maneno ya Fadhili aliyosema hataki kuniona nikipeleka pua yangu kule kwa dada Bupe.
Nikiwa mezani nikiandaa kifungua kinywa kwaajili ya siku mpya Fadhili alifika na kuketi mezani.
“Dogo naona sikuhizi upo ‘on time’ kabisa” Fadhili alizungumza huku akiosha mikono yake tayari kwa msosi.
“Naipenda kazi yangu baba” nikazungumza kwa sauti laini.
“Inapendeza sana, si unaona hata mother hapigi kelele tena” Fadhili alizungumza huku akipakua chakula kutoka kwenye hotpot. 
“We si hunipendi bwana, nimeona labda niimarishe kazi yangu pengine unaweza ukarudisha moyo wako nyuma” nilizungumza kwa kumtania huku nikiachia tabasamu la upendo.
“Unafikiri sikupendi Tumu, Mimi nakupenda sana tena sana” Fadhili alizungumza huku akimimina chai kwenye kikombe.
“Mnh yani wewe!” nikazungumza huku nikitabasamu nikiwa siamini masikio yangu.
“Unafikiri Tumu! Mimi nakupenda sana, tena nilikuwa natamani hata uwe mama watoto wangu” Fadhili alizungumza huku akipeleka mdomoni kipande cha mkate.
Maneno yale ya Fadhili yaliufanya mwili wangu usisimke utafikiri sijui nilikuwa nimemwagiwa kitu gani. Nikamtazama machoni kwa umakini zaidi kuona kama kile alichokuwa anakizungumza hakikuwa na masihara.
“Kwani tatizo liko wapi?” nikahoji kwa umakini.
“Tatizo lipo Tumu!” alizungumza huku akitafuta kipande cha mkate.
“Niambie sasa, tatizo ni nini?” nikaendelea kuhoji.
“Tatizo mimi sikuelewi Mwantumu”
“Kivipi?”
“Kwanini Imran akinikuta na wewe ananimaindi?” Fadhili akahoji.
“Kwa kweli hata mimi sielewi”
“Basi mimi nafikiri jamaa ameshakula zigo” alizungumza Fadhili huku akiachia tabasamu na macho yake akinitazama kwa kuniiba.
“Hakuna bwana Fadhili, mimi humu ndani sitakuja kutembea na mwanaume yeyote yule na nimeapa hivyo” nikazungumza kwa msisitizo.
“Mnh hata mimi?” Fadhili akahoji kwa mtego.
“Sijui labda wewe…lakini sijui kama itawezekana pia” nilijikuta nikizungumza kwa kigugumizi. Nilishindwa kumpa jibu la kuwezekana kwasababu tayari nilikwisha amua kuwa na Endrus peke yake.
“Kwanini isiwezekane, au ndio hunipendi siku hizi” Fadhili akazungumza kwa sauti ndogo lakini iliyokuwa ikikoroma kama redio mbovu.
ITAENDELEA



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2t5RtUh

No comments:

Post a Comment