Tuesday, February 4, 2020

Yajue madhara ya kunywa pombe wakati wa ujauzito

Matumizi ya pombe wakati wa ujauzito ni moja ya njia ya kuzuia kupata matatizo ya kuzaliwa nayo na udhaifu kwa mtoto. Pia kuna matatizo kadhaa yanaweza kutokea kwa kichaga kutokana na matumizi ya pombe wakati wa ujauzito .
Madhara haya ya pombe huweza kuwa ya kujitambua  tabia na madhara madhara ya mkusanyiko wa dalili na viashiria kwa mtoto vinavyoitwa fetal alcohol syndrome-FAS. Kutokana na shirika madhara ya pombe yanayoambatana na dalili na viashiria
Fulani yanaongezeka sana. Pombe imekuwa ikituiwa vibaya sana wakati wa ujauzito ukilinganisha na madawa mengine.
Dalili za mtoto ambaye mama alikuwa akitumia pombe kwa kiasi kikubwa
Kutokuwa vema kabla na baada ya kuzaliwa
Mtindio wa ubongo
Udhaifu wa kuzaliwa wa kichwa na uso
Magonjwa ya moyo
Tabia zisizoeleweka
Matatizo ya mfumo wa fahamu
Kuhusu fetal alcohol syndrome
Kiwango kikubwa cha pombe kwenye damu ya mama kipindi cha ujauzito huweza kuwa na uharibifu kwa kichanga akiwa tumboni na maendeleo ya mtoto baada ya kuzaliwa. Baadhi ya madhaifu ya kiuumbaji aina Fulani kwa mtoto hutokea na huhusiana na utumiaji pombe, mkusanyiko wa madhaifu hayo huitwa kwa lugha nyingine fetal alcohol syndrome. Madhaifu makubwa na madogo yamerekodiwa katika kumbukumbu na hutokea kwa mtoto 1-2 kati ya watoto 1000 wanaozaliwa.
Kiwango kidogo au kikubwa cha utumiaji pombe vyote huathiri au huweza kuathiri utengenezaji umbo la mtoto na maendeleo ya ukuaji wake, jinsi mama anavyokunywa pombe kwa kiwango kikubwa mtoto atapata dalili kali. Watoto waliozaliwa na wamama waliokuwa wanatumia pombe kwa kiwango kikubwa sana wameonekana kuwa na madhaifu ya mwili mengi ukilinganisha na wale waliozaliwa kwa watumiaji wa kiwango cha wastani. Asilimia 32 ya vichanga waliozaliwa kwa watumiaji wa kiwango cha juu wakati wa ujauzito, walizaliwa na madhaifu ya kiuumbaji, asilimia 14 tu ya vichanga walikuwa na madhaifu ya kiuumbaji kwa wamama waliokuwa wanatumia pombe kwa wastani na asilimia 9 tu kwa wale walioacha pombe baada ya kupata ujauzito. Vihatarishi nyongeza mbali na pombe vinavyohusiana na tatizo la FAS ni umri wa mama, kipato cha chini na ulevi wa kupindukia
Kiasi gani cha pombe ni salama kwenye ujauzito?
Hakuna kiwango salama cha matumizi ya pombe kwenye ujauzito kilichotambuliwa. Kwa usalama ni kutofikiri kutumia pombe wakati wa ujauzito.
Je kuna uhusiano wa kiwango cha pombe na matokea mabaya ya ujauzito?
Hakuna. Miongozi mwa wanawake waliokunywa ounce 5 ya pombe kwa kila siku, 1/3 ya watoto walikuwa na FAS, 1/3 walionesha madhara sumu kabla ya kujifungua, na 1/3 waliobaki walikuwa kawaida. Kundi jingine lililotumia ounce 1-2 kila siku asilimia 10 ya watoto walikuwa na dalili za FAS. Hata kiwango kidogo cha pombe kimekuwa kikisababisha FAS!. Matumizi ya pombe kwa kiasi kidogo bado yamekuwa yakihusika kusababisha mtoto kuwa na IQ kidogo na matatizo ya kujifunza kwa watoto wenye anatomia ya kawaida.
Je pombe husafilishwa kwenye kondo la mtoto?
Kemikali ya ethyl iliyo kwenye Pombe hupita kwenye kondo na kuingia kwa kwenye mzunguko wa damu wa mtoto. Kiwango cha ombe kwenye damu ya mama huwa sawa na kile kwenye damu ya kichanga tumboni.
Je mama aliyekuwa teja wa pombe anatakiwa aache kunywa pombe?
Mama aliyekuwa teja wa pombe anatakiwa apewe msaada wa wataalamu ili kusaidiwa kuacha pombe, madhara a kujifungua kabla ya mda huongezeka kwa watumiaji wa pombe
Dalili za kuacha pombe ghafla zinaonekana wakati gani wa ujauzito?
Dalili za kukatisha kutumia pombe huanza kuonekana upesi pale mtu anapoacha kutumia pombe, mara nyingi ndani ya masaa 4 hadi 12. Hata hivyo inawezekana dalili za kukatika kutumia pombe kuonekana siku chache baadae. Mtu asipopata tiba hufikia kilele cha dalili ndani ya masaa 48 na huweza kuendelea kufikia miezi 3 hadi 6 na huwa na dalili kiasi kuliko awali. Dalili na viashiria ni kutetemeka, wasiwasi, mapigo ya moyo kwenda kasi, shinikizo la damu la juu, kutokwa jasho, kichefuchefu, kukosa usingizi na hutegemea utegemezi wa pombe na hali ya mgonjwa.
Mara ujauzito unapotambuliwa kuacha kutumia ama kupunguza husaidia kuondoa madhara kwa mtoto?
Kemikali ya ethyl na ethanol iliyo kwenye pombe hupita kwenye kondo la nyuma na kuingia kwenye damu na ubongo wa mtoto. Inafikilika kwamba madhara hutokana na sumu iliyo kwenye pombe na mazao ya uchakataji wa pombe mwilini. Kuacha au kupunguza kutumia pombe mara ujauzito unapotambuliwa huweza kupunguza matatizo ya kuzaliwa kwa mtoto hata hivyo kuna uwezekano kwamba inaweza hili lisitokee. Hivyo tafiti zaidi zinatakiw akufanyika ili kuonyesha usahihi wa jambo hili.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/31nYxJ2

No comments:

Post a Comment