Tuesday, February 4, 2020

Ukiona Mwanamke anaonyesha dalili za kukutongoza basi mfanyie haya chaap!!



Iwapo mwanamke anaonyesha dalili za kukutongoza ambazo umependezwa nazo, haitakua jambo zuri kwako kama utapuuza swala hili kwa kufanya matendo yasiyotakikana.
Baadhi ya wanaume wengine wanaweza kudai kuwa wanawake ambao wanatongoza waume hawafai kukubalika kwani si kawaida.
Well, jibu ni kuwa kama binadamu yeyote, pia mwanamke kwa kawaida anakuwa na hisia za kutaka kupenda. Hivyo wengi wa wanawake huishia kujaribu kuwatongoza wanaume kwa njia ambazo wahataki kujulikana
Kutaka kutambua kama mwanamke anakutongoza ni rahisi. Unaweza kuona kuwa tabia zake zinabadilika kabisa na zile ambazo unazifahamu. Pia miondoko yake inakuwa ya ushawishi.
So utafanyaje wewe kama mwanaume kuhakikisha kuwa haupotezei nafasi hii ambayo wanaume wengi huiita ‘kuletewa chakula hadi mdomoni bila kutoa kijasho’?
1. Kiri na kile anachosema 
Hii ni kukubaliana na mambo ambayo anayotaka wewe na yeye mfanye pamoja. Hii inaweza kuwa kujaribu kurudia maneno ambayo yeye anayaongea. Mfano mwanamke anayekutongoza anaweza kukuambia kuwa anataka mwende mutembee katika kilabu fulani. Wewe unafaa kukubaliana naye kwa kusema maneno kama “Kwa hivyo unataka tutembee klabu fulani?”
2. Tabasamu kwa kitu alichosema 
Tabasamu ama smile ya ukweli kwa kawaida huondoa wasiwasi kwa yeyote. Hivyo mwanamke ambaye anakutongoza unaweza kumuonyesha tabasamu kuonyesha kuwa unakubaliana na kile anachosema. Hii inatoa nafasi kwake yeye kuendeleza kuonyesha hisia zake kwako.
3. Tumia maongezi ya mwili aka body language 
Tumia maongezi ya mwili ili kuonyesha ya kuwa uko wazi kupokea chochote ambacho kitatoka kwa msichana huyu. Simama kwa pozi la kutulia, usikunje miguu wala mikono, unaweza kumsogelea na kumtomasa kwa upole kama inahitajika. Unaweza pia kumsogelea hadi sehemu yake alipo lakini muachie nafasi kidogo kwake kupumua.
4. Usipapatike 
Mwanamke aina hii kama ataanza kukutongoza kwa kukupapasa, unafaa kutulia na kurelax. Fanya kushika viganja vyake iwapo atajaribu kukushika mikono ama mabega. Usijaribu kuharakisha kuingiliana naye ama kujaribu kumhepa, hii ni kwa sababu inaweza kuzua usumbufu ama kuona ukosefu wa usalama kati yenu.
5. Kiri utongozi wake 
Kwa kiasi fulani unaweza kukubaliana na mambo ambayo anakuambia kama njia moja wapo ya kukutongza. Unaweza kugusia maswala fulani ya kumchokora hisia zake ili afunguke zaidi akuelezee mambo yanayomfanya akuzimie. Hivi kutamfanya yeye kufungua milango zaidi ya kujieleza bila wasiwasi.
6. Mfanye akutamani 
Kumbuka ya kuwa ukosekaji kwako kwake kutamfanya yeye kukutamani zaidi na zaidi. Munaweza kutongozana kiasi flani lakini fahamu ya kuwa unahitaji kupotea kwa macho yake kwa muda ili aweze kuingiwa na hamu ya kukutamani zaidi. Unaweza mara kwa mara kukutana na yeye lakini si kila siku. Pia hakikisha kuwa haujifanyi kama humtambui kabisa ama kujifanya hayuko kwa akili yako






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/36WU3du

No comments:

Post a Comment