Tuesday, February 4, 2020

Riwaya fupi


Inawezekana uko katika mahusiano tata na hujui wapi pa kutokea,najua unapokuwa katika hali hiyo huwezi kusikiliza hata ushauri kwa mtu wakati mwingine hata wanaokushauri unaweza kuwaona hawafai,unapokuwa katika hali hii usijali sana kiasi cha kuumiza kichwa kuna kitu cha kufananya. 
Ili kufanikiwa katika mahusiano ni lazima uruhusu moyo wako kuwaamini wengine ,siku zote tegemea matokeo chanya kwa jamaa zako wa karibu ili uweze kuishi bila stress. 
Mahusiano mengi yenye mafanikio yana maana kubwa sana hasa katika kumbukumbu ya maisha ya watu husika,kumbuka kitu kidogo tu kinaweza kuimarisha mahusiano na wakati mwingine kuamsha hisia za mahisiano yaliyotozorota. 
Ikiwa unataka kuimarisha mahusiano yako vizuri,chukua couple uanayoipenda iwe ya rafiki wa kawaida au wapenzi alafu jifunze kupitia wao mambo mengi kwa mfano wanapokoseana hutumia njia zipi kusameheana. 
Pia njia rahisi ya kuimarisha na kujenga mahusiano yako ni lazima uchunge kauli zako ,hapa namaanisha kuwa jifunze kuziba mdomo mpaka utafakari unachotaka kukisema. 
Maneno huumiza moyo,hivyo unapoamua kuropoka maneno kwa kujifurahisha au kuhisi unawafurahisha watu unakuwa unapoteza nguvu ya mahusiano. 
Hakikisha kuwa maneno yako yanaendana na matendo yako,kwa mfano;kama unawaambia rafiki zako kuwa uko sawa wakati wanakuona hauko sawa hawawezi kukuamini na watapunguza uaminifu wao kwako. 
Hapa namaanisha kuwa jifunze kusema ukweli kama unasumbuliwa na jambo lolote usiliweke moyoni,rafiki na jamaa zako ndio wa kwanza kukusikiliza na kukusadia. 
Unatakiwa kuhitajika kuongea maneno yanayoonesha uhalisia wa hali yako ,kama ukisema una furaha basi furaha yako ianzie usoni na wakati mwingine furaha hiyo ioneshwe kwa vitendo na kwa hisia. 
Siku zote unakumbushwa kuwa wewe na marafiki zako mnapaswa kuaminiana kwa kila kitu hiyo ndiyo maana ya urafiki wa kweli.Japo kuwa kuna wakati unakumbana na majanga ya aibu lakini unapaswa kuyasimlia kwa watu unaowaamini njia hii itakusaidia kuwa huru. 
Hakikisha unawaambia rafiki zako siri zinazoutesa moyo wako kabla hawajajua kwa kuona matendo yako au kupitia kwa wengine,hiyo itawaumiza na wataona kama hawana umhimu kwako ,jifunze kwamba rafiki zako ndio wanaoelewa unachokihitaji. 
Japo kuwa kuna watu hawawaamini .marafiki zao kwa kuhisi kuwa wanaweza kuwaharibia mambo yao ,usiangallie hayo tafuta njia rahisi ya kumtafuta rafiki wa kweli ambaye yuko tayari kulia na wewe kwenye shida zako. 
Kumbuka kuwa wewe na rafiki zako katika mahusiano yenu ya ukaribu mnakuwa mmetengenezwa kuwa pamoja katika shida na raha na hivyo mnatakiwa kuwa makini na kuwa tayari kwa ajili ya mwenzako bila kujali mazingira yanaruhusu au hayaruhusu. 
Mwisho..






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2OpxdoI

No comments:

Post a Comment