Sunday, February 2, 2020

PETE YA KIKE Sehemu Ya 31.... MWISHO





Ghafla surian ndio anaingia huku akiwa mpole sana... Yani haamini kama leo anatenganishwa na mke wake... Sasa asha alishtuka kuskia ni majini mana asha ana urafiki na shaimati...
"hata wewe pia ni jini?"
"ndio"
Ghafla mama akaingilia kati na kusema
"sasa nataka nimjue mke wa mwanangu surian"
"ni mimi... Shikamoo mama"
Aliitika maimuna na kumsalimia
"marahaba.... Kumbe majini manajua hata kusalimia"
"mama, sisi hatuna tofauti nanyie, ni uwezo tu ndio tumekusudiwa nao"
"sawa.... Sasa mwanangu,? Nimepata taarifa juu ya ndoa ya wewe na mtoto wangu wa kiume, tukiwa kama wazazi wa mtoto wake,... Tumekaa na kujadili swala hili kua, hatukubaliani na ndoa hio, kwani wewe ni kiumbe na huyu ni binadamu, hio ndio sababu ya kuikataa ndoa hio"

ENDELEA........

Wazazi wa suria walijipachika roho ya ujasiri, kwa kumnusuru mtoto wao kwani kisheria katika dini, ndoa halali ya binadamu wote ama majini wote, na sio jini kwa binadamu, hivyo kwakua wazazi ni watu wenye kufuata dini hawakuhitaji mtoto wao aingie huko, kwani sio imani yao inavyo ruhusu,....

Baada ya maimuna kusikia hivyo wala hakushituka, kwani swala hilo alisha lijua toka awali wakiwa nje ya jengo hilo,...
"lakini mama, sisi tumefunga ndoa ya halali"
Aliongea muna kama kujitetea kwa wakwe zake,
"ni sawa, lakini hakuna dini inaruhu ndoa ya jini na binadamu, tafadhali sana mwanangu, hebu mpe uhuru mtoto wetu"
Aliongea mama asha, tena kwa busara ya hali ya juu, kwani hapakuwa na ugomvi wa aina yeyote.
Ni swala la kuelewana wazazi na maimuna,....
"surian, toa maamuzi basi mume wangu"
Muna alimwambia mumewe atoe maamuzi juu ya wazazi wake
"mke wangu, kama wazazi wametia uwalakini, ulizani mimi nitafanya nini?? Ila nami sina raha na ndoa hii kutokana na masharti ya mali na hata ndoa kwa ujumla,... Nakupenda sana muna lakini umezidi kuwa na masharti mengi mno,... Hapa mjini nina miezi minne kama sio mitano, lakini umenipa sharti la kuto waona wazazi wangu,.. Tunamiliki kampuni wazazi wangu wanateseka mpaka mama yangu anakwenda kupewa kazi za vyooo... Mpaka nakosa raha na haya maisha mana nakosa uhuru wa maisha Kiukweli... Naona bora nibaki masikini mwenye uhuru na furaha nikiwa na familia yangu"

Alimaliza kuongea surian kisha shaimati akadakia kwa kumwambia maimati kuwa
"sasa nawewe? Ni masharti gani ulimpa ambayo hayapo? Kumbe umejiharibia mwenyewe, ungeanza kuonekana na familia yake"
Aliongea shaimati kana kwamba hata yale masharti yote hayakuwa ya kweli....
"samahani mume wangu, nilikupa masharti ili kujua uvumilivu na upendo juu ya wazazi wako, na sikuwa na maana nyingine"
"sawa... Lakini ndio hivyo, wazazi wangu wamekataa ndoa yetu"
Aliongea surian kisha shaimati akasema
"muna,.. Hapo ulipo una ujauzito... Na ili urudi katika hali yako ya zamani, huyo mtoto ni halali ya viumbe vya sayari ya mwezi"
Aliongea shaimati akiwa na maana kwamba kuna viumbe ambao wao ni kuchukua viumbe walio tumboni na hawazaliwi kama ilivyo kawaida bali anatoweka ndani kwa ndani na kumfanya mwanamke alio jitolea kiumbe hicho kurudi kama alivyo zamani, yaani bikra... Ni ukweli usiopingika kuwa majini wamepewa uwezo wa kipekee na sio kama binadam.....

Maimuna alipewa muda wa kufikiri mana surian yeye yupo tayari kuachana na maimuna,.... Lakini sasa wakati maimuna anafikiria jibu la kutoa, kumbe alikuwa akiwasiliana na mkuu wao wa majini kuwa ndoa inavunjika kutokana na matakwa ya wazazi kwani mtoto wao na yeye ni mili tofauti kabisa....

"sawa, ila ujauzito huu hatokuwa halali yangu wala halali yenu, ni sadaka kwa viumbe wa sayari ya mwezi,... Kama mtaridhia basi nami nipo tayari kwa hilo"
Maimuna aliona hakutokuwa na baraka pale wazazi watakapo weka mgomo juu ya ndoa hio, hivyi kakubali ndoa ivunjwe kisheria, ila mtoto ni sadaka ya viumbe wa mwezini....
"sawa, hata sisi tumekubali"
Aliongea surian kisha mzee Rashid akashusha dua mana ni mzee wa msikiti hivyo kuna taratibu za kuvunja ndoa kisheria,....

Ndani ya dakika 15 kila kitu kilikubalika na sasa surian na maimuna hawana ndoa tena, na mabaya zaidi mtoto sio haki yao wote, na ili iwe haki yake huyu maimuna basi kuna upande atatakiwa kuishi kama mjane, lakini kwakua bado anauhitaji ubikra, basi hana budi mtoto huyo kumtoa sadaka katika viumbe waishio mwezini,.. Na sadaka hio hutolewa wakiwa ndani ya himaya yao wao majini wenyewe,... Lakini licha ya ndoa kuvunjwa, maimati alimchukua surian na faima akawatoa pembeni..

"surian, Kiukweli Nilikupenda sana, lakini kwa bahati mbaya wazazi wako hawakuridhia... Lakini hakuna budi juu ya hili kwasababu wazazi ndio kila kitu katika hii dunia,.. Nimekubaliana na yote na sina kinyongo na wewe wala familia yako... Katika masharti ya mali, haikuwa kweli kwani nilikuwa nakupima juu ya upendo kwa wazazi wako,..."

Aliongea maimati huku surian akisema kuwa
"sawa nimekuelewa, na sina kinyongo juu ya hilo, japo nimekuwa boss bila kutoa msada kwa wazazi wangu, lakini hakuna shida nitapambana kadri ya uwezo wangu ili niiwezeshe familia yangu"
Aliongea hivyo surian akiwa na maana kwamba mali zote wanazomiliki kwa sasa zitapotea kwasababu mwenye mali ndio huyo anarudi atokako
"tuachane na hilo... Faima?? Pia wewe ni mmoja kati mtu ulio changia mimi kukubali ndoa hii ivunjike kwani una upendo na heshima ya kipekee,.. Kiukweli unastahili sifa... Ninachokuomba, mpende surian, mpe kila atakachokikosa kwangu,.. Mwisho kabisa, mlinde kama nilivyokuwa namlinda mume wangu, ila kwa sasa anakwenda kuwa wako... Inaniuma lakini sina jinsi"
Maimuna aliongea huku akitokwa na machozi kana kwamba asili yake ya ujini ndio chanzo kikubwa cha kumkosa surian,
"usijali dada,... Kwani surian nilianza kumpenda toka tukiwa wadogo na nikaendelea kumpenda hata mlipokua naye huko.. Na nitaendelea kumpenda mpaka kesho"
"ahsante sana kwa hilo faima... Mimi nadhani tumemaliza... Na hapa tutajiandaa kisha saa nane usiku tunaondoka rasmi,... Aaaaaaaaaa.. Surian, nyumba hii haitokuwa ya halali kwako, ila kampuni ya MICCO nakuachia ikiwa kama faida yako ya kuwa nami kwa upendo.. Faima?? Nimeacha kampuni kwa ajili yenu,... Hakuna masharti ilimradi muwe mnasaidia watu na kutoa sadaka bila kujali dini wala kabila na wala dhehebu na bila kuchagua umri"
Aliongea maimuna huku surian na faima wakiitika kwa pamoja
"sawa sawa dada muna, tutafanya kama ulivyo agiza"
"sasa wewe surian unaniitaje dada"
Aliuliza maimuna huku surian akijibu
"lakini kwa sasa hatuna mahusiano, hivyo ni mtu na dada yake"
Alisema suria
"Kiukweli inaniuma sana lakini sawa, mie ni dada yako.. Nitakuwa nakuja kuwatembelea.."
Ni maneno ya maimuna, na hapo ndio mwisho wa ndoa ya surian na jini maimuna kwani ni mtu na kiumbe kitu ambacho sio sahihi kibinadamu japo wapo walio oa majini lakini hakukuwa na kipingamizi, na kama wazazi wa surian wangelikubali, basi ndoa isingevunjwa.....
"muna?"
Suria alimuita maimuna
"abee kaka"
"pete ya kike unaisahau"
Alisema surian huku akiivua pete ile..
"hapana surian, hii pete nakuachia kama zawadi, mana najua Murati sabaha bado anahitaji kuwa nawe, hivyo hakikisha hii pete ya kike haitoki kidoleni mwako, mana ukiiitoa tu, Sabaha atakuingilia na kukutesa atakavyo"
"ooohhhh ahsante sana dada muna... Shukrani sana kwa hili"
PETE YA KIKE ambayo ni pete ya maimuna lakini kaamua kumuachia surian kama zawadi na iwe mlinzi badala yake... Waliagana wote kwa roho moja na hakukua na mwenye kinyongo kati yao

Surian aliichukua familia yake yote na kwenda Kuanza maisha mapya akiwa na mchumba wake faima.. Wakati huo faima ana furaha ya hali ya juu kwani surian karudi kwake kama ndoto zake zilivyo dai kuolewa nae..

Suria aliifikisha familia yake nyumbani kisha yeye akaelekea kazini akiwa na faima.. Tena hata asha alikuwapo katika gari hio,.. Sadiki alitetema baada ya kusikia honi ya gari ikipigwa nje ya geti,.. Sadiki alikua akimalizia kula lakini ghafla tu chakula kilishindwa kupita kooni, mana kafanya kosa kubwa sana ambalo hana imani kama litasameheka,... Ikiwa ni nyakati za saa nane mchana,....
"shadya?"
Aliita boss surian, kwa sasa kampuni ni yake peke yake... Mana mwanzo haikuwa yake kwani mmiliki ni mwanamke..
"abee boss"
"njoo pamoja na sadiki"
Aliwaita wote wakakaa kikao chao kidogo pale ndani, na nyakati zote hizo kiwanda kilikuwa kikifanya kazi kama kawaida..
"shadya,??? Kwa huruma yako juu ya mama yangu,... Kuanzia leo utakuwa meneja mkuu wa kampuni ya MICCO,. Halafu huyu faima huyu ambaye ni ndugu yako, huyu ni mke wangu mtarajiwa, hivyo ni boss wa pili kwenu..... Sadiki??"
"yes boss, yes boss"
"Kiukweli mimi sina hukumu juu yako. Ila niliskia mashtaka kuwa ulimtongoza dada yangu, na ndio sababu ya kumfukuza mama yangu.. Hivyooo...... Dada asha??"
"abeeeee"
"wewe ndio utajua cha kufanya juu ya Sadiki mana wewe ndie ulie shuhudia yote hayo.... Toa hukumu juu yake"
Aliongea suria huku sadiki akitetemeka mana anaamini dhahiri kabisa asha hawezi kumuacha kwa makusudi alio yafanya juu yake...... Lakini asha hakukumbuka mabaya pekee japo mabaya ndio makali zaidi katika moyo wake, likiwemo swala la kumfukuza mama mzazi wa boss..
"Nisamehe asha,.... Na sikua na nia ya kukuchezea, nilihitaji kukuoa asha"
Aliongea sadiki ikiwa ni msamaha kwa asha...
"surian, mimi naona tumuache tu.. Mana hakujua atendalo ila mi najua kajifunza kutokana na hili, hatoweza kurudia tena"
Alisema asha huku suria akijibu
"ahhh kama umemsamehe wewe, mimi sina shida..... Sasa sadiki, utakuwa meneja masoko. Mana nafasi yako ya awali nimempa shadya"
"sawa boss, ahsante sana boss.... Asha nakushukuru sana dada angu"
"ok.... Mimi naona kazi ziendelee na kama kawaida,..... Dada asha... Wewe utakuwa mkaguzi wa kiwanda kizima, mnaweza kushirikiana hata na wifi yako hapa"
"hakuna shida..."
"sasa,....mimi wacha nitoke, nikanunue kiwanja nijenge wazee watulie wale matunda yetu... Naomba mfanye kazi kwa bidiiiii"
"sawa boss"

Saaaa nane usiku ikiwa ndio saa ya safari ya majini hao, kama ilvyo ada ya wao kusafiri kila saa nane......

Saa kumi alfajiri, shaimati na maimati wakiwa ndani ya himaya ya majini,... Na anahitai kuwa na bikra hivyo kisheria ni lazima utoe sadaka ya mtoto kwa viumbe waishio katika sayari ya mwezi,... Hivyo kabla hajaingia katika himaya ya mabinzi bikra, pale pae mwezi uliwaka kwa kupitiliza,... Ndani ya sekunde saba tu.. Maimuna hakuwa na mimba tena,... N uzuri zaidi hata bikra anayo kutokana na uwezo waliopewa viumbe hao... Binadamu hata utoa watoto kumi,. Bikra hupewi ng'ooooo,.. Sasa kuanzia hapo maimuna sio mama na wala sio mke wala mchumba wala demu wa mtu,.. Ni msichana mpyaaaa.....

BAADA YA MIAKA 250 (MIAMBILI HAMSINI) KUPITA...

Ikiwa ni miaka mingi imepita,... Koo nyingi zilizaliwa katika koo za suria, lakini mpaka sasa hazipo.... Kuna koo kama tano zimepita na hata koo ya sasa haijui kama kuna tajiri alie itwa surian,... Baada ya miaka hio surian kufariki dunia, ndugu na watoto wa suria walio wahuni waligombea mali na kuzifilisi mali hizo, hivyo uzao uliofuata baada ya uzao wa suria ukaendelea kuwa masikini kwani baadhi ya watoto wa suria walikuwa wahuni, hivyo waliuza mali zao na kuzitumia vibaya......

Uzo ulizidi kuzaliwa lakini ni koo hio hio ya mzee surian aliofariki miaka 220 iliopita, hivyo surian alifariki akiwa na miaka 55 na kuacha watoto wahuni waliofuja mali mpaka kuteketea zote......

IKIWA NI MIAKA YA SASA.... JIJINI ARUSHA......

Uzao ulizaliwa mara dufu mpaka majina yakajirudia, yakafa, yakajirudia yakafa... Takriban mizao mitano imepita na yote imekufa....

SASA HUU NI UZAO WA SITA KUTOKA UZAO WA SURIA,

ikiwa ni familia ya kifukara sana inayo ishi jijini Arusha,.... Familia hio au uzao huo ulifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume, alie itwa SUHAIBU.......

Lakini sasa katika msitu mmoja mzito
ikiwa ni mida ya jioni, yapata kama saa 11.30, alionekana dada mmoja wa makamo akiwa anahema sana huku akikimbia, nikisema msitu namaanisha msitu kwelikweli,.. Dada huyo alikuwa akikimbia mithili ya mtu anaetaka kuepusha maisha yake, kana kwamba kuna mtu au kitu kilichokuwa kikimkimbiza katika msitu huo,....
"uuuuuu nakufa jamaniiii"
Ni sauti ya dada huyo mwenye umri mkubwa tu, akiwa kama anaomba msaada katikati ya miti, majani, migomba, miba, na vingine vingi vipatikanavyo msituni,.. Lakini Kiukweli hakukua na mtu wala kitu kilichokuwa kikimkimbiza,... Alisimama mahali na kujifanya kama kajificha katika migomba iliostawi mpaka kuweka kiza kinene katika msitu huo, haijulikani alikuwa akikimbizwa na nini,...

Lakini ghafla anaanza tena kukimbia kana kwamba kamuona adui wake aliokuwa akimkimbiza katika msitu huo,
Mdada huyo hakufika mbali alinyongwa na kamba za miguu na kudondoka chini, sasa akawa hawezi hata kuamka hivyo akawa anapiga tu kelele kana kwamba mtu anaemfukuza yupo jirani yake, ila kwa jinsi tunavyo ona hakukuwa na mtu.. Lakini ghafla akiwa katika hali ya kujinasua,.... Alifika huyo aliekuwa akimkimbiza,......
"uuuuuuuuuuuuuwiiiiiii"
Alipiga kelele kubwa kuashiria hatari ya kudhuriwa na kitu fulani kisicho julikana.....

MWISHO WA STORI HII YA PETE YA KIKE....... ILA STORI HII INA MWENDELEZO WAKE NA ITAKUA NA JINA LINGINE NA WAHUSIKA WENGINE..... STORI HIO IPO TAYARI








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2GPW1BO

No comments:

Post a Comment