Sunday, February 2, 2020
PETE YA KIKE Sehemu Ya 24
lakini aliona bora apokee simu hio..
Sasa alivyo pokea tu kabla hajasema hallo,.. Asha keshasema
"Hellow, Samahani, naongea na boss sure"
Aliongea asha kwa sauti ya kuvutia zaidi,..
"samahani utakuwa umekosea namba... Mimi sio boss sure"
Sasa huku kwa asha, ghafla alikata simu na kushtuka...
"kasemaje? Ndio yeye au"
Mama alimuuliza mtoto wake baada ya kukata simu
"mama... Mbona ni sauti ya kaka surian"
Aliongea asha kana kwamba kaijua sauti ya kaka yake,...
"we mshenzi wewe, usinikumbushe machungu ya mtoto wangu, we niambie kakwambiaje"
Mara simu ikaita tena,....
"haya huyo kapiga yeye, pokea umsikie mwanao"
Aliongea asha huku akimpa mama yake simu
"asha mwanangu, mpokelee mwenzio bwana acha utani"
"hapana mama... Ni sauti ya kaka surian"
Aliongea asha huku mama akaichukua ile simu na kuipokea kisha akaiweka sikioni....
ENDELEA......
Hakuna japo zuri kama siku kuongea na mtu uliopotezana nae kwa muda fulani,... Mama mwenye shida yake ni kusikia hio sauti ambayo asha anasema ni suria ambaye ni mtoto wake,... Mama kushika simu na Kutanguliza samahani, mana wamemsumbua mtu wa watu kumbe sio boss walio mtarajia... Mama kwa busara na hekima zake, aliipokea simu na kusema kuwa
"Hallow baba, Samahani tulikosea namba tu"
Aliongea mama huyo, lakini suria alishtuka na kujikaza kusema
"hakuna shida mama angu siku nje..."
Simu ilikata, lakini surian alishtuka kwa hio sauti, kwani kaifananisha na Sauti ya mama yake mzazi,....
Surian hajavumilia kusubiri alipiga tena aongee na mwanamke huyo...
"samahani, namba unayopiga kwa sasa haipatikani, tafadhali jaribu tena baadaye"
Surian alikasirika sana kwa kutopatikana kwa namba hio,...
"nini baba Rashidi"
Mkewe alimuuliza kwani alimwona akiwa na jazba ya ghafla tu...
"skia muna,... Wiki ijayo nataka kwenda kuwaona wazazi wangu, na tutakwenda wote"
Aliongea surian tena kwa hasira ili mke asije kuweka masharti mengine
"lakini zile siku ziliisha, ni wewe tu mume wangu"
Aliongea maimuna huku akimuuliza tena
"kwani kumetokea nini"
"kuna namba nimepigiwa nayo, nikasikia sauti ya mama yangu kabisa, sasa sjui ni yeye au zinafanana tu"
"uaijali,... Wiki ijayo tutakwenda"
Aliongea mwanamke huyo japo anajua kabisa mama yake alishawahi kuja kuomba kazi pale ila hana uhakika kama alipata au laah..
Sasa huku kwa akina asha,... Ilionekana taxi ikibeba mgonjwa huku asha akilia sana, na aliokuwa akipakiwa katika gari ni mama yake... Kana kwamba sauti ya mtoto wake ilimshtua mno mpaka kupoteza fahamu.... Asha alikuwa akilia sana, sasa mbaya zaidi simu ipo kwenye ndoo ya maji... Kumbe wakati ule ilikuwa hivi... Wakati surian anaongea
"Hallow baba, Samahani tulikosea namba tu"
Aliongea mama huyo, lakini suria alishtuka na kujikaza kusema
"hakuna shida mama angu siku nje..."
Sasa wakati surian anaendelea kuongea, kumbe mama kaijua sauti ya mtoto wake, hivyo akapata mshtuko na kuachia simu ikaingia kwenye beseni la maji, ndio pale suria akaishia "SIKU NJE..." ni kwamba simu iiingia kwenye maji, sasa asha hakujali simu, kwani mama yake alikuwa na hali mbaya,.. Kwa bahati nzuri baba yao huyo kaja.. Ndipo akaita taxi ikaja kuachukua, simu bado ipo kwenye maji...
Wakati huo huku kwa surian anazidi kupiga simu, lakini bado anapewa taarifa za kuto patikana kwa simu hio, sasa hatuliii hata kidogo, toka alipo ifananisha sauti ya mama yake...
Huku hospitali mama yake akiwa katika matibabu, mpaka wakati huo hajazinduka wala kutoa neno lolote,.. Hio ni jinsi gani anavyo mpenda mtoto wake wa kiume, na imani ya kwamba surian alifariki alikuwa hana kabisa kwani anamuamini mungu kuliko maneno ya watu,
Kesho yake ikiwa katika majira ya saa nne za asubuhi,... Shadya anahaha kwani Mwenye nafasi ya usafi wa vyoo leo hayupo,... Lakini ghafla asha katokea akiwa anakuja ofisini kwa Shadya...
"samahani dada, habari yako"
Asha alimsalimia Shadya
"salama tu, ina maana wewe ndio unafika kazini"
"ndio,... Kiukweli dada nauguliwa na mama yangu yule aliokuwa anafanya usafi wa vyoo"
Aliongea asha huku Shadya akishangaa kusikia kua huyo ni mtoto wa mama usafi,
"ina maana yule mama ni mama yako"
"ndio"
"mmmmhhh ok, kwahio kapatwa na nini"
"jana alianguka ghafla tu"
"jamani poleni sana"
"ahsante,.... Aahhh nimekuja kushika nafasi yake, japo yangu ipo kule idarani lakini nataka nishike nafasi yake"
Aliongea asha kana kwamba kaja kumsaidia mama yake ile nafasi ya usafi wa vyoo,....
"lakini ukumbuke nawe una nafasi yako asha"
"ni kweli dada, lakini chooni ni sehemu muhimu zaidi, mana wakaguzi wakija itakuwa sio vyema wakute uchafu"
Aliongea asha, na Shadya alimuelewa vyema kisha akamruhusu
Tukija huku hospitali ambako mama yake surian kalazwa,. Alipata nafuu na ndio mana asha aliamua kufika kazini ili kazi zisiharibike, lakini mama surian kajua yule ni mtoto wake,. Nani kama mama... Yaani sauti tu inamfanya amjue mtoto wake aliompoteza katika macho yake ndani ya miezi mitatu kama sio minne, tena ni bora ijulikane kuna alipokwenda, lakini haijulikani mahali alipokwenda, na ndio mana familia ilipata mfadhaiko wa moyo kwa kumkosa kipenzi chao....
"mama asha, haya tatizo ni nini"
Mzee Rashidi alimuuliza mke wake sababu ya kuzimia siku ya jana usiku
"mwenetu, jana kwa mara ya kwanza nimesikia sauti ya mwanangu"
Aliongea mama surian huku mzee huyo akishangaa kwa maneno ya mke wake,..
"mbona sikuelewi mke wangu"
"suria,... Suria mtoto wetu yupo hai.. Nimemsikia jana kwa masikio yangu"
Aliongea mama huyo huku mzee akisema
"namba yake uliitoa wapi"
"mume wangu, kuna ujinga tulikuwa tunafanya.. Lakini tunashukuru kwamba tumejua mapema"
Aliongea mama huyo na wakati huo kapata nafuu vizuri kabisa....
Huku ofisini surian ni wa kupiga simu, tena ile namba kaisevu kabisa kwa jina la LIKE MOTHER (kama mama) akiwa na maana ni kama mama, kwa ile sauti ambayo kaisikia ni kama ya mama yake, hivyo hakuweza kuisevu mama, bali kaisevu KAMA MAMA... Kila akipiga namba ile humjulisha haipatikani,.... Na laiti angelijua kuwa wanafanya kazi katika kampuni yake sijui ingelikuwaje,... Ndani ya ofisi yake akiwa kavua tai, yaani anatamani wiki ijayo ifike leo, mana leo ni Jumanne, sasa ni mpaka Jumapili ya wiki ijayo, sio hii inayokuja hapana... Sasa akifikiria ni mpaka wiki ijayo anaona ni mbali sana lakini kaipanga mwenyewe kana kwamba mpaka wiki hio atakuwa na asalio zuri la pesa yake, mana ikumbukwe kuwa hata maboss hujilipa wenyewe mishahara, unakuta boss anajilipa elfu 30 au hata 50 kwa siku, hivyo kapanga hio wiki kwa maana atakuwa ana fungu la jasho lake, mana kama mke kakataa na majasho yake haina haja ya kumbembeleza zaidi... Kwani masharti yake ni makubwa mno....
Asha akiwa chooni, baada ya kufanya usafi, yeye hajifichi kwasababu ni umri sahihi ambao unahitajika katika kampuni hio,.... Alikuwa ana mawazo sana, namba ya boss sure ipo kichwani kwake,.... Akiwa anawaza sana kuhusu ile sauti kama ya mdogo wake kabisa,... Kiukweli ilimpa mawazo hata yeye,...
"aahh mambo dada"
"poa"
Alikuwa ni tariki aliokua akiingia uwani kujisaidia,... Lakini kama unavyomjua tariki ni sharobaro anapenda kujipiga picha mara kwa mara,, sasa saa ngapi hajaanza kuji selfii kwenye sinki za kunawia.... Asha alimuona huyu mtoto ni mjinga kweli, mana anajipiga picha chooni
"sasa ndio nini hivyo.... Hivi mnajua simu zitawaumbua hizo"
Aliongea asha huku tatiki akicheka...
"aahhh dada wewe ni mzuri na bado mdogo sana, nashangaa hujui mambo ya kidigitali zaidi"
"digitali au ujinga"
"aaahhh, hapa watanikoma wazee wa WhatsApp, natupia kama mbili Facebook, afu hii inafaa profile ya WhatsApp hiii"
Alijiongelea tariki huku akicheka na simu yake,... Lakini asha kuna wazo lilimjia hapo hapo....
"we mkaka, simu yako si ina WhatsApp"
"ndio kwani vipi"
"naomba nimuangalie mjomba angu kama yupo WhatsApp"
Aliongea asha huku akijibalaguza mana alisha mtolea uvivu kwa kujipiga picha chooni...
"we si umesema hazinifai hizi simu"
"nisamee bure, naomba nimuangalie"
"nyoooo, haya taja namba"
Tariki alikubali kumsaidia ili asha amuone mjomba wake,...
"ni 0714419487"
"mmmhhh namba zenyewe kumbe tigo"
"heeeee sasa hapa tanga kwani tunatumia mtandao gani zaidi kama sio tigo"
Sasa tariki aliiweka ile namba kwenye simu yake, kisha akawa ana refresh ili itokee kwenye listi ya namba za wasapu asha aone picha ya mjomba wake, lakini sio kuwa ni mjomba wake, anataka kuhakikisha kama ipo WhatsApp, na je picha itakuwa ni nipi??... Kweli namba ilikuja na tariki aliisevu kwa herufi A hivyo ikawa ya kwanza kwenye listi ya namba zake za WhatsApp.... Lakini sasa kabla hajabonyeza ile picha ilioko kwenye profile ya hio namba, ghafla sadiki katokea hapo chooni....
"riki? Saaa sita hii muda wa kazi unafanya nini huku"
"apana boss, ni aisha kuna mtu alikuwa anataka kumbipu kasema hana simu"
"ebu toka nenda kazini... Mwehu wewe"
tariki aliondoka lakini asha hakuweza kuona ile picha,...
"asha, sasa umefanya nini... Chukua simu yako, hata kama hunipendi lakini siwezi kukupokonya simu nilio kununulia"
Aliongea sadiki huku akimpa simu, lakini asha aliikataa ile simu na kusema kuwa...
"diki, hebu niache Kwanza, kwa sasa sipo vizuri kiakili kwani mama yangu anaumwa... Hivyo hebu niache Kwanza"
Ameongea asha huku sadiki akisikitika sana,...
"Shadya ameniambia hilo swala... Haya hali yake vipi na anaendeleaje"
"kwa sasa ana nafuu kidogo"
"nini tatizo kwani"
"kichwa tuuu, na maumivu ya mwili, si unajua tena umri wake na hizi kazi sio sahihi"
Aliongea asha na sasa hamjibu diki vibaya, mana kama kweli ile namba itakuwa ya ndugu yake, basi hana budi kumpenda diki, tena atampenda mpaka basi....
"hebu ngoja mwezi huu uishe... Huo mwezi ujao nitajua cha kufanya"
Aliongea sadiki huku akiondoka na kusema
"lakini hebu tuliza kichwa chako,... Afu kuna deni kule hospitalini?? Manaaaaa.... Shika hii utakwenda kulipa kama anadaiwa matibabu na maradhi yote kwa ujumla"
Sadiki alianza kujipendekeza kwa kutoa pesa, na asha nae hakutaka kuvunga kwani anatamani kupata mwanaume wa kumchuna zaidi afu sadiki alivyo na sifa alitoa bila kuhesabu kisha akampa kitu kama laki mbili au tatu hivi,... Sadiki aliondoka zake kwenda kiwandani kutembelea baadhi ya idara ambazo zinahitaji umaki wa hali ya juu katika uandaaji wa matirio,...
Tukija huku ofisini kwa suria akiwa katulia zake hana kazi ya kufanya mana yeye ni kama anakuja tu ile kuambiwa boss yupo lakini hana kazi ya kufanya kwasababu wafanyakazi wapo wengi wa kuzifanya kazi hizo... Ghafla alimuona mke wake kaeti kwenye kiti, kana kwamba kaja sasa hivi tu...
"pole kwa uchovu mume wangu"
"ahsante mke wangu... Umekuja na chakula, mana nahisi njaa"
"nimekuja twende lanchi"
"aahhh sasa kwanini usije na chakula chako ulichopika wewe"
Aliongea surian, na hapo mke kaja kimazingala sio kwamba kaja kwa miguu...
"natamani kukupikia mume wangu, ila kingepoa bwanaaa"
"kwaio"
"twende hotelini tukale"
"mmmhhh haya twende"
"lakini hatuendi na gari"
"heeeeee sasa tunakwendaje"
"kwa mguu"
"mungu wangu eeeee... Hayo ni masharti au tumeamua"
Suria aliuliza kuwa hayo ni masharti au wameamua mana maimuna kwa masharti ndio mwenyewe...
"hapana mume wangu, sasa hivi hakuna masharti yeyote amua utakaloweza"
Aliongea maimati au maimuna huku wakichukuana, surian yeye hawezi kuwa invisible (kuto onekana) hivyo surian alionekana kutoka mwenyewe lakini yupo na mke wake wanakwenda kula hoteli kwa kutembelea kwa miguu,... Wakiwa wote muna katumbukiza mkono wake kwenye mkono wa surian, lakini mke haonekani ila yupo nae....
"bwana mbona watu wananipamia bwana"
Aliongea muna huku surian akicheka
"nani kakwambia uwe invisible, na utakanyagwa mpaka ukome"
"twende tukachukue gari bwana, mijitu kama haioni"
"sasa wao wana makosa gani, mana wao wananiona mimi tu"
"waambie bwana"
"acha ukichaaaa"
Sasa watu wakawa wanamshangaa surian akiwa anaongea, mana hakuwa akiongea na simu wala nini,.
Walifika mahali husika mjini kati wakiwa wanapata chakula cha mchana, surian kakaa kwenye kiti, na kwa pembeni yake kuna kiti ambacho kakalia mke wa surian, lakini kiti hakionekani kukaliwa, yaani kipo kama hakina mtu lakini kina mtu... Basi walianza kula, tena huku wanacheka sana, ila sasa watu wanaona surian anacheka mwenyewe bila kuchekeshwa, mana watu wanamuona surian pekee,...
Huku kiwandani tariki akiwa na simu yake aliweza kuona picha iliowekwa pale kwenye profile picha, ambayo ni picha ya surian lakini tariki yeye hamjui surian na wala hajui kama ndio boss wake, na mbaya zaidi hio ndio sura aliotumwa na faima, ila sasa hajui kama ni hio mana boss wake hamjui ana sura gani, na asha kamwambia ni mjomba wake,... Riki alifunga simu yake na kuendelea na kazi kwani hamjui mtu anaye mwangalia,... Sasa tariki akaona ngoja aombe namba za meneja sadiki mana ndio boss anaemjua, ili amuangalie picha kwenye WhatsApp faima amuone asije kukosa penzi juu yake... Tariki aliweza kuipata namba ya sadiki,..... Nyakati za jioni wafanyakazi wakiwa wanajiandaa kutoka, yeye riki alisha toka kana kwamba hakutaka kusubiri bus la wafanyakazi,.. Na yote hio awahishe kile alicho kitumwa na faima,... Lakini sasa alipofika mjini kati, alishangaa kumuona mjomba wake asha,...
"heeeeee huyu si ndio yule kwenye picha"
Tariki alijisemea kimoyo moyo huku akimsogelea surian...
"kweli ni yeye mbona"
Alijisemea tena huku akifungua ile picha na kuiangalia kwa mara nyingine tena, na kuhakikisha ni yeye mjomba wake,... Tariki alikimbia mbio mpaka kazini na kumkuta asha ndio anapanda basi kwenda nyumbani
"asha asha.... Mjomba ako nimemuona kule mjini, twende ukamuone"
Aliongea tariki na kumfanya asha atetemeke, mana sio mjomba wake kama alivyo mwambia tariki, bali ni mdogo wake kabisa....
"unasemaje tariki"
"twende sasa unapoteza muda"
"tariki unasema kweli"
"bwana wewe, twendeeeeeee"
Asha alijikuta analia kabla hata ya kumuona mdogo wake wa damu aliosingiziwa kumuua,... Na lazima awe yeye kwasababu tariki asingelimjua kama sio ile namba alio mpa,....
"sasa unalia nini asha... Twende ukamuone mjomba wako"
Sasa asha akiwa anazidi kulia kwa furaha huku wafanyakazi wakimwangalia,.. Ghafla geti dogo linasukumwa, kana kwamba kuna mtu au watu wanaingia.... Wafanyakazi hawaamini kwa kile wanachokiona, hata asha mwenyewe haamini macho yake.......
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2ROggGo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment