Sunday, February 2, 2020

PETE YA KIKE Sehemu Ya 19



"enhee, imba niskie"
Alionge faima kama kwa dharau, kwani anajua moyoni mwake yupo aliojaa....
"najua neno nakupenda kwako umelisikia mara nyingi, ila yote yana uzito wa tofauti tofauti... Je nakupenda yangu kwako ina uzito kiasi gani Fey?? Nakupenda sana fey.. Niangalie basi, najua yupo umpendae, lakini kama unavyosikia tetesi za hapa na pale kuwa mtu huyo kafariki dunia fey,... Tumuombee huko aliko... Ila isiwe sababu ya kuninyima nafasi,.. Nahitaji kutulia na mwenzi wangu... Nina pesa lakini sitaki kuliongelea hilo kwani wewe sio mfanya Biashara kuwa tuzungumzie mambo ya fedha... Fey,.. Moyo unataka kuangua huu.. Fanya jambo basi jamani... Mana pamoja na fedha zangu lakini haziwezi kuzuia anguko la moyo wangu... Hebu ona... Ona sasa moyo huu hapa unachungulia.. Ona huo huo"
Tariki alibwabwaja maneno mia kidogo, ila hakuna aliopanda mahindi akavuna mchicha... Kwa mara ya kwanza faima anatabasam kwa maneno mazuri kutoka kwa tariki,....

ENDELEA.......

Hakika wanaume ni watu wabaya sana, wanaweza kumfanya mwanamke awe atakavyo, iwe kwa mapenzi motomoto au pesa motomoto, mwanamke lazima ukae kwenye namba husika,... Faima aliokuwa mgumu kana kwamba hata kuitika salamu kutoka kwa tariki, kwake ni ngumu, lakini tariki kapiga domo mpaka fey katabasam kwa mara ya kwanza

"waalakhi leo najipa ushindi japo sijafunga goli"
Aliongea tariki huku fey akimuuliza riki kuwa
"wajipa ushindi wa nini"
"Kiukweli fey, sikuwahi kuliona tabasamu lako, Kiukweli limenipa amani ya moyo na kuona kipo kivuli katika moyo wangu, japo baado hakijasogea"
Aliongea tarikwa maneno fulani ya uchombezaji,..
"mmhh una maneno riki,..."
"sio maneno fey,... Ni moyo wangu hautulii kabisa bila kupata mwenza"
"bwana, ebu niache niende nyumbani kwanza"
Aliongea fey kwani mahala walipofika kuna njia ya panda ya kwenda kwao... Hivyo wata achana hapo,.
"ni sawa fey, nipe imani juu ya makutano mengine"
"siwezi kukupa imani now coz, siwezi kukuamini moja kwa moja... Nitakujibu swali lako"
Riki kusikia maneno hayo moyo wake ulimpasuka na kuhisi bahati imemuelemea kuliko wengine
"sawa madam fey,... Ila jua kwa sasa napata jua na hakuna anayeweza kunipa kivuli, ispokuwa wewe fey... Wacha nikuache ili nikupe nafasi ya moyo wako juu yangu... Bye, ulale salama"
"nawe pia"
Kwa sasa fey hakuwa na majibu mabaya kqa riki, kwani keshajua ni mwanaume mwenye maneno mazuri yaliomfanya kutabasamu kipindi kigumu kama hiki ambacho kampoteza mpenzi wake,....

ILANI YA WAHALIFU WA KIMTANDAO

TAHADHARI SANA KWA WEWE UNAYE UZA KAZI HII KATIKA MITANDAO YAKO YA KIJAMII...

HATUA KALI ZITACHUKULIWA KWA KIFUNGU CHA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA MITANDAO, KWA KOSA LA KUHUJUMU KAZI ISIO YAKWAKO..

NDUGU MSOMAJI, HAKIKISHA ANAEKUUZIA SIMULIZI HII NI MMILIKI HALALI MWENYE NAMBA HII, +255714419487... LAA SIVYO NAWE NI MMOJA KATI YA WAHUJUMU WA KAZI ZA WATU, KATIKA MITANDAO YA KIJAMII.....

KWA WALE NDUGU ZANGU WA KUPOSTI KWENYE KURASA ZAO,
HAKIKISHA, UNAPATA IDHINI KUTOKA KWA MMILIKI HUSIKA KWA SIMU NO, +255714419487 WhatsApp
ILI UPEWE MAELEZO, VIGEZO, NA MASHARTI YA KUPOSTI KWENYE UKURASA WAKO WOWOTE ULE..

JIEPUSHE KUKOPI KAZI HII BILA IDHINI YA MMILIKI HUSIKA

TAFADHALI SANA HATUPO KWA AJILI YA KUPELEKANA PABAYA KISHERIA.....

TUWE MAKINI NA KAZI ZA WATU KATIKA MITANDAO YETU YA KIJAMII

Baada ya tariki kuachana na fey, alikutana na rafiki yake jumbe,
"we riki nini sasa"
"acha weweeeee.... Nani kasema mi nakataliwa... Mtoto keshaanza kuingia laini mpaka kalegea kama papai"
"muongo riki"
"aahh... We baki na mineno yako, eti mi muongo"
Aliongea riki akiwa na rafiki yake mr jumbe,

BAADA YA SAAA.... SIKU.... KADHAA KUPITA

Ikiwa leo ndio siku ya Jumatatu, ni siku rasmi ya kufungua kampuni ya MICCO (Moon Islamic Cloth Company) Boss mkuu ambaye ni surian akiwa katika ofisi yake, yaani yeye kuwa wa kwanza katika ofisi yake ndio masharti ambayo kapewa ndani ya siku hizi za karibuni,.. Wafanyakazi walianza kumiminika katika kampuni hio, walimu wa kufundisha wafanyakazi jinsi ya kuzitumia mashine na kutengeneza mavazi maalum ya Kiislamu,.. Shadya au Cecilia ambaye yeye ndio mwenye kujua nani akae wapi na nani akae wapi, kwani yeye ndie alie wapokea na ndio mwenye kujua kila sekta ya mfanyakazi, hivyo walipangwa wote na idara zote zikawa na watu,... Walifelea watu kadhaa tu, lakini haikudhuru kitu chochote,

Walimu Walianza kazi ya kufundisha wafanyakazi hao, jinsi ya kuanza kufuma uzi mpaka kuja kuwa nguo, ikiwa kiwanda kimeanza na nguo za dini pekee,.... Surian akiwa ofisini kwake anaendelea kugawa vitengo kwa wafanyakazi wa ofisini, yaani mameneja, wapokea oda, wahasibu na wengine wengi ambao wana vigezo vya kukaa ofisini na sio kiwandani,....

Mama yake surian akiwa kawekwa kwenye nafasi ya chooni, na hio ni kwasababu tu asionekane kwakua umri wake hauruhusu kufanya kazi katika kampuni hio,...
"samahani sana mama angu, Kiukweli nimefanya juu chini niweze kujenga riziki yako,... Binafsi hata mimi Sitamani ufanye kazi huku,.. Lakini nakuweka huku ili boss asikuone mana huku hawezi kufika"
Aliongea shadya kama kumwelezea mama huyo ili asijiskie vibaya kwakua umri wake hauruhusu kufanya kazi hapo
"usijali mwanangu, pia nakushukuru sana kwa kunisaidia... Nitafanya kazi mpaka utajiskia raha mwanangu.."
Aliongea mama yake surian huku shadya ama Cecilia akisema kuwa
"usijali mama,.. Pia utakua ukijificha pindi unapohisi boss anakuja, afu pia kwakua namba yako ninayo, basi pale nitakapo ona boss anakuja huku nitakupigia haraka ili asikuone"
"sawa mwanangu, mimi nikiona tu simu yako, nitajificha mwanangu... Mungu akuzidishie mama"
"usijali... Na mshahara wako, utalipwa laki nne"
Aliongea shadya huku mama akibaki mdomo wazi, mana anajua kazi ya kusafisha choo hua haina malipo mazuri sasa anashangaa atalipwa laki nne ingali sio pesa kubwa lakini kwa maisha yao yalivyo magumu kwa sasa, hio pesa kwao ni kubwa sana... Na kama unakumbuka huo mshahara sio wa mfanyakazi wa chooni, bali jina la huyo mama lilipewa kipau mbele cha kusimamia wafanyakazi huko idarani, lakini kwakua umri wake hauruhusu kufanya kazi, hivyo ili boss asimuone ilibidi amueke huku chooni, kisha atafute msichana mingine ampe nafasi ya idarani...
"mwanangu, ina maana nitalipwa pesa yote hio"
"hehehehe mama bwana, Usijali hio ni pesa ndogo na pia ukifanya kazi vizuri utaongezewa mshahara"
Aliongea shadya lakini mama huyo bado haamini kwa malipo ambayo analipwa, ikiwa ndio mshahara wa Kwanza wa kazi yake...
Mama alitaka hata kupiga magoti kwa kushukuru,....

Shadya alikwenda idarani na kumweka msichana mwingine kwenye idara aliotakiwa kukaa mama yake surian,
"kazi yako ni kusimamia wafanyakazi na kuhakikisha wanatoa bidhaa bora na zenye uwingi unao hitajika"
"sawa dada, nitafanya kazi kadri ya uwezo wangu"
Aliongea dada huyo huku shadya akimtajia mshahara wake
"utalipwa laki moja na themanini, ikiwa ndio mwanzo wa mshahara"
"waoooo, ahsante sana dada... Nashukuru sana kwa kupata mshahara mzuri"
Dada huyo alifurahi sana,.. Sasa mshahara huo ndio wa mtu wa chooni, na ule wa kitengo chake ndio ule analipwa mama yake suria,... Yaani hapo kuna mgeukano wa kazi na mishahara yao,...

Basi kazi zilienda vizuri na kila mfanyakazi alishika kitengo chake huku akifundishwa katika mashine yake,.. Kiwanda ni kikubwa sana kana kwamba mpaka sasa kina wafanyakazi mia nne tu, hivyo bado wafanyakazi takribani mia moja ili kufikia idadi ya wafanyakazi mia tano,

Ofisini wakiwa wamesha kamilika wafanyakazi 21, akiwemo mmoja ambaye ni mfanya usafi katika ofisi na vyoo vya ofisini,... Ila choo cha ofisi ya boss kipo ndani ya ofisi yake na hua mkewe ndio kaamua kumfanyia usafi mume wake, hivyo ofisini kwa surian, atakuja kufanya mkewe peke yake.... Kumbe hata majini wana wivu na wanaume kiasi hicho, kwani hakutaka kutoa nafasi kwa mume wake afanyiwe usafi ofisini kwake,... Hivyo mfanya usafi ataishia nje ya ofisi ya boss na hatakiwi kuingia ndani,.. Hio sio masharti bali ni wivu wa jini maimuna

Jioni saa kumi na moja mama asha akiwa nyumbani kwake anapiga stori na familia yake, wakiwa watu watatu tu, mana walikuwa wanne pamoja na surian, lakini kwa sasa wapo watatu mana surian katoweka nyumbani hivyo hawajui kama kafariki au yupo hai.. Lakini kwa sisi wasomaji tunajua surian yupo hai na mama huyo anafanya kazi kwa mtoto wake bila kujua,...
"yaani bana asha, nalipwa mshahara mkubwa jamani, haaaaa... Yaani mpaka natetemeka"
Aliongea mama huyo huku mzee Rashidi ambaye ndio baba yake surian akiuliza kuwa,
"kwani kitengo gani wamekupa"
"baba asha, kwani mimi nimetaka Mashauzi, mimi nafanya usafi wa chooni"
"haaaaaaaaaa, mama muongo... Ina maana mfanya usafi wa chooni ndio alipwe pesa yote hio"
Aliuliza asha huku mzee rashid akianza kuogopa kana kwamba labda mkewe kapendelewa kutokana na mwili wake, mana mama surian pamoja na umri mkubwa alio nao lakini anazeheka na umbo lake,...
"kwahio mama asha, unalipwa laki nne afu unadeki vyoo"
"ndio baba, asha"
"uuuuufyuuuuuuuuuu"
Baba asha alipumua kwa kuchoka na kujua mkewe keshajilipua na vijana mana, mama yake suria kama ni wale wamama wasio jielewa, basi ndio ule wakati wa kuchukua vijana wadogo, japo ana umri mkubwa lakini uzuri na umbo, ni kama bado anavyo,.. Na yote hio ni kwasababu ya matunzo alio tunzwa na mume wake, kwa umri huo kijijini ni mzee wa miaka 70, lakini kwakua yupo mjini basi anakuwa anakwenda na umri wake....
"baba asha, mbona umepumua kwa nguvu hivyo"
"aaaaa tutaongea usijali"
Aliongea mzee huyo huku mama asha akiwa na wasiwasi kuwa mume wake anataka kusema nini,
"asha mwanangu, naskia nafasi bado zipo, kwanini nawe usiende mwanangu..."
Aliongea mama huyo kuwa kwanini asha asiende kuomba kazi,
"aahhh mama, hebu wacha kwanza nitulize akili yangu kwanza mama... Mana sasa hivi hata simu yangu nimeuza na laini nimetupa mana staki mawazo"
Aliongea asha huku mzes rashid akisema
"huyu mtoto ana kichaa huyu, yaani kauza na simu afu laini katupa"
"baba asha, huezi jua... Haya wewe asha kwanini ufanye hivyo"
"mama.... Yaani kwenye group letu la wasapu nasemwa mimi tu, meseji zinakuja naambiwa mimi muuaji... Sitaki kabisa mimi sitaki"
"lakini ni bora ungezima simu tu"
"msijali, nitakwenda kuomba kazi ila sio leo"
"sasa kama sio leo mwanangu, nafasi si zitajaa"
"kama sio riziki yangu baba, hata nikienda sasa hivi sitapata"
"lakini ni vyema kuwahi"
"basi nitakwenda wiki ijayo"
Aliongea asha kuwa kakubali kwenda kuomba kazi wiki ijayo,.. Sasa lile agizo la maimuna kumtaka surian aajiri familia yake ndio linakwenda kutimia,...

"habari za kazi mume wangu"
Maimuna au maimati alimsalimia mume wake huku akimvua tai, mana suria yeye ndio wa kwanza kuingia kazini na ndio wa mwisho kutoka kazini, hatakiwi kuonwa na mtu yeyote yule ndani ya wiki hizi za karibuni,....basi suria alikwenda kuoga kisha akapata chai ili kusubiri chakula cha jioni, wakiwa wawili tu na mke wake,.... Sasa wakati surian kakaa kwenye sofa akipata chai, na mkewe akiwa jikoni anafanya mambo ya chakula cha jioni,.. Ghafla alianza kushikwa shikwa nyuma ya shingo yake....
"mke wangu acha utani... Hebu kapike mi nataka kulala"
Aliongea surian,... Lakini na huku jikoni, maimuna naye kuna kitu kahisi ndani ya nyumba yake,... Huku sebuleni, surian anazidi kushikwa na anaemshika yupo nyuma ya sofa, na kwakua suria anajua ni mke wake hivyo katulia na kusapoti kushika mkono wa huyo mwanamke ambaye anamshika,... Lakini surian kuangalia huo mkono, laaaaaaa haulaaaaaa








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/31f961a

No comments:

Post a Comment