Tuesday, February 4, 2020
KITUMBUA CHA KIHINDI SEHEMU YA 07
ILIPOISHIA
Bi.Fahreen akajikuta akiishiwa nguvu na kulegea huku akishindwa kujizuia kutetemeka. Nakeshiwar alishika kitasa cha mlango wa chooni na kumgeukia mke wake.
“Leo iko problem” alisema Nakeshiwar akiwa amesimama sawa na mlango.
Kule chooni Magosho alijikuta akijikojolea kwa kitete alichokuwa nacho. Alisikia jinsi kitasa cha mlango ule wa chooni kilivyokamatwa barabara na Mr. Nakeshiwar. Akajikuta akiijutia nafsi yake kwa kukubali kuingia chumbani mle.
“Masikini ninahukumiwa bila hatia” alijisemea Magosho huku akiwa amejikunyata kwenye pembe ya choo kile kilichokuwa kidogo kiasi cha kukosa pa kujificha. Alikuwa akimhurumia sana mdogo wake Ashura ambaye angebakia mpweke baada ya kifo chake ambacho kingemkuta muda mfupi uliofuata. Ghafla kitasa cha mlango ule kilinyongwa na mlango ukaanza kusukumwa ndani. Masikini Kijana Maosho akahisi haja kubwa nan doo zikikaribia kumtoka kwa pamoja.
ENDELEA….7
Mr. Nakeshwar alipokuwa akisukuma mlango simu yake ya mkononi iliita. Aliipokea na kuanza kuongea na mtu aliyempigia huku akiwa amesimama kwenye mlango wa choo ambao ulikuwa wazi. Aliuwachia ghafla mlango ule na kurudi kitandani ambako alichukua mafaili yake na kuyaweka kwenye bahasha kisha akamgeukia mke wake.
“Najua kuna kasoro. Lakini niache niende sitachelewa kurudi” alisema Nakeshiwar na kutoka kwa kasi ya ajabu mle chumbani. Inawezekana simu aliyopigiwa ndiyo iliyomfanya kuwa na haraka kiasi kile.
Magosho akiwa nyuma ya mlango wa choo hakufahamu kilichokuwa kinaendelea huko nje. Alikuwa amesimama sawasawa na ukuta huku akiwa amefumba macho. Bi.Fahreen alimfuata nyuma mume wake na kuhakikisha kuwa alipanda gari na kuondoka. Alirejea chumbani kwake na kufungua mlango wa chooni. Alimtoa Magosho haraka sana kisha akaenda kujitupa kitandani. Hakuamini kama alikuwa amepona kuachika ama kuuliwa na jamaa yule wa kihindi.
Magosho alijikuta miguu ikigongana na kushindwa kutembea. Hakuweza kuelewa ni kwa namna gani aliweza kutoka chumbani mle akiwa salama. Mawazo yake aliamini kuwa ndani ya nyumba ile angetolewa kwa machela tena akiwa maiti. Akaapa kuwa hatothubutu kumkaribia tena Bi.Fahreen.
* * *
Ashura aliendelea kufanya biashara vizuri kutokana na mtaji aliopewa na kaka yake mpendwa Magosho. Mtaji wake wa kuchoma vitumbua ulikuwa kiasi cha kumuwezesha kufungua saluni ndogo ya wanawake. Pamoja na kwamba saluni ilikuwa ikimuingizia pesa kwa kiasi kikubwa lakini biashara yake ya kukaanga mihogo na kuchoma vitumbua hakuiwacha. Aliweza kufanya vyote hivyo kwa wakati mmoja. Asubuhi alijikita katika kuchoma vitumbua na mchana alikwenda saluni.
Kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele ndivyo akili ya Ashura ilivyokuwa ikikomaa kibiashara. Malengo yake yalikuwa ni kukua zaidi na kuwa miongoniwa wafanya biashara wakubwa sana jijini Dar. Hivyo wakati wote alikuwa akiumiza kichwa chake kuona ni mbinu gani atumie katika kukua kwake kibiashara.
Pesa ambazo alizikusanya kwenye kupika vitumbua na nyingine alizopewa na kaka yake mpendwa alichanganya na pesa zilizopatikana saluni kisha alizipeleka dukani kununulia vifaa vya saluni. Kitendo kile kilipelekea Ashura kubakiwa na pesa za mtaji wa vitumbua tu tena zilikuwa ni za mtaji mdogo sana. Aliamini mtaji wake ungeweza kurejea katika hali yake ya kawaida punde saluni ile itakapoanza kumuingizia pesa kwa kasi kutokana na zana mpya ambazo aliziongeza.
Siku moja akiwa kwenye biashara yake ya vitumbua alifika mteja mmoja aliyekuwa anahitaji vitumbua.
“Hivi Ashura ni kweli au unajichetua tu?” mteja yule alizungumza wakati Ashura alipokuwa akimfungia vitumbua mteja wake.
“Kwanini mteja wangu?” alihoji Ashura huku akiendelea kumfungia mteja wake.
“Mnh una moyo shoga” mteja yule alizungumza huku akipokea vitumbua vyake kutoka kwa Ashura.
“Mbona sikuelewi jamani”
“Leo umefika saluni kwako?”
“Hapana, namalizia hapa niende kufungua”
“Mnh, kweli hujui kitu?” alihoji mwanamke yule.
“Mbona sikuelewishoga, kwani kuna nini?” alihoji Ashura huku akimtazama kwa makini mteja yule.
“Mnh umbea huu nao” mwanamke yule akajisemesha.
“Hebu niambie bwana ni kitu gani kinaendelea” Ashura alianza kupatwa na mashaka kutokana na maneno ya yule mteja wake.
“Shoga umeumia, kama kweli haufahamu basi hiyo ndio taarifa” alizungumza mwanamke yule na kuanza kundka.
“Wewe hebu subiri kwanza” Ashura alijaribu kumuita mwanamke yule ili ampatie maelezo ya kueleweka.
Nakwambia mwanamke yule alikuwa kama vile ametumwa kwenda kumwaga umbea na kuondoka. Pamoja na kwamba Ashura alipaza sauti kumuita lakini hakugeuka nyuma wala kuongeza neno lolote. Alikuwa akitembea huku akijitikisa kishankupe na kamkono kake akikachezesha utafikiri kalikuwa kanadondoka.
Ashura alifunga haraka haraka biashara yake na kuita boda kuelekea huko saluni ambako Shankupe yule alikuw amejaribu kumpatia taarifa zilizokuwa hazieleweki.
Ndugu msomaji huwezi kuamini alichokikuta huko saluni kwake binti yule aliyekuwa mchakarikaji katika kusaka mshiko. Saluni ilikuwa imevunjwa na vibaka kisha vifaa vyote vilikuwa vimeibwa. Ama kweli ng’ombe wa masikini hazai, na wa moja havai mbili.
Alishindwa kujizuia kutoa machozi na kulia kwa kwikwi kutokana na uchungu uliokuwa ukifukuta ndani ya kifua chake. Aliinua macho yake na kuangalia mawinguni huku akisikitika kama vile anatupa lawama kwa Mungu kutokana na kile kilichokuwa kimemtokea.
“Kwanini mimi Mungu wangu! Kwanini kila siku ni mimi tu na kaka yangu?” alizungumza kwa uchungu Ashura huku akiendelea kumiminika machozi kwenye mashavu yake.
Hata kama angelia hadi kupasuka unadhani ingesaidia nini? Akajikokota kwa taabu kujirudisha nyumbani huku akihisi mzigo mkubwa sana wa dunia ulikuwa kichwani mwake.
Mtaji ule wa saluni ulipatikana kwa mbinde tena kwa muda mrefu sana. Kutokana na sababu ile ingewachukua muda mwingine mrefu sana kukusanya pesa kwaajili ya kufungua tena saluni. Kwa kifupi Ashura aliamua kukata tamaa ya kufanya biashara ya saluni pamoja na kwamba ndiyo aliyokuwa akiitegemea kama njia kuu ya kumtoa kimaisha yeye pamoja na kaka yake Magosho.
****
Taarifa za kuvunjwa kwa saluni ya Ashura na kuibiwa ilimfikia Magosho na kumfanya kuwa na simanzi wakati wote. Alimhurumia sana mdogo wake, hakupenda kumuona akipata taabu ama kuwa ni mtu mwenye hudhuni. Alifahamu wazi kuwa tukio lile lilikuwa limemuumiza sana mdogo wake kipenzi Ashura.
Akiwa amekaa kwenye jiwe moja kubwa lililopo nje ya nyumba ya Mr. Nakeshiwar akiendelea kuwaza na kuwazua namna ya kujikwamua kimaisha yeye na mdogo wake. Mambo yote yaliyokuwa yakimtokea aliyaona kama vile alikuwa ni chukizo kwa Mungu. Kama kweli Mungu ndiye mpangaji wa kila jambo, ni kwanini ameamua kuipangia familia yake matatizo kiasi kile. Hata hivyo hakuwa na namna kwasababu hata yule aliyekuwa anamlaumu hakuwa anampa maelezo wala majibu yoyote. Akavuta pumzi na kuziruhusu kutoka nje kwa kuzisukuma kwa nguvu. Alitamani kupata pesa za haraka ili kurudisha mtaji wa dada yake na kurejesha Amani ya moyo wa ndugu yake huyo. Lakini angezipata wapi hizo pesa? Mshahara ambao alikuwa akipewa ulikuwa hautoshi ingawa uliongezwa mara mbili na yule mwanamke wa kihindi.
Bi.Fahreen ambaye alikuwa ndani akatoka huku kiunoni mwake akiwa amejifunga Kitambaa kirefu kilichofika hadi chini na juu alivalia kiblauzi kifupi ambacho kiliacha wazi tumbo lake. Na begani alikuwa ameweka mtandio uliokuwa wa kitambaa laini. Kwa ufupi ni kwamba alikuwa amevalia kiasili, yaani kihindi. Alipomuona Magosho amejiinamia mama yule akamsogelea taratibu na kwenda kuchutama mbele yake.
“Vipi Goso, iko problem?” alihoji Bi.Fahreen kwa sauti iliyo jaa huruma na upendo.
“Hapana mama” Magosho alijibu kwa mshituko kidogo kwasababu hakuwa ametegemea kupokea swali kutoka kwa mtu yoyote yule hasa kwa wakati ule.
“Hapana wakati iko najiinamia kama jingajinga” alizungumza mama yule kwa msisitizo.
“Ndio mama nina tatizo”alijibu Magosho kwa unyonge pasipo kumtazama Mwanamke yule usoni.
“Mimi weza saidia veve?” alihoji Bi.Fahreen kwa umakini mkubwa.
Magosho akawa kimya akitafakari lile swali la Bi.Fahreen. Aliamini kabisa alikuwa na uwezo wa kumsaidia. Lakini hakupenda kutoa matatizo ambayo yalikuwa yakimkabili ndani ya familia yake. Siku zote alipendelea kujaribu kwanza kupambana na changamoto na kama angeshindwa basi angemwambia mtu mwingine hasa kama kungekuwa na ulazima.
Sababu nyingine iliyokuwa ikimpa kigugumizi Magosho ni kwamba alikwisha zifahamu tabia za mama yule wa kihindi ambazo hakuwa anazipenda. Alikuwa akijitahidi kujiweka mbali naye ili asije kumletea balaa kutoka kwa mume wake. Hivyo aliamini kama angemueleza suala lile, lingekuwa ni sababu tosha ya kuwaweka karibu jambo ambalo hakutaka hata kulisikia. Aliinua macho na kumjibu.
“Hapana mama. Hakuna tatizo”
“Veve si iko sema iko problem?”
“Mwili tu umechoka, lakini naamini utakuwa vizuri punde” Magosho akajibaraguza.
“Pole sana Goso. Mimi taka veve sindikize mimi” alisema Bi.Fahreen.
“Wapi mama!” Magosho alihoji kwa kuhamaki.
“No swali! Sema sindikize mimi”
“Lakini mama, nilikuwa nataka kuandaa chakula cha mtoto” Magosho alijaribu ili kuweka vikwazo makusudi vya kutoka na mwanamke yule.
“Nakuwa jeuri sio?”
“Hapana mama”
“Nabisana na mimi?”
“Hapana mama, nilikuwa nasema tu?”
“Bosi yako iko ndani nalala, nataka veve sindikize mimi. Kama iko kataa sema”
“Sawa mama twende” alijibu Magosho huku akijiinua kutoka pale kwenye jiwe. Ilibidi akubali tu kwasababu kama angekataa kufanya vile, yule mwanamke angekwenda kushitaki kwa mume wake na kumletea shida Magosho. Hivyo hakupenda kuongeza matatizo juu ya matatizo mengine.
Walikwenda kuchukua gari ya Mr. Nakeshiwar na kuondoka nayo ikiendeshwa na Bi.Fahreen. Mazingira ambayo gari ile ilipokuwa ikielekea hayakuwa mageni sana kwa Magosho. Siku moja alikwisha fika akiwa na mke wa bosi wake yule yule Bi.Fahreen. Kumbukumbu za matukio yaliyomtokea siku ile zikamjia. Kule ndiko siku hiyo Bi.Fahreen aliyokuwa amezidiwa na kulegea kutokana na ugonjwa wa ajabu. Gari ile ilikwenda kusimama mahali pale pale ambapo ilisimama siku walipofika kwa mara ya kwanza. Bi.Fahreen akamgeukia Magosho na kumtazama kidogo kisha akanyunyizia tabasamu la huba.
“Mbona kama iko poteza raha. Iko problem?” alihoji Bi.Fahreen huku akimtazama Magosho usoni.
“Hapana mama niko sawa” alisema Magosho huku akiachia tabasamu la bandia.
“Najua Goso, mimi hapana penda ona veve kosa raha. Naleta hapa leo fundise gari” alisema Bi.Fahreen kwa sauti iliyokuwa imejaa upendo.
Maneno ya kufundishwa kuendesha gari yalizidi kumchanganya Magosho. Alikumbuka kuwa siku waliyofika eneo lile maneno yalikuwa ni yale yale na mwisho wake kukatokea balaa.
“Huyu mhindi wa watu leo atanifia. Sijui nikimbie?” Magosho aliwaza.
“Vipi mbona iko kaa kimya?” alihoji Bi.Fahreen.
“Niko sawa mama” Magosho alijibu huku akisubiria tukio ambalo lingefuata. Siku ile aliambiwa aende kukaa kwenye kiti kilichokuwa na usukani lakini asiteremke bali wapishane mule mule ndani ya gari, jambo ambalo mwisho wake likazua balaa.
“Basi kuje kae huku” alizungumza Bi.Fahreen. Magosho alitaka kushuka ili aende kukaa ule upande uliokuwa na usukani ambao alikuwa amekaa Bi.Fahreen.
“No. hapana veve suka, pitie hapa hapa” alizungumza Bi. Fahreen kama alivyozungumza siku hiyo ya balaa.
“Mnh!” Magosho akajikuta akiguna. Ni wazi balaa lililotokea siku chache za nyuma lilikuwa na dalili zote za kutokea tena kwa mara nyingine siku ile.
TUTAKUTANa
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2vQVD41
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment