Tuesday, February 4, 2020

JE VIPELE VINAVYOZUNGUKA CHUCHU YA TITI VINAMAANISHA NINI?? VIPELE HIVI NI NIN HASA?





Vipele hivi nim tezi ya MONTGOMERY.kila binadamu ana tezi hizi. Tezi hizi zinakuwa kwenye sehemu nyeusi inayozunguka chuchu kitaalamu inaitwa areola. Muonekano wa tezi hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu.Titi la mwanamke lin tezi hizi zisizopungua 9.

MABADILIKO WAKATI WA UJAUZITO
Wakati wa ujauzito mama hupata mabadiliko kwenye matiti ikiwemo tezi hizi kuongezeka ukubwa na idadi yake kuongezeka.Haupaswi kuogopa kwani sio tatizo la kiafya. Kikawaida tezi hizi uongezeka katika kipindi cha kuanzia miezi mitatu ya ujauzito

KAZI ZA TEZI HIZI NI

1.Kuzuia maambukizi kwenye titi.
Tezi hizi huwa zinazalisha kimiminika mithili ya mafuta ambacho husaidia kuua wadudu waletao magonjwa.Hii inakusaidia kuzia wadudu wasidhuru titi.

2.Kufanya ngozi ya chuchu na sehemu inayoizunguka kuwa laini kutokana na kimiminika hicho zinachozalisha
3.Kusaidia mtoto kuliona titi.
Tezi hizi zina umuhimu wakati wa kunyonyesha hasa pale mtoto anapokua bado hajaanza kuona.Mtoto huwa anajua harufu ya maji maji ya kwenye kizazi (amniotic fluid) hivyo tezi hizi zinazalisha kimiminika ambacho kinakua na harufu sawa na hayo maji ili kumwezesha mtoto kulipata titi kwa kutumia harufu.

JINSI YA KUSAFISHA
Kwa wale ambao tezi hizi zinakuwa kubwa na kutengeneza kimiminika kwa wingi, hupaswi kuminya/kukamua. Kimiminika chake kinapozidi juu unasafisha na kitambaa na maji masafi. Hakikisha kitambaa chako ni kisafi.

ZIPO SABABU ZINAZOPELEKEA TEZI HIZI KUWA KUBWA.
1.kusismka mwili.Mfano wakati wa tendo la ndoa
2.maambukizi
3.Baridi kali
4.kuvaa nguo zinazobana sana matiti.








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/31o7SAJ

No comments:

Post a Comment