Kukosa choo ni tatizo kubwa katika jamii zetu japo huwa halionekani kama ni tatizo. Hata hivyo kuna vyakula ambavyo vinapatikana kwa urahisi na vinasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa njia rahisi kabisa.
Kwa kawaida mtu mwenye afya njema anatakiwa kwenda chooni angalau mara tatu kwa siku,lakini si ajabu kusikia mtu hajaenda chooni siku tatu na tunaona ni kawaida sana kwenda chooni mara moja kwa siku.
Tatizo la kukosa choo (Constipation) linatokana na chakula tunachokula kuchelewa kuunguzwa tumboni hivyo kuchukua muda mrefu katika mfumo wa usagaji.
Tatizo hili linasababishwa na mfumo wa chakula kukosa baadhi ya mahitaji ili kufanya kazi yake ya usagaji. Vitu hivi ni maji na vyakula vya fiba (Vyakula vyeneye nyuzinyuzi) ambavyo ni muhimu sana kuharakisha zoezi la usagaji wa chakula tumboni.
Baadhi ya Vitu vinavyosababisha Tatizo la kukosa Choo:
Kutokunywa Maji ya Kutosha
Kutokula vyakula vyenye fiba kama matunda na mboga za majani
Ulaji wa nyama nyekundu kwa wingi
Unywaji wa maziwa kupita kiasi
Kutofanya kaziza kushughulisha mwili na kukosa mazoezi
Vyakula Vinavyosaidia Kutibu Tatizo La Kukusa Choo
Tende
Tende zikiwa kavu au kama juisi inasaidia kuondoa tatizo la kukosa choo. Tende zina fiba kwa wingi hivyo kusaidia zoezi la usagaji chakula tumboni. Pia Tende zina kemikali ya sorbitol–aina ya sukari ambayo inatajwa kusaidia usagaji chakula.
Maji
Kunywa maji kwa wingi kunasaidia kutibu tatizo la kukosa choo kwa kuwa maji yanachochea usagaji wa chakula na kufanya choo kuwa laini. Fiba zinahitaji maji ili kufanya kazi ya kufagia uchafu tumboni na maji yanapokosekana hunyonya toka katika uchafu tumboni na kufanya choo kuwa kikavu na kusababisha ugumu wa kutoka.
Wataaramu wa afya wanashauri kunywa galsi 6 mpaka 8 za maji kila siku( Lita 1-2 kwa siku)
Kama kunywa maji ni ngumu kwako basi jaribu kuweka vipande vya matunda kama ndimu ,limao,tikiti maji na aina nyingine ya matunda.
Kahawa na Vinywaji vingine vya moto
Kahawa na vinyaji vingine vya moto husaidia kusukumwa kwa chakula tumboni na kupata choo.
Matumizi ya muda mrefu ya kahawa yanaweza pia yakaongezea tatizo. Kama unatumia kahawa kwa wingi unashauriwa kunywa maji mengi pia,vinginevyo itaongezea tatizo la kukosa choo
Ulaji wa Matunda au Saladi
Matunda yanasaidi kutibu tatizo la kukosa choo kwa vile yana fiba kwa wingi. Lakini matunda yanasaidia kuongeza maji maji hasa matunda kama matikiti.
Pia ulaji wa matunda ni muhimu kuzingatia muda wa kula, ni vyema kula matunda saa moja au dakika 30 kabla au baada ya chakula. Kula matunda mara baada ya kula kama wengi wanavyofanya ni makosa na kunakukosesha faida zinazotarajiwa.
Ulaji wa Mboga za Majani
Mboga za majani kama ilivyo matunda ni chanzo kizuri cha faiba ambazo ni muhimu sana katika usagazi na usukumaji wa chakula.
Mchicha, Spinachi,karoti na mboga mboga nyingine ni muhimu kuwepo katika chakula cha kila siku.
Maharage na aina nyingine za kunde kunde pia zina fiba kwa wingi na zinasaidia kupunguza tatizo.
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2pSNCsR
No comments:
Post a Comment