ILIPOISHIA:
Mara nikashtuka kusikia mlango wa chumba changu ukigongwa! Mwanzo nilihisi kama nimesikia vibaya lakini haikuwa hivyo, ni kweli mlango ulikuwa ukigongwa, nikakurupuka huku macho yakiwa yamenitoka pima, nikajua hatimaye ndege mjanja nimenasa kwenye tundu bovu!
SASA ENDELEA...
“Chandeee! We Chandeee!”
“Naaam!”
“Funguaa,” sauti ya baba mdogo ilisikika nje huku akiendelea kugonga mlango kwa nguvu, nikajua nimekwisha. Nilichokifanya, nilirudi pale kitandani ambako mama mdogo alikuwa amekaa, amekodoa macho akiwa hajui nini cha kufanya! Ama kwa hakika arobaini za mwizi zilikuwa zimetimia.
“Ingia uvunguni,” nilimwambia, harakaharaka akafanya kama nilivyomwambia, nikasokomeza nguo chafu kule uvunguni na kumfunika kabisa. Nikaenda kufungua mlango huku kijasho chembamba kikinitoka.
“Mbona umechelewa kufungua mlango kiasi hiki?”
“Nilikuwa nimelala ba’mdogo, shikamoo!”
“Ulikuwa umelala? Halafu mbona unatokwa na jasho jingi kiasi hiki?”
“Najihisi kama nina homa, na feni ya humu ndani mbovu,” nilimwambia huku nikitetemeka mwili mzima. Hofu niliyokuwa nayo moyoni mwangu ilikuwa haielezeki, nikajiinamia.
“Sasa weweee...” alisema baba mdogo huku akiingia chumbani kwangu, nilitamani nitoke nduki kali kwelikweli, ila mwili haukuwa hata na nguvu za kukimbia, nikarudi na kukaa kitandani huku nikitumia shuka langu kujifuta jasho.
Laiti kama baba mdogo angejiongeza kidogo tu, angeweza kugundua kwamba nilikuwa namdanganya kwa sababu mazingira ya mle ndani yalikuwa yanaonesha wazi kabisa kwamba kuna tukio lilikuwa limetoka kufanyika, tena muda huohuo!
“Kama unaumwa kwa nini huniambii? Au kwa nini hata humwambii mama’ako mdogo? Utakuja kufa humu ndani buree,” alisema huku akinitazama kwa macho yaliyoonesha kwamba ameukubali uongo wangu.
“Jiandae uende ukapime malaria,” alisema huku akitoa noti ya shilingi elfu kumi na kunikabidhi.
“Nilitoka asubuhi sana leo, kuna mahali nilikuwa nimeenda kufuatilia fedha zangu fulani hivi, ukisharudi hospitali uje nina mazungumzo na wewe kuhusu biashara yetu,” aliniambia huku akiinuka kutaka kutoka, ghafla akawa ni kama amekumbuka kitu.
“Mama’ako mdogo yuko wapi?”
“Hata sijui, huko nje sijatoka kabisa!”
“Tena nimekumbuka!” alisema baba mdogo huku akirudi na kukaa pale kitandani kwangu, akanionesha na mimi ishara nikae pembeni yake.
“Ujue Chande wewe ni mwanaume mwenzangu na siku hizi umeshakuwa mkubwa kwa sababu kwanza unaingiza wanawake wakubwa humu ndani kuliko hata mama yako mdogo! Katika siku za hivi karibuni unamuona mama’ako mdogo yupo karibu na mwanaume gani hapa mtaani maana nyendo zake zinanitia mashaka.”
“Mh! Kwa kweli sifahamu baba kwa sababu muda mwingi mimi huwa sikai nyumbani, lakini muda mwingi ninapokuwa hapa huwa namuona yupo bize na biashara yake.”
“Ujue hawa wanawake siyo watu wa kuwaamini kabisa! Nahisi kuna mjinga mmoja ananilia mali zangu! Siku nikimgundua nitaua mtu haki ya nani tena! Nampenda sana mke wangu.
“Sasa nakupa kazi, hebu mfanyie uchunguzi wa chinichini bila mwenyewe kujua! Nataka jina tu la huyo anayecheza na mali za watu, nitamchinja kama mbuzi na nitahakikisha natenganisha kabisa kichwa, bora nikafie gerezani!
“Yaani mimi nahangaika kumlea mwanamke anapendeza halafu mtu mwingine aje kujilia kirahisirahisi tu, tena siku nikimkamata itabidi kwanza nimuoe ndiyo nimchinje,” alisema baba mdogo huku akionesha kutokuwa na hata chembe ya masihara.
Mapigo ya moyo yalinilipuka na kuanza kunienda mbio kwelikweli, nikawa navungavunga kwa kumtetea mama mdogo, ila nikamhakikishia kwamba nitaifanya kazi yake kama alivyonituma.
“Wahi kwenda hospitali, akija usimwambie kwamba nilirudi,” alisema baba mdogo huku akitoka na kuurudishia mlango, nikashusha pumzi ndefu na kutoka kuhakikisha kama kweli ameondoka. Ilibidi kwanza nikimbilie msalani kwa sababu hali niliyokuwa nayo ilikuwa haielezeki, nadhani kama angeendelea kunibana kidogo tu haja ndogo ingenitoka.
Harakaharaka nilirudi ndani na kutoa mafurushi ya nguo kule chini ya kitanda, nikampa ishara mama mdogo atoke, akatoka huku na yeye akitetemeka kuliko kawaida. Hakukuwa na mazungumzo, harakaharaka alijifunga kitenge chake vizuri, akaelekea ndani kwake mbiombio.
“Ooh! Ahsante Mungu,” nilisema huku nikiinua mikono juu kama ishara ya kumshukuru Mungu wangu, ama kwa hakika nilikuwa nimeponea kwenye tundu la sindano. Baada ya mama mdogo kwenda kule ndani kwake, harakaharaka nilienda bafuni kujimwagia maji kwa sababu hali niliyokuwa naihisi ilikuwa haielezeki.
Nilirudi chumbani kwangu na kuanza kujiandaa, zile nguo nilizokuwa nimezivua awali, nilizivaa tena na kujiweka sawa. Muda huohuo nilimsikia mam’dogo akiwa anajimwagia maji bafuni!
Nikafunga mlango harakaharaka na kutoka huku bado nikiwa na hofu kubwa ndani ya moyo wangu, bado nilikuwa siamini kama nimenusurika kwenye mtego ule hatari. Wakati namalizia kufunga mlango, mam’dogo naye alikuwa anatoka bafuni, akaniangalia kwa macho ya kuibia kisha harakaharaka akaelekea ndani kwake.
Nadhani maneno ya mumewe yalikuwa yamemjaza hofu kubwa ndani ya moyo wake kuliko kawaida kwa sababu hata lile tabasamu lake la siku zote lilipotea kwenye uso wake. Nilitoka kimyakimya na safari ya kuelekea ‘hospitali’ ilianza.
Kumbe baba mdogo hata hakuwa ameenda mbali kwa sababu wakati natoka getini, nilikutana naye akiwa anaingia, mkononi akiwa amebeba mkate, nadhani ni kwa ajili ya kunywea chai.
“Ndiyo unaenda hospitali?”
“Ndiyo baba!”
“Sawa, basi usichelewe! Kama hela haitakutosha utanipigia simu,” aliniambia huku akinipisha nipite, nikaondoka ‘wanguwangu’ na kupotelea mitaani, huku moyoni nikiwa sijui nini kitakachotokea kule ndani kati yake na mkewe.
Licha ya misukosuko hiyo iliyotokea, bado mipango yangu ya kwenda kuonana na Jack ilikuwa palepale, nilipofika kituoni, nilimpigia simu, akapokea na kuanza kulalamika eti kwa nini sijafika mpaka muda huo.
“Foleni mama, nipo jirani nakuja lakini kuna bonge la foleni, usijali nakuja!”
“Fanya haraka bwana,” alisema Jack kwa sauti ya kudeka flani hivi, nikakata simu na kushusha pumzi ndefu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2DvC6qp
No comments:
Post a Comment