Episode 1 sehemu ya nane
Niliangalia hali nikaona itakuwa ni taabu nilichoamuwa nikamuomba afande tuingie ofisini kwake,
"Una shida gani?
"Twende ofisini nitakwambia,,
Alikubali tukazama ofisini,
"Una shida gani?.
"Afande nisaidie kwa hili naomba uwaambie wale wanawake waondoke uwambie warudi saa moja ila vicky umuache ukifanikisha hilo nitakupa laki mbili keshi sawa mkuu,
"Mh!!! Kwasababu ni pesa acha nikusaidie,
Afande alitoka nje akamuita vicky,
"Mheshimiwa nakuomba ndani mara moja,
"Sawa afande,,
Vicky aliingia akanikuta ofisini,
"Izzo mambo vp?.
"Safi tu mpenzi wangu,
"Pole mpenzi ndio dunia hii my love,
"Nimeisha poa swty,
Afande akiwa nje akawaamuru wale watu waliokuja kwenye kesi yangu waondoke,
"Jamani nawaomba mrudi jioni saa moja mrudi kumchukua mtu wenu kuna vitu tunamalizia lakini tutamuachia saa moja,
"Afande nilikuwa naomba kuonana naye kidogo,
"Dada zainabu kwa sasa huwezi kumuona ila jioni uje umchukue,
"Sawa,
Walitii wakaondoka kila mtu njia yake,,
"Izzo tunakuachia ila kuwa makini maana misaada yako huruma yako inaweza kukuponza siku nyingine,,
"Sawa afande nimekuelewa,
"Basi mheshimiwa mchukue mtu wako akapumzike,
"Asanteni sana nimeishaonana na afande shabani chassamba atakupatia mzigo wako mkuu,
"Sawa nashukuru mheshimiwa, maneno hayo aliambiwa vicky na mkuu wa kituo,
Niliondoka na vicky tukaingia kwenye gari,
"Izzochapa leo mzee yupo sijui nikupeleke hotel ukapumzike?
"utakavyoona mwenyewe,
"Nitakavyoona vipi?.
"Wewe umesema nini?.
"Izzochapa mbona umekuwa mkali?
"Hebu simama hapo mbele mm nishuke,
Akasimama aliposimama nikatoka kwenye gari,
"Nikamwambia Safari njema kapumzike na babu yako,,
"Izzo izzo iiiiiizo,,
Sikuitika niliondoka zangu nilitafuta sababu ya kuondokea pale mana nilichanganyikiwa sana kwa kuondokewa na laaziz wangu shamsa ,,,,,,,,,,,,
Niliita boda boda nikapanda nikaondoka zangu kuelekea kwangu kujua hatima ya mwili wa shamsa,
Kila nilipomkumbuka shamsa nilihisi kupagawa nilimpenda sana tena kutoka moyoni mwangu,,
Nilifika nyumbani niliposhuka kwenye boda boda kila mmoja alishangaa sana kwani walijiuliza nimeachiwa vipi?
Niliingia ndani kwangu kuangalia mazingira nilikuta vitu vimevurugika ndani nikashangaa sana, nilianza uchunguzi ila kuangalia mezani niliona simu ya shamsa nikaichukua niliangalia simu zilizoingia mda wa jana,
Nilikuta namba ya rwanda na meseji iliyosema, *ejo nzaba ngeze dar es salaam* iliandikwa kwa lugha ya kinyarwanda maana yake (kesho nitakuwa dar es salaam)
Nilipofuatilia sms zote nilibaini ni mdogo wake na shamsa alikuwa anakuja dar es salaam kuonana na dada yake,
Alikuwa anafika siku hiyo niliyotoka sero. Kwa bahati simu ya shamsa ilikuwa wazi na mdogo ake ndio alikuwa njiani anakuja nikaona akifika bora nikampokee. nikaenda kwa mjumbe kuuliza hatma ya mwili wa shamsa,
"Izzochapa mwanangu jana shamsa alizikwa makaburi ya mwananyamala yale ya uwanjani pale spatter karibu na torabora,
"Kesho unaweza kunipeleka kwenye kaburi lake?
"Sawa nitakupeleka,,
Nilirudi nyumbani midaa ya saa moja na nusu zainabu alinipigia simu,
"Izzo mbona naambiwa umetoka polisi uko wapi?
"Niko mitaani tutawasiliana baadae,
"Izzochapa umepatwa na nini unatoka polisi bila hata kunitaarifu?
"Niache sitaki kelele,
Nilikata simu nikaizima kabisa, hali ya shamsa kufa ilikuwa inanisumbua kichwa,,
Nikiwa na mawazo simu ya shamsa iliita nikaipokea,
"Hallow, "wowe ninde? (Wewe ni nani) "Izzochapa umugabo wa shamsa (izzochapa mume wa shanse)
"Ndi hano ubungo, (niko hapa ubungo),
"Sawa ndikuza ahongaho, (sawa niko nakuja)
"Sawa,
Baada ya dakika 30 nilifika ubungo nikamkuta mdogo wake shamsa stendi,
"Karibu, "ulakoze, (asante)*
Nilimfikisha nyumbani tukaongea mawili matatu alipomuulizia dada yake nikamwambia kasafili ila keshokutwa atakuwepo hapa,
"Sasa wewe baki hapa chakula hicho hapo utakula mimi nitarudi kesho,
"Sawa na kibazo, (sawa haina shida),
Nilitoka nikaenda kwangu kwa -zainabu nilipofika nilipiga hodi ila nilipigwa na butwaa kukutana na sura ya mtoto wa kike mzuri mwenye umbo matata angalia picha hapo chini,,
************Itaendelea************
episode 2 sehemu ya nane
"Karibu, "asante,
Nilipotaka kuingia ndani akaniuliza,
"Sijui ni nani mwenzangu?.
"Baba mwenye nyumba,
"Ooooh!!! Shemeji?... mr Izzochapa?... "Nikamjibu yesa,,
"Oooh!!!!! Karibu mume wangu,
Aliniambia huku akinikumbatia duh!!!!... mwili ulinisisimkaa kwa kuguswa na kifua chake na shavu langu kukutana na shavu lake na mikono yake kunishika kiuononi,
"Asante hujambo?.
"Sijambo pole na matatizo shemeji,
"Asante, "karibu ndani,,
Niliingia ndani nikakutana na mke wangu zainabu amekaa kwenye sofa ila alionesha ni mwenye kutokwa machozi,,
"Mke wangu vipi hali yako?.
"Nzuri tu,,
"Mbona kama ulikuwa unalia?
"Mume wangu kwanini ulinizimia simu.
"Lakini si nimekuja?
"Tatizo siyo kuja,
"Ila nini?
"Izzochapa unajuwa fika kuwa ulikuwa kwenye matatizo sasa ulipozima simu ulitegemea nini? Au mimi niwaze nini?
"Mke wangu lakini si nilikuwa nimetoka polisi,,
"Hata kama je hao waliokushitaki mimi najuaje kama hawana kinyongo na wewe?.
"Hizo fikira zako tu.
"Sawa nashukuru,,
"Unashukuru kwa lipi?.
"Izzochapa kama ungekuwa unanijari kama mkeo ungetoka jera ungeanza kuja kwako kwanza kabla ya kwenda kwa hao vimada wako,
"Kwa hiyo nilikuwa kwa vimada?
"Utajua mwenyewe,
Zainabu alikuwa anaongea maneno makali sana nilipoona hali hiyo nilinyanyuka nikaenda zangu chumbani yeye akabaki pale sebureni na mdogo wake,
Baada ya mda alikuja chumbani akafanya yake kisha akatoka alipofika sebureni akamtuma mdogo wake,
"Sasha kamkaribishe shemeji yako chakula,,
"Sawa,
Dk0 nilisikia hodi,
"Karibu,
Aliingia sasha,
"Shemeji karibu chakula,,
"Asante,
Sasha alirudi sebureni baada ya mda alipoona sijaenda sebureni akamtuma tena sasha,,
"Hebu kamjaribu tena,
Sasha alikuja tena,
"Hodii..
"Karibu,
Safari hii alikuja mpaka kitandani akanishika mguuni,
"Shemeji twende tukale,
"Nakuja,, "aaah!! Shemeji twende,
Aliongea huku akinishika mkono niliamka kitandani,
"Shemeji (sasha) tangulia nakuja,
"Sawa,,
Nilitoka nikaenda mezani nikavuta sahani ila Sasha akaichukua,
"Shemeji ngoja nikupakulie,,
"Sawa,
Nilikula baada ya kula nikarudi chumbani nikajimwagia maji baada ya kuoga nikapanda kitandani nikalala,
Mda kidogo na zainabu akaja kulala,
"Izzochapa mume wangu nisamehe,
Nilimkalia kimya,
"Izzochapa nina hamu na wewe mume wangu,,
Nikakaa kimya,
"Izzochapa mume geuka basi huku,
Aliongea huku akinivuta,
"Zainabu kuwa mwangalifu nitakupatia usijali,,
Alikaa kimya hakurudia tena kuniita kila mtu akalala kivyake,
Palikucha nikajiandaa ili niende kumuona mjumbe anipeleka kwenye kaburi la shamsa,
Baada ya kujiandaa nilikaa sebureni kusubili kunywachai ila kichwani nilikuwa na mawazo nitamueleza nini mdogo wake shamsa kuwa shamsa alifariki?.
Swala hilo liliniumiza kichwa sana ila nikaijuwa mwisho wa juwa kuzama siku hiyo lazima nimwambie ukweli,,
Nikiwa katika mawazo yangu kengele iligonga kuashiria kuna mgeni nje,
"Sasha kafungulie mgeni,
"Sawa,
Aliingia mbaba na mmama,
"Karibuni, "asante,
Baada ya dk2 wakauliza,
"Tumemkuta zainabu?.
"Ndio,
"Sasha kamwite dada yako,
Sasha alienda kumuita dada yake akaja sebureni,
"Karibuni jamani shikamooni?
"Marahaba za siku?
"Nzuri,
Waliongea baada ya mda wakaeleza shida yao kuwa walikuja kuchukua pesa iliyobaki wakati wanauziana nyumba hiyo tunayoishi,
"Yaani wazee wangu sasa hv nina hali mbaya labda mwisho wa mwezi,,
"Na sisi tuna shida ya pesa mwanangu,
Nilingilia kati,
"Wazee mnadai kiasi gani cha pesa?
"Mil.70,
"Sawa piga hesabu kwa dora inakuwa kiasi gani?.
Walipiga hesabu zao kisha nikaingia chumbani nikachukua dora katika zile dora nilizopata kipindi kile nataka kwenda india nikawapa,.
Zainabu alishangaa nimetoa wapi pesa zile alafu kilichomshangaza zaidi ni madorale tu hakuna pesa ya Tz,,
Baada ya hapo nilikunywa chai nikaondoka,,
Nilimpitia mjumbe tukaenda makaburini ila huko makaburini nikamkuta Gefy na Eliza...
episode 3 sehemu ya nane
Nilipowaona sikusita kwenda kwenye lile kaburi,
Nilifika kwenye kaburi nikawasalimia,,
"Habari zenu?.
"Nzuri, waliitika kwa sauti ya unyonge "nzuri,
Nilipitiliza nikakaa pembeni ya kaburi machozi yakaanza kunitoka kwani nilikumbuka mengi sana kuhusu shamsa,
Gefy alinyanyuka na Yasinta akanyanyuka wakashikana mikono wakaanza kuondoka, niliwasindikiza na macho mpaka wakaishilia,
"Mjumbe samahani naomba ukaniletee yule mgeni wangu hapa,
"Yule binti aliyeko kwako?
"Ndio,
"Sawa, ngoja niende,
"Si unaweza kutumia gari?
"Ndio,
"Chukua funguo nenda na gari yangu,
"Sawa,
Mjumbe aliondoka akaenda kumleta mdogo wake na shamsa,
"Shamsa umeniacha ila nilikupenda kwa dhati kutoka moyoni, aaaahaaa haa!!!! haaa!!!... shamsa mke wanguuuu,,,,...,, nilikupenda sanaaa mimi leooo siamini 😫😫kama umeniacha peke yangu,,
Nililia sana kumbe mda huo nalia mjumbe alikuwa nyuma yangu pamoja na mdogo wake shamsa,,
"Shamsa eee... hataaa hukuniagaaa mke wanguuuu ningeweza ningekuamsha mke wanguuu nikakuagaaa😩😩haaaaa!!! Mh!!!!!! Shamsa mke wanguu...
Nikiwa naomboleza nilisikia sauti nyuma ya kilio tena ya msichana kugeuka nilikutana na uso wa mdogo wake shamsa,,
"Dada wafyuyee utambonyeee (dada umekufa bila kuniona),, dasa wafyuye utaharutse mulugo (dada umekufa hujarudi nyumbani)
Tulilia sana ila hakuna linalokosa mwisho hatimae tulinyamanza nikamsimulia kifo cha dada yake kilivyotokea akakubaliana na hali halisi,,
Tulirudi nyumbani ila kila mmoja alikuwa hoi kwa uchungu tuliongea mengi hatimae tukaelewana nilimpa na story ya dada yake kuachika kwa gefy akanishukuru kwa msaada niliompa dada yake ila kumbe na yeye ujio wake alikuja kumpa taarifa dada yake vifo vya wazazi wao,,
Tuliongea mengi sana hatimae nikamwambia tutaishi pamoja pale na tutasaidiana kimaisha,
Saa moja nilirudi kwangu kwa mke wangu zainabu),.
Nilimkuta Sasha ila zainabu alikuwa hajafika,
Nilimuangalia sasha nikatadhimini kimini alichokuwa amevaa kwani kilikuwa kimeacha sehemu za mwili wazi kutokana uzuri wake nilijikuta namtamani shemeji yangu,,
epidode ya 4 sehemu ya nane
Nilimuangalia kuanzia chini mpaka juu lkn nikamezea tu,
Mawazo yalihama nikaanza kumuwaza shamsa nikafikilia na kuwaza ni nani atakuwa anahusika na kifo chake? Au ni wale jamaa walionituma India? Upande mwingine nilimfikilia eliza kuwa anaweza kuwa anahusika kwa kiwango kikubwa ila kwanini afanye vile Elizabeth? Aaaaah anaweza kwa kuwa alijua kuwa nipo nae kimapenzi maana siku ambayo naenda dodoma nilimkimbia mbele ya shamsa, lakini wale jamaa waliokuwa wamenipa kazi ya kwenda india nao wanaweza kuhusika kwa kuwa sikufanya kazi yao,
Sasha alinishitua kutoka kwenye mawazo niliyokuwa nayo kwa kunikalibilisha chakula,
"Shemeji karibu chakula,
"Asante,,
Nilijinyoosha nikaenda chumbani nikatoa nguo nikazama bafuni nikajimwagia maji baada ya kujimwagia maji nikarudi sebuleni kula,,
Mpaka wakati huo zainabu alikuwa hajarejea nikamuuliza mdogo wake,
"Sasha dada yako hajarudi?
"Bado,
"Sawa,
Niliangalia saa nikagundua ilikuwa ni saa 4 usiku, nilikula baada ya kula nikatoka nje nikakaa kwenye kibaraza nikawa natafakari mwisho wa haya maisha yangu ni nini?..
*nimempoteza shamsa kwa kifo cha utata sijui wauaji walilenga nini au niliwakwaza nini kama wamemuuwa shamsa mimi nitabaki kweli? Nikiwa katika mawazo yangu simu yangu iliita kuangalia alikuwa ni Vicky sikupokea kwani nilikuwa namtafutia sababu ya kumtoa kwenye list yangu nibaki na zainabu tu,
Alipoona sipokei akatuma ujumbe mfupi,
*sawa nashukuru ila wewe siyo wa kunifanyia haya*
Nikamjibu,
*yapi?*
*huwezi kuacha kupokea simu yangu*
*achana na mimi endelea kuwa na hicho kibabu chako*
*sawa ila juwa wakati tunapendana ulinikuta nacho*
*na ndio maana nimekuacha nacho*
*sawa izzochapa nashukuru sana kwa majibu yako mazuri*
*asante kwa kushukuru hata na mimi wakati nakutana na wewe nilikuwa na mke pia*
*unasemaje?*
*kama ulivyosikia au husikii vizuri siku hizi?*
*Izzochapa hapo ndipo unapotaka kunikoroga*
*kivipi*
*una mke?*
*ndio na wewe mbona una kibabu chako sijapaniki*
*sawa asante*
*na wewe asante*
Niliacha kuchat naye nikaendelea kuwaza yangu mpaka saa tano zainabu alikuwa hajarejea na siyo kawaida yake,
*huyu naye kaenda wapi mpaka sasa hajarudi nyumbani? Mbona hawa wanawake wanataka kunitoa roho mimi?*
Niliendelea kuvuta subra ilipofika saa sita nikaona aaaa!!!!!.. wapi acha nimpigie simu,
Nilimpigia simu ila iliita mpaka ikakata nikajaribu tena ila wapi,
Aaaaa jamani ndio nini sasa hapokei simu?
Niliacha kumpigia simu nikakaa kimya ilipotimu saa sita na nusu nikaona mwanga wa mataa ya gari getini kisha honi ikafuatia mlinzi akaenda kufungua,,
Zainabu aliingia na gari yake akapaki baada ya kupaki akashuka cha kusitaajabisha alipita bila hata salamu na mimi nikamuangalia nikamnyamanzia baada ya dakika tano nikaingia ndani kuona kama ataniambia chochote.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2QQltgL
No comments:
Post a Comment