Katika enzi zangu moja ya vitu ambavyo vilikua vikinikera katika kuanzisha mahusiano mapya ilikua ni kumfuatilia binti kwa muda mrefu sana, kwa bahati nzuri kwa upande wangu nilikua najua mapema, nikiongea na mwanamke kwa siku mbili tatu hua najua kama hapa nakubaliwa au napoteza tu muda wangu. Mara huwa najitoa mapema kabisa, lakini kuna watu ving’ang’anizi na kuna mabinti ‘wagumu’ sana.
Umeshawahi kukuta watu wanatongozana kwa miaka miwili mwanaume hakati tamaa na binti naye hakubali, wakati mwingine labda anamtaka mhusika lakini anazuga zuga kwa kigezo cha kusema kuwa anampima kama yuko siriasi au la. Wasichana wengi pia huamini kuwa kuchelewa kukubali basi hawataonekana Malaya hivyo kumzungusha mtu miezi mpaka kuwa sitaki nataka.
Binafsi naamini hakuna uhusiano kati ya umalaya na muda wa kukubali, hata ukinikubali ndani ya dakika tano hainiumizi kichwa kwani wakati mwingine mambo hu ‘click’ tu na haina uhusiano na tabia. Sasa kuna wale wanawake ambao hutongozwa muda mrefu na hapa nikimaanisha kutongozwa kwa muda wa kuanzia miezi mitatu mpaka miaka kadhaa ndipo hukubali, basi kama ushatongozwa muda mrefu kabla ya kukubali fahamu mambo haya matatu.
(1) Muda Haumaanishi Upendo; Hiki ni kitu cha kwanza kabisa mbacho dada zangu mnatakiwa kukijua, nishawahi kukutana na wanawake wengi, anakulalamikia “Jamaa alinifuatilia miaka miwili lakini baada ya kumkubalia kimapenzi akaniacha ndani ya muda mfupi!” Wadada wengi hudhani kuwa mwanaume akimfuatilia kwa muda mrefu, akionyesha kujali kwa muda mrefu basi ndiyo anampenda kweli, labda nikupe habari mbaya si kweli na mara nyingi huwa ni kinyume chake kabisa.
Wanaume wengi hatukubali kushindwa, hivyo unapomtongoza mwanamke akakukatalia basi utajitahidi kufanya kila kitu ili kumpata, hata kama ni kupiga simu kila siku, hata kama ni kununua zawadi kila siku na wakati mwingine kujifanya rafiki wa kawaida na hata kujitambulisha kwao. Tena mara nyingi mwanamke anapokusumbua sana, hasa wale ambao husema “Nina mtu wangu!” basi wanatia hasira sana hao watu.
Unajikuta unawaza “Mimi nina kasoro gani… atanikataaje… kwanini kamkubali yule fala…” utafanya kila kitu ili tu kumpata na kumuonyesha kuwa wewe ni mwanaume na ukishampata mwanamke wa namna hiyo hakuna haja tena ya kubaki naye. Ingawa si wote lakini wanaume wengi wanaotongoza muda mrefu, miezi sita, mwaka au hata miaka mitatu anakufuatilia basi jua kuwa anataka kutembea na wewe na kukuacha.
Hakuna kingine kwani unapomzungusha mwanaume muda mrefu anajua kuwa humpendi na unapokuja kumkubali baadaye basi huhisi labda ni kwakua umeachwa na mpenzi wako, umezeeka huna mtu au umeona amepata hela na si upendo wa kweli. Kwa maana hiyo kwakua ulishamsumbua atatembea na wewe mara moja, mbili, tatu kisha atakuacha ukapambane na hali yako.
Hakuna uhusiano kati ya upendo wa kweli na kutongoza muda mrefu, kuna ambao kweli hukung’ang’ania kwakua wapenda lakini wengi, narudia wengi ni kwakua tu wanataka kukupata na kusema “Kitu chenyewe ulichokua unaringia ni hiki!” Hivyo dada yangu kama mtu unamtaka mkubali tu na si kutaka kumpima eti atakutongoza muda gani? Hicho si kipimo sahihi cha upendo bali ni kipimo cha ving’ang’anizi tu!
(2) Alikua Anaendelea Na Maisha Yake Kabla Ya Wewe Kumkubali; Wadada wengi huwaza kuwa wanapowakubalia wanaume waliowahangaikia muda mrefu basi wataonyeshwa mapenzi ya maana kwani ni wavumilivu na kweli walikua wanawasubiri. Nikupe tu habari mbaya, labda tu kama huyo mwanaume naye hayajui mapenzi au hakuwahi kuwa na mwanamke kabla au nayeye tongoza yake ni ya shida.
Lakini hakuna mwanaume (labda wapo ila mimi si wajui) ambao eti atakaa miaka miwili bila kufanya mapenzi kisa anasubiri wewe umkubalie!(wapo wale amabo hawajafanya kabisa wameokoka) Daa huyo si mjui, kwamaana hiyo wakati anakutongoza unamkatalia basi jua kuna kwingine anatongoza na anakubaliwa na anaendelea na maisha yake. Kitu kingine nikuwa kutongoza muda mrefu nacho ni kipaji, wanaume wa namna hii utakuta ana wasichana kumi wote anawatongoza na anasubiria kukubaliwa.
Ninachotaka kusema hapa nikuwa, wakati unamkatalia usifikiri kafunga zipu anasubiri miujiza ukubali, hapana ana maisha yake, tena hata kama alikua anakupenda kweli mwanzoni, ulipomkataa alijua kuwa humpendi hivyo akaacha kukufuatilia akatafuta mwingine na akampenda, lakini kwakua ni mwanaume na hapati gharama yoyote kukutumia meseji za asubuhi na jioni basi anaendelea kukukumbuka ili ukikubali anagonga na kupita.
Usidhani kwamba eti kwakua alikuambia anakupenda atakaa miaka miwili bila mpenzi akisubiri wewe uachwe na mpenzi wako ndiyo uende kwake! Watu wa namna hiyo ni wachache sana, hivyo unapomkubali mwanaume mabaye kakuhangaikia miaka nenda, miezi sujui mitatu minne basi jua kuwa ana mpenzi wake, anamaisha yake na kwako ukikubali atapita akinogewa atajenga kibanda na ukimboa basi atakutupilia mbali na kuendelea na maisha yake.
(3) Hawezi Kuacha Kila Kitu Kwaajili Yako;Wanawake wengi baada ya kukubali hutaka kuona mwanaume akiacha kila kitu na kuwa nayeye, kwamba kama alikua na mpenzi aachane naye na kuwa nao. Yaani wanahisi walikua wanasubiriwa wao kukubali ndiyo maisha ya huyo mwanaume yaendelee, hapana ni wachache sana ambao wataachana na watu wao kwajaili yako, hata kama mwanzoni walikua wanakupenda kweli lakini ukimzungusha muda unamboa.
Kwanza kabisa unapokuja kumkubali mwanaume baada ya muda mrefu anajua kuwa, kuna sehemu uliachika, tena kama ulimuambia kuwa “Nina mtu wangu” ukamuonyesha na mipicha au ukawa ni wakupost na kuonyesha namna unavyopendwa huyo ndiyo kabisa kama ana akili atagonga na kusepa. Hii ni kwasababu anajua kuwa umemkubali kwakua umeachwa na si kwakua unampenda, atakutumia tu ili kulinda uanaume wake na kuendelea na maisha yake.
Hata kama hatakuacha lakini jua kuwa bado ataendelea na mtu wake wa wakati unamkubali, hivyo usiteka kumkubali uakaanza na mshariti “Sitaki hiki, usiwe unafanya hivi, usifenye kile, ukitaka tugombane sijui usinifanyie vile…” haitasaidia kitu, atakusikiliza na kuyafuata mwanzoni ila nawewe ukishampenda na kukolea kwake basi ataanza kukusumbua, ni nadra sana kuona mwanaume anaacha kila kitu chake eti kwakua umeibuka tu huko na kumkubali baada ya miaka No!
NINI CHA KUFANYA HAPA; Najua ni swali mabalo unajiuliza, wewe ambaye una imani kuwa mwanaume akikutongoza kwa muda mrefu ndiyo upendo, ufanye nini unapotongozwa? Nikuambie tu kitu kama mwanaume unampenda, unaona ni sahihi kwako basi kubali mapema kabisa, sisemi siku hiyo hiyo bali usimsumbue miezi mitatu eti kisa unapima nia yake! Hapana utapima lakini haitakua na maana yoyote.
Kama unamtaka mkubali, kuna uwezekano akakupenda zaidi usipomzungusha kuliko kumzungusha akakinahi. Lakini kama umemzungusha muda mrefu, unapomkubali mkubali kwakua na wewe una hamu naye, unamtaka lakini si kwakua eti unadhani anakupenda kweli na unaona yuko siriasi. Dada yangu unaweza kumkubali ukadhani yuko siriasi na wewe kwakua kakufuatilia miaka miwili kumbe mtu mwenyewe alishaoa muda mrefu!
Nimalizie kwa kusema kuwa hakuna uhusiano kati ya muda uliokubali na umalaya, hakuna uhusiano kati ya kuolewa na muda uliokubali wala hakuna uhusiano kati ya upendo na usiriasi wa mwanaume na muda wa kukubali. Kama unamtaka mtu bwana mkubali na si kupoteza muda wakati unampango wa kukubali, muhimu usikubali ukiwa huna uhakika kama unamtaka, subiri ukiwa na uhakika kuwa kakuvutia ndiyo umkubali.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/37u2cYx
No comments:
Post a Comment