Sunday, November 24, 2019

ZIFAHAMU SABABU ZA KUWASHWA SEHEMU ZA SIRI





Kuwashwa sehemu nyeti au sehemu za siri yaweza kuashiria dalili za magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya uke kwa wanawake na pia inaweza kuwa ni muwasho tu ama kuvimba kwa sehemu za siri za wanaume (uume). Kwa wanaume au wanawake wote kwa pamoja muwasho unaweza kusababishwa na matatizo ya ngozi, magonjwa mbalimbali ya zinaa au allery.
Pia mtu huweza kuwashwa sehemu za makalio. 
Sababu ya kuwashwa makalioni, yaweza kua ni kutojisafisha vizuri, kula vyakula vyenye viungo vingi sana, kuhara, vidonda kwenye njia ya haja kubwa, maambukizi ya fangasi, bawasiri kwa jina la kitaalamu huitwa (hemorrhoids), minyoo na kadhalika.
Watu wengi wamekuwa na tatizo la muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu flani na huisha wenyewe baada ya kitu hicho kikiondolewa, vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi, ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kumuona daktari wako.
Nini husababisha muwasho sehemu za siri za Mwanaume?
Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zilezile zinazosababisha muwasho sehemu zingine za mwili. Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo kikuu cha kuwashwa uume. Sababu zingine ni maradhi ya fangasi, ugonjwa wa upele (scabies), kuwepo kwa chawa,allery, maambukizi ya bakteria n.k
  • Nini hupelekea muwasho wa sehemu za siri kwa Mwanamke?
  • Maambukizi ya Fangasi Ukeni (Vaginal Yeast Infection), Ni moja ya tatizo kwa wanawake linalosababishwa na fangasi waitwao Candida. Dalili kuu ni uwashwa ukeni, kuvimba na kutoa uchafu mweupe kama maziwa ukeni.
  • Ugonjwa wa kuvimba uke (Vulvovaginitis), Ni ugonjwa unaoathiri kwa kuvimbisha sehemu za nje za uke na uke wenyewe. Dalili kuu ni kuwashwa ukeni, mkojo kuuma na kukereketa wakati wa kukojoa na kutokwa na uchafu ukeni.
  • Kuvimba Uke baada ya hedhi kukoma (Postmenopausal Atrophic Vaginitis), Ni ugonjwa wa kuvimba kwa uke baada ya hedhi kukoma. Hali hii huongeza maambukizi ukeni na huweza kusababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa.
  • Maambukizi ya Trikomonasi (Trichomonas Infection), Ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na kimelea aitwaye Trichomonas vaginalis. Dalili kuu ni muwasho katika uke au uume na kutokwa na uchafu ukeni.
  • Ugonjwa wa Minyoo (Pinworm Infection), Ni maambukizi ya minyoo wadogo sana wenye umbo la pini wanaoweza kuambukiza utumbo na kusambaa maeneo mbalimbali. Ugonjwa huu huwatokea sana watoto wa kati ya miaka 5 na 10.
  • Inflamesheni ya Urethra (Urethritis), Ni maambukizi kwenye urethra (ujia wa kutolea mkojo nje) yanasababisha kuvimba kwa urethra. Dalili kuu ni mkojo kuchoma, maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kutokwa uchafu.
  • Genital Warts, Ni vivimbe vidogo vinavyotokea juu ya ngozi sehemu za siri. Ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiana na unasababishwa na virusi viitavyo Human papillomavirus (HPV). Vivimbe vinaweza sababisha muwasho na maumivu.
  • Saratani ya sehemu ya nje ya Uke (Vulvar Cancer), Ni saratani ya sehemu ya nje ya uke inayoambatana na kuwashwa sehemu ya nje ya uke.
  • Ugonjwa wa Wasiwasi (Generalized Anxiety Disorder), Ni ugonjwa ambao unaotokana na hofu ya matukio fulani. Wakati mwingine husababisha kujikuna sehemu mbalimbali hata sehemu za siri.
    • Ugonjwa wa Sjogren (Sjogren’s Syndrome), Ni ugonjwa katika mfumo wa kinga ya mwili unaoathiri tezi zinazosaidia mwili kutengeneza unyevu nyevu kwenye macho na mdomo. Ugonjwa huu huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume.
    • Kisukari, Ni ugonjwa sugu wa kimetaboliki unaosababishwa na kasoro katika utengenezaji wa Insulin au utendaji kazi wake. Kisukari kilichokomaa kinaweza sababisha maumivu ya tumbo, kichefuchefu, kizunguzungu na kuwashwa sehemu za siri.


      🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






    from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/35wVEGW

    No comments:

    Post a Comment