Anti samahani, kuna kijana anataka kuniposa lakini umbile lake linaniogopesha. Ni mwembamba na hana makalio. Wengi husema wanaume wenye maumbo hayo wanakuwa na maumbile makubwa. Mimi ni mwoga sana, ikiwa hivyo nitashindwa.
Nifanyeje ili nijue kabla hajanioa?
Achana na maneno ya mitaani, maumbile ya mtu hayapimwi namna hiyo. Anaweza kuwa hivyo na asiwe na sifa ulizozisikia. Naamini kama umempenda kwa dhati vyovyote alivyo utakabiliana naye ilimradi asiwe amepitiliza. Tofauti na hapo hakuna kitu cha ajabu kilichowahi kuonwa ambacho kitakushinda. Ukianza mambo ya nifanyeje nimjue, utajikuta umeingia kwenye mahusiano kabla hajakuoa, unadhani atakupa fursa ya kumuangalia bure, lazima mtamalizana hivyo achana na wazo hilo kabisa. Jambo la msingi unalotakiwa kulifanya wakati huu ni kumshawishi mkapime afya zenu, mjue kama mpo salama au laa kabla ya kufunga ndoa. Hayo mambo mengine yanawezekana kulingana na utaalamu wenu, hakuna kikubwa wala kidogo kitakachokuzuia kuwa ndani ya ndoa na kupata burudani upasayo.
Nimemaliza mwaka sijaonana na mpenzi wangu. Kuna mwanamke nataka awe rafiki yangu wa kimapenzi na nimeshamweleza hilo mara kadhaa na akanikubalia, lakini natimiza mwaka sasa sijaonana naye zaidi ya kuzungumza kwenye simu. Vitendo vyake vinaashiria hanipendi, lakini nikizungumza naye kwenye simu anasisitiza kuwa ananipenda na mimi ni wake wa daima. Nifanyeje?
Hujaniambia anaishi wapi, ila nahisi ni Makka au Madina ambako unahitaji fedha nyingi kama gharama ya usafiri. Kama kweli unampenda na anaishi hapahapa nchini, si ujipange uende kuonana naye? Ukifanya hivyo, ndiyo utajua mbivu na mbichi. Husikii watu wakilalamika kuwa simu zinadanganya? Utaamini vipi maneno wakati huoni vitendo wala mhusika humuoni, kama ameolewa? Jiongeze. Sifa ya mwanaume ni kujiongeza siku zote. Ukikalia kulalamika kuwa anakupenda kwa maneno, atakupenda kweli kwa mtindo huo hadi unazeeka. Nenda kajionee mwenyewe kama ni wako au wa wenzako unashirikiana nao kumtunza. Wengine hulalamika kuuziwa mbuzi kwenye gunia, lakini wewe unajiuzia mwenyewe mbuzi kwenye gunia.
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/35mOPrk
No comments:
Post a Comment