Thursday, November 28, 2019

WANAWAKE TU : Wanaume mkae kando kidogo ,Sababu zinazopelekea kukosa hedhi





Dk Christopher  Peterson 

Sababu kuu ya kukosa hedhi ambayo wengi pia tumeizoea ni ujauzito.
Kwa kawaida mwanamke hapati hedhi kwa kipindi chote cha ujauzito, kutokana na sababu za kibaiolojia.

Lakini sababu nyingine zinaweza kuwa ni matatizo ya kwenye via vya uzazi na mfumo wa uzazi kwa ujumla au tezi zinazosaidia kuratibu viwango vya homoni mwilini kama nilivyoeleza hapo awali.
Ni muhimu kupata ushauri wa daktari ili kuchunguza moja ya matatizo haya.
Kwanza kabisa tatizo hili husababishwa na sababu za asili. Katika kipindi tofauti, mwanamke anaweza kujikuta anakosa hedhi kutokana na ujauzito, kufikia umri wa kupoteza uwezo wa kuzaa na hata kunyonyesha pia.
Sababu nyingine ni matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango. Kuna wanawake wanaotumia vidonge vya uzazi wa mpango wanaweza kukosa hedhi kwa kipindi fulani. Hata hivyo, baada ya kuacha kutumia vidonge hivyo, inaweza kuchukua muda kadhaa kabla ya kuendelea kupata hedhi.
Na hata njia zingine za uzazi wa mpango kama vile sindano na vipandikizi vinaweza kusababisha kukosa hedhi.
Baadhi ya matumizi ya dawa pia yanachangia tatizo hili. Aina fulani ya dawa imethibitika kuwa na uwezekano wa kuharibu mfumo homoni mwilini na kusababisha kukosa hedhi kwa kipindi fulani.
Baadhi ya aina hizi za dawa ni kama za magonjwa ya akili, saratani, sonona, shinikizo la damu na aleji.
Ni kawaida kwa mwanamke anayetumia dawa hizi kukosa hedhi kwa kipindi chote cha tiba.
Lakini sababu za aina ya maisha pia zinachangia kukosa hedhi. Mathalani uzito uliopungua kupita kiasi. Uzito uliopungua kupita kiasi kwa zaidi ya asilimia 10 chini ya uzito wa kawaida, unaweza kuvuruga utendaji kazi wa mfumo wa homoni mwilini. Kwa wanawake wenye matatizo ya kukosa hamu ya kula wapo hatarini sana kupata tatizo hili.
Msongo wa mawazo pia unaweza ukasimamisha kwa muda utendaji kazi wa “hypothalamus”- eneo ambalo ubongo unahimili vichocheo na kuratibu mzunguko wa hedhi. Matokeo yake hedhi inaweza kusimama. Ratiba ya mzunguko inaendelea baada ya nsongo wa mawazo kupungua. Mwandishi wa makala haya ni daktari wa binadamu


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/37JiQDF

No comments:

Post a Comment