Thursday, April 25, 2019

KANUNI 4 MUHIMU ZA KUDUMU PENZINI




1. Samehe na kusahau.
Unapomsamehe mpenzi wako kwa kosa lolote alilokosa basi hakikisha umemsamehe kiukweli na ujitahidi kusahau kosa alilotenda itasaidia uwe na amani ya moyo zaidi kuliko kumsamehe kwa usoni tu lakini moyoni ukawa na Donge bado, hii hupelekea kupunguza mapenzi kwa kiasi Fulani kwake na kujikosesha furaha ya mapenzi.Anapokosea siku nyingine usimkumbushe kosa lake la nyuma kwa sababu itamfanya ajione mwenye huzuni na ajione kuwa hakusamehewa.

2. Mpe nafasi na uhuru mpenzi wako.
Mnapokuwa kwenye mahusiano jitahidini kwa hali na mali kupeana nafasi/uhuru kwenye mambo mengi hasa yale ya kitaaluma zaidi na kimaisha.anapokwambia yupo kwenye kikao cha kikazi jaribu kumuelewa na umpe support ya kutosha kwenye kazi zake au biashara zake au hata masomo yake.usipende sana kulalamika pale anapochelewa kurudi kazini au kutoka kwenye biashara zake bali mpokee kwa upole na baada ya kupumzika ndipo muulize kwa upole na kimahaba zaidi kwanini siku hizi anachelewa sana kurudi au kwenye biashara zake au shuleni tofauti na zamani.
Hii itajenga zaidi kuliko kubomoa kwa kulalamika na kupayuka mbele yake na huku yeye akiwa hata hajapumzika na itamfanya siku nyingine aione nyumba chungu kitu ambacho si kizuri kwenu wote wawili.

3. Mfanye mwenza wako ajivunie kuwa nawe kila wakati.
Hakikisha katika mapenzi yenu kila siku unamfanya mpenzi wako ajivunie kuwa nawe na hakikisha humfanyi ajute kwa kukuchagua wewe miongoni mwa wote aliowaona. Usijidanganye hata siku moja kuwa kwa kumpata tu na kwa yeye kukupenda basi hajaona mwingine wa kuweza kuwa naye. Wapo wengi sana anaoweza kuwa nao lakini amekuchagua wewe katika hao wote, kwa hiyo usimfanye aanze kuwafikiria wale wengine wanaomfuatilia kila siku na kumsumbua.Ukianza kumwacha aanze kuwafikiria wengine aidha kwa wewe kuwa unamkosesha amani ya mapenzi kila mara au kwa mengine mabaya ndani ya mapenzi basi ipo siku utaishia pabaya.

4. Msadie kwa khali na mali kila inapowezekana.
Kwenye mahusiano huwa kuna kupanda na kushuka miongoni mwa wapenzi na hasa kiuchumi na hata kisaikolojia. Hakuna kitu kizuri kwenye mapenzi kama mtu kupata tatizo na akasaidiwa na mpenzi wake katika hali ambayo hakuitegemea, namaanisha mpenzi wako akipata tatizo lolote hakikisha wewe ndo unakuwa wa kwanza kulifahamu na kulifanyia kazi.

Sio matatizo yote yanamalizwa kwa pesa so hata ushauri na kumpa mawazo chanya inasaidia sana na kumfanya awe na furaha kuwa nawe.Kama unampenda usione tabu kumsaidia kwa kuogopa kuonekana eti unahonga, huyo ni mpenzi wako kwa hiyo jiamini na umpe kile anachostahili kusaidiwa na mpenzi wake.

Yapo mambo mengi sana ambayo kama mkiyafanya kwenye mapenzi basi uhusiano wenu utakuwa wa kudumu na wenye furaha sana ingawa hapa nimezungumzia kwa uchache sana lakini nina imani itasaidia sana kwa wote walio kwenye mahusiano .

Mapenzi hayana ndumba au limbwata hata siku moja, unapoona wapenzi wengi wana furaha kwenye mapenzi yao ni kwa sababu wanavumiliana kwa mengi na kusameheana kwa mengi. Sana Na Unaweza Kuyarekebisha Kwa Kukaa Chini Na Mpenzi Wako Mkayamaliza Kwa Dakika 5 Tu Lakini Wengine Huwa Issue Kubwa Kwao Na Kusababisha Mwisho Mbaya. Kanuni sita (6) za kudumu katika mahusiano ya kimapenzi.

from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2IFs4HL

No comments:

Post a Comment