Saturday, February 29, 2020

SABABU AMBAZO HUCHOCHEA MWANAMKE AKUSALITI










Mapenzi ni matamu ukipata mpenzi mnaependana. Mahusiano mengi huvunjika na chanzo kikuu huwa ni ‘uplayer’ kama ninavyopenda kuuita namba sita mgongoni. Lakini wanaume wengi hujiuliza kwa nini mwanamke wangu hatosheki na mimi. Tatizo litakuwa ni wewe mwanaume ndie unayechangia ama pia labda ni mkewako ambaye ana shida. So leo hapa tumekuja na majibu kamili uzijue kwa nini wanawake wengi huplay wanaume zao.
#1 Tamaa.
Tamaa huvunja mahusiano mengi. Si kila mwanamke anapenda alivyo ilhali wengine wanaweza kuwa wanapenda pesa. Hivyo basi kama wewe ni mwanaume na mfuko wako hauna kitu basi ujue si kila mwanamke anaweza kuishi na wewe. Hivyo basi usitarajie uwe hauna kitu ukadhani kila mwanamke anaweza kuvumilia na hali ulionayo. Mwanamke hutafuta mwanaume atakayetimiza mahitaji yake na wewe uwe tu kama msaada wake.
#2 Mapenzi.
Je wewe uko bora kitandani. Swala hili mara nyingi husumbua sana. Kila mwanamke ana kiwango chake cha kufika kileleni. Mwanaume kama huwezi kumridhisha mkeo kitandani basi jua kuwa kunaweza kutokea matatizo. Wanawake wengine hutafuta wanaume ambao wanaweza kuwaridhisha kitandani na wewe ukawa mwanamke jina tu.
#3 Tabia.
Hapa napo kuna tatizo. Wewe mwanaume tabia zako ni zipi? Huezi tarajia uwe na tabia zinazokera na mimi niwe niko na wewe tu. Ok, sawa pesa unazo sikatai lakini je, mlo wako ukoje? Uvaaji wako ni upi? Mazungumzo yako ni ya aina gani? Tabia ulizo nazo kama ni mbaya hata siwezi kutoka na wewe mbele za watu. Haoa sasa itabidi nikatafute mwenzako ambaye naweza toka out nae.
#4 Distance.
Hii nayo pia huchangia sana wanawake kutokuwa waaminifu. Mapenzi yamenizidia na wewe uko mbali baba nifanyeje? Nitavumilia sawa lakini itafika pahali nitashindwa. Rafiki zangu kwa raha zao na wapenzi wao mimi huku navumilia nitashindwa. Pia hapa si kila mwanamke si mwaminifu. Kuna wengine ambao wanaweza kuvumilia pia. Hivyo basi yategemea na mtu mwenyewe. Lakini distance mara nyingi huvunja mahusiano.
#5 Mawasiliano.
Je wewe hutumia muda mwingi kuwasiliana na mpenzi wako? Waeza pata mwanaume anakaa mwezi mzima bila hata kumjulia hali mpenzi wake. Mawasiliano ni muhimu sana katika maisha ya wapenzi wawili. Ukikaa muda mrefu bila hata kutoa sababu ya kimya chako mwanamke anaweza kufikiria umemuacha.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2T7kLwC

UKIWA NA MAMBO HAYA MUMEO ATAKUPENDA SANAA



1. MWENYE HISIA ZA UCHESHI:
Ikiwa
unafurahishwa na utani wake, ni jambo
litakalomvutia sana. Lakini ukiwa mwepesi
wa kuchukia na kukasirika, yumkini
mumeo asivutike nawe. Jitahidi kuwa na
hisia za utani na ucheshi... _
2. MWENYE KUSAMEHE:
Unapoelewa kuwa
mumeo sio mtu mkamilifu na unapokuwa
na uwezo wa kumsamehe kwa dosari
zake, hii itamaanisha kuwa unamiliki
mojawapo ya sifa muhimu sana ambazo
wanaume wanazitaka kwa udi na uvumba.
Ukiwa na mchezo wa kumrukia kwa kila
kosa dogo analolifanya au ukawa na
ukosoaji uliopitiliza, tambua kuwa mumeo
hatakuwa mwenye kukufurahia, hata kama
ni miongoni mwa wale wasiosema.
Niliwahi kumnasihi memba wangu mmoja
wa Ndoa Maridhawa kuwa: “Kama
wamtafuta mume asiyekosea, hutampata
na utaishi bila mume”. _
3. MWENYE ASHIKI:
Mwanamke ambaye sio
romantic huwa hamvutii mwanaume. Ili
mwanaume avutike unatakiwa kumfanya
ahisi raha na uwe mwepesi wa
kumchokoza. Ikiwa unadhani kuwa
mwanaume ndiye tu anayepeswa
kukuchokoza, basi hapo unajitesa na
haitakuwa na faida kwako. Boresha uwezo
wako wa uchokozi na kuwa romantic
utaona namna mumeo atakavyokuwa
akikutamani.








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2weqKqs

MWANAMKE KUJIACHIA





Narudia tena aibu ziachwe jmn kweny ndoa zetu mwanamk full kujiachia ndio manake, wengne mnaona haya Ata kugusa kidevu cha mumeo ndevu hazichezew eti mke anaona aibu kaaah jaman mbona mnazitia doa ndoa  hamjui kama  wanaume hulewesha kwa mawadda na hutulia kwenye ndoa mlijue ilo wanawake weka aibu kule mahabba weka mbele iyo ndo habari MWANAMKE KUJIACHIA

Aibu aibu peleka uko mtoto wa kike  chakula pia Kula nae mumeo tena mliashane mana wadada wengne ni too much mpaka Kula na mumewe mtoto wa kike anaona aibu hebu koma shost  some time mume anarudi kazini hutumwa mtoto akapokee jaman mume ana thaman yake na mtoto yake mpoo mana hapo mwanamke kisa mtoto na zile aibu zake amepata kisingizio mtoto hebu kuwa na adabu mwanamke na mumeo pia muangalie upo usimbanie macho muangalie vizur usimtizamie kwa chini kama ulofumaniwa muangalie bibi Yule ni wako muangalie unapotaka aibu za nin??? MWANAMKE KUJIACHIA

Inafika wiki mwanamk hajaketi na mumewe kumliwaza wala kumfanyia masg, ewe MWANAMKE kwa namna hii unakaribisha michepuko wewe mwenyew hebu acha izo tabia usifanye usungo tena mumeo akiwepo kazini uwe una mliwaza umtakie kazi njema na mtumie sms nzur upoo  apo lazima atakuwa na mood ya KUFANYA kaz kwa amani mwamke kujiachia aibu peleka uko haya muonee shemegi yako upo  ila sio baby daddy wako una nin? ?shoga uone haya umeiba?? MWANAMKE KUJIACHIA

Nawashangaa sana wengne hawakumbuki Ata sku walocheza na waume zao kisa anaona aibu mtoto wa kike Mwaname atavumilia mwisho atachoka kwa tabia hizi unachojua ww kupika na kupakuwa usiku ukasubiri tendo la ndoa tu hujuwi kucheza na mumeo hata kwenye tendo kachumbari huzikati upo upo kama gogo kisa aibu mtoto wa kike hemu acha izo tabia michepuko watakuibia halaf uje useme mume wangu hajatulia hajatulia au hukuweza kumtuliza ?changamka mwanamke!








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/389lotF

Friday, February 28, 2020

NAMNA YA KUJITUNZA WAKATI WA DAMU YA MWEZI(PERIODS)




Damu ya mwezi si ugonjwa wala haifai kuwa sababu ya wanandoa kutengana ila ni muhimu ukajua namna ya kujitunza ili usimghasi mume katika kipindi hiki.
_

Kimila ni aibu kwa mumeo kuona damu yako- ila kwa dharura- kwa hivyo jaribu kuwa muangalifu unapokaa, unapolala na unapotumia choo kisafishe ili mume asikumbane na mapande ya damu. Vilevile hakikisha unaifunga pad yako kwa karatasi(isiyoonyesha ndani) kabla hujaitia kwenye pipa la taka. Kuna watu huwa na tabia ya kutupa pad iliyotumika ikiwa wazi Haipendezi.

_

Ni aibu kwa mwanamke aliyeolewa kurundika chupi chafu. Fua chupi pindi tu inapochafuka kwa damu. Kwenye upande wa kitanda unaolala, tandika leso/khanga nzito chini ya shuka ili damu ikichuruzika isipite kwenye mattress. Vilevile, weka akiba ya upande wa leso/khanga kitandani ili unapochafua shuka kwa bahati mbaya uweze kuifinika bila kulazimika kumuamsha mume kwa ajili ya kutoa shuka.

_

Usiache kuoga na mumeo kwa sababu upo mwezini. Tangulia chooni ujisafi sehemu ya siri na kutupa pad kabla mume hajaingia bafu kisha muoge kama kawaida. Hakikisha unajikamua kidogo ili damu isibaki tupuni na kuchuruzika wakati mnaoga. Harufu mbaya ni sababu nyengine inayotenganisha wanandoa wakati wa damu ya mwezi. Hakikisha unaoga angalau mara 2 kwa siku na unabadilisha pad kulingana na wingi wa damu yako. Usishinde na pad moja siku nzima utanuka vumba.
_

Unapostanji chukua muda wako kutia kidole kwenye sehemu yako ya siri ili kutoa uchafu na ujikaushe vizuri kabla hujavaa pad kwani majimaji husababisha harufu mbaya Mavuzi huleta ugumu katika usafi wa sehemu ya siri. Jinyoe siku kadhaa kabla hujaanza period ili iwe rahisi kujisafi.
_

Wakati wa damu ya mwezi ndio unapofaa kunukia vizuri zaidi kuliko nyakati zengine. Tumia manukato. Fukiza chumba, nguo, nywele na sehemu yako ya siri. Vaa kikuba. Tandaza vilua na asumini kitandani. Usiache kujiremba na kuvaa viguo vya kumtega mume. Damu ya mwezi isiwe sababu ya wewe kutopendeza.








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/388NbKM

JIFUNZE NAMNA YA KULAINISHA VIGANJA AU MIKONO



_

Moja ya hasara ya mwanamke aliye hodari na kazi za nyumbani ni viganja vya mikono kuwa vigumu au vikavu. Kama unafua na maji na sabuni, kuosha vyombo, kusafisha nyumba, kubadili watoto nepi au diapers,kupika n.k . usishangae kuwa na viganja vigumu au vikavu. Hakuna haja ya kuogopa na toa wasiwasi hii ni aina ya kufanya mikono yako iwe laini na ya kuvutia.
_ Huna haja ya kwenda kwa spa’s wala kwa wataalamu. Baada ya kazi zako fanya haya; 🕸Kunywa maji kwa wingi na kisha tumia njia hizi zifuatazo; 🕸Chukua container weka chumvi kiasi. 🕸Weka olive oil ndani ya container.
_ 🕸Weka sabuni ya maji ya kuoshea mikono, tumia aina unayoipenda inaweza kuwa anti-bacterial au yoyote ya maji. Ni vizuri kutumia sabuni ya maji,  sababu ya kawaida hautaosheka vizuri mkono sababu maji na mafuta hayachanganyiki.
_ 🕸Kausha mikono yako vizuri, kisha weka mchanganyiko huo kwenye viganja vyako kiasi cha ½ kijiko cha chai kisha sugua pole pole. Sugua ndani na nje ya viganja na ndani ya vidole na kucha. 🕸Osha kwa maji ya uvuguvugu .
Kausha mikono kwa kutumia taulo kavu.
Pakaa lotion ya mikono .

_ AOsha mikono na maji ya uvuguvugu na sabuni kuondoa grease na bacteria. 🕸kisha kausha na taulo kavu.
Chukua sukari vijiko viwili(2) vya chai na olive oil pia vijiko viwili(2). Pakaa mikononi kwa pamoja haraka .
Sugua mikono yote kwa pamoja ndani na nje kwa kutumia mchanganyiko huo. 🕸Osha mikono kwa maji ya uvuguvugu. 🕸Tumia rose water pia nzuri . 🕸Kisha pakaa lotion ya mkononi. Waweza tumia pia sunflower oil na hata mafuta ya nazi pia mazuri.

_ TIPS Usifanye mara moja ukategemea matokeo ya kudumu au milele. Tumia baby oil au lotion kabla ya kulala. Tumia lotion zinazotengenezewa na mimea zaidi. Acha lotion kwa dakika kumi(10)kwenye viganja,ile layer ya juu ya ngozi itanyonya lotion na italoki moisture ndani ya ngozi.Fanya hivi mara mbili(2) kwa wiki.
_ Vaa gloves au plastic wakati unafanya kazi kama kuosha vyombo au gardening.








from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/32CfWhI

NAMNA YA KUMUAMSHA MUME ANAPOLALA






Mkande mabega, miguu, mikono mpaka aamke. Akishaamka anaweza kukwambia uendelee kumkanda. Mpe busu umwambie unampenda lakini anafaa kuanza kujitayarisha.
Mpandie kwa juu ukiwa ukiwa km ulivyozaliwa Uwe unamsumbua sumbua kwa kumbusu au kumnong'oneza maneno matamu sikioni.

Chukua mkono wa mumeo uueke kwenye sehemu ya mwili wako anayoipenda kama kifua, kalio au sehemu ya siri alafu ufanye kama anakupapasa vile na huku unamwambia, kwa mfano, "My love unajua ukiendelea kulala utakosa utamu wa waridi uliolipia mahari? Amka mume wangu" hapo alale nani?
: Busu pia linafaa. Mpige mabusu kuanzia utosini hadi miguuni ukilenga zile sehemu zenye hisia zaidi. Utaona kaamka na bwana Abdallah nae kasimama wima.

Unaweza kuchagua sehemu moja, kwa mfano shingo, ukampiga busu mpaka umtoe lovebite. Lazima ataamka kabla hujamaliza kumbusu
:  Kama mumeo ni mwepesi wa kuamka unaweza tu kumuita kwa sauti ya chini. Kwa mfano "Habibi wangu sipendi kukusumbua lakini amka muda wa kwenda kazini umefika. Amka mume wangu natamani kuona unavyoniangalia".
: Sio unamwambia "We babake Ali hebu amka jamani unataka jua likupige la meno ndio ujue muda wa kazi umefika".
: Jamani haifai! Mhurumie na umpetipeti mumeo kama unavyopeti mtoto mchanga. Kama7 mumeo ana uelewa mzuri wa ndoa utaona na yeye anakuamsha kwa mahaba kama unavyomuamsha......."""''''';,,,,,,,,,
HAYO NDO MAPENZI HAYO NDO MAHABA. HAYO NDO MATHAWABU. NDUGUZANGU.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/38bCaZf

MDADA: MFANYIE HAYA MUMEO KUMPAGAWISHA KITANDANI MASHINE ISIMAME MUDA WOTE






Mtaalam wa mapenzi, Bi. Layla Quinn, anasema wamaume ni viumbe rahisi sana kuridhishwa tunapokuja katika suala la unyumba. Mwanzoni, kitu kinachomhamasisha mwanaume kujamiiana ni muonekano wako (mwanamke) tu wakimahaba, lakini kadri siku zinavyokwenda ndani ya mahusiano, inakuwa ngumu kupandisha munkari wake, hata kama wewe ni mwanamke mrembo barabara!
Bi. Layla anaendelea kusema kuwa, kumridhisha mwanaume wako kitandani inaweza ikawa rahisi kama tu utakumbuka kuweka mambo katika hali ya mvuto ( Remember to keep things intereting!). Tafuta namna ya kuleta hamasa, iliyokuwepo siku za mwanzo mwanzo, na kwa hakika utakamata usukani. Sasa swali linakuja…..Nini unatakiwa kufanya, ili kumridhisha mwanaume wako kitandani? Kujibu swali hilo, Bi. Layla amekuja na sheria 10 zifuatazo, ambazo kama zitazingatiwa kwa makini, basi mwanamke hatokuwa na shida ya kumridhisha mwanaume wake kitandani na nyanja nyingine muhimu za mahaba.

# 1 Vaa vizuri. Utamu wa kujamiiana unaweza ukawa kwenye tendo lenyewe, lakini matamanio ya kufanya tendo hilo, yanategemeana na mambo mengine mengi. Vaa vizuri wakati wa kulala wakati wote, na sio tu wakati wa usiku, ambao unataka kufanya mapenzi. Vaa nguo nyororo, yenye mtelezo unaomwagika mwilini. Kwa vazi hili na mtembeo wa kimahaba chumbani, mwanaume wako hatotaka kutoa mikono yake mwilini mwako.
#2 Usiwe mtu wa aibu aibu linapokuja suala la kujamiiana. Mwaume anaweza akakupenda kwa mapozi yako na aibu kwanza (lugha iliyotumika hapa ni “innocence”), lakini hamna mwanaume atakaye endelea kuvumilia mwanamke, ambaye anastushwa kirahisi na kila kitu (mitindo ya kujamiiana), isipokuwa mtindo wa kifudi fudi, maarufu kama “Kifo cha Mende”. Wanaume wanapenda wanawake, ambao ni wataalam kitandani. Wanaume wanapenda wanawake, ambao wanajiamini na wanabuni manjonjo mbalimbali wakati wa shughuli. Kama unataka kumridhisha mwanaume wako kitandani, basi soma mbinu mbalimbali, ambazo zinatumiwa na wapenzi mbalimbali.
#3 Fanya mazoezi na onekana Bomba. Wanaume ni watu wakujali sana muonekano wa mwanamke. Kwahiyo, sio lazima kuonekana kama walimbwende wa vichupi, lakini mtazamo wa karibu na hapo, utakuongezea mvuto zaidi kitandani. Ndio, mwanaume wako “anakupenda kama ulivyo” na tila lila nyingiiiii…..lakini lazima tuukabili ukweli kwamba watu wenye kufanya mazoezi wanaonekana na mvuto zaidi, hakuna kupinga hilo. Hata kwetu Bongo katika nyakati hizi za utandawazi, wakina kaka wengi wanawaona wanawake kama wakina Naomi Campbell na Jennifer Lopez, ambao wanatamani kuwa nao. Lakini hauhitaji kuwa kama wakina Naomi na Jennifer kumridhisha mwanaume wako, bali hakikisha tu upo katika umbo zuri la kumpelekesha kirahisi kitandani, Basi!
#4 Kuwa Mchokozi. Hapa haimaanishi ule uchokozi wa kuleta ugomvi, lahasha! Bali, ni ule uchokozi, ambao kwa lugha ya kingereza unafahamika kama “Tease”, kwa maana hiyo basi tunasema “Tease him”. Cheza nae michezo mbalimbali na burudika nae ipasavyo, na michezo isiwe ya kitandani tu, kama karata na kadhalika, bali michezo ya hata nje ya kitanda kama kukimbia na kucheza kidali po! Kama unataka kuwa mjuzi kitandani, basi unatakiwa umfanye mwanaume wako akutake wakati wote na popote pia. Kujamiiana sio kitasa ambazo unawasha na kuzima mnapokuwa chumbani tu. Mchokoze chokoze wakati mnasakata muziki jukwaani, na mchokoze chokoze (katika mitindo ya kimahaba, bila kuvuka mipaka) wakati yupo na marafiki zake.
#5 Jiamini na Jipende. Ndio, utaonekana vizuri zaidi ukipunguza maunene, lakini hiyo haimaanishi kwamba haupo bomba. Hakuna kinacho kera wanaume, kama mwanamke, ambae anauonea aibu mwili wake mwenyewe wakati anafanya mapenzi. Jiamini kuhusu mwili wako wakati upo mtupu, na jaribu mambo mbalimbali na mwanaume wako.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2VxWDoA