Tuesday, March 24, 2020

KWANINI WATU WANAPOKUWA MAKABILA TOFAUTI WANADUMU ZAIDI KWENYE MAHUSIANO KULIKO WALIO KABILA MOJA?



Image may contain: one or more people, people standing, people walking, outdoor and nature
Swali hili nimejiuliza kwingi lakini walau leo ninalo jibu nililojijibu binafsi, Kwanza kabisa TUZIHESHIMU MILA NA TAMADUNI ZETU... Kila mzazi hupenda kumjenga mtoto wake katika tamaduni za kwao, Kwa vyovyote vile yaliyo lijaza kabila fulani hayo ndo yenye uhalisia wake, Tabia iwayo yoyote inatokana na makuzi na malezi ya nyumbani kwenu, Hata usipokuwa 100% lakini tayari uko na vinasaba vya kwenu, Simaanishi kuongelea ukabila bali naongelea UIMARA WA PENZI LA WATU WASOKUWA KABILA MOJA... Ikiwa wapenzi ni kabila moja maana yake TABIA ZA KABILA LAO NI MOJA na sio wote wanaanguka kupitia hilo laa hasha kinachotesa hapo ni TABIA HUSIKA! Unamkuta mtu anapendwa kudekezwa lakini yeye ni Mwinyi yaani anataka awe yeye tu kupewa heshima, Mwenza nae anapenda kudekezwa na yeye hajui kudekeza mwenzie, Tafsiri yake hizo ni tabia za kabila lao UNADHANI WATAKUWA NA MAHUSIANO ENDELEVU?
Penzi lolote likigubikwa na migongano ya kila mara, Maneno makali na machafu AUTOMATICALLY MOYO HUHISI UPWEKE na hapo ni ngumu sana kubebeana madhaifu! Lakini ukikuta Wapenzi ni makabila tofauti kwanza wanaogopana kwa namna ya makuzi na malezi ya matabaka yao, Ni rahisi sana wapenzi hawa kubebeana kwa sababu TABIA ZAO SI AINA MOJA... Anaependa kubembelezwa itambidi ajishushe kwa mwenza wake, na kwa kawaida PENZI LINABORESHWA NA HESHIMA hivyo upande wa pili utafanya kulingana na mahitaji ya upande mwingine, Sijasema usioe/kuolewa na mtu wa kabila lako wala sikufundishi uoe ama uolewe na kabila jingine ila namaanisha NABII HAKUBARIKI KWAO.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/33OFTeQ

No comments:

Post a Comment