Thursday, March 26, 2020

Mizinga Kutoka Kwa Mpenzi Wako ikizidi Sana Fanya Haya Atanyooka tu



Siku zote katika Mapenzi hatukatazi kusaidiana ila kuna wengine wanazidisha vizinga kiasi kwamba inakuwa sio uhusiano tena ni ‘chanzo cha Mapato’, kwa kuliona hilo Siasa Huru imekuandalia njia za kufata pindi unapoona tabia hiyo imekomaa kwa mpenzi wako.

MFUNDISHE KUKUSAIDIA

Wanaume wengi wanalisahau jambo hili la kutokuwafundisha wapenzi wao, wajibu wa kutoa, Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya daladala analipa, wakati mpenzi wake ana kazi yake, Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna pesa zinavyokuwa hazitoshi na akaweza
kubana matumizi.

KUWA BAHILI
Wapo wanaume tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa pesa kwa kutoa ofa na zawadi kibao, Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa wewe unazo, Wakati akiwa anaamini hivyo, ukweli ulionao moyoni ni kwamba huna fedha za kutosha.

Unachotakiwa kufanya mapema ni kudhibiti matumizi yako hata kama pesa zinakuwepo, Ifahamike kuwa kutoa hakusababishi uhitaji, kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji, Weka maisha yako katikati

usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.

MUWEKE WAZI
Mueleze wazi kuwa huna wakati mpenzi wako anakuomba na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza, Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile. Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana pesa au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea Mwanamke akijua hilo naye ataongeza mizinga ili afaidi.

Elewa tu mapenzi si kukomoana, mapenzi ni kusaidiana, Jenga tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku moja na wewe ukiwa na tatizo akusaidie,Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa kero, Kumbuka kumpiga ‘mizinga’ mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi.


  Pata Ajira Ya ndoto yako yenye mshahara mnono na Masharti (Experience) nafuu ukiwa na App ya ajira forum Ajiriwa sasa πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2JdsN14

No comments:

Post a Comment