Sunday, March 22, 2020
UTANIKUMBUKA TU SEHEMU YA TANO-05
Edga alitaharuki sana aliposikia Kayumba kamtaja Catherine kwa huzuni huku akitiririsha machozi,hakutaka kujua papo hapo sababu hasa iliyopelekea hali hiyo, zaidi alimshika mkono wakarejea maskani. Baada ya chakula, sasa Edga alitaka kujua ukweli alionao Kayumba kipi kinacho msibu. Alishusha pumzi kisha akasema "Kayumba, nakumbuka niliwahi kukuuliza sababu gani ambayo inakufanya mara kadhaa uso wako usionyeshe tabasamu. Lakini hukutaka suala hilo tulizungumzie badala yake ukadai tuzungumzie masuala ya kazi,lakini pia leo wakati tunatoka kazini, kuna gari fulani hivi ulikuwa ukulikodolea macho, na baada nikakusikia ukitaja jina Catherine. Hivi huyu Catherine ndio nani kwako, na kwanini umelitaja jina ilihali ukiwa na majonzi? Tafadhali sana Kayumba usinifiche we niambie tu ukweli ", aliongea Edga kwa sauti ya chini huku akimtazama Kayumba katika mwanga hafifu uliopenya mahali walipolala kutokea umeme uliokuwa ukimulika kwenye moja ya nyumba. Kayumba alishusha pumzi ndefu kwanza, alijisonya mara mbili mfululizo huku moyo wake ukihisi uchungu, hali ya kuwa kinywa chake nacho kikihisi uzito kunena kile kilicho mkuta ingawaje baadaye alianza kumsimulia hali jinsi ilivyokuwa. Alisema "Edga, kuna wakati najikuta naogopa kulala. Sababu kila nikifumba macho yangu namuona Catherine. Ubongo wangu umevurugika, kiasi kwamba siwezi kukaa masaa matatu pasipo kumkumbuka Catherine. Catherine ni mwanamke ambaye nilianza naye mahusiano angali wadogo sana, kijiji kizima kilatambua uwepo wa penzi langu na yeye mpaka tunafika umri wa utu uzima. Nilimpenda sana Catherine wangu kiasi kwamba wanawake wengine nikawaona hawafai", Kayumba kabla hajaendelea kusimulia akayafuta machozi yake yaliyokuwa yakimtiririka,kwisha kufanya hivyo alisema "Ilikuwa hivi...." akaanza kukumbuka.
*********
"Kayumba mpenzi wangu, pole sana kwa matokeo lakini siku zote kuferi shule sio kuferi maisha", ilisikika sauti ya Catherine akimwambia Kayumba,pindi wawili hao walipokutana na kuanza kuzungumza mstakabali wa penzi lao mara baada kuona dhahiri shahili Elimu u karibu kuwaweka mbali baada Catherine kuchaguliwa kuwa moja ya wanafunzi waliofauru kuendelea na Elimu ya sekondari. Catherine aliongea maneno hayo huku akiwa amemkumbatia Kayumba
"Ni kweli kabisa Catherine, ila hilo lisikupe shida. Akili yangu kwa sasa inawaza kutafuta pesa ili nihakikishe unafikia malengo yako. Nakupenda sana Catherine wangu", alijibu Kayumba. Catherine aliangua kicheko, kisha akaongeza kusema "Na mimi nakuombea mpenzi wangu, na sitosita kuendelea kukwambia kuwa nakupenda sana zaidi ya sana. Nitasoma kwa bidii, ili nipate kazi nzuri itakayo nipa kipato kizuri ambacho kitatufanya tujenge familia bora"
"Ahahahah hahahaha", Kayumba alicheka. Alipohitimisha kicheko chake akasema "Catherine, unajua wanaume wengi wa sasa wanaamini kwamba mchumba hasomeshwi, dhana hiyo imejengeka baada wale wasaliti kuwa fanya wapenzi wao kuumizwa. Kwa maana sasa, mimi Kayumba nataka nionyeshe dhana hiyo ni potofu. Nitapigana mpaka dakika ya mwisho kuhakikisha unatimiza malengo yako "
" Amini mpenzi wala sitokusaliti japo nitakuwa mbali na wewe ", isisitiza Catherine mbele ya macho ya Kayumba. Wawili hao walifurahia sana, na sasa walisubiri siku ile ambayo Catherine ataondoka kwenda kuanza masomo ya kidato cha kwanza iweze kuwadia. Mazungumzo mengine kadha wa kadha yalifuatia, lakini hayakuchukuwa muda mrefu sana Catherine akamuaga Kayumba huku akidai kuwa anakwenda kuandaa chakula cha usiku.
"Usiku mwema mpenzi wangu Kayumba..", kwa sauti ya chini Catherine alimuaga Kayumba wakati huo akiwa kando yake hatua kadhaa mbele. Kayumba alimtazama akatikisa kichwa ilihali tabasamu likiupamba vema uso wake, kisha akajibu "Usiku mwema pia".. Yote hayo Kayumba aliyakumbuka na sasa alikuwa akimueleza rafiki yake Edga. Hakuisha hapo, kwa sauti iliyoambatana na kilio Kayumba alisema "Basi tulisubiri ile siku ya yeye kwenda kuanza masomo iweze kuwadia, wakati huo siku hiyo ikisubiriwa mimi niliendelea kutafuta pesa kwa kulima vibarua. Siku hiyo ilifika, kuanzia hapo mimi na Catherine tukawa tunaonana kwa nadra hasa hasa pindi nimpelekeapo fedha za kutatulia shida mbali mbali. Ilinilazimu kusafiri mpaka mjini kumpelekea fedha, msaada pekee nilikuwa mimi sababu hakuwa na mama wala baba. Wazazi wake walifariki miaka mingi sana iliyopita aliishi na bibi yake ambaye naye hali yake ilikuwa duni. Hivyo Catherine mpaka anahitimu kidato cha nne, anaingia cha tano. Ghalama zote zilikuwa juu yangu mimi lakini kati kati ya msimu upatikanaji wa fedha ukawa mgumu kijijini kwetu. Nikawaza nitafanya nini, na hapo ndipo nilipoamua kuvaa moyo wa kijasiri, kijijini kwetu kuna mzee mmoja ni tajari, anang'ombe, mbuzi na mifungo mingineyo achilia mbali maduka mjini. Mzee huyo alikuwa na kawaida moja, kila baada ya siku mbili anasafiri kuelekea mjini,na saa za kurudi alipenda kurudi jioni sana kwenye giza totoro. Akili ya haraka ikanijia, nilipoona nachelewa kupata fedha ikanibidi nipange njama ya kumpora begi alilopenda kutembea nalo. Niliamini fika begi hilo litakuwa na fedha za kutosha,sikuona hatari kwa maisha yangu yote sababu ya penzi la Catherine. Kwani wakati nawaza hayo, Catherine tayari alikuwa amerudi nyumbani shauri kwa muda. Kweli nilifanya hivyo, na nilibahatika kuondoka na begi lake. Lakini kumbe wakati nakimbia baadhi ya watu waliniona, pasipo mimi kujua. Nguvu ya pesa aliyokuwa nayo yule mzee ilimfanya kunifungulia mashtaka na wala hakutaka mzunguko mrefu moja kwa moja nikafikishwa mahakamani". Alisema Kayumba kwa kirefu, na punde si punde akakumbuka tukio hilo. Ilikuwa ni siku ya vilio sana mahakamani, mzee Masasa baba yake Kayumba alilia kiume hali ya kuwa Bi mitomingi mama Kayumba na Catherine hawakuweza kuzuia sauti zao. Waliangua vilio, ni pale baada Kayumba kusomewa shatka lake linalo mkabili. Miaka saba ndiyo ilikuwa hukukumu yake, ajabu wakati ndugu jamaa na marafiki wakiwa katika hali ya majonzi, Kayumba yeye alionekana kutabasamu. Aliposhuka kizimbani, Catherine kwa sauti ya kilio alisema "Pole sana mpenzi wangu, najua umefanya haya kwa kujali ndoto zangu. Sina baba sina mama. Na wewe ndio ulikuwa nguzo yangu tegemezi achilia mbali bibi yangu. Leo hii unaondoka?.."Catherine alilia.
" Catherine. Hupaswi kulia, najua bado tupo pamoja ndani ya moyo wako. Na hivyo basi pesa nilizokupa ni Nyingi sana, zitakusaidia kwa kiasi kikubwa. Ila tu, ombi langu naomba upendo wangu usiutupe.. ", alijibu Kayumba wakati huo akivutwa na moja ya askari. Pumzi ndefu alishusha Kayumba baada kumsimulia Edga namna alivyomjali na kumthamini Catherine. Hakika ni kumbukumbu ambayo iliuumiza moyo wake. Alikaa kimya kidogo, punde alivunja ukimya huo akasema na kusema." Baada changu kumalizika nilitamani sana nimuone Catherine. Nikapata habari kwamba yupo Dar es salaam, tayari amepata kazi na maisha yake anayeendesha vizuri. Nilifurahi sana, sikuwa na ndoto ya kukanyanga ndani ya jiji hili, lakini ilinilazimu kuja kumuona mpenzi wangu nikiamini kuwa atafurahi sana kuniona. Ila sasa kilicho tokea Edga, huwezi amini Catherine amenikataa,amenikana akidai kuwa penzi langu kwake limepata na wakati kwa kigezo kikubwa kuwa yeye ni msomi, hawezi kuwa na mimi mtu nisiye na Elimu. Edga! Catherine wa kunifanyia mimi haya? Inamaana amesahau fadhila zangu zote? .. ", alisikitika sana Kayumba,achilia mbali Edga ambaye alionyesha upole wa hali ya juu. Kisa cha Kayumba kilimuacha mdomo wazi, maumivu aliyoyahisi hayakuwa na mfano. Lakini baadaye, Edga alimgusa Kayumba kisha akamwambia
" Pole sana Kayumba rafiki yangu, siku zote mtu hujifunza kutokana na makosa. Hakika ni kosa kubwa sana ulilolifanya braza, mchumba hasomeshwi. Labda nikujuze kitu kimoja, wanafunzi vyuoni wanakawaida ya kuwa na wapenzi wengi. Dhana hii nafikiri itakuwa imemkumba na Catherine wako na ndio maana akaona heri atoke na msomi kuliko wewe usiye na Elimu. Na kama sivyo basi hakupenda kutoka moyoni na utambue kuwa yale hayakua mapenzi, ilihali ulimuonyesha kujali lakini yeye hakuliona hilo, hivyo basi huna budi kumuacha aende!! Kwa maana kila jambo hutokea kama kipimo cha maisha. Ngoja nikwambie jambo muhimu katika maisha yako. Ni vizuri sana unaufahamu mto,maji ya mto hukabiliana na vikwazo mbali mbali lakini havizuii maji kutiririka. Mto unapokutana na miamba hata mara moja hauwezi bali hutengeneza njia yake juu ya mwamba huo. Mto unanguvu kiasi kwamba binadamu hujenga madaraja juu yake ili waweze kuvuka na pale unapojaa huweza hata kuyabomoa. Amini jitihada huwa hazizidi kudra, hebu kuwa wewe kama mto. Nina imani ipo siku atakukupumbuka tupige kazi ", Alisema Edga. Maneno ambayo yalimfanya Kayumba kuyatafakari mara mbili mbili. Punde akaachia tabasamu hafifu.
USIKOSE SEHEMU IJAYO
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2y1wIMc
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment