Saturday, February 29, 2020

Hizi Hapa Hatua 5 Za Kuzungumza Na Mpenzi Wako Aliyekasirika.




Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha.
Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. 
 
Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya.

Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana.

Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika.

MPUNGUZE MHEMKO
Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano.

Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi.

MSOME SAIKOLOJIA YAKE
Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira.

Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira.

MRUHUSU AKUJIBU
Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake.

EPUKA MARUMBANO
Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena.

“Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano.

MUOMBE MSAMAHA
Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.”

Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2T7lqOt

Kwanini Wanawake Hudanganya Juu Ya Idadi Ya Wanaume Walio Lala Nao ?




Wanawake wengi wanadanganya idadi ya wanaume ambao wamesha lala nao. Kwasuala hili wamekuwa wanadanganya ili ku ficha kuwa sio wazuri kwenye mahusiano au ni namna gani amekuwa akishidwa kufikisha ahadi za mahusiano na kuachika au kuacha mahusiano yaliyo pita. Wanawake wengi wanakuwa na wasiwasi juu ya uwazi wao juu ya idadi ya wavulana walio nao au mahusiano yao wavulana watawadhani kuwa sio wakamilifu kwenye mahusiano napia sio wazuri kwenye mahaba kitandani. Pia wanahofu baadhi ya wanaume watawaona kuwa malaya au hawatulii kwenye mahusiano, kabla hujamsababisha mwanamke kwenda kwenye huo uongo wake, kuna vipengele muhimu kuvijua ili uweze kufika wakati wa kumuuliza hayo. 

Wakati muafaka wa kumuuliza msichana juu ya mahusiano yake yaliyopita.

Kama unataka kumuuliza mwanake uliyempata juu ya mahusiano yaliyo pita au wangapi amelala nao kitandani inatakiwa kuwa na muda sahihi. Huwezi kuuliza swali hilo wakati mnatoka kwa mara ya kwanza au wakati mpo kwenye mapumziko kama hotelini au bar. Hii itakuwa umeharibu kila namna ya wewe kupata ukweli. Kila mwanamke atakuwa na aibu au woga kwa mwanaume anaye uliza swali zito kama hili mapema hata mahusiano hayajaanza kuwa makini. Pale mvulana anapofanya hivyo basi mwanamke lazima atadanganya na kuficha. Ni rahisi kuuliza swali hilo baada ya kuwa mmezoeana na kuwa mnatoka out mara kadhaa. Pale mwanamke atakapoona upo naye na unajali kujua basi atakuwa radhi kukwambia ukweli.

Japokuwa kwa wavulana ni rahisi kwao kutaja kuwa nilisha lala na wanawake kumi au zaidi. Pale mwanamke anapo taja hivyo anadharaulika na ndio maana haishangazi kwa wanawake kudanganya.
 

Je wavulana wanayo haki kuuliza?

Labda kama msichana ambaye upo naye unajua alikuwa malaya wa kujiuza au mcheza filamu za ngono basi hamna haja ya wewe kuuliza maana itakuwa haikuhusu. Kwamaana jambo ambalo haulijui ukweli wake halitakuumiza moyo wako. Kwakuongezea nikwamba kila msichana/mwanamke hudanganya juu ya idadi ya wavulana alio kuwa nao au alio wahi kulala nao. Na hili halitasababisha kubadilisha mahusiano yenu mnayo taka kuyaanza. 

Kwanini wavulana hawapati ukweli kwenye suala hili!

Kuna ngono wanawake walizo zifanya ambazo hawataki kuzizungumzia kamwe. Kwasuala hilo nikama kunyanyapaa. Kwa mfano, Alijikuta amebakwa au amefanya ngono bila kupenda wakati akiwa high school au chuo. Kwahiyo hutakuja kujua kuhusiana na jamaa aliye lala naye wakati akiwa amelewa na kufanya naye ngono. Kwa wanawake wengi nivigumu kujadili juu ya hilo.

Itakuwa ni vyema kwa wavulana kumkubali mwanamke bila kutaka kujua yaliyo pita kwake. Wanawake wanadanganya, lakini nia ni kutunza utu wake na heshima ya mwanamke. Hawataki wavulana wawachukulie kama mtumwa wa mapenzi au malaya kutokana na aliyo yapitia. Wavulana wengi hudanganya juu ya emotional kwenye msichana anaye mvulia au tamaa za mwili kwa mwingine. Wanawake nao hudanganya juu ya wavulana walio ngonoka nao. Nijambo la kuficha kwa mvulana kudanganya hisia zake za kweli na msichana kudanganya ili asijulikane marangapi kalalwa kitandani.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2I8vv7r

Fanya Mazoezi Haya kwa Wiki Tatu Kuongeza Nguvu za Kiume.




Kuna jambo linanishangaza sana, utakuta mwanaume anapata muda wa kukaa kitako muda wa dakika tisini au zaidi akiangalia mpira, au masaa manne, matano na wengine wanakesha kabisa katika baa wakinywa na kula tu, lakini wanasahau kabisa kutenga muda tena mdogo tu kama dakika tano mpaka nane kwa siku kwa ajili ya kuimarisha nguvu za kiume kwa kufanya mazoezi ya kuongeza nguvu za kiume.

Mwanaume anefanya mazoezi ya kuimarisha misuli ya uume hawezi kuwa sawa na mwanaume asiyefanya mazoezi haya sio tu katika kuimarisha nguvu zake za kiume lakini pia kuweza kujitawala katika tendo la ndoa na kuweza kumfikisha mwanamke katika raha ile inayotakiwa.

Mazoezi  haya yakifanywa kwa dhati yanaweza kumpa mtu matokeo mazuri sana ilimradi afuate utaratibu atakao takiwa aufuate.

Hizi ni miongoni mwa faida zinazopatikana kwa kufanya mazoezi haya ni hizi zifuatazo:

Kwanza humpa uwezo mwanaume kuweza kusimamisha uume wake kwa muda mrefu zaidi kuliko ambavyo alikuwa anaweza kuusimamisha  kabla ya kufanya mazoezi haya.

Pili mazoezi haya hufanya mtiririko wa damu kwenye uume uwe mzuri hivyo kuufanya uume uwe na nguvu na kuondoa kabisa tatizo la nguvu za kiume.

Tatu humpa uwezo mfanyaji wa mazoezi haya kukawia kumwaga mbegu hivyo kumpa nafasi mwanamke aweze kufikia katika kilele chake pasi na kumkatishia njiani.'

Vifaa Unavyohitaji

1.   Mafuta ya mizeituni (Olive Oil) au mafuta ya nazi au Alizeti au mafuta ya mgando (gel)

2.   Jiko  lolote ili upate mvuke wa kutosha unaweza kutumia jiko la mchina, stove, au hata la mkaa lakini isiwe moto mwingi uwe kiasi tu lengo ni mvuke

3.   Kitambaa kisafi na laini na maji safi ya uvuguvugu
Namna ya kufanya mazoezi ya Kuongeza nguvu za kiume

1. Loweka kitambaa chako katika maji ya uvugu vugu kisha anza kwa kuusafisha uume wako kwa kitambaa laini cheye maji ya uvugu vugu kama unauchua uume kwa kuuvuta mbele. Fanya zoezi hili kwa dakika tatu.

2.  Pakaa mafuta yako kwenye viganja vyako viwili vya mikono yako kama vile unataka kujipaka mafuta mwilini.

3.  Weka viganja vyako ili vipate mvuke wa moto kutoka katika ama jiko la mchina, stove au kitu chochote utakachotumia. Ukiona viganja vimepata joto kiasi cha kutosha siyo mpaka uungue mikono, kisha

4.  Kamata uume wako ukiwa unauchua kwa kuuvuta mbele kwa nguvu kidogo sana ukianza na mkono wa kulia alafu wa kushoto au kushoto halafu kulia vile utakavyoona inafaa. Joto kwenye mikono likiisha rudisha mikono yako uipashe tena ili ipate joto kisha rudia  kuuvuta vuta tena uume kwa muda wa dakika kumi.
Kumbuka

Mazoezi haya hufanywa mara mbili asubuhi tu mtu ukiamka na wakati ukitaka kwenda kulala na ni kwa muda wa wiki tatu. Utaona matokeo yake.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2Talq0k

Vitu 7 Viinavyowaboa Wanawake Ukivifanya Mkiwa Kitandani.





  Sababu ya kwanini mara ya kwanza mapenzi yalikuwa matamu kitandani kati yako na yeye ni kwa sababu ulikua hujui nini cha kutarajia.


Hakuna mtu anaependezwa na mpenzi anaeboa. Na kwa mioyo yetu ya kiume hakuna sehemu inayotuumiza na kutuacha tumejawa maswali mengi na paniki kede kede kama pale mambo yanapokuwa hayaendi vizuri kitandani.

Kiumeni.com kama jadi yetu ya kukufanya wewe uwe mwanaume bora zaidi, tumekuandalia mambo saba ambayo yanasababisha hali hii itokee na kumfanya mwenza wako aboreke kitandani na kuishia kutoa visingizio vingine visivyokuwa na maana sababu anaona aibu kukwambia. Visome kwa umakini na uvielewe kama unataka wawe wanarudi na kutaka utamu zaidi.

1 - Unaomba ruhusa

Kama ukiwa unauhusiano wa muda mrefu na mwanamke na umeshaelewa lugha yake ya mwili na hisia zake, hakuna kinachomuondoa kwenye hali ya kihisia kama kuombwa ruhusa ya kiofisi kuendelea na jambo hasa juu ya yale mambo yetu mazuri, hauhitaji karatasi ya mahakama ya ruhusa kuendelea kumpa vishawishi na kumtekenya. Mpenzi mzuri ni yule anaejua kumpa vishawishi na kumfanya asisimke kwa akshi hata kama akili haikua katika hayo mawazo bila ya kukata ushuru wa kuuliza uliza kiasi cha kumuhalibia hisia nzuri zilizokuwa zinaanza kumuingia, vitu vyepesi kama macho mazito ya mahaba au miguso flani ya kumpa akshi ni njia nzuri ya kumuandaa.

2 - Unatabilika

Kama mmekuwa pamoja kwa muda mrefu, hii ndio litakuwa tatizo kubwa maana sababu ya kwanini mara ya kwanza mapenzi yalikuwa matamu kitandani kati yako na yeye ni kwa sababu ulikua hujui nini cha kutarajia. Kama ukiwa unataka kurudisha khali kama awali inakupasa ubadilishe ratiba na ufanyaji wa mambo ili kuleta hali flani ya upya katika uhusiano wenu.

Usiogope kujaribu vitu vipya ambavyo wote kwa pamoja mnaweza kuvipenda, usiache ikafikia hali kiasi akawa anajua mpaka ni kitu gani utachokwenda kinachofatia unachokwenda kukufanya, kwa mfano kama huwa unatumia dakika 5 ukimtaalisha kimapenzi, siku nyingine jaribu kabadilika na kutumia dakika 20 huku ukimsisimua kwa maneno matamu na kumpandisha ashiki kwa kumpapasa kivingine tofauti na unavyopendelea kufanya. Atashangaa mababidiliko na kabla hajajua mtakua nchi za mbali mkitalii.

3 - Mapenzi ya kukurupuka

Mwanamke wako sio punda wa kupandwa bila matayarisho, hajawa doli la kuchezea. Wanawake wote hupendwa kutayarishwa na kupewa mapenzi ya huba yenye hisia, sio mapenzi ya kikurya "Mama Robhii, raraa ni kurariie!". Sio kwa staili hii jamaa, jaribu kuwa mvumbuzi wa mambo, ongeza viungo mtoto wa watu alegee na kusisimka kwa huba na mahaba, usiwe na haraka maana tayari yupo kitandani, mmenye kama ndizi kidogo huku unakula taratibu, kidogo tena huku ukiyaachanisha maganda taratibu na kwa staili ndo unakula tena, we ni mpenzi wake na sio mbakajia, mfanye akuone kama malaika ulioshushwa toka mbinguni kwa kazi moja ya kumpenda na kumpa raha duniani.

Usipojiongeza kwenye mambo mazuri ya kitandani, mwingine mjuzi zaidi yako atakupokonya tonge mdomoni.

4 - Haujiongezi inavyopaswa


Japo wanawake wengi huwa ni rahisi kukubaliana na staili ya mapenzi kutokana na wenza wao, ila iwapo kama unatumia staili hio hio kila mkikutana na hamna vionjo vyovyote vinavyobadilika lazima mwenza wako achoke na kuboleka na utendaji wako wa kazi. Kwahio kama ukitaka asikuchoke inabidi ujiungeze na ufanye mabadiliko ya hapa na pale.

Ndio, umepatishia sahihi lazima ubadilike kimahaba, na sio kitandani peke yake hata nje ya hapo, mnongoneze wakati mnapata chai ni nini utamfanyia giza likiingia, au mtumie meseji tata za jinsi unavyowaza na kutamani giza liingie uwe mikononi mwake, mtoe kwenye mtoko na mpe malavidavyi ya kutosha na utamuacha anawaza umetokea sayari ipi.

Ukifanya kubadilika kila muda utafanya na yeye pia abadilike na kukuonyesha utundu wake wa kike ulipo.

5 - Sehemu moja ya matukio

Kama mwanamke wako unampeleka sehemu moja tu ya tukio, mpaka amekalili jinsi silingi bodi ilipokatikia, upo kwenye matatizo makubwa. Ila mabadiliko ya uwanja yanaweza kutatua hili tatizo hivyo usiwe na wasiwasi. Jaribu kujaribu kufanya matukio hata sehemu ambazo hategemei, mpeleke kwenye sofa, mpeleke bafuni na kama unamaji ya moto patakua patamu huko. Kama unagari, mmh napo unaweza kumaliza vile vile, ukawa mtu usiyetabilika tukio linalofuata litakuwa wapi na itamfanya msichana wako akuone mtu wa masapraizi ya kutosha.

6 - Hautumii maneno au unayatumia kupitiliza

Kutumia sana maneno flani matata kumnongoneza masikioni humfanya mwanamke apandishe mrukhani kwa fujo, ila usitumie maneno yaleyale maana kurudia rudia maneno huyaondolea maana husika na kuyafanya butu. Jaribu kuyatumia katika wakati muafaka na mudi iliyosahihi na fanya uchaguzi mzuri wa maneno matamu yanayoongeza akshi za kimahaba.

Ukimwambia anachokufanyia kinakuuwa maini kwa sauti nzuri ya besi iliyolegea kwa kumnongoneza au ukimwambia ametoka bomba na ukafatiwa na maneno elekezi ya kile ambacho unataka umfanyie kitabadilisha kabisa hali ya kuboreka kwa msichana wako akiwa kitandani na wewe.

7 - Fanya majaribio

Kama upo na mwanamke kwa muda mrefu na unataka mambo chumbani yanoge, unapaswa kubadilisha mikao, jaribu mikao mingine ya kimapenzi, zungumzeni na mwambiane anapendelea nini na angependa kujaribu kipi, mawasiliano ni nguzo kubwa inayoweza kubadilisha mazingira na kufanya staili anayoitamani.

Unaweza tumia dawa ya aibu kama Dompo, Sainti Anna au Dodoma Wine.

Kumbuka kinyume cha maboreko ni mafurahisho, ukitaka kufurahi jaribu kitu kipya ambacho hujawahi fanya au fanya unachokipenda ila kwa mguso tofauti na fikra mpya.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2I7equE

Hizi Ni Tabia za Wanawake Kulingana na Maumbile Yao.



Inasemekana wadada wana tabia tofauti katika mapenzi kulingana na maumbo ya miili yao, 
  1. Wasichana wafupi wanaongoza kwa wivu wa mapenzi na kuwajali wapenzi wao
  2. Wasichana warefu huwa hawawajali wapenzi wao na hawaogopi mahusiano kuvunjia hawajui kubembeleza hata kidogo
  3. Wasichana wenye DIMPOZ, MWANYA, MATEGE MBINUKO, MAHIPS NA KITHEMBE, hawa huongoza kwa kutokuwa WAAMINIFU katika mapenzi.
  4. Wasichana WANENE huongoza kwa MAPENZI YA KWELI yaani akipenda amependa kweli
  5. Wasichana WEMBAMBA hawa huwa ni WABISHI sana na hawa wanaongoza kwa kutendwa!
  6. Wasichana wenye NGOZI NYEUSI wanaongoza kwa KUTOA MIMBA na kupenda wanaume warefu na weupe
  7. Wasichana weupe wakiongoza kwa kuzalia nyumbani, na hawa weupe wengi wao huolewa wakiwa na watoto tayari huku wakipenda kuolewa na waarabu kuliko wanaume weusi.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2I7weG8

Ulishajiuliza Unapenda Nini Kwa Mpenzi Wako ? 18 hours ago Leo kwenye safu hii nimekuja tuongelee suala hili la wapenzi kupendana na kufikia kuwa mwili mmoja je, umewahi kujiuliza maswali kuhusiana na mwenza wako? Maswali haya yanawahusu wote. Mnatafuta nini ndani ya wenza wenu ni kitu gani mnaangalia/mnakiona ndani ya mtu unayeamua kuwa naye kama mchumba/mume/mke. Je, ni macho yake au tabasamu, ama ni muonekano wake, uchangamfu au upole, ni kitu gani unachokiona ndani ya mtu kinachokuvutia. Wengine wanavutiwa jinsi mtu anavyofikiria, au mwili wake, wewe je? Unaweza ukawa umevutiwa na kitu kimojawapo, lakini unajua uhusiano mzuri haujengwi na vitu hivi tu, kuwa na uhusiano mzuri na mwenza wako inahusisha vitu vingi sana tofauti na tabasamu lake iwe unatafuta mtu wa kuwa naye au kama tayari upo katika uhusiano hakikisha mnakubaliana vitu muhimu ambavyo mkividharau kisa umempenda kwa sababu ya shepu yake au ucheshi wake vinaweza kuharibu uhusiano huko mbele ambapo ni pagumu zaidi. Vitu unavyotakiwa kuangalia zaidi Hivi ni baadhi ya vitu unavyotakiwa kuangalia ndani ya mwenza wako kama unataka uhusiano mzuri na kama kweli atakuwa mke au mume, epuka kuangalia vitu vya awali kama hivyo nilivyovitaja hapo. Anakupa heshima yako, haijalishi kama yeye ni mkubwa kwako, na hapa heshima siyo salamu kama wengi mnavyodhani. Anaheshimu maamuzi yako, kama ni katika kazi au kitu unachoamua kufanya na siyo kukucheka au kukudharau. Hakukatishi tamaa anakuunga mkono kwenye kila jambo na kukupa moyo wa kushinda kila wakati. Hakasiriki ukijipa muda na marafiki au familia yako, unatakiwa kuwa na uhuru wa kujichanganya na watu wengine siyo yeye tu. Anasikiliza mawazo yako na kukushauri Mnashea vitu unavyovipenda kama vile kuangalia muvi, aina ya muziki, kucheza. Angalau muwe na kitu kimoja ambacho wote mnapenda ili muwe na kitu cha kufanya pamoja, vitu vingine mnaweza kutofa-utiana haina shida kwa sababu hata mapacha waliozaliwa pamoja kuna wakati huwa wanato-fautiana lakini iwe kuna kitu mnaendana ambacho mtashiriki pamoja. Mpenzi huyo asiwe mkaidi kwa kila kitu unachomwambia, hii inawahusu wapenzi wote si wanaume ama wanawake tu. Awe anaheshimu mipaka yako, siyo atake kujua kila kitu chako kama vile kukagua simu au wapi unapokuwa saa 24, kama mpo katika uhusiano mnatakiwa mheshimiane maana mwanzo wa kufuatiliana saa zote ndiyo mwanzo wa ugomvi usiyoisha. Asiogope kukuambia anavyojihisi, hii itawasaidia hata pale mtakapokuwa na matatizo ili muweze kusuluhisha mambo yenu, itawaondoa kwenye hali ya kila mtu kumuwekea mwenzake kinyongo. Kumbuka uhusiano unahusisha watu wawili, wewe na patna wako muwe na usemi ndani ya uhusiano wenu na msiogope kuambiana mnachohisi na kusikilizana pia. Ndani ya kila uhusiano kuna kugombana, hiki ni kitu cha kawaida kabisa. Wale mnaowaona wana furaha katika uhusiano wao wameweza kujua jinsi ya kuyamaliza matatizo yao.



Leo kwenye safu hii nimekuja tuongelee suala hili la wapenzi kupendana na kufikia kuwa mwili mmoja je, umewahi kujiuliza maswali kuhusiana na mwenza wako? Maswali haya yanawahusu wote.

Mnatafuta nini ndani ya wenza wenu ni kitu gani mnaangalia/mnakiona ndani ya mtu unayeamua kuwa naye kama mchumba/mume/mke. Je, ni macho yake au tabasamu, ama ni muonekano wake, uchangamfu au upole, ni kitu gani unachokiona ndani ya mtu kinachokuvutia. Wengine wanavutiwa jinsi mtu anavyofikiria, au mwili wake, wewe je?

Unaweza ukawa umevutiwa na kitu kimojawapo, lakini unajua uhusiano mzuri haujengwi na vitu hivi tu, kuwa na uhusiano mzuri na mwenza wako inahusisha vitu vingi sana tofauti na tabasamu lake iwe unatafuta mtu wa kuwa naye au kama tayari upo katika uhusiano hakikisha mnakubaliana vitu muhimu ambavyo mkividharau kisa umempenda kwa sababu ya shepu yake au ucheshi wake vinaweza kuharibu uhusiano huko mbele ambapo ni pagumu zaidi.
 

Vitu unavyotakiwa kuangalia zaidi

Hivi ni baadhi ya vitu unavyotakiwa kuangalia ndani ya mwenza wako kama unataka uhusiano mzuri na kama kweli atakuwa mke au mume, epuka kuangalia vitu vya awali kama hivyo nilivyovitaja hapo.

Anakupa heshima yako, haijalishi kama yeye ni mkubwa kwako, na hapa heshima siyo salamu kama wengi mnavyodhani.

Anaheshimu maamuzi yako, kama ni katika kazi au kitu unachoamua kufanya na siyo kukucheka au kukudharau.

Hakukatishi tamaa anakuunga mkono kwenye kila jambo na kukupa moyo wa kushinda kila wakati.
Hakasiriki ukijipa muda na marafiki au familia yako, unatakiwa kuwa na uhuru wa kujichanganya na watu wengine siyo yeye tu.
 

Anasikiliza mawazo yako na kukushauri

Mnashea vitu unavyovipenda kama vile kuangalia muvi, aina ya muziki, kucheza. Angalau muwe na kitu kimoja ambacho wote mnapenda ili muwe na kitu cha kufanya pamoja, vitu vingine mnaweza kutofa-utiana haina shida kwa sababu hata mapacha waliozaliwa pamoja kuna wakati huwa wanato-fautiana lakini iwe kuna kitu mnaendana ambacho mtashiriki pamoja.

Mpenzi huyo asiwe mkaidi kwa kila kitu unachomwambia, hii inawahusu wapenzi wote si wanaume ama wanawake tu.

Awe anaheshimu mipaka yako, siyo atake kujua kila kitu chako kama vile kukagua simu au wapi unapokuwa saa 24, kama mpo katika uhusiano mnatakiwa mheshimiane maana mwanzo wa kufuatiliana saa zote ndiyo mwanzo wa ugomvi usiyoisha.

Asiogope kukuambia anavyojihisi, hii itawasaidia hata pale mtakapokuwa na matatizo ili muweze kusuluhisha mambo yenu, itawaondoa kwenye hali ya kila mtu kumuwekea mwenzake kinyongo.

Kumbuka uhusiano unahusisha watu wawili, wewe na patna wako muwe na usemi ndani ya uhusiano wenu na msiogope kuambiana mnachohisi na kusikilizana pia.

Ndani ya kila uhusiano kuna kugombana, hiki ni kitu cha kawaida kabisa. Wale mnaowaona wana furaha katika uhusiano wao wameweza kujua jinsi ya kuyamaliza matatizo yao.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/3aj2yC3

Unayetembea na Mume, Mke wa Mtu Hii Inakuhusu Sana !




LICHA ya kuwepo na msemo wa mke au mume wa mtu ni sumu bado watu wengi wameendelea kutenda tendo hilo. Hawahofii madhara yake. Wanaona kama ni jambo la kawaida. Wanahalalisha jambo hilo utafikiri kufanya hivyo ndiyo jambo jema. 

Kutembea na mke au mume wa mtu ni tabia. Huanza taratibu na baadaye hukua. Kama vile ilivyo kwa mlamba asali, kadiri anavyopata utamu ndivyo anavyozidi kulamba. Kila anayefanya kitendo hiki huwa na sababu zake.

Kuna ambao wanaingia kwa sababu ya mawazo. Alikuwa na mpenzi au mchumba wake wakaachana, ghafla anajikuta ameingia katika penzi la mke au mume wa mtu kwa sababu ndiye aliyempata kwa wakati huo.

Wengine wanaingia katika janga hili kwa sababu ya tamaa tu. Wengi sana wanaingia kwa sifa hii. Wanataka maisha mazuri hivyo wakiyaona yanapatikana kwa mke au mume wa mtu, wanaingi. Hawaangilii matokeo ya baadaye, zaidi tamaa ndizo zinazomuongoza.

Hapo ndipo unapokuta mwanamke anapokubali kufanywa chombo cha starehe. Mume wa mtu anayetembea naye anamtumia kama chombo cha kumuondoa mawazo yake. Anamfanya kama chombo cha kumstarehesha pale anapokuwa amegombana na mkewe.
Bahati mbaya zaidi mwanaume wa aina hiyo hupenda kuumiliki huo mchepuko wake. Hataki amuone na mwanaume mwingine. Anahakikisha kwa kila namna anamfunga kwa kila njia anayoijua ilimradi asichepuke.

Anahakikisha anampatia kila kitu. Kama ni fedha, nyumba na hata magari ya kifahari anampa. Anafanya hivyo ili asisalitiwe. Na akithubutu kufanya hivyo lazima mhusika akione cha moto. Hapo mwanamke hana ujanja, anakubali kuepusha shari.

Matokeo yake anajikuta anapoteza muda. Anashikiliwa na mtu ambaye tayari ana mtu wake rasmi. Yeye ni wa ziada lakini mwanaume anamfunga asipate mtu mwingine. Atazalishwa, atalea watoto na kujikuta uzee ukimnyemelea pasipo kuwa na ndoa.

Vivyo kwa wanaume, nao wanapoteza muda. Wanajikuta wameshikiliwa na wanawake wenye fedha. Hawataki wawe na wanawake wengine. Wanaume hao nao pia hupoteza muda. Lakini wengine huingia kwenye tabia hii kwa tamaa za kimwili.

Kila anayekutana naye anataka awe wake. Haijalishi ni mke au mume wa mtu, yeye anamtamani na kumtaka awe wake. Marafiki zangu, kuna kila sababu kila mmoja wetu kujiuliza mara mbilimbili kabla hujaamua kuchepuka na mume au mke wa mtu.

Fikiri kuhusu madhara ya kupoteza muda. Fikiri kuhusu mustakabali wa maisha yako ya baadaye. Utatumika hadi lini? Utakuwa mtumwa wa fedha hadi lini? Tamaa zako zitakufikisha wapi? Kwa nini usimpate wako? Utakayekuwa na uhuru naye.

Mume au mke wa mtu huwezi kuwa na uhuru naye. Atatumia muda mchache kwako lakini bado atalazimika kuihudumia familia yake. Wewe utabaki kuwa wa ziada. Bahati mbaya anakubana wewe usioe au kuolewa na mtu mwingine.

Kuna umuhimu wa wewe kuwa na mchumba wako. Mtakayeanza na kumaliza pamoja safari ya hapa duniani. Mtu ambaye mtaelewana kwa kila hali, mtafikia hatua ya kufunga ndoa na kulea familia yenu pamoja.
Utakuwa mtu wa wiziwizi. Hujiamini. Utazaa au kuzalishwa watoto wa nje ya ndoa. Jambo hilo ni hatari pia katika mustakabali wa watoto. Ndoa wewe utazisikia kwa wenzako. Ni jukumu lako kuchagua njia iliyo sahihi. Kuchagua mwenza sahihi pasipo kusukumwa na jambo lolote.

Maisha ya uhusiano ni zaidi ya fedha. Uhusiano ni utu. Mtu ambaye mtajaliana kwa kila jambo. Katika shida na raha. Katika uzima na magonjwa, hayo ndiyo maisha mazuri ya uhusiano. Kinyume na hapo ni janga. Utafurahia maisha kwa kipindi fulani, baadaye utapata machungu.






from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/398ACk8