Thursday, May 30, 2019

WANAUME MSIWAFANYIE HIVI WANAWAKE





Mungu anasema si vyema mtu (Mwanaume) awe peke yake. (Mwanzo 2:18), na ni kweli Mwanaume hakuumbwa kuwa peke yake eti jeshi la mtu mmoja hata Mungu anajua, upweke unaleta disorder. Lakini wakati unasubiri au ukiwa kwenye mchakato wa kutafuta mwenzi wa maisha usitumie wanawake kama magazine za waiting room Airport ukiwa unasubiri muda wa kupanda ndege. Usijiingize kwenye mahusiano na mtu eti unavuta-vuta muda kupata mtu sahihi. Ni mbaya sana.
Unamtongoza dada wa watu na kumsumbua mpaka anajiaminisha kuwa unampenda kumbe hayuko hata kwenye ndoto zako, unataka tu mtu wa kupotezea mawazo. Yeye (Msichana) anajenga imani kwako na kuanza kukuingiza kwenye mawazo ya hatima (future) yake. Anakubwagia limoyo lake lote, kumbe wewe hata hisia huna. Inaumiza sana.
Bora utumie hiyo nafasi kujikita kwenye michezo au gym au mchakato wa kibiashara, au online courses ili uvute muda ukiwa unajiandaa kupata mtu sahihi wa maisha yako. Kwa nini umwambie mtu unampenda sana na uko tayari kufa kwaajili yake, wakati unajua unamtamani tu na sio kweli kuwa unampenda? Kwanini uumize hisia za mtu kwa makusudi?
Kwa nini ujiingize kwenye maisha ya mtu na kumvurugua utaratibu wake kumpotezea muda wake?
Huenda usingakaba hiyo nafasi angekuwa huru kupata mtu wake wa maisha. Lakini we umekaa kwenye maisha yake kama jiwe kwenye mlango wa kaburi la Lazaro, mbele hasogei nyuma harudi, kila siku unamuumiza tu. Umekuwa kitunguu kwenye maisha ya mtu haishi kulia kwa sababu hisia zako haziko kwake.
Hii ni tabia mbaya sana. Kama unasoma post hii na uko kwenye mahusiano na mtu ambaye unampotezea wakati tu huna malengo naye nakusihi umuache mara moja. Kumbuka utapata watoto wa kike najua hautapenda mtu awe kwenye maisha ya mwanao akimpotezea muda.
Haya mambo tunafanya wanaume hata Mungu hapendi. Watu wanafeli masomo, watu wanakunywa sumu, wengine wanafia vitandani mahospitalini wakitoa mimba tulizokataa, wengine wamepata magonjwa ya mioyo kwa sababu ya hayo maumivu tumesababisha. Hayana faida hayo maisha, unajiwekea tu laana na mikosi itakayosakana maisha yako. Na ni utoto na upumbavu kutumia uanaume wako, uongo na ujanja ujanja kuchezea hisia za mtu. Amua kubadilika. Huu sio ujanja ni ufala.
TUKUMBUKE MUNGU ANAONA NA UNACHOKIFANYA NI MBEGU UNAPANDA.
#USIJE_KUSEMA_HUKUAMBIWA.


from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/30SOUkZ

JIFUNZE KUMUDU HISIA ZAKO ILI USIENDESHWE NA MAPENZI



Mapenzi ya kweli ni yale ambayo watu huumizana kiasi,,hugombana kiasi,,husumbuana kiasi,,hulizana kiasi,,zaidi ya yote hawa wawili hutumia busara na hekima kufutana machozi na kuruhusu tabasamu kurejea ndani yao na kupanga maisha pamoja,,kusikilizana,,kuheshimiana,,kufanya yampayo amani kila mmoja wao,,zaidi ya yote kila mmoja kuijua thamani ya mwenza wake na upendo wake,,,,HILO NDILO PENZI LENYE NGUVU


from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2wuwtW4

LOOK AT HER IN THIS DRESS






from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2JMuk0z

USHAURI MWANAMKE WA KUOA


Nawaandikia ninyi vijana wa kiume na wanaume wote, maana mna nguvu na mmejaliwa na mwenyezi Mungu utashi, hekima na busara. Yote hayo ni ili muweze kutawala kila kitu tokea kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu huu. Wekeni wivu pembeni na Yafuateni haya;
1. Oa mwanamke ambae unaweza KUSALI nae na sio kwa sababu anajua KUFANYA MAPENZI vema.
2. Mwanaume bora KAMWE hapimwi kwa idadi ya wanawake alionao au aliotembea nao BALI kwa idadi ya wanawake aliowaambia “Mimi ni mume wa mtu” au ninae mtu tayari.
3. Kuna aina ya wanawake unatakiwa kuwaepuka kabisa kwa gharama yoyote ile, “wanawake wanaodhani uzuri wao ndio bora zaidi kuliko tabia zao”
4. Kila mwanamke anavutia akivaa nguo fupi inayoonesha maungo yake wazi, ila kama utakuta mwanamke amevaa nguo ndefu au za kusitiri mwili wake na bado anavutia, huyu ni dhahabu! Anathamini mali za mumewe!
5. Kamwe usimpe mwanamke mimba ya mtoto kabla hujampa mimba ya malengo na ukayatimiza.
6. Tafuta mwanamke ambae atakupa challenge ya maisha na kuongeza uwezo wako wa kufikiri na sio mwanamke wa kila kitu Ndio mzee!
7. Wanawake wakamilifu hawapatikani popote duniani, ila wanawake bora wapo kila mahali.
8. Mwanamke anaweza kukusaliti, ila Mungu hawezi kukusaliti, hivyo basi kabla hujapata mwanamke Mpate Mungu kwanza. Kuna raha sana kuwa ndani ya Mungu asikwambie mtu!
9. Kama unajijua umefikisha miaka 25 na kuendelea epuka mambo ya kivulana, kuvaa suruali katikati ya makalio, kuvaa hereni, kubadili badili wanawake kama unachambua mitumba ya karume etc
10. Usitumie kichwa chako kunyoa kiduku, tumia kichwa chako kuwaza mambo yenye tija ikiwemo kutafuta pesa na kuongeza hazina ya maarifa.
MBARIKIWE SANA WANAUME WOTE WENYE BUSARA..


from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2YYl1Om

MKE ALIYE MTAMU WA MANENO YAKE NA KAULI NZURI NI TIBA KWA MME WAKE



Habari yako msomaji wangu, natumaini upo salama,leo nataka niseme na wanawake wenzangu,,nataka nikuambie tu kuwa safari ya ndoa ni ndefu si sawa na safari za kwenda mikoani,,hivyo usijidanganye kwa kujifariji kwa furaha ya muda mfupi,,kuna mambo yanatokea mwanamke unakuwa sababu ya kupoteza kwa furaha katika mahusiano yako kwa kukosa lugha nzuri,unadhani unajenga au unamkomesha mmeo kumbe unabomoa na kufungua upenyo wa upendo kupungua na kutafuta mahali pa kibinti tu kinachojua kubembeleza na kujali,,mwisho utafute mchawi nani kumbe mdomo wako,,hebu kuwa mtamu wa maneno yako,,kuwa na kauli nzuri zenye nidhamu na ubembelezi,,acha kupayuka payuka jitambue uwe wa wakitofauti.

from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2wuWwMy

FAIDA ZA MASIKILIZANO KWENYE MAHUSIANO




Masikilizano huleta maelewano thabiti yanayopelekea kudumishwa kwa penzi,,,,mapenzi hayahitaji ujuaji uliopitiliza bali yanahitaji upeo ambao utaruhusu mawazo yenu wote yawapeleke njia ambayo ni sahihi,,,usawa kwenye mapenzi ni sahihi ili isije mmoja akaelemewa na mzigo halafu akakinai mapenzi,,,,,hebu ishini kwa kuongozwa na upendo na kila mmoja aweke tamaa pembeni ili mfikie malengo yenu mapema.

from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2YY8yKx

MPE VIPAUMBELE MPENZI WAKO





Vipaumbele kwenye maisha vipo vingi na kila kimoja kina nafasi yake,,,mwenza wako kuna wakati anahitaji muda wako tu na si kingine,,,wakati mwingine atahitaji umwoneshe kuwa yeye ana nafasi gani katika maisha yako ili awe na uhakika wa usawa,,,uhalisia wa ukweli wa penzi lako kwake,,,,,,unaposhindwa kumpa kipaumbele au muda wako,,,tambua kuwa atahisi kuwa una mwingine muhimu zaidi yake na hata upendo wake kwako utakuwa wa mashaka sababu ya kukosa uhakika kama anapendwa au hapendwi.

from UHONDO KITANDANI http://bit.ly/2wtqSPs