Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikiria au kubeba viungo (organs) fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi (Opening) na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiriwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo.
Ngiri (Hernia) ni uvimbe (eneo lililotuna) kutokana na viungo vya ndani ya mwili kusukuma kuta za misuli inayozunguka au kushikilia viungo hivyo. Hernia hutokea wakati kuna udhaifu au kuna tundu kwenye kuta za misuli inayoshikilia na kuviweka viungo vya tumbo kwenye sehemu yake (peritoneum). Udhaifu huo unaweza kuviruhusu viungo vya ndani kusukuma na kupenyeza, na kujenga eneo lililotuna. Unaweza kuwa na hernia ikiwa unaweza kuhisi namna ya eneo laini lililotuna kwenye maeneo ya tumbo au kinena au kwenye kovu ambalo lilitokana na upasuaji. Eneo hili lililotuna linaweza likapotea ukiminya sehemu hiyo au ukijilaza. Unaweza kupata maumivu kwenye eneo hilo hasa ukikohoa, ukiinama au ikinyanyua kitu kizito.
Dalili za Ngiri
Tumbo kuunguruma, kiuno kuuma, kupata choo kama cha mbuzi, kushindwa kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume kulegea, kutokuwa na hamu ya kulundia tendo la ndoa, korondani moja kuvimba, mgongo kuuma.
Dalili zingine za ugojwa wa ngiri ni pamoja na;
Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu.
Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia.
Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.
Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika endapo utawahi kupata tiba sahihi
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/34YsWhW
No comments:
Post a Comment