Wednesday, November 13, 2019

Sababu ya wanawake wa kabila hili kutoboa midomo na kuweka visahani







Surma ni kabila linalopatikana nchini Ethiopia na Sudan ambapo katika kabila hili wanawake hutolewa meno ya mbele upande wa chini na kutobolewa mdomo wa chini ili kuwekwa visahani. 

Utamaduni huo nchini huko ni urembo kwani jinsi mwanamke anavyokuwa na tundu kubwa mdomoni ndiyo jinsi thamani yake inavyozidi kuwa kubwa na kupelekea  kutolewa mahali kubwa zaidi kuliko yule mwenye kisahani kidogo mdomoni. 

Mila na desturi za watu hawa kipindi cha mahali huwa ni ng’ombe ambapo mwanamke mwenye tobo kubwa mdomoni hutolewa idadi kubwa ya ng’ombe kulinganisha yule mwenye tobo dogo. 

Na visahani hivi kwenye midomo yao  ya chini huvaliwa wakati wakiwaandalia waume zao chakula na wakati wa sherehe maalumu za kimila. 

Katika historia utamaduni huu wa kutobolewa mdomo wa chini na kuwekwa visahani ulianza wakati wa biashara za utumwa ambapo wanawake walianza kutobolewa midomo na kuwekwa visahani ili wasiwavutie wanaume waliokuwa wanakuja kununua watu. 







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2QdUag9

No comments:

Post a Comment