Monday, November 11, 2019

Simu imetowesha amani katika familia yangu. Naitegemea 90% katika kazi zangu za kila siku







Zaidi ya asilimia 90 ya shughuli zangu za siku zinategemea matumizi ya simu. Lakini simu hii imekuwa inaniletea ugomvi wa mara mwa mara nyumbani, kila siku ugomvi. 

Shida ni kwamba mke wangu amekuwa akichukua simu yangu mara kwa mara na kuanza kuikagua, akiona namba yenye mashaka basi ataanza kuhoji na kumpigia muhusika. Mara nyingine nimekuwa mbabe na hata kumpiga na kumwambia aachane na simu yangu lakini anarudia tabia hiyo hiyo. 

Ukiweka password nayo ni maneno na malumbano kwamba kuna mambo naficha. Ni kweli nachepuka ila sio kwa kiwango hicho anachonidhania. 

Nimetafuta alternative ya kuweza kuwasiliana na wadau wangu wa kazi na watumishi wenzangu bila simu nimeshindwa lengo likiwa ni kuachana na matumizi ya simu kabisa. 

Je mwanamke huyu nimfanyaje? Kwanini hakomi kunifuatilia kwa undani katika mawasiliano yangu?







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/34PI2pO

No comments:

Post a Comment