Wednesday, November 13, 2019

Mfahamu zaidi Mwanamama Leleti Khumalo, Muhusika Mkuu wa Filamu ya Sarafina






Muvi ya SARAFINA ni moja ya muvi au sinema maarufu sana Afrika na Dunia nzima iliyoigizwa mwaka 1992 kwa ushrikiano wa waigizaji wa marekani (Hollywood) na wale wa Afrika Kusini iliyokua na lengo la kuonesha jinsi ambavyo sera ya ubaguzi wa makaburu dhidi ya Waafrika na Wazawa wa Afrika kusini ilivyokuwa ikiendelea na ilivyokuwa ikiwaathiri watu wa Afrika ya kusini kipindi kile ililenga zaidi mauwaji ya halaiki ya wanafunzi wa Soweto nchini Afrika Kusini waliokuwa wanapinga unyanyasaji wa Makaburu hao. 

Kama ulishafatilia au kuangalia muvi hii utagundua kuwa mhusika mkuu katika muvi ile alikuwa Sarafina ambaye aliigiza kama mwanafunzi wa kike aliyekuwa akiwaongoza wanafunzi wenzake kupinga ubaguzi na  uovu uliokuwa ukifanywa na viongozi wa makaburu dhidi ya wananchi weusi na wazawa  wa Afrika Kusini wakati ule. 

Leo nimekuletea wasifu wa Leleti Khumalo maarufu kama Sarafina ili Uweze kumkumbuka na kumfahamu vizuri 

WASIFU WAKE 

Leleti khumalo alizaliwa 1970, ni mwigizaji wa Ki-Zulu wa Afrika Kusini aliyejipatia umaarufu  kutokana na nafasi yake ya kuongoza kama Mhusika mkuu katika filamu ya SARAFINA!, Na katika filamu nyingine kama vile HOTEL RWANDA, YESTERDAY na INVISCUS. 

Leleti Khumaro alimaaarufu kama Sarafina alizaliwa katika kitongoji cha KwaMashu , kaskazini mwa Durban, Afrika Kusini. Leleti Khumalo (Sarafina) alionyesha nia ya kuigiza akiwa katika umri mdogo sana, Khumalo alijiunga na kundi la vijana la kuchekesha  liitwalo Amajika, lililoongozwa na Tunokwe. 



Mwaka 1985 alijaribu kuimba muziki akiwa na Mtayarishaji na Mwigizaji maarufu wa Afrika Kusini Mbongeni Ngema ambapo wimbo alioimba ulikuwa na kuwa wa kimataifa ambao ulijulikana kama  Sarafina!; Ngema ndiye aliyeandika sehemu kubwa ya wimbo huo wa Sarafina kwa Leleti Khumalo. Na Mbongeni Ngema ndiye mwanaume ambaye baadae alimuoa Sarafina. 

Mwaka 1992, Sarafinsa alishirikiana sambamba na Mwana mama muigizaji kutoka Marekani aitwaye Whoopi Goldberg (amabye ndiye aliyekua mwalimu wa akina Sarafina katika somo la Historia katika muvi ile, na alijulikana kama ( Mary Masombuka), Miriam Makeba na John kani katika filamu iliyotengenezwa chini ya kampuni ya Darell James Rootd , Filamu iliyoitwa ”SARAFINA!”, ambayo ilisambazwa duniani kote, na ikawa filamu kubwa zaidi kutolewa Barani Afrika. Leleti Khumalo baadae alichaguliwa kuwania tuzo za Image pamoja na waigizaji wenzake; Angela Bassett, Whoopi Goldberg na Janet Jackson. 

Katika upande mwingine, mwaka 2015 Leleti alikaribishwa katika visiwa vya Zanzibar , Tanzania, kama mgeni rasmi wa sherehe maarufu Filamu za Kiafrika ambapo waandaaji wa sherehe hiyo walikuwa wakiadhimisha miaka 18 ya sherehe hizo  zinazojulikana kama Zanzibar Film Festivals. 

Filamu alizoagiza. 

Miongoni mwa filamu ambazo mwanamama huyu aliwahi kuigiza ni; 

·         Uzalo (2015 -) 

·         Winnie Mandela (2011) 

·         Invictus (2009) …. Mary 

·         Faith’s Corner (2005) …. Faith 

·         Hotel Rwanda (2004) …. Fedens 

·         Yesterday (2004) …. Yesterday 

·         Cry, the Beloved Country (1995) (as Leleti Kumalo) …. Katie 

·         Sarafina! (1992) …. Sarafina 

·         Voices of Sarafina! (1988)







from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/32FlS83

No comments:

Post a Comment