ZAIDI yako hakuna mwingine. Ni wewe mwenye kutaka uwe na amani na furaha katika uhusiano wako.
Ni wewe mwenye uwezo wa kuleta amani ama huzuni katika uhusiano wako. Zaidi yako hakuna mwingine.
Hata maumivu kwa wengi, wangeweza kuachana nayo kama wao wangeamua. Kama wangekuwa makini, kuongea na wenzao vizuri, kutumia maneno ya busara na hekima kuwekana sawa, wengi wangeepukana na maumivu.
Hata wale wenye kunyanyaswa na kuteswa. Pia wangeweza kuepuka mateso hayo kama wakiamua. Kama uliye naye hakupendi, hakujali na hakuthamini, kwanini ushindwe kuepuka mambo hayo?
Kila mmoja anapaswa kuwa na mtu anayempenda na kumjali. Kama mwenzako haoneshi hata dalili ya kukujali na kukupenda unakaa naye wa kazi gani?
Hata katika kituo changu cha ushauri, huwa sishauri watu kuachana. Ila kuna hatua inafika inabidi ufanye hivyo.
Kama mapenzi maana yake ni kujaliana, kuthaminiana na kuoneana huruma, ni kwa namna gani usimshauri mtu kuachana, kama baada ya kufanya kila kitu kuonesha anampenda fulani ila mwenzake hamjali?
Bado amini kila kitu kiko katika himaya yako. Kama uliye naye anakupenda, unaweza kudumisha hali hiyo kwa kumpenda, kumjali na kumsikiliza.
Wengi hukosea pale wanapokuwa na watu wanaowapenda na kuamini kuwa wao hawatakiwi kuonesha kuwa wanawapenda sana.
Baadhi humezwa na fikra za vijiweni, eti ukionesha unampenda atakutesa. Upuuzi ulioje! Kama huoneshi unampenda yeye atajivuna vipi kuwa na wewe?
Watu hawajivuni kuwa na fulani mwenye sura nzuri au mwenye fedha nyingi. Hujivunia kuwa na watu wenye kuwapenda na kuwajali.
Kama anakupenda sana leo wewe humjali, jua unatengeneza aina ya fikra katika akili yake itakayokuja kukujutisha baadaye.
Ndiyo, kwa kuwa katika maisha yake anahisi unathamani, leo atakunyenyekea na kukulilia sana, mbali na kuwa unamfanyia matendo mabaya.
Ila itakuja siku. Siku ambayo akili yake itawaza tofauti na moyo wake kukinai mateso. Hiyo siku ndipo utajua thamani na hadhi halisi ya kumjali mtu na kumthamini katika maisha yako.
Hakuna mwingine wa kulinda thamani na hadhi ya mapenzi yako. Kama kuna amani katika uhusiano wako, ni wewe mwenye jukumu la kulinda.
Ni kosa kuamini kuwa eti kwa kuwa kuna hali ya kutoelewana basi ni jukumu la mwenzako tu kufanya mambo kuwa sawa.
Hapana. Kwa kuwa mapenzi ni suala lenu nyote, basi hata changamoto zake pia zinapaswa kutatuliwa na wote.
Hata kama kakosea yeye. Wakati mwingine inapaswa ukae na kutafakari kwa kina kwanini kakosea na si kila muda unampa lawama tu.
Japo wapo wanaokosea kwa makusudi, ila wengi katika uhusiano wa kweli hukosea bahati mbaya. Kuwa makini kosa dogo lisifanye nyumba yenu kubomoka.
Kaeni chini kisha elekezaneni katika namna inayofunza na kufurahisha. Kwani nani m-bora kati yenu?
Kila mmoja huwa na mapungufu kwa namna yake. Linda thamani ya mapenzi yako kwa kutambua hilo na si kujifanya bwana mkubwa na kila kitu unajua wewe.
Hapana, hiyo haifai. Kuishi ni pamoja na kujifunza. Funzaneni. Wengi walioachana na kuwa na watu wengine leo wanajuta. Waliowapata wamekuwa ni ovyo zaidi kuliko wale waliokuwa nao mwanzo.
Thamani na ubora halisi wa mahusiano yenu utapatikana kwa kuvumiliana na kurekebishana. Kama wewe si mkamilifu, ni kwanini utake kuachana na mwenzako kwa sababu ya mapungufu yake?
Kuwa na mwenendo utakaoleta hamasa kwa mwenzako kuwa bora zaidi. Kuna wakati mwenzako anaweza kuwa ovyo kutokana na namna unavyoishi.
Ishi katika namna ambayo itamfanya mwenzako ajivunie na kuona thamani na ubora wako halisi katika maisha yake.
Kila mtu anataka kuwa na mtu bora na makini. Kila mmoja hujivunia kuwa na mtu anayesifiwa na kupewa thamani na hadhi katika jamii.
Sasa kwanini usiwe mtu huyo? Kwanini usijenge ubora utakaomfanya mwenzako si tu kuogopa kukupoteza katika maisha yake ila pia hata kulazimika kujiweka katika mazingira ya ubora zaidi ili asiweze kukupoteza.
Watu wenye kuwafanya wapenzi wao wawe na amani na kujiona wamebahatika kuwa nao katika maisha hujikuta nao wakifurahia zaidi mahusiano yao kutokana na wahusika kufanya kila mbinu kuwafurahisha ili wasije wakawakinahi katika maisha yao.
WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
from UHONDO KITANDANI https://ift.tt/2sJG5h7
No comments:
Post a Comment